Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma inapenda kuwashukuru Wadau wake na wananchi wote kwa
ujumla waliotembelea tovuti (www.ajira.go.tz), waliofika ofisini kuonana
na Maafisa kupata ufafanuzi wa maswala mbalimbali, waliopiga simu,
waliotuma barua pepe na kutuandikia maoni pamoja na kuuliza maswali kwa
kipindi cha mwezi Novemba, 2016.
Hoja tulizozipokea kwa njia zote zilizoainishwa hapo
juu zimejumuishwa na kutolewa majibu ya jumla kwa hoja zinazofanana kwa
faida ya wadau wote ili kuendelea kuelimisha umma kuhusu masuala ya
Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira Serikalini, majibu binafsi pia yametumwa
kwa wadau wote waliotuma hoja zao mahsusi na maoni katika njia
walizozitumia.
Swali la 1
KUHUSU UTARATIBU WA KUFUATA ILI KUREJESHWA KAZINI.
Husika na kichwa cha habari hapo juu, mimi ni mmoja
kati ya wale walio fanya usaili mwezi Septemba 2015 na kufaulu kisha
kupokea barua ya kupangiwa kituo cha kazi kwa Cheo cha Afisa maendeleo
ya jamii Daraja la Pili. Hata hivyo baada ya kukamilisha usajili ikiwa
ni pamoja na kujaza fomu ya mkataba jina langu halikuingizwa katika
orodha ya malipo (payroll) na baada ya kufuatilia nilipata taarifa kuwa
cheti changu cha (higher diploma) hakikutambuliwa katika scale za
mishahara hivyo nilipaswa kurejea chuo ili kupata cheti chenye rank
zinazo tambuliwa ndipo nirejeshwe kazini kama kawaida. Sasa nimemaliza
masomo na nina Degree ya maendeleo ya jamii, Naomba kurejeshwa kazini
kulingana na makubaliano ya awali na naomba nipewe utaratibu wa kufuata
ili kufikia hatua hiyo.
Jibu lolote litanipa Mwanga ktk harakati za kimaendeleo
ndani ya Taifa langu, natarajia busara toka kwako katika kutatua tatizo
langu,
Jibu
Hongera kwa kufaulu na kupangiwa kituo cha kazi. Pamoja
na hilo tunakupa pole kwa kutoweza kuingia katika orodha ya wanaolipwa
mishahara na Serikali kama ambavyo umeeleza. Kwa jinsi ulivyotoa maelezo
yako tunaweza kukushauri kufanya yafuatayo:-
i. Waajiri wote waliopo katika Serikali huajiri
watumishi kwa kila kipindi cha mwaka mmoja wa fedha endapo watapewa
kibali na kukifanyia kazi katika muda uliopangwa na si vinginevyo. Hivyo
si rahisi mwaka husika utakapopita bila kutekeleza ajira hizo kuweza
kuendelea nazo, vinginevyo kuwepo na ruhusa ya kufanya hivyo kutoka
katika Mamlaka husika.
ii. Kwa kuwa sasa umekwishafanikiwa kupata Shahada ya
Maendeleo ya Jamii ni vema ukiona matangazo ya kazi yanayohusiana na
kada hiyo na kukidhi vigezo uombe kazi ili uweze kuajiriwa.
iii. Kwa kuwa ajira yako ilishapitiliza mwaka bila ya
kukamilika kama ulivyoeleza si rahisi kuendelezwa kutokana na taratibu
za muda wa utekelezaji wa vibali vya ajira ambavyo huwa ni ndani ya
miezi mitatu tangu tarehe ya kuidhinishwa.
Tunakushauri kuendelea kutembelea tovuti ya
Sekretarieti ya ajira kwa ajili ya kuona matangazo ya fursa za ajira
zilizopo na maeneo ya waajiri wengine kama tulivyoshauri.
Swali la 2.
Hivi mtu ambaye alifanya usaili wa ajira za utumishi wa
uma na alikuwa anasubiri matokeo ya usaili, kabla matokeo kutoka ajira
zikasitishwa ,je mkianza kuajiri ataajiriwa kwa usahili huo ?
Jibu
Tunashukuru kwa swali lako, Ni kweli Serikali
ilisitisha kwa muda mchakato wa ajira mwezi juni kwa ajili ya kupisha
zoezi linaloendelea la watumishi hewa, Aidha endapo zoezi la kusitishwa
kwa ajira halitazidi kipindi cha miezi sita tangu usaili ulipofanyika na
endapo ulifanya usaili na ukawa umefaulu ajira zikifunguliwa unaweza
kupangiwa kituo cha kazi na kuajiriwa. Sekretarieti ya ajira ina
utaratibu wa kuhifadhi kwenye kanzidata waombaji kazi waliofaulu ambayo
hudumu kwa kipindi cha miezi sita (6) kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji
za Sekretarieti ya Ajira.
Swali la 3
Habari za kazi mheshimiwa na pole kwa majukumu ya kulijenga Taifa.
Ninaomba kuishauri serikali kupitia upya ama kutunga
sheria mpya ili kulinda maslahi ya sisi wazawa na Taifa kwa ujumla, kama
ifuatavyo;
1. Baadhi ya wawekezaji wachache si wengi, hawatoi
mikataba ya kazi kwa wafanya kazi kama sheria ya ajira inavyoelekeza na
mfanya kazi akihoji kuhusu hili ananong'onezwa kuwa hiyo ni njia ya
kupunguza watu wakati mfanya kazi anatimiza wajibu wake. Tatizo hili
lipo sana kwa baadhi si wote, wawekezaji wenye asili ya asia hasa
India.
2.Baadhi ya wawekezaji hasa wenye asili ya asia hawatoi
bima ya afya kwa wafanya kazi kama sheria mpya ya kazi inavyoelekeza
waajiri kufanya hivyo.
3.wawekezaji wengi 90% , wamegeuza nchi yetu kama
shamba la bibi, kwa kulipa mishahara duni, ya kinyonyaji bila kuzingatia
ujuzi au kiwango cha elimu alichonacho mfanya kazi. hapa sijui kama
hili tatizo ni la wizara kwa kutotoa muongozo wa malipo ya mishahara kwa
kuzingatia elimu ya mfanyakazi au la?. mimi si mwanasheria.
graduate amemaliza masters degree ,engineering analipwa
laki nne(400,000) sawa na gate man , hata ukiwa na phd , the same
payment but mfanya kazi mwenzio mwenye certificates ambaye anatoka nchi
ya muwekezaji , hana experience , anachofanya na wewe hicho hicho ,
analipwa milioni ishirini(20,000,000) Tzsh.
Serikali inakosa mapato kupitia makusanyo hafifu ya
kodi, wasomi wataendelea kukwepa kurudisha mikopo helseb kwakua laki nne
hata wao haziwatoshi na hakuna kazi lazima wafanye wasirudi geita.
nijitolee mfano mimi niliacha kazi viettel now halotel last year for
this neo- colonialism exploitation under the umbraler of investment.
my take: serikai itunge sheria kwa wawekezaji kulipa
mishahara elekezi kama wafanya kazi wa serikali wanavyo lipwa na haki
zote pia, maana watanzania wote hatuwezi kufanya kazi serikalini. Kama
wizara itafanya hivyo, naamini kabisa , hakutokuwa na wadaiwa sugu wa
bodi ya mikopo , kodi kubwa itakusanywa na nchi itasonga mbele bila
kumpigia magoti tapeli yoyote mweupe. Naamini serikali sikivu na ya
kizalendo ya hapa kazi tu, hili inaweza kulitekeleza. nakutakia kheri
katika ujenzi wa Taifa.
Kind regards;
Jibu
Tumepokea maelezo ya swali pamoja na maoni yako. Hata
hivyo tungependa kukushauri kuwa kuwa suala la mikataba ya ajira na kima
cha chini cha mishahara kwa Taasisi binafsi (Private sectors)
linashughulikiwa na Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye
Walemavu. Hivyo ni vema suala hili likaelekezwa katika ofisi hiyo ili
liweze kujibiwa ipasavyo.
Swali la 4.
AJIRA YANGU YA AFISA USHIRIKA DARAJA II-WILAYA YA KITETO
Ndugu Katibu Mkuu, Husika na kichwa cha habari hapo
juu. Mnamo Septemba mwaka jana nilifanya usaili mara mbili yaani kwa
kuandika na kwa mahojiano ya kazi ya Afisa Ushirika. Baada ya interview
zote mbili tuliambiwa tusibirie baada ya mwezi tutapata majibu kama
tumepata kazi au la.
Mnamo November 2015 yalitoka majina ya watu na vituo
vyao vya kazi lakini kwenye orodha hiyo jina langu halikuwepo. Baadae
mwezi Machi, 2016 nilipigiwa simu kutoka Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma niende kuchukua barua ya kuajiriwa. Nilienda kuichukua
barua ile na nikawa nimepata ajira kama Afisa Ushirika Daraja II katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Nilienda kuripoti kwenye kituo changu
cha kazi. Nilipofika pale nilielezwa kwamba serikali imesisitisha ajira
za watu wote waliokuwa wameajiriwa mwaka 2016 na kutakiwa kurudi
nyumbani hadi itakapowaita. afisa utumishi wa Wilaya ya Kiteto
akaniambia kwa kuwa serikali imesistisha ajira hawezi kunipokea hadi
hapo tangazo la kuwarudisha wale waliokuwa wamesimamisha litakapotoka
ili miweze kuripoti. Sasa ndugu Katibu Mkuu kwa hali yangu kama hii
nifanyeje? na je serikali ishatoa waraka wa kuwarudisha kazini watumishi
waliojiriwa mwaka huu ambao walipisha zoezi la uhakiki wa watumishi
hewa?
Naomba mwongozo wako
Jibu
Pole sana Bw. Gwawilo kwa usumbufu utakaokuwa umeupata.
Ni kweli kama ulivyoeleza Serikali ilisitisha ajira mnamo mwezi Juni,
2016 kwa ajili ya kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa, Aidha kwa
kuwa tayari ulishapewa barua kwa ajili ya kwenda kuripoti kwa mwajiri
wako huko Kiteto tunakushauri uendelee kuwasiliana na mwajiri wako
ulipopangiwa kwa ajili ya kupata mrejesho na maelekezo zaidi kwa kuwa
Sekretarieti ya Ajira ilikwisha kamilisha kazi ya kukupangiwa kituo cha
kazi.
Swali la 5.
Hongereni sana kwa kazi mnazofanya. Samahani naomba
kujua jambo moja. Mwezi mei vijana takribani 3000 waliajiriwa lakini
mwezi June ajira zao zilisitishwa. Sasa kuna taarifa kuwa ajira zile
zimefutwa na vijana wale watapaswa kuomba upya pindi ajira zitakapo
tangazwa. Je kuna ukweli juu ya jambo hili?
Jibu
Asante kwa swali na tunashukuru kwa pongezi zako. Mpaka
sasa Sekretarieti ya Ajira haijapokea taarifa ya kufutwa kwa ajira
ulizozitaja, Serikali ilisitisha ajira mpya mwezi Juni mwaka huu kwa
ajili ya kupisha zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa na mara baada ya
zoezi hilo kukamilika na kuanza mchakato wa Ajira kwa kada mbalimbali
mamlaka husika zitatoa taarifa kamili ikiwa ni pamoja na waombaji kazi
ambao walisharipoti kazini na kusitishiwa ajira zao.
Swali la 6.
Habari za kazi,kwanza nitangulize shukurani zangu za
dhati kwa utendaji kazi wenu, mimi nifanya usaili chuo cha ardhi wa
maandishi na baadae usaili wa mahojiano, baadae Mh rais akasitisha ajira
.Nilikuwa nataka kujua kama mchakato ulishamalizika ama bado tuendelee
kusubiri. Ahsante
Jibu
Tunashukuru kwa pongezi zako na tumepokea swali lako,
tunapenda kukujibu kuwa kwa sasa zoezi la uhakiki bado linaendelea na
litakapokamilika taarifa kamili itatolewa na Mamlaka zinazohusika kwa
hatua inayofuata.
Swali la 7.
Poleni sana na kazi na hongereni kwa kazi nzito
mnayoifanya kwa mafanikio makubwa! Nilipitia moja ya majibu ya hoja za
wadau za mwezi oktoba kwa swali ambalo kuna mtu aliuliza kuhusu majina
ya watu waliokua wamehifadhiwa kwenye kanzidata juu ya usalama wao
kutokana na ajira kusitishwa! Katika majibu yenu mlisema majina
yanahidhiwa kwa muda wa miezi 6 hivyo sababu ajira zilisitishwa mwez
june ikifika mwezi desemba majina hayo yataondolewa! Maoni yangu ni kuwa
kwanini watu hawa wasiendelee kuwepo kwenye kanzi data sababu ajira
zimesitishwa ivo kuwaondoa kwenye kanzidata wakati ajira bado hazipo
naona kama hawatendewi haki, ombi langu ni kuwa naomba mliangalie swala
hili kwa mara ya pili tena ili watu hao walio kwenye kanzi data
wasiondolewe mpaka ajira zitakaporuhusiwa hata yakikaa kwa mwezi mmoja
tu baada ya ajira kuruhusiwa! Nitoe shukrani zangu tena kwa mara nyingne
niwatakie utendaji mwema wa kazi naamini ombi langu kitapokelewa na
kufanyiwa kazi.
Jibu.
Asante na hongera kwa kutufuatilia kwa ukaribu. Kwa
mujibu wa Taratibu zetu za uendeshaji wa mchakato wa ajira majina ya
waombaji kazi waliofaulu lakini hawakupangiwa vituo vya kazi kwa sasa
huhifadhiwa kwenye kanzi data kwa muda usiozidi miezi sita, Aidha
ushauri wako tumeupokea na tunaufanyia kazi kadiri itakavyowezekana.
Swali la 8
Habari za kazi,pole na majukumu ya kazi, kwanza
nashukuru sana kwa kunipangia nafasi ya kazi baada ya kufaulu interview.
Nilirepot kituo cha kazi tangu mwezi wa nne(4) mwaka huu (2016)
nasikitika kabla sijapata check number tangazo la kusitisha ajira
likatoka,lakini kuna wengine ambao walipata tukio nzuri la kupata check
number kabla ya kusitishwa ajira.
Sababu napenda sana nafasi hii nimeendelee kuwa
mvumilivu nikiwa kituo cha kazi mpaka pale nitakapoingizwa kwenye
payroll. kwa wale waliokuwa wamepata check number nakusitishwa
mshahara wao kuna tamko linaloonyesha kwamba mwezi huu warudishwe tena
kwenye system natumai wataanza kupata mshahara. Naomba msaada wenu
angalau kujua na mimi nitaingizwa wakati gani kwenye payroll angalau na
mimi nianze kupata mshahara. muwe na kazi njema na siku njema pia.
Jibu
Asante kwa swali lako. Ni kweli ajira zilisitishwa ili
kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa ambalo linaendelea,
Tunachokuomba kuendelea kuwa mvumilivu hadi hapo mamlaka husika
zitakapotoa taarifa za kukamilika kwa zoezi hilo. Aidha kwa kuwa tayari
ulishapangiwa kituo cha kazi tunakushauri kuendelea kuwasiliana na
Mwajiri wako kwa ajili ya taarifa zaidi kuhusu ajira yako.
Swali la 9.
Ndugu Mheshimiwa, salam, Naomba kujua kuhusu swala
hili: Je uhakiki utakapokamilika, Sekretarieti ya ajira itatangaza tena
upya zile nafasi za kazi zilizokuwa zimetangazwa na taasisi za serikali
ule mwezi wa tano kabla ya zoezi la uhakiki kuanza? Kwakuwa ajira za
serikalini zilisitishwa kwanza kwaajili ya zoezi la uhakiki lililoanza
tangu mwezi wa sita, kwa mfano Chuo kikuu cha dar-es-salaam kilitangaza
nafasi za kazi mwezi wa tano na nyingine mwezi wa saba, je sekretarieti
ya ajira itarudia kuzitangaza nafasi zile? Au utaratibu utakuwaje?
Jibu
Tunashukuru kwa swali lako, Kwa mujibu wa kumbukumbu
zetu nafasi hizo zilizotangazwa na Chuo kikuu cha Dar es salaam
hazikutangazwa kupitia sekretarieti ya ajira hivyo ni vizuri kuwasilisha
swali lako chuo husika kwa ajili ya majibu ya kina.
Swali la 10
Habari za kazi mkuu, naomba kuuliza sisi tulioajiriwa
mwezi mei na hatukupata mshahara tutarudishwa lini kazini?maana wenzetu
waliopata walau mshahara mmoja wameitwa.Asante natumaini swali langu
litajibiwa.
Jibu
Ni kweli wapo baadhi ya waombaji kazi ambao walifanya
usaili ambapo wale ambao walifaulu walipangiwa vituo vya kazi kwa
waajiri mbalimbali kabla ya kusitishwa kwa jili ya kupisha zoezi la
uhakiki wa watumishi hewa Serikalini. Aidha kwa kuwa tayari
ulishaajiriwa kabla ya usitishwaji wa ajira hiyo tunakushauri uendelee
kuwasiliana na mwajiri wako kuhusu ajira yako kwa kuwa Sekretarieti ya
Ajira ilishamaliza kazi yake.
Swali la 11.
Habari, Hongereni kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya
katika kuhakikisha wananchi wa kitanzania wanapata ajira bila kuwepo na
upendeleo au rushwa ya aina yeyote ile. Napenda sana kuipongeza
sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma. Mwenyezi Mungu awabariki
sana. Baada ya pongezi zangu nilipenda kutaka kufahamu mwenendo wa ajira
mpaka sasa unavyoenda. Kama sijakosea mnamo tarehe 04/11/2016 Rais wetu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimu Dr. John Pombe Joseph
Magufuli akiwa Ikulu alipata nafasi ya mahojiano na waandishi wa habari
lengo likiwa kufafanua na kuuelezea umma juu ya utendaji wake wa kazi
baada ya kumaliza mwaka wake wa kwanza toka achaguliwe kuwa rais. Moja
ya maswala aliyotolea ufafanuzi ni pamoja na ajira. Mheshimiwa Rais
alisema kuwa swala la ajira kusimamishwa halipo tena na ajira
zimeendelea kutoka katika taasisi tofauti za umma ikiwemo Wizara ya
Afya.Sasa naomba kuuliza mbona hamtangazi ajira na ikiwa Rais ameshasema
ajira zinatolewa kwa sasa huku uhakiki wa watumishi hewa ukiendelea?
Ningefurahi endapo swali langu mngenijibu kwa kunipatia maelezo.
Nashukuru sana na Kazi njema.
Jibu.
Tunashukuru kwa pongezi zako. Tunaomba kukufahamisha
kuwa nafasi hizo za wizara ya Afya, hasa kwa kada za madaktari na
wauguzi mchakato wake wa ajira haupitii Sekretarieti ya Ajira kama
nafasi hizi husimamiwa na kuratibiwa moja kwa moja na wizara husika.
Aidha kwa nafasi za kazi zinazopitia sekretarieti ya Ajira zinatangazwa
baada ya kupata kibali/vibali vya Ajira toka Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi Wa Umma na Utawala Bora, kwa nafasi ambazo tumekuwa tukipata
vibali zimeendelea kutangazwa kadri zinavyojitokeza.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
27 Barabara ya Bibi Titi Mohamed,
S.L.P 63100,
Maktaba Complex,
11102 Dar es Salaam
Kijana
Issa Juma aliyeripotiwa kufariki dunia Jumapili iliyopita, muda mfupi
baada ya kubadili dini na kubatizwa katika mto mmoja kwa imani ya
Kikristo akijiunga na kanisa la Efatha kwa jina la Paulo, amezikwa kwa
imani ya Kiislam.
Uamuzi
huo umefikiwa baada ya kuwepo mvutano kati ya Kanisa la Efatha na
viongozi wa dini ya Kiislam wakitaka kijana huyo azikwe kwa imani yao,
lakini mwisho kauli ya wazazi wa marehemu ilikuwa na nguvu zaidi na
hivyo kuzikwa kwa imani ya Kiislam.
Akizungumzia
uamuzi huo, mama mdogo wa marehemu ambaye jina lake halikupatikana
alizungumza kwa niaba ya mama mzazi, Rehema Juma alithibitisha kuwa
walimzika ndugu yao Jumanne wiki hii kwa imani ya Kiislam.
Kifo
cha kijana huyo kiliibua sintofahamu ikiwa ni saa chache baada ya
kuzaliwa kwa mara pili kwa imani ya Kikristo na haikufahamika mara moja
chanzo chake kama alikuwa na ugonjwa ama ni masuala ya kiimani.
Serikali
imevipiga marufuku Klabu za ligi kuu Tanzania hususani Simba, Yanga na
Azam kuwatumia wachezaji wa kigeni mpaka watakapokamilisha taratibu zao
za uhamiaji.
Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya klabu ya
Ndanda FC kutuma malalamiko TFF kwamba Simba iliwatumia wachezaji wake
wawili wa kigeni Daniel Agyei na James Kotei kwa madai kwamba hawana
vibali vya kufanya kazi nchini.
Klabu hizo zimepewa maagizo
kwamba wachezaji na makocha wote wa kigeni ambao hawajakamilisha
taratibu za uhamiaji hawatoruhusiwa kuzihudumia klabu zao hadi hapo
watakapokamilisha taratibu hizo.
Idara ya uhamiaji kupitia kwa
afisa uhamiaji John Msumule leo alitoa tamko kwa klabu zote za Ligi Kuu
Tanzania bara kutoendelea kuwatumia wachezaji wake wa kigeni hadi
watakapotimiza masharti ya uwepo wao nchini kisheria na uhamiaji
wamezitaka klabu za Simba, Yanga na Azam FC kuhakikisha wachezaji wake
na makocha wao wa kigeni wanapata vibali vya kufanyia kazi nchini pamoja
na kuishi.
Hata hivyo kwa upande wa Yanga wao wachezaji wao
wana vibali vya kazi na vya kuishi nchini isipokuwa makocha wao ndio
wana vibali vya kazi pekee.
Kwa upande wa watani zao wa jadi
Simba wao hawajatimiza vigezo hivyo kwa wachezaji wao wa kigeni na
makocha wao, hivyo hawaruhusiwi kuendelea kuwatumia wachezaji wao ambao
hawana vibali mpaka watakapo vipata vibali ingawa uongozi wa klabu ya
Simba ulisema kuwa wachezaji hao wamekamilika kila kitu.
The International Summer School (ISS)
at the University of Oslo, invites applications for admission into
either Self-financed/sponsored or Scholarships to vie for higher
education training opportunities tenable in the Kingdom of Norway.
The detailed information about
Scholarships, the application process and the program itself can be
found on the University’s website namely:- www.uio.no/summerschool .
Kindly note that, the deadline for
scholarship application is 1st February, 2017 and that for qualified
self-financed/sponsored is 1st March, 2017.
You are strongly advised to read thoroughly and understand the details on how and where to apply.