Saturday, 19 November 2016
Friday, 18 November 2016
Thursday, 17 November 2016
JKT: TANGAZO MUHIMU KWA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI 2016

TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linapenda kuutaarifu umma juu ya utapeli
unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu wanaojifanya wanauwezo wa
kuwaingiza vijana wa kitanzania kwenye mafunzo ya JKT kwa lengo la
kupatiwa malipo.Utapeli huo unafanyika kwa njia ya simu za mkononi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno tofauti tofauti.
Jeshi la Kujenga Taifa linasisitiza kuwa ujumbe huo siyo sahihi na wananchi wanatakiwa kujiepusha na utapeli huo wenye lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Taarifa za mchakato wa uchukuaji wa vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT utolewa na Makao Makuu ya JKT kwa mfumo ulio rasmi wa mawasiliano ikiwemo luninga, radio, magazeti na tovuti ya JKT.
Aidha, JKT kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, inafuatilia kujua ni mtu gani au kikundi kipi kinahusika na utapeli huo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
Tarehe 17 Oktoba 2016
RAIS MAGUFULI ATIA SAINI SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, inawataarifu kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini Sheria ya
Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge la 11 la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 5 Mjini Dodoma.
Rais Magufuli amesaini Sheria hiyo tarehe 16 Novemba, 2016.
Dkt. Magufuli amewapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwa Sheria hiyo.
"Naamini kuwa Sheria hii itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa" amesema Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
17 Novemba, 2016
SUA:The 32nd Graduation, Prize Awarding Ceremonies and Convocation Meeting.
Graduands and Members of the General Public are hereby informed that the 32nd SUA Graduation Ceremony will be held on Friday 25th November, 2016 at Solomon Mahlangu Campus (SMC), “Nelson Mandela Freedom Square”, Mazimbu in Morogoro, starting at 11:00 am. During the day, the Chancellor of SUA will confer degree and non-degree awards to the 2015/2016 academic year graduands. Read more >>
Wednesday, 16 November 2016
Breaking News:HAYA HAPA MAJINA YA WADAIWA SUGU BODI YA MIKOPO TANZANIA
Siku zote MASWAYETU BLOG ni kuhakikisha wewe hapo mdau wetu unapata kitu roho inapenda,Yafuatayo ni majina(list ya wadaiwa sugu bodi ya mikopo ) toka mwaka 1994 to 2014.













































