Mwanamuziki Roma Mkatoliki amezungumza na waandishi wa habari leo kuhusu
tukio la utekaji lililomkuta yeye pamoja na wenzake watatu usiku wa
Jumatano wakiwa katika studio za Tongwe Records Masaki jijini Dar es
Salaam.
Roma amesema kuwa walikuja watu waliokuwa na silaha za moto, wakawaamuru
kuingia kwenye gari na kisha wakafungwa vitambaa usoni na pingu mkononi
na kupelekwa eneo ambalo halijulikani.
Wakiwa katika eneo hilo walihojiwa kwa siku tatu huku wakipigwa kabla ya
kwenda kutupwa wakiwa wamefungwa katika eneo ambalo kwa haraka
hawakujua ni wapi.
Tumekuandikia kile alichosimulia.
Wakati naendelea na shughuli zangu, walifika watu ambao sikuweza
kuwafahamu mbaya zaidi walikuwa na silaha za moto na amri yao ya kwanza
ilikuwa ni ingia ndani ya gari.
Baada ya kuingia tu ndani ya gari,
nakumbuka wale watu walitufunga usoni na vitambaa na kutuamuru tuiname
chini kwa order ya kwamba inama chini na usiinuke na wakiwa wameshika
silaha za moto.
Hofu yetu ikatufanya wote tuiname chini na gari ikaanza kuondoka maeneo ya studio na ikaelekea ambako sisi hatukupajua.
Tulipofika hiyo sehemu ambayo hatuijui tukiwa tumefungwa usoni, na walitufunga na pingu.
Tukaenda sehemu ambayo hatuijui, kwa
kuhisi tu hujui chochote na ndio sehemu ambayo tulikaa kwa siku zote
tatu kwasababu ilikuwa ni Jumatano, Alhamis, tunakuja kupata sisi
usalama ilikuwa ni Ijumaa usiku kuamkia Jumamosi.
Kwahiyo siku zote watu kilichokuwa
kinaendelea huko ambako tupo na hatupafahamu, kuna mahojiano yalikuwa
yanaendelea baina yetu na wale watu, mahojiano yenyewe ndio hizo details
ambazo nasema tumesharipoti katika vyombo vya dola wanaendelea na
upelelezi, wakimaliza upelelezi, wao wenyewe wataongea watatoa taarifa.
Lakini mahojiano hayo yaliendana na vipigo ambavyo nimeonesha majereha.
Kila mtu alipata majereha, kila mtu alipigwa, kwahiyo mahojiano yalikuwa
yanaendelea na hizo torture mpaka siku ya Ijumaa usiku sababu hatukuwa
tunaweza kugundua ni saa ngapi.
Tulitolewa hapo tulipokuwepo na
kuingizwa ndani ya gari na safari ilipoanza hapo tukiwa tumefungwa
vilevile lakini safari hiyo tulifungwa na mdomo, tukafungwa na miguu
tukiwa ndani ya gari tukaenda umbali ambao hatukuweza kujua ni wapi
mpaka kufika eneo ambalo tukatupwa tukiwa katika hali hiyo wote wanne.
Ilikuwa ni usiku sanam hatukuweza kujua ni wapi lakini tulifikiri ni kwenye dimbwi tu la maji tumetupwa.
Niliweza kujifungua mimi wa kwanza
nikawafungua na wenzangu, hatukujua ni maeneo gani lakini yalikuwa
maeneo ya baharini, tulikuwa na maumivu sana.
Nilivyoweza kuwafungua wenzangu
tukajikuta tuko salama, tukaanza kutembea kwa muda kiasi na baada ya
muda tukakutana na kibao fulani kimeandikwa mahaba beach tukagundua kuwa
pale ni maeneo ya Ununio.
Tulitembea kwa umbali mrefu sana mpaka
tulipoweza kupata msaada baada ya hapo tukaenda kuripoti maelezo yote
katika kituo cha polisi.
ALIPOFIKA NYUMBANI
Tulipofika Mbezi mimi nagonga mlango, ndani hakuna mtu, nikazunguka
mlango wa nyuma nikavunja mlango wa nyumbani kwangu. Kuingia ndani
familia hakuna, hilo lilikuwa pigo jingine kwangu sababu sikujua familia
yangu nayo imeenda wapi.
Hiyo ikawa hofu nyingine, kwahiyo
tulichokifanya nikawaambia tubadilishe nguo nikachukua nguo nikawa
wenzangu, tutokea katika zile nguo za matatizo.
Nikawaambia kama familia haipo nadhani
hapa si salama, ilikuwa inaelekea alfajiri saa kumi saa kumi na moja
ikabidi tutoke tutafute bajaji tukiwa katika mavazi salama ikawa ni
nafuu kwetu.
Tulipotafuta bajaji tukaomba namba ya
simu ya bajaji kumpigia mtu. Na mtu wa kwanza kumpigia ni bosi wetu
J-Murder, hakutuamini kwamba ni sisi kwasababu ya kile alichokuwa anajua
kinaendelea uraiani.
Kwa ufupi Haya ni baadhi ya Maneno ya Roma
1. Kwanza natoa shukrani kwa Mungu, kwenu, kwa wananchi na hasa wasanii wenzangu, nimeona mmesimama imara, pia serikali.
2.Kilichotokea ni kama case study maana kimetuunganisha wote bila kujali itikadi zetu, tuendelee kushikamana.
3.Niwaambie ukweli tu, mpaka sasa hatuna uhakika na usalama wetu, mahali tulipokuwa si pazuri kabisa.
4.Kama alifanyiwa daktari, baadaye akafanyiwa msanii, usishtuke kesho akafanyiwa mwandishi wa habari, au Mbunge.
5.Kinachotusikitisha zaidi ni maneno ya baadhi ya watu wanaodai kuwa tumepewa pesa ili tuitengeze hii, siyo sawa.
6.Ukweli ni kwamba tukio ni la kweli na tumepigwa sana, hadi sasa hatuko sawa kiafya.
7.Siku hiyo, walikuja watu wakiwa na silaha, na wamefunika nyuso zao, wakatuamrisha kuingia ndani ya gari.
8.Walitufunga macho na kutupeleka kusikojulikana, walitutesa sana, wametupiga sana.
9.Baada ya kupitia katika kipindi cha mateso makali, tuliachiwa usiku, tukaazna kutembea bila kujua tuko wapi.
10.Siwezi kujua kama tukio hili linahusiana na muziki wangu, maana kuna hadi house boy wetu pia amehusika.
Wiki moja iliyopita niliacha ahadi yangu ya kuwa makala ijayo
nitakueleza namna ya kupata wafadhili katika fursa yako. Na nilipokea
barua pepe nyingi na ujumbe mfupi wa maandishi kwamba wanasubiri kwa
hamu. Basi bila shaka siku uliyoingojea kwa hamu ndiyo hii. Kaa mkao wa
kulisha ubongo kisha twende sawa ili niweze kukata kiu yako.
Enzi za utoto ndiko kulikonifanya niweze kujua ukweli juu ya jambo hili.
Unajua ni kwanini? Wakati tupo wadogo pale kijini kwetu palikuwa na
kanisa ambako watoto wengi tulikuwa tunapenda kwenda zaidi hasa pale
walipokuwa wanakuja wazungu. Wengi tulikuwa tunapenda kwenda katika
kipindi hicho wakija wageni hao kwa sababu walikuwa wanakuja na vitu
vizuri kwa ajili yetu na kuweza kutugawia watoto wote ambao tulikuwepo
siku hiyo. Walikuwa wanatugawia vitu kama saa, nguo, baiskeli na vitu
vingine vingi ambavyo wakati huo vilikuwa vinatuvutia sana.
Nafikiri kwa kisa hicho kama utakuwa miongoni wa waliokuwa wanapata
zawadi hizo nitakuwa nimekukumbusha mbali sana. Lakini kwa kipindi hicho
hakuna aliyejali kwamba wale wazungu wamepajuaje kanisani petu pale
kijijini zaidi ya kufurahia zawadi zao! na wakati hawajawai kufika hata
siku moja katika bara letu hili! Kadri nilivyozidi kukua nikazidi
kufanya uchunguzi ambao ulikata kiu yangu, naamini pia utakata kiu yako.
Kumbe ukweli ni kwamba kuna njia ambazo huwa zinatumika mpaka kuweza
kuwapata wafadhili ambao wapo nje ya nchi na wakaweza kukusaidia katika
kutekeleza jambo lako.
Jambo ambalo huzingatiwa zaidi katika kupata wafadhili , wao huangalia
mtu ambaye amekwisha kuanza kulitekeleza jambo lake kwa kiwango fulani.
Kama nilivyokueleza mfano wa kanisa hapo juu ili wawaze kukufadhili ni
lazima uwe umeshalianzisha kanisa hilo. Usiwatafute wafadhili kwa kupiga
‘stori’ tu bila kuwa na kitu maana kuna usemi unasema mwenye nacho
huongozewa. Je, unataka kufahamu ni njia zipi za kutumia ili kuwapata
wafadhili?
Zifuatazo ndizo njia za kupata wafadhili katika mradi wako; 1. Intaneti/wavuti (website)
Hii ndio njia ya kwanza ambayo kiukweli itakufanya ambayo hata wewe
ukiweza kuitumia leo utakwenda kunufaika zaidi. Ikumbukwe ya kwamba
kuitumia intaneti vizuri ni pesa mkononi ambayo itakufanya utengeneze
pesa zaidi. Namna ya kutumia njia hii ni kwamba, ingia ‘google’ ile
sehemu ya kuandika jambo ambalo unalihitaji, kisha andika jambo lako.
Kwa mfano unacho kituo cha kulelea watoto yatima na unataka kupata hao
wafadhiri.
Unaweza kuandika hivi (Organization supporting orphan children) baada ya
hapo, ‘google’ itafunguaka kurasa mbalimbali zenye matokea zaidi hata
ya elfu tano. Tuliza akili yako na uanze kufungua moja baada ya
nyingine. Ukifungua nenda sehemu ya ‘home ya page’ hiyo kisha tafuta
sehemu ya ‘contact page’ , baada ya kuipata sehemu hiyo zichukue namba
zao za mawasiliano na uanze kuwasiliana nao watu hao. Huenda pia wakawa
hawajaweka namba ya zao za simu au e-mail zao ila kukawa na sehemu ya
wewe kujaza taarifa zao zijaze kisha utaona ni jinsi gani mtakavyoweza
kuwasiliana nao. 2. Kujitolea na kujipendekeza.
Baada ya kutembelea hizo kurasa zao anza sasa na kujitolea na
kujipendekeza kwa kutuma mawazo yako chanya, tuma picha mbalimbali za
huku afrika ikiwemo vivutio tulivyonavyo, tuma shughuli unazofanya kama
ni kilimo, biashara na vitu vingine baada ya hapo anza kutuma picha za
jambo lako ambalo unalitaka ufadhili kama ni kituo cha kulelea watoto
yatima tuma majengo yake kama tayari kimeanza kutoa huduma tuma picha
mbalimbali.
Kufanya hivi kutawafanya wafadhili hao waweze kupenda kuja kukutembelea
na kuona hivyo vitu vya utalii vilivyomo katika nchi yako. Hakikisha ya
kwamba huwaombi fedha wafadhili hao mwanzoni tu mwa mawasiliano yenu
maana watakuona wewe ni tapeli. 3. Jifunze kwa watu ambao tayari wana wafadhili.
Kwa kuwa kuna watu tayari wamekwisha wapata wafadhili ni muda wako
muafaka wa kuwauliza waliwapata vipi wafadhili hao? Kufanya hivyo
kutakufanya uweze kuwapa wafadhili katika jambo lako. Pia kama utakuwa
hajaweza kuwapata wafadhili wa kutoka ya nje unaweza kujua namna ya
kuwapata wafadhili wa ndani ya nchi ambao nao wana mchango mkubwa katika
kukufanikisha jambo lako kwa muda sahihi. Kuwa ni mtu wa kutaka
kujifunza zaidi kwa kufuatalia mwenyewe kwa ndani kuliko kusikia tu.
Norway imetangaza kuwepo kwa mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi baada
ya kugundua bomu lililotengenezwa nyumbani kwenye mji mkuu Oslo siku ya
Jumamosi.
Kwa sasa imedhibitika kuwa ilipangwa kufanywa kwa shambulizi mjini hapo
kama ilivyokuwa kwa miji ya nchi nyingine mfano Stockholm, St Petersburg
na London iliyoteak siku za hivi karibuni.
Kijana wa miaka 17 raia wa Urusi amekamatwa akihusishwa na tukio hilo.
Mwanasheria wa kijana huyo anasema kuwa hizo ni njama tu, Vyombo vya
dola vinasema kuwa wamefanya mahojiano na kijana huyo na amekiri
kuliunga mkono kundi la IS.
MADIWANI wa Manispaa ya Dodoma wamemwondoa Meya wao, Jafari Mwanyemba
kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye kutokana na kumtuhumu
kuhusika na tuhuma mbalimbali zikiwamo za ubadhirifu wa fedha.
Kura hizo zilipigwa mjini hapa kwenye Mkutano Maalumu wa Madiwani wa kujadili tuhuma dhidi ya Meya Mwanyemba.
Kati ya madiwani wa manispaa hiyo 56, 47 ndio walipiga kura ya kutokuwa
na imani naye dhidi ya kura nne zilizodai kuwa na imani naye, wakati
kura moja iliharibika na madiwani wanane hawakupiga kura.
Akitangaza matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa, Godwin Kunambi
alisema kuanzia saa 8.30 adhuhuri hiyo, Mwanyemba si Meya wa Manispaa
ya Dodoma na kutokana na kanuni za manispaa, Naibu Meya Jumanne Ngede
ndiye atakayekuwa akiongoza hadi uchaguzi wa kuziba nafasi
utakapofanyika miezi miwili kuanzia sasa.
Alisema kutokana na kanuni za halmashauri hiyo namba 4 (8), baada ya
Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa kurudisha ripoti kwa mkurugenzi katika
kipindi cha siku 14, alitakiwa kuwasilisha kwenye mkutano maalumu wa
madiwani kwa uamuzi wa tuhuma dhidi ya meya huyo ambapo madiwani
wameamua kumng’oa kwa kupigia kura.
Kutokana na kupigwa kura ya kumng’oa, kanuni za halmashauri zinamruhusu aliyekuwa Meya wa Manispaa ndani ya mwezi mmoja kukata.
Formal application for admission is made on an Application form.
The forms are available
below for downloading. Please click on the links provided below.
Download the application form, fill-out the hard copy accordingly.
Attach copies of Academic Certificates/Transcripts, and together with a
non-refundable, non-creditable application fee of Tshs 20,000.00 (For
Tanzanian) or US$25 (For Foreigner) should accompany the application
and