Saturday, 24 December 2016

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DEC TAREHE 24.12.2016

Share:

Friday, 23 December 2016

Rais Magufuli Amteua Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Kuchukua Nafasi ya Damiani Lubuva

Share:

Mwandishi wa ITV Aliyekamatwa Kwa Amri ya Mkuu wa Wilaya Aachiwa Kwa Dhamana

Mwandishi  wa kujitegemea wa kituo cha televisheni cha ITV, Halfani Lihundi ameachiwa kwa dhamana kutoka katika kituo cha Polisi cha Changamoto, Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha alikokuwa anashikiliwa tangu juzi, na kutakiwa kuripoti kituoni hapo Desemba 27, mwaka huu.

Alikuwa anashikiliwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, baada ya kuripoti habari inayoelezwa na mkuu huyo wa wilaya kuwa haikuwa sawa na kuamuru kukamatwa kisha, kulala mahabusu na hatimaye kufanikiwa kutoka jana saa tisa alasiri.

Awali, waandishi wa habari wa Arusha walikusanyika kituoni hapo ili kujua hatma ya mwenzao na baadaye kuamua kwenda kumuona Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ili kumweleza kuwa mwenzao amekamatwa kwa sababu ya migogoro ya wananchi.

Wakati Lukuvi anatoka kwenye kikao cha kujadili migogoro ya ardhi kilichofanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, waandishi waliimba wimbo wenye lengo la kufikisha ujumbe kuwa, wanataka wenzao aachiwe huru. Waliimba; “Solidarity Forever, Bring Back Halfani Lihundi.”

Lukuvi alisema hahusiki na suala hilo na kuwasihi wanahabari kwenda naye Usa River kwenye mkutano ambapo Mnyeti atatoa tamko juu ya suala hilo.

Lakini Mnyeti alipokuwa akitoka kikaoni hapo aliulizwa na waandishi kuhusu suala hilo na kosa lipi limefanya Lihundi kushikiliwa Polisi, lakini hakuzungumza chochote na kuelekea kwenye gari lake kusubiri msafara wa Lukuvi. 
Awali, ilidaiwa kuwa Mnyeti ndiye aliyeamuru Lihundi akamatwe kwa madai ya kuandika habari za uchochezi za kijiji cha Leguruki, Arumeru.

Alisema alipotaka kujua kosa analoshitakiwa nalo Lihundi, alijibiwa hana kosa ila yupo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya. Hata hivyo, RB ya Polisi Usa River 4763/2016 inaonesha ana kosa la uchochezi.
Share:

Aliyenajisi binti wa miaka 9 Ahukumiwa Miaka 30 Jela

Mahakama  ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu Shabani Huseni (29), kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kunajisi mtoto wa miaka tisa.

Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Catherine Kihoja alisema upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi watano ambao wameweza kuthibitisha mashitaka bila kuacha shaka yoyote.

“Kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa umeweza kuthibitisha mashitaka hivyo, mshitakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshitakiwa,’’alisema Hakimu Kioja.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo Wakili wa Serikali, Neema Moshi, aliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria kwa kuwa mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho ameathirika kisaikolojia na kupata madhara kiafya kutokana na kutokwa na harufu mbaya sehemu zake za siri.

Aidha, mshitakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kile alichodai kwamba hana ndugu, ombi ambalo lilitupiliwa mbali.

Inadaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo tarehe isiyofahamika Julai mwaka jana eneo la Kipunguni B, Moshi Baa wilayani Ilala ambapo alimbaka mtoto wa miaka tisa.
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DEC TAREHE 23.12.2016

Share:

Thursday, 22 December 2016

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YOTE YA VYUO VYOTE TANZANIA YA WANAFUNZI WALIOFANIKIWA KUHAMA VYUO NA KUBADILISHA KOZI ZAO 2016/2017

Image result for TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA
KUONA MAJINA YA WALIOFANIKIWA KUHAMA VYUO >>BONYEZA HAPA<<

KUONA MAJINA YA WALIOFANIKIWA KUHAMA KOZI >>BONYEZA HAPA<<
Share:

MAJIBU YA MASWALI NA HOJA ZA WADAU KWA MWEZI NOVEMBA, 2016 KUHUSU AJIRA MBALIMBALI

 Image result for SERIKALI YA TANZANIA




Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwashukuru Wadau wake na wananchi wote kwa ujumla waliotembelea tovuti (www.ajira.go.tz), waliofika ofisini kuonana na Maafisa kupata ufafanuzi wa maswala mbalimbali, waliopiga simu, waliotuma barua pepe na kutuandikia maoni pamoja na kuuliza maswali kwa kipindi cha mwezi Novemba, 2016.
Hoja tulizozipokea kwa njia zote zilizoainishwa hapo juu  zimejumuishwa na kutolewa majibu ya jumla kwa hoja zinazofanana kwa faida ya wadau wote ili kuendelea kuelimisha umma kuhusu masuala ya Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira Serikalini, majibu binafsi pia yametumwa kwa wadau wote waliotuma hoja zao mahsusi na maoni katika njia walizozitumia.
Swali la 1
KUHUSU UTARATIBU WA KUFUATA ILI KUREJESHWA KAZINI.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, mimi ni mmoja kati ya wale walio fanya usaili mwezi Septemba 2015 na kufaulu kisha kupokea barua ya kupangiwa kituo cha kazi kwa Cheo cha Afisa maendeleo ya jamii Daraja la Pili. Hata hivyo baada ya kukamilisha usajili ikiwa ni pamoja na kujaza fomu ya mkataba jina langu halikuingizwa katika orodha ya malipo (payroll) na baada ya kufuatilia nilipata taarifa kuwa cheti changu cha (higher diploma) hakikutambuliwa katika scale za mishahara hivyo nilipaswa kurejea chuo ili kupata cheti chenye rank zinazo tambuliwa ndipo nirejeshwe kazini kama kawaida. Sasa nimemaliza masomo na nina Degree ya maendeleo ya jamii, Naomba kurejeshwa kazini kulingana na makubaliano ya awali na naomba nipewe utaratibu wa kufuata ili kufikia hatua hiyo.
Jibu lolote litanipa Mwanga ktk harakati za kimaendeleo ndani ya Taifa langu, natarajia busara toka kwako katika kutatua tatizo langu,
Jibu
Hongera kwa kufaulu na kupangiwa kituo cha kazi. Pamoja na hilo tunakupa pole kwa kutoweza kuingia katika orodha ya wanaolipwa mishahara na Serikali kama ambavyo umeeleza. Kwa jinsi ulivyotoa maelezo yako tunaweza kukushauri kufanya yafuatayo:-
i. Waajiri wote waliopo katika Serikali huajiri watumishi kwa kila kipindi cha mwaka mmoja wa fedha endapo watapewa kibali na kukifanyia kazi katika muda uliopangwa na si vinginevyo. Hivyo si rahisi mwaka husika utakapopita bila kutekeleza ajira hizo kuweza kuendelea nazo, vinginevyo kuwepo na ruhusa ya kufanya hivyo kutoka katika Mamlaka husika.
ii. Kwa kuwa sasa umekwishafanikiwa kupata Shahada ya Maendeleo ya Jamii ni vema ukiona matangazo ya kazi yanayohusiana na kada hiyo na kukidhi vigezo uombe kazi ili uweze kuajiriwa.
iii. Kwa kuwa ajira yako ilishapitiliza mwaka bila ya kukamilika kama ulivyoeleza si rahisi kuendelezwa kutokana na taratibu za muda wa utekelezaji wa vibali vya ajira ambavyo huwa ni ndani ya miezi mitatu tangu tarehe ya kuidhinishwa.
Tunakushauri kuendelea kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya ajira kwa ajili ya kuona matangazo ya fursa za ajira zilizopo na maeneo ya waajiri wengine kama tulivyoshauri.
Swali la 2.
Hivi mtu ambaye alifanya usaili wa ajira za utumishi wa uma na alikuwa anasubiri matokeo ya usaili, kabla matokeo kutoka ajira zikasitishwa ,je mkianza kuajiri ataajiriwa kwa usahili huo ?
Jibu
Tunashukuru kwa swali lako, Ni kweli Serikali ilisitisha kwa muda mchakato wa ajira mwezi juni kwa ajili ya kupisha zoezi linaloendelea la watumishi hewa, Aidha endapo zoezi la kusitishwa kwa ajira halitazidi kipindi cha miezi sita tangu usaili ulipofanyika na endapo ulifanya usaili na ukawa umefaulu ajira zikifunguliwa unaweza kupangiwa kituo cha kazi na kuajiriwa. Sekretarieti ya ajira ina utaratibu wa kuhifadhi kwenye kanzidata waombaji kazi waliofaulu ambayo hudumu kwa kipindi cha miezi sita (6) kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji za Sekretarieti ya Ajira.
Swali la 3
Habari za kazi mheshimiwa na pole kwa majukumu ya kulijenga Taifa.
Ninaomba kuishauri serikali kupitia upya ama kutunga sheria mpya ili kulinda maslahi ya sisi wazawa na Taifa kwa ujumla, kama ifuatavyo;
1. Baadhi ya wawekezaji wachache si wengi, hawatoi mikataba ya kazi kwa wafanya kazi kama sheria ya ajira inavyoelekeza na mfanya kazi akihoji kuhusu hili ananong'onezwa kuwa hiyo ni njia ya kupunguza watu wakati mfanya kazi anatimiza wajibu wake. Tatizo hili lipo sana kwa baadhi si  wote, wawekezaji wenye asili ya asia hasa India.
2.Baadhi ya wawekezaji hasa wenye asili ya asia hawatoi bima ya afya kwa wafanya kazi kama sheria mpya ya kazi inavyoelekeza waajiri kufanya hivyo.
3.wawekezaji wengi 90% , wamegeuza nchi yetu kama shamba la bibi, kwa kulipa mishahara duni, ya kinyonyaji bila kuzingatia ujuzi au kiwango cha elimu alichonacho mfanya kazi. hapa sijui kama hili tatizo ni la wizara kwa kutotoa muongozo wa malipo ya mishahara kwa kuzingatia elimu ya mfanyakazi au la?. mimi si mwanasheria.
graduate amemaliza masters degree ,engineering analipwa laki nne(400,000) sawa na gate man , hata ukiwa na phd , the same payment  but mfanya kazi mwenzio mwenye certificates ambaye anatoka nchi ya muwekezaji , hana experience , anachofanya na wewe hicho hicho , analipwa milioni ishirini(20,000,000) Tzsh.
Serikali inakosa mapato kupitia makusanyo hafifu ya kodi, wasomi wataendelea kukwepa kurudisha mikopo helseb kwakua laki nne hata wao haziwatoshi na hakuna kazi lazima wafanye wasirudi geita. nijitolee mfano mimi niliacha kazi viettel now halotel last year for this neo- colonialism exploitation under the umbraler  of investment.
my take: serikai itunge sheria kwa wawekezaji kulipa mishahara elekezi kama wafanya kazi wa serikali wanavyo lipwa na haki zote pia, maana watanzania wote hatuwezi kufanya kazi serikalini. Kama wizara itafanya hivyo, naamini kabisa , hakutokuwa na wadaiwa sugu wa bodi ya mikopo , kodi kubwa itakusanywa na nchi itasonga mbele bila kumpigia magoti tapeli yoyote mweupe. Naamini serikali sikivu na ya kizalendo ya hapa kazi tu, hili inaweza kulitekeleza. nakutakia kheri katika ujenzi wa Taifa.
Kind regards;
 Jibu
Tumepokea maelezo ya swali pamoja na maoni yako. Hata hivyo tungependa kukushauri kuwa kuwa suala la mikataba ya ajira na kima cha chini cha mishahara kwa Taasisi binafsi (Private sectors) linashughulikiwa na Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Walemavu. Hivyo ni vema suala hili likaelekezwa katika ofisi hiyo ili liweze kujibiwa ipasavyo.
Swali la 4.
AJIRA YANGU YA AFISA USHIRIKA DARAJA II-WILAYA YA KITETO
Ndugu Katibu Mkuu, Husika na kichwa cha habari hapo juu. Mnamo Septemba mwaka jana nilifanya usaili mara mbili yaani kwa kuandika na kwa mahojiano ya kazi ya Afisa Ushirika. Baada ya interview zote mbili tuliambiwa tusibirie baada ya mwezi tutapata majibu kama tumepata kazi au la.
Mnamo November 2015 yalitoka majina ya watu na vituo vyao vya kazi lakini kwenye orodha hiyo jina langu halikuwepo. Baadae mwezi Machi, 2016 nilipigiwa simu kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma niende kuchukua barua ya kuajiriwa. Nilienda kuichukua barua ile na nikawa nimepata ajira kama Afisa Ushirika Daraja II katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Nilienda kuripoti kwenye kituo changu cha kazi. Nilipofika pale nilielezwa kwamba serikali imesisitisha ajira za watu wote waliokuwa wameajiriwa mwaka 2016 na kutakiwa kurudi nyumbani hadi itakapowaita. afisa utumishi wa Wilaya ya Kiteto akaniambia kwa kuwa serikali imesistisha ajira hawezi kunipokea hadi hapo tangazo la kuwarudisha wale waliokuwa wamesimamisha litakapotoka ili miweze kuripoti. Sasa ndugu Katibu Mkuu kwa hali yangu kama hii nifanyeje? na je serikali ishatoa waraka wa kuwarudisha kazini watumishi waliojiriwa mwaka huu ambao walipisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa?
Naomba mwongozo wako
Jibu
Pole sana Bw. Gwawilo kwa usumbufu utakaokuwa umeupata. Ni kweli kama ulivyoeleza Serikali ilisitisha ajira mnamo mwezi Juni, 2016 kwa ajili ya kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa, Aidha kwa kuwa tayari ulishapewa barua kwa ajili ya kwenda kuripoti kwa mwajiri wako huko Kiteto tunakushauri uendelee kuwasiliana na mwajiri wako ulipopangiwa kwa ajili ya kupata mrejesho na maelekezo zaidi kwa kuwa Sekretarieti ya Ajira ilikwisha kamilisha kazi ya kukupangiwa kituo cha kazi.
Swali la 5.
Hongereni sana kwa kazi mnazofanya. Samahani naomba kujua jambo moja. Mwezi mei vijana takribani 3000 waliajiriwa lakini mwezi June ajira zao zilisitishwa. Sasa kuna taarifa kuwa ajira zile zimefutwa na vijana wale watapaswa kuomba upya pindi ajira zitakapo tangazwa. Je kuna ukweli juu ya jambo hili?
Jibu
Asante kwa swali na tunashukuru kwa pongezi zako. Mpaka sasa Sekretarieti ya Ajira haijapokea taarifa ya kufutwa kwa ajira ulizozitaja, Serikali ilisitisha ajira mpya mwezi Juni mwaka huu kwa ajili ya kupisha zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa na mara baada ya zoezi hilo kukamilika na kuanza mchakato wa Ajira kwa kada mbalimbali mamlaka husika zitatoa taarifa kamili ikiwa ni pamoja na waombaji kazi ambao walisharipoti kazini na kusitishiwa ajira zao.
Swali la 6.
Habari za kazi,kwanza nitangulize shukurani zangu za dhati kwa utendaji kazi wenu, mimi nifanya usaili chuo cha ardhi wa maandishi na baadae usaili wa mahojiano, baadae Mh rais akasitisha ajira .Nilikuwa nataka kujua kama mchakato ulishamalizika ama bado tuendelee kusubiri. Ahsante
Jibu
Tunashukuru kwa pongezi zako na tumepokea swali lako, tunapenda kukujibu kuwa kwa sasa zoezi la uhakiki bado linaendelea na litakapokamilika taarifa kamili itatolewa na Mamlaka zinazohusika kwa hatua inayofuata.
Swali la 7.
Poleni sana na kazi na hongereni kwa kazi nzito mnayoifanya kwa mafanikio makubwa! Nilipitia moja ya majibu ya hoja za wadau za mwezi oktoba kwa swali ambalo kuna mtu aliuliza kuhusu majina ya watu waliokua wamehifadhiwa kwenye kanzidata juu ya usalama wao kutokana na ajira kusitishwa! Katika majibu yenu mlisema majina yanahidhiwa kwa muda wa miezi 6 hivyo sababu ajira zilisitishwa mwez june ikifika mwezi desemba majina hayo yataondolewa! Maoni yangu ni kuwa kwanini watu hawa wasiendelee kuwepo kwenye kanzi data sababu ajira zimesitishwa ivo kuwaondoa kwenye kanzidata wakati ajira bado hazipo naona kama hawatendewi haki, ombi langu ni kuwa naomba mliangalie swala hili kwa mara ya pili tena ili watu hao walio kwenye kanzi data wasiondolewe mpaka ajira zitakaporuhusiwa hata yakikaa kwa mwezi mmoja tu baada ya ajira kuruhusiwa! Nitoe shukrani zangu tena kwa mara nyingne niwatakie utendaji mwema wa kazi naamini ombi langu kitapokelewa na kufanyiwa kazi.
Jibu.
Asante na hongera kwa kutufuatilia kwa ukaribu. Kwa mujibu wa Taratibu zetu za uendeshaji wa mchakato wa ajira majina ya waombaji kazi waliofaulu lakini hawakupangiwa vituo vya kazi kwa sasa huhifadhiwa kwenye kanzi data kwa muda usiozidi miezi sita, Aidha ushauri wako tumeupokea na tunaufanyia kazi kadiri itakavyowezekana.
Swali la 8
Habari za kazi,pole na majukumu ya kazi, kwanza nashukuru sana kwa kunipangia nafasi ya kazi baada ya kufaulu interview. Nilirepot kituo cha kazi tangu mwezi wa nne(4) mwaka huu (2016) nasikitika kabla sijapata check number tangazo la kusitisha ajira likatoka,lakini kuna wengine ambao walipata tukio nzuri la kupata check number kabla ya kusitishwa ajira.
Sababu napenda sana nafasi hii nimeendelee kuwa mvumilivu nikiwa kituo cha kazi mpaka pale nitakapoingizwa kwenye payroll.  kwa wale waliokuwa wamepata check number  nakusitishwa mshahara wao kuna tamko linaloonyesha kwamba mwezi huu warudishwe tena kwenye system natumai wataanza kupata mshahara.  Naomba msaada wenu angalau kujua na mimi nitaingizwa wakati gani kwenye payroll angalau na mimi nianze kupata mshahara. muwe na kazi njema na siku njema pia.
Jibu
Asante kwa swali lako. Ni kweli ajira zilisitishwa ili kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa ambalo linaendelea, Tunachokuomba kuendelea kuwa mvumilivu hadi hapo mamlaka husika zitakapotoa taarifa za kukamilika kwa zoezi hilo. Aidha kwa kuwa tayari ulishapangiwa kituo cha kazi tunakushauri kuendelea kuwasiliana na Mwajiri wako kwa ajili ya taarifa zaidi kuhusu ajira yako.
Swali la 9.
Ndugu Mheshimiwa, salam, Naomba kujua kuhusu swala hili: Je uhakiki utakapokamilika, Sekretarieti ya ajira itatangaza tena upya zile nafasi za kazi zilizokuwa zimetangazwa na taasisi za serikali ule mwezi wa tano kabla ya zoezi la uhakiki kuanza? Kwakuwa ajira za serikalini zilisitishwa kwanza kwaajili ya zoezi la uhakiki lililoanza tangu mwezi wa sita, kwa mfano Chuo kikuu cha dar-es-salaam kilitangaza nafasi za kazi mwezi wa tano na nyingine mwezi wa saba, je sekretarieti ya ajira itarudia kuzitangaza nafasi zile? Au utaratibu utakuwaje?
Jibu
Tunashukuru kwa swali lako, Kwa mujibu wa kumbukumbu zetu nafasi hizo zilizotangazwa na Chuo kikuu cha Dar es salaam hazikutangazwa kupitia sekretarieti ya ajira hivyo ni vizuri kuwasilisha swali lako chuo husika kwa ajili ya majibu ya kina.
Swali la 10
Habari za kazi mkuu, naomba kuuliza sisi tulioajiriwa mwezi mei na hatukupata mshahara tutarudishwa lini kazini?maana wenzetu waliopata walau mshahara mmoja wameitwa.Asante natumaini swali langu litajibiwa.
Jibu
Ni kweli wapo baadhi ya waombaji kazi ambao walifanya usaili ambapo wale ambao walifaulu walipangiwa vituo vya kazi kwa waajiri mbalimbali kabla ya kusitishwa kwa jili ya kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa Serikalini. Aidha kwa kuwa tayari ulishaajiriwa kabla ya usitishwaji wa ajira hiyo tunakushauri uendelee kuwasiliana na mwajiri wako kuhusu ajira yako kwa kuwa Sekretarieti ya Ajira ilishamaliza kazi yake.
Swali la 11.
Habari, Hongereni kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya katika kuhakikisha wananchi wa kitanzania wanapata ajira bila kuwepo na upendeleo au rushwa ya aina yeyote ile. Napenda sana kuipongeza sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma. Mwenyezi Mungu awabariki sana. Baada ya pongezi zangu nilipenda kutaka kufahamu mwenendo wa ajira mpaka sasa unavyoenda. Kama sijakosea mnamo tarehe 04/11/2016 Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimu Dr. John Pombe Joseph Magufuli akiwa Ikulu alipata nafasi ya mahojiano na waandishi wa habari lengo likiwa kufafanua na kuuelezea umma juu ya utendaji wake wa kazi baada ya kumaliza mwaka wake wa kwanza toka achaguliwe kuwa rais. Moja ya maswala aliyotolea ufafanuzi ni pamoja na ajira. Mheshimiwa Rais alisema kuwa swala la ajira kusimamishwa halipo tena na ajira zimeendelea kutoka katika taasisi tofauti za umma ikiwemo Wizara ya Afya.Sasa naomba kuuliza mbona hamtangazi ajira na ikiwa Rais ameshasema ajira zinatolewa kwa sasa huku uhakiki wa watumishi hewa ukiendelea? Ningefurahi endapo swali langu mngenijibu kwa kunipatia maelezo. Nashukuru sana na Kazi njema.
Jibu.
Tunashukuru kwa pongezi zako. Tunaomba kukufahamisha kuwa nafasi hizo za wizara ya Afya, hasa kwa kada za madaktari na wauguzi mchakato wake wa ajira haupitii Sekretarieti ya Ajira kama nafasi hizi husimamiwa na kuratibiwa moja kwa moja na wizara husika. Aidha kwa nafasi za kazi zinazopitia sekretarieti ya Ajira zinatangazwa baada ya kupata kibali/vibali vya Ajira toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na Utawala Bora, kwa nafasi ambazo tumekuwa tukipata vibali zimeendelea kutangazwa kadri zinavyojitokeza.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
27 Barabara ya Bibi Titi Mohamed,
S.L.P 63100,
Maktaba Complex,
11102 Dar es Salaam
Share:

Aliyekufa muda mfupi baada ya kubatizwa azikwa kiislam


Kijana Issa Juma aliyeripotiwa kufariki dunia Jumapili iliyopita, muda mfupi baada ya kubadili dini na kubatizwa katika mto mmoja kwa imani ya Kikristo akijiunga na kanisa la Efatha kwa jina la Paulo, amezikwa kwa imani ya Kiislam.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kuwepo mvutano kati ya Kanisa la Efatha na viongozi wa dini ya Kiislam wakitaka kijana huyo azikwe kwa imani yao, lakini mwisho kauli ya wazazi wa marehemu ilikuwa na nguvu zaidi na hivyo kuzikwa kwa imani ya Kiislam.

Akizungumzia uamuzi huo, mama mdogo wa marehemu ambaye jina lake halikupatikana alizungumza kwa niaba ya mama mzazi, Rehema Juma alithibitisha kuwa walimzika ndugu yao Jumanne wiki hii kwa imani ya Kiislam.

Kifo cha kijana huyo kiliibua sintofahamu ikiwa ni saa chache baada ya kuzaliwa kwa mara pili kwa imani ya Kikristo na haikufahamika mara moja chanzo chake kama alikuwa na ugonjwa ama ni masuala ya kiimani.
Share:

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DECEMBER TAREHE 22.12.2016

Share:

Uhamiaji Yazipiga Marufuku Simba, Yanga na Azam Kutumia Wachezaji wa Kigeni


Serikali imevipiga marufuku Klabu za ligi kuu Tanzania hususani Simba, Yanga na Azam kuwatumia wachezaji wa kigeni mpaka watakapokamilisha taratibu zao za uhamiaji.

Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya klabu ya Ndanda FC kutuma malalamiko TFF kwamba Simba iliwatumia wachezaji wake wawili wa kigeni Daniel Agyei na James Kotei kwa madai kwamba hawana vibali vya kufanya kazi nchini.

Klabu hizo zimepewa maagizo kwamba wachezaji na makocha wote wa kigeni ambao hawajakamilisha taratibu za uhamiaji hawatoruhusiwa kuzihudumia klabu zao hadi hapo watakapokamilisha taratibu hizo.

Idara ya uhamiaji kupitia kwa afisa uhamiaji John Msumule leo alitoa tamko kwa klabu zote za Ligi Kuu Tanzania bara kutoendelea kuwatumia wachezaji wake wa kigeni hadi watakapotimiza masharti ya uwepo wao nchini kisheria na uhamiaji wamezitaka klabu za Simba, Yanga na Azam FC kuhakikisha wachezaji wake na makocha wao wa kigeni wanapata vibali vya kufanyia kazi nchini pamoja na kuishi.

Hata hivyo kwa upande wa Yanga wao wachezaji wao wana vibali vya kazi na vya kuishi nchini isipokuwa makocha wao ndio wana vibali vya kazi pekee.

Kwa upande wa watani zao wa jadi Simba wao hawajatimiza vigezo hivyo kwa wachezaji wao wa kigeni na makocha wao, hivyo hawaruhusiwi kuendelea kuwatumia wachezaji wao ambao hawana vibali mpaka watakapo vipata vibali ingawa uongozi wa klabu ya Simba ulisema kuwa wachezaji hao wamekamilika kila kitu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger