Mbunge
wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha
NCCR-Mageuzi, David Kafulila leo ametangaza kukihama chama hicho na
kusema kuwa atajiunga na Chama cha Demokrasia na Manendeleo (CHADEMA).
Friday, 16 December 2016
Ndalichako Asitisha Ajira za Walimu Wa Masomo ya Sanaa
WAZIRI
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako,
ametoa masharti mapya ya ajira za ualimu nchini, huku akisema Serikali
haitaajiri walimu wa masomo ya sanaa (arts) kwa kuwa wapo wa kutosha.
Akizungumza
mjini Dodoma jana wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakuu wa
Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Profesa Ndalichako, alisema
Serikali kwa sasa haiwezi kuajiri walimu wa masomo hayo kwa kuwa inataka
kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ambao idadi yao ni
ndogo.
“Pamoja
na uamuzi huo mpya, ajira za walimu wapya wa masomo ya sayansi nazo
zimebadilika kwani wale wote waliohitimu ualimu wa sayansi na hisabati,
wanatakiwa watume vyeti vyao kabla ya kupangiwa kituo cha kazi.
“Kuhusu
wale walimu wa ‘arts’, kule tuna walimu wa ziada ambao tutajaribu
kuwapanga kutokana na shule, kwani wengi walikuwa wamepangwa shule moja.
Kwahiyo, tutaangalia utaratibu wa kuwapanga kulingana na mahitaji,’’ alisema Profesa Ndalichako.
Akizungumzia
suala la ubora wa elimu nchini, Profesa Ndalichako aliwataka walimu
wakuu hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu kwa kuwa wao ndio
wanaowaandaa wanafunzi kabla hawajaenda vyuoni.
“Vilevile
pelekeni takwimu sahihi za wanafunzi waliopo katika shule zenu
kuisaidia Serikali katika kupanga bajeti ili iweze kutoa fedha sahihi.
“Hapa
kuna kimbembe, yaani wakati mwingine huwa najifanya nimepoteza takwimu
ya shule fulani, nikiziomba na kutumiwa, zinakuwa ni tofauti na zile za
mwanzo.
“Hili nawaomba mkalisimamie ili iwe rahisi kwetu kupanga bajeti yenye tija,’’ alisema.
Kuhusu
ujenzi wa maabara katika shule za sekondari, waziri huyo alisema kwamba
kutokana na nyingi kukamilika, Serikali itatoa vifaa vya maabara
kuanzia Januari mwakani baada ya kuwa vimeingia nchini kutoka
vilikoagizwa.
Awali,
akisoma risala ya walimu hao, Rais wa TAHOSSA, Bonus Nyimbo, aliiomba
Serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi
shuleni kwa kuwa zimekuwa zikichangia kushuka kwa ufaulu kwa baadhi ya
wanafunzi.
“Ili
kuboresha elimu, tunaiomba Serikali itoe waraka wa kupiga marufuku
matumizi ya simu kwa wanafunzi kwani simu nyingi tunazozikamata tunakuta
mule hakuna taaluma,’’ alisema Nyimbo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Molel,
ambaye pia kampuni yake ilipewa tuzo ya heshima katika kuendeleza elimu
nchini, alisema ni jukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake ili
kuiendeleza elimu ya Tanzania.
“Kila
mmoja anapaswa kutimiza wajibu, wazazi, walezi na walimu, waambieni
wanafunzi wasiwe na ‘expectation’ (matarajio) makubwa kwani wanapokuwa
na matarajio hayo, wakienda vyuo vikuu wanakuwa wasumbufu,” alisema.
Wakati
hayo yakiendelea, juzi taarifa ilitolewa jijini Dar es Salaam na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna
Tarishi, ikisema kwamba, walimu wahitimu wa masomo ya sayansi na
hisabati waliohitimu shahada na astashahada mwaka 2015, wanatakiwa
kuwasilisha nakala za vyeti vya elimu ya sekondari vya kidato cha nne na
sita na taaluma ya ualimu kwa uhakiki.
Pamoja na hayo, hivi karibuni Serikali ilitangaza kusitisha ajira zote nchini ili kukabiliana na wimbi la watumishi hewa.
Sambamba
na uamuzi huo, nyongeza za mishahara kwa watumishi wa Serikali nazo
zilisimamishwa ili kukabiliana na watumishi hao hewa ambao walikuwa
wakiingizia hasara Serikali.
Nape awaaomba msamaha wapinzani.
Alikuwa
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
amewaomba radhi viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini kwa
lolote ambalo aliwakwaza wakati akitekeleza majukumu yake katika nafasi
hiyo.
Nape
amewaangukia wapinzani pamoja na makundi mengine ya watanzania ikiwemo
viongozi wenzake ndani ya chama leo wakati akikabidhi rasmi ofisi kwa
kiongozi mpya anayechukua nafasi hiyo, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo Dar es Salaam, Humphrey Polepole katika ofisi ndogo za makao
makuu ya chama hicho, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
"Nawaomba
msamaha viongozi wenzangu, wanachama, waandishi na hata wapinzani pale
ambapo nimewaumiza katika kufanya kazi yangu, samahani sana. Nategemea
ushirikiano niliopatiwa mimi na wanahabari utaendelea kwa ndugu yangu
Humphrey Polepole, ni mtu mwenye weledi mpana" amesema Nape
Nape
pia amekiri kuwa chama hicho kimemsaidia zaidi kwenye maisha yake
kuliko yeye alivyokisaidia wakati akiitumikia nafasi hiyo.
"Nakiri
mbele yenu kuwa chama kimenisaidia zaidi kuliko mimi nilivyokisaidia
Chama, nashukuru Mungu kuwa nimemaliza kazi hii salama, nilipata wosia
wa Mzee Kinana kuwa nishukuru nikimaliza salama"
Walimu wapya wa Sayansi, Hisabati wabanwa
WALIMU wa Sayansi watakaoajiriwa na serikali, watalazimika kutuma vyeti vyao kabla ya kupangiwa kituo cha kazi.
Hiyo ni sehemu ya mabadiliko katika utaratibu wa ajira wenye lengo la
kuimarisha ufundishaji kwa waliohitimu Ualimu wa Sayansi na Hisabati.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa).
Pamoja na kuzungumzia mabadiliko hayo katika mfumo wa ajira, alisema ni
nia ya serikali kuimarisha elimu ya sekondari, ikiwa ni pamoja na
kuimarisha ufundishaji wa masomo hayo ya Sayansi.
Aidha, Profesa Ndalichako aliwataka Walimu wakuu nchini, kusimamia ubora wa elimu kutokana na wao kuwa karibu na wanafunzi.
Akifafanua, alisema walimu wakuu wanawajibu wa kuwa wasimamizi na
wakaguzi wa kwanza wa wanafunzi ili kuiboresha elimu ya Tanzania,
wakizingatia kuwa elimu ya Sekondari ni kiungo muhimu katika kuendeleza
elimu nchini.
Vile vile, aliwataka wakuu hao kupeleka takwimu sahihi za wanafunzi
waliopo katika shule zao ili kuisaidia serikali katika kupanga bajeti
ili iweze kutoa fedha sahihi.
“Hapa kuna kimbembe wakati mwingine huwa najifanyisha nimepoteza takwimu
ya shule fulani nikitumiwa inakuwa tofauti na ile ya mwanzo, niwaombe
walimu mkalisimamie hili ili iwe rahisi kwetu kupanga bajeti yenye
tija,’’ alisema.
Prof. Ndalichako alisema kutokana na maabara nyingi kukamilika, serikali
itatoa vifaa vya maabara kuanzia Januari mwaka mwakani. Katika mkutano
huo, Waziri pia aliwaomba Makatibu Tawala na Wakurugenzi, kuwalinda
walimu wanaofuata kanuni, taratibu na sheria katika utendaji kazi wao na
kudhibiti wanasiasa kuingilia masuala ya elimu.
Pia aliwataka walimu wakuu kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka pamoja na kufanya usafi katika shule zao.
Akisoma risala, Rais wa Tahossa, Bonus Nyimbo aliiomba serikali itoe
waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi shuleni, kwani
imekuwa ikichangia kushusha ufaulu wa baadhi ya wanafunzi.
Nyimbo ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwenge ya mkoani
Singida, aliiomba serikali iajiri pia walinzi, watumishi na madereva ili
waweze kufanya kazi kwa ufasaha. Alisema changamoto nyingine,
wanayokabiliwa nayo ni baadhi ya wanachama kutoelewa vizuri katiba
pamoja na kutokulipa ada kwa wakati.
“Kwa upande wake Mkurugenzi wa Global Education Link, AbdulMalik Molel
ambaye kampuni yake ilipewa tuzo ya heshima katika kuendeleza elimu
nchini”, alisema ni jukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake ili
kuiendeleza elimu ya Tanzania.
MAJALIWA CAHARUKA
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa miezi sita ya kujitathimini
mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayofanya kazi zake wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha, kama yanafanya kazi kwa misingi ya sheria na
maadili.
Baadaye, yatahakikiwa na kama yatabainika yanachochea migogoro, yatafutwa.
Pia, Majaliwa amezicharukia NGOs nyingine zinazoitangaza vibaya Tanzania
kimataifa kwa kupiga picha za kudhalilisha watoto wakiwa wanatembea
kwenye mawe huku wamevaa kandambili kubwa, kuonesha nchi ni masikini.
Ametaka NGOs hizo kuondoka nchini, la sivyo serikali itazishughulikia.
“Hizi NGOs zingine si muondoke, nendeni kwingine mkafanye kazi. Halafu
nyie mnaotuma picha za kudhalilisha watoto wakiwa wamevaa kandambili
kubwa, kudai nchi za nje eti Tanzania ni masikini, tutawashughulikia,”
alisema Majaliwa alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ngorongoro jana.
Aidha alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
atakuja wilayani hapo kukagua kazi walizozifanya, wanazozifanya na
miradi wanaosaidia jamii.
Majaliwa aliwaambia watumishi hao wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wakurugenzi wa mashirika yasiyo ya
serikali, yanayofanya shughuli zake wilayani hapo, kuwa serikali haitaki
mashirika chochezi wa migogoro na itayafuta.
Alisema serikali haitasita kuyafuta mashirika yanayofanya kazi wilayani
humo, ambayo yapo kwa nia ya uchochezi na kuacha kufanya kazi katika
malengo yaliyokusudiwa.
Waziri Mkuu alisema wilaya hiyo, ina mashirika yasiyo ya serikali 30 ambayo yamesajiliwa, lakini yanayofanya kazi ni 19 tu.
Alisisitiza kuwa haiwezekani serikali isajili mashirika hayo, lakini utendaji kazi wake uwe hafifu.
Alisema ukifuatilia, mashirika hayo utagundua kuwa yanapokea fedha
nyingi, lakini hakuna cha maana wanachokifanya kwa wananchi. Alisema
serikali ina taarifa ya NGOs hizo zinazopewa fedha na wafadhili.
“Najua taarifa zenu mnapokea kiasi gani cha fedha na mnazifanyia nini,
lakini namleta Mkaguzi wa serikali ili akague mnatumiaje fedha zenu,
nawapa miezi sita tu halafu ukaguzi utaanza, maana kuna mashirika mengi
lakini kazi mnazofanya hazionekani,” alisema Majaliwa.
Alisema baadhi ya mashirika, yana akaunti nchi jirani ya Kenya na
mengine kama PWC anapewa Sh bilioni 2.5 kwa mwaka na shirika la UCRT
linapokea Sh bilioni 1.5 kwa mwaka, lakini hajui yanafanya nini.
“Nina taarifa zenu mnapata hela nyingi, lakini mnahudumia vipi jamii
hakuna, sasa ngojeni ukaguzi ufanyike halafu nitachukua maamuzi maana
kila siku Loliondo kuna nini hapa mnasajiliwa halafu hakuna cha maana,”
alisema.
“Kuna nini Loliondo, kwani kila mara Loliondo nina taarifa za kila NGOs
zinazofanya kazi hapa, najua mnachokifanya, sasa nawaambia serikali
haitawafumbia macho kuona hiki ninachokifanya hapa na ikigundulika
mnafanya kinyume na matakwa ya usajili tutazifuta”.
Alisema serikali itazifuta NGOs zote, ambazo zitabainika ni kiini cha
migogoro Loliondo. Alitoa hadhari kwa kampuni zinazofanya kazi zake bila
usajili, kuwa zikigundulika, zitachukuliwa hatua.
Aliwageukia watumishi wa umma na kuwatahadharisha wale wanaotoa taarifa
za migogoro ya ndani kwa wahusika wa NGOs na kisha kuzituma nje ya nchi
kwenye mitandao ya kijamii na barua pepe.
Alisema kuwa nao watashugulikiwa, kwa kuwa wanapaswa kuwa majibu ya migogoro na si wasambazaji wa habari mbaya za nchi.
Alisisitiza watekeleze kikamilifu kauli ya ‘Hapa Kazi Tu’ ; na si
kutumia NGOs kwa ajili ya kudai kuwasaidia wananchi, huku wakijua kuwa
wananchi hawanufaiki na fedha hizo wanazopewa na wafadhili Awali
akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Wilaya hiyo, Majaliwa alitoa
tahadhari kwa madiwani kuacha kushirikiana na watu wa Uhasibu wanaotoa
hela kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema baadhi ya madiwani, wanakwamisha miradi ya maendeleo kwa kula fedha kwa sababu ya ukaribu walionao.
Akizungumzia nidhamu ya fedha, Majaliwa alisisitiza kila mtumishi lazima
afanye kazi kwa bidii, ikiwemo kutoa huduma bila kuwabagua wananchi kwa
itikadi zao za vyama.
MWANAFUNZI ALIYEFUKUZWA CHUO CHA UDOM KWA KUONGOZA MGOMO ARUDISHWA CHUO AMALIZIE MASOMO
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma imetengua
uamuzi wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ya kumfukuza mwanachuo
Phillip Mwakibinga na kuamuru arudishwe ili kumalizia masomo yake.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, John Chaba
kwa niaba ya Jaji Awadhi Mohamed aliyekuwa akisikiliza shauri hilo.
Mwakibinga alikuwa akisoma Shahada ya Kiswahili mwaka wa tatu wakati
akisimamishwa na alikuwa Waziri Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii.
Katika uamuzi huo, mahakama ilisema mlalamikaji hakupewa nafasi ya
kusikilizwa na hivyo kukiuka haki ya asili ya mlalamikaji. Pia
mlalamikaji hakupewa haki ya kusikilizwa na hakuandikiwa mashtaka rasmi.
“Baraza liliegemea upande moja bila kumhoji wala nafasi ya kusikilizwa na kujitetea,” alisema.
Mwakibinga alifukuzwa Udom Januari 14, mwaka jana, kwa madai ya kuongoza
mgomo ambapo siku hiyo baraza la chuo lilikaa na kumfukuza bila kupewa
nafasi ya kusikilizwa.
Alifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kutaka mahakama kutengua
uamuzi huo. Kwa mujibu wa wakili wa Mwakibinga, Elias Machibya alisema
awali waliomba ruhusa ya kufungua kesi na wakapewa Februari 5, mwaka
jana wakiomba kutengua maombi ya baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma.
“Tulipata kibali cha kufungua kuomba kutengua maamuzi ya Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kumfukuza,” alisema.
Alizitaja sababu kuu tatu za kupinga mwanafunzi huyo kufukuzwa chuo kuwa
ni pamoja na kutopewa nafasi ya kusikilizwa, hakuna hatua za nidhamu
zilizochukuliwa, walimfukuza wakidai aliwahi kuhusika na migomo ya
nyuma.
Alidai barua ya kumfukuza ilisainiwa na Profesa Shaban Mlacha.
Januari 14, mwaka jana uongozi wa Udom ulimfukuza Mwakibinga ambaye
wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi, Kitivo cha
Sayansi ya Elimu ya Jamii, na kupewa barua ya kusimamishwa kutokana na
kosa la kuhamasisha mgomo.
Uongozi huo ulisema Mwakibinga amefukuzwa kabisa kwa kuwa alishawahi
kujihusisha na mgomo wa mwaka 2010/2011 akafukuzwa lakini akakata rufaa
na kuomba msamaha kwenye Kamati nidhamu.
“Baada ya kukata rufaa Kamati ikamuonea huruma ikamrudisha kabla ya
kurudi alitakiwa aje na kiapo kutoka kwa mwanasheria kwamba
hatajihusisha na mgomo tena lakini akarudia tena kosa hilo."
Mwakibinga amesema amefurahia uamuzi huo kwani ndio sababu ya msingi ya
kufungua kesi na mahakama imetenda haki. Alisema anasubiri barua ya
hukumu ambayo itatoka kesho ndipo taratibu zake za kurudi chuo
zitakapoanza.
Thursday, 15 December 2016
HAYA HAPA MAJINA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA JKT AWAMU YA PILI 2016
BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI KUANGALIA MAJINA JA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI 2016














