Sunday, 18 December 2016

CCM washinda Meya, Naibu Meya Kigamboni

UCHAGUZI wa kumpata Meya wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, umefanyika na hatimaye Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Maabadi Hoja amechaguliwa kuwa Meya wa kwanza.
Uchaguzi huo ulifanyika jana kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando, ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi, alisema mgombea huyo wa CCM ndiye aliyeshinda.
Washiriki wengine walitoka vyama vya CCM, Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Mhando alisema Hoja alipata kura tisa dhidi ya Celestine Maufi (CUF) aliyepata kura tano na kura moja iliharibika.
Pia, Mhando alisema katika uchaguzi huo, Amini Sambo ambaye ni Diwani wa Kata ya Kibada, pia kutoka CCM, alishinda nafasi ya Naibu Meya, akipata kura 10 dhidi ya Ernest Mafimbo wa CUF, aliyepata kura tano. “Tunashukuru uchaguzi umefanyika vizuri Kigamboni, sasa tumepata Meya na Naibu Meya,” alisema Mhando.
Uchaguzi wa Meya na Naibu wake kwa upande wa Kigamboni, umefanywa baada ya Wilaya ya Temeke kugawanywa na kuwa wilaya mbili za Temeke na Kigamboni.
Mhando alieleza kuwa uchaguzi huo ambao ni wa mara ya kwanza kwa halmashauri hiyo, ulifanyika kwa amani bila kuwapo na malalamiko.
Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndungulile, baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, alisema uchaguzi ulifanyika bila tatizo lolote na kwamba baada ya uchaguzi kuisha, kinachofuata ni kazi.
Alisema kwa muda mrefu mambo mengi katika halmashauri hiyo, yalisimama kwa kukosa Baraza la Madiwani. Akizungumza na gazeti hili, meya huyo, Hoja alisema anajipanga kuiweka Halmashauri hiyo mpya kimji. Aliahidi kuanza na kusimamia mipangomiji na miundombinu.
“Manispaa yetu ni mpya na haijapangwa, tunataka kuiweka kimji zaidi na tutaanza na mipangomiji kwani kuna ujenzi holela na pia tutasimamia miundombinu,” alisema Hoja.
Hii si mara ya kwanza kuchaguliwa kushika nafasi hiyo. Alichaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Temeke mwaka 2010 baada ya kushinda udiwani wa kata hiyo kwa mara ya kwanza.
Baada ya kufanyika uchaguzi mkuu mwaka jana, Hoja alipata tena udiwani katika kata hiyo, lakini aliposhindania nafasi ya meya, hakushinda nafasi hiyo. Lakini, baada ya Temeke kugawanywa kuwa wilaya mbili za Temeke na Kigamboni, Hoja amegombea tena na kushinda.
Kwa upande wake, akihojiwa, Naibu Meya mpya, Sambo, anasema hii ni mara ya kwanza kushika nafasi ya udiwani. Alichaguliwa mwaka jana.
Sambo alisema anaishukuru Serikali kwa kusogeza huduma karibu, kwa kuifanya Kigamboni kujitegemea kama halmashauri.
Alisema yeye na viongozi wenzake watashirikiana na serikali, kuifanya halmashauri hiyo mpya kuwa ya mfano. Halmashauri ya Kigamboni inaundwa na kata tisa za Pembamnazi, Kimbiji, Somangila, Kisarawe, Kibada, Vijibweni, Kigamboni, Mjimwema na Tungi.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DEC TAREHE 18.12.2016

Share:

Saturday, 17 December 2016

Tangaza Biashara Yako Au Bidhaa Yako Kwenye Mtandao huu Kwa BEI NZURI Kabisa


Tunakaribisha  matangazo  ya  aina  zote.Bei  zetu  ni  nzuri  sana  na  kamwe  hutajuta  kutangaza  biashara  yako  kupitia  mtandao  huu.
Kwa Siku tunafunga na Pageviews zaidi  ya  laki tatu kama graph  inavyoonyesha  hapo  chini
Share:

Dr Mwele Malechela(Aliyetumbuliwa) : Safari itasonga kwa msaada wa Mungu

Share:

Mahakama yatupa pingamizi la serikali katika kesi ya mbunge Godbless Lema.

Share:

Baada ya Dkt. Mwele Malecela kutumbuliwa, Prof. Yunus Mgaya ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu NIMR

Share:

Waziri Simbachawene atoa agizo jipya kwa machinga

Share:

Waziri Mkuu Amsimamisha Kazi Mwekahazina Wa Wilaya Ya Bahi,Aagiza arudishwe Longido kujibu tuhuma zinazomkabili

Share:

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)


Taarifa kutoka IKULU inasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 16 Desemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mwele Malecela.
Share:

Waziri Mkuu: Waliouza Kiwanja Cha Shule Wachukuliwe Hatua

Share:

Taarifa ya Bodi ya Mikopo kwa wadaiwa sugu kuhusu mwisho wa kulipa kwa hiari

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imeongeza muda kwa wadaiwa sugu kulipa madeni yao hadi Desemba 30, 2016.
Share:

Wafanyabiashara Morogoro watelekeza masoko yao na kuhamia katikati ya mji.





Siku chache baada ya Rais Dokta John Pombe Magufuli kuwataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zote nchini kuacha kuwabughudhi wamachinga na badala yake wawatafutie maeneo maalumu ya kufanyia biashara zao hali imekuwa tofauti kwa Manispaa ya Morogoro baada ya wafanyabiashara mbalimbali kuyatelekeza masoko na kupeleka bidhaa zao katikati ya mji huku wafanyabiashara wa madu
Share:

Sungusungu wavamia kijiji na kutembeza viboko.


Kwa hali isiyo ya kawaida sungusungu zaidi ya mia nane wamevamia kijiji cha Welezo katika kata ya Tinde wilayani Shinyanga na kutembeza kichapo kwa wakazi wa kijiji hicho hali ambayo imezua taharuki na kusababisha kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo kuingilia kati na kumsimamisha kazi mwenyekiti wa kijiji hicho kwa kosa la kufanya uzembe uliosababisha vurugu.
Share:

Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Disemba 17 2016

Share:

Friday, 16 December 2016

Kafulila ahama NCCR, ahamia Chadema


Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila leo ametangaza kukihama chama hicho na kusema kuwa atajiunga na Chama cha Demokrasia na Manendeleo (CHADEMA).
Share:

Ndalichako Asitisha Ajira za Walimu Wa Masomo ya Sanaa

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ametoa masharti mapya ya ajira za ualimu nchini, huku akisema Serikali haitaajiri walimu wa masomo ya sanaa (arts) kwa kuwa wapo wa kutosha.

Akizungumza mjini Dodoma jana wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Profesa Ndalichako, alisema Serikali kwa sasa haiwezi kuajiri walimu wa masomo hayo kwa kuwa inataka kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ambao idadi yao ni ndogo.

“Pamoja na uamuzi huo mpya, ajira za walimu wapya wa masomo ya sayansi nazo zimebadilika kwani wale wote waliohitimu ualimu wa sayansi na hisabati, wanatakiwa watume vyeti vyao kabla ya kupangiwa kituo cha kazi.

“Kuhusu wale walimu wa ‘arts’, kule tuna walimu wa ziada ambao tutajaribu kuwapanga kutokana na shule, kwani wengi walikuwa wamepangwa shule moja. Kwahiyo, tutaangalia utaratibu wa kuwapanga kulingana na mahitaji,’’ alisema Profesa Ndalichako.

Akizungumzia suala la ubora wa elimu nchini, Profesa Ndalichako aliwataka walimu wakuu hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu kwa kuwa wao ndio wanaowaandaa wanafunzi kabla hawajaenda vyuoni.

“Vilevile pelekeni takwimu sahihi za wanafunzi waliopo katika shule zenu kuisaidia Serikali katika kupanga bajeti ili iweze kutoa fedha sahihi.

“Hapa kuna kimbembe, yaani wakati mwingine huwa najifanya nimepoteza takwimu ya shule fulani, nikiziomba na kutumiwa, zinakuwa ni tofauti na zile za mwanzo.

“Hili nawaomba mkalisimamie ili iwe rahisi kwetu kupanga bajeti yenye tija,’’ alisema.

Kuhusu ujenzi wa maabara katika shule za sekondari, waziri huyo alisema kwamba kutokana na nyingi kukamilika, Serikali itatoa vifaa vya maabara kuanzia Januari mwakani baada ya kuwa vimeingia nchini kutoka vilikoagizwa.

Awali, akisoma risala ya walimu hao, Rais wa TAHOSSA, Bonus Nyimbo, aliiomba Serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi shuleni kwa kuwa zimekuwa zikichangia kushuka kwa ufaulu kwa baadhi ya wanafunzi.

“Ili kuboresha elimu, tunaiomba Serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi kwani simu nyingi tunazozikamata tunakuta mule hakuna taaluma,’’ alisema Nyimbo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Molel, ambaye pia kampuni yake ilipewa tuzo ya heshima katika kuendeleza elimu nchini, alisema ni jukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake ili kuiendeleza elimu ya Tanzania.

“Kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu, wazazi, walezi na walimu, waambieni wanafunzi wasiwe na ‘expectation’ (matarajio) makubwa kwani wanapokuwa na matarajio hayo, wakienda vyuo vikuu wanakuwa wasumbufu,” alisema.

Wakati hayo yakiendelea, juzi taarifa ilitolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi, ikisema kwamba, walimu wahitimu wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu shahada na astashahada mwaka 2015, wanatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti vya elimu ya sekondari vya kidato cha nne na sita na taaluma ya ualimu kwa uhakiki.

Pamoja na hayo, hivi karibuni Serikali ilitangaza kusitisha ajira zote nchini ili kukabiliana na wimbi la watumishi hewa.

Sambamba na uamuzi huo, nyongeza za mishahara kwa watumishi wa Serikali nazo zilisimamishwa ili kukabiliana na watumishi hao hewa ambao walikuwa wakiingizia hasara Serikali.
Share:

Mwanzilishi wa JamiiForums afikishwa mahakamani,Ashindwa Kutimiza Masharti ya Dhamana

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger