Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua
kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa majina ya wanafunzi
waliochaguliwa na joining instructions za kujiunga na vyuo vikuu
2016/2017-SECOND ROUND
CHUO KIKUU TUMA-MBEYA (2ND ROUND) >>BONYEZA HAPA<<
CHUO CHA MWL.NYERERE DAR & ZANZBAR CAMPUS (2ND ROUND)>>BONYEZA HAPA<<
Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa
bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi
kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14.
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Yahya Kamuhanda (49) mkazi wa kijiji
hicho. Mtui aliwataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo
Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hassan
Nasibu, wote wakazi wa Kijiji cha Uvinza.
Alisema askari walipata
taarifa kutoka kwa raia wema kwamba Kamuhanda anajiandaa kufanya uhalifu hivyo waliweka mtego eneo la Uvinza
Madukani alikokwenda kununua mahitaji.
Alidai kuwa alipotambua anafuatiliwa alitupa bomu ndipo polisi walimpiga risasi mguuni na wananchi
walimvamia na kumshambulia kabla ya askari kutumia nguvu kumwokoa
asiuawe kwa kipigo.
Mtui alisema mtuhumiwa alipohojiwa alisema
alificha bunduki kijijini kwao Lukole wilayani Ngara mkoani Kagera,
ambako askari walikamata SMG yenye namba 78GA5062 ikiwa imefukiwa
ardhini.
Pia, walikamata magazini saba, moja ilikuwa na risasi 40, nne
(risasi 30 kila moja) na mbili (risasi 20 kila moja) na risasi 75
zilikuwa kwenye mfuko wa sandarusi. Pingu moja na funguo zake, maski
tisa na laini 20 za mtandao wa Halotel ambazo hazijasajiliwa.
Mtui
alisema mtuhumiwa huyo alifariki dunia juzi akipatiwa matibabu kwenye
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni). Alisema majeruhi wote
watano walipata matibabu hospitalini hapo na waliruhusiwa kurudi
nyumbani.
Ilikuwa
kama mchezo wa kuigiza kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada
ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Emmanuel
Mkumbo kufikishwa ili apandishwe kizimbani kujibu mashtaka sita,
likiwamo la kutishia kuua.
Tukio
zima la kumpeleka mahakamani, kumpandisha kizimbani na kumsomea
mashtaka kwa muda wa dakika 30 hivi lilitawaliwa na vituko. Kwanza, ni
jaribio la kuwaficha wanahabari.
Kabla
ya kufikishwa mahakamani, Polisi mkoani Morogoro iliwaarifu wanahabari
kuwa ingetoa taarifa kuhusu mkurugenzi huyo lakini saa 4:30 asubuhi
wakati Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro,
Ulrich Matei akijiandaa kuzungumza nao, alipigiwa simu akatoka nje ya
ukumbi na aliporejea alisema hawezi kutoa taarifa tena na akaondoka.
Waandishi
walipofika mahakamani saa 5:00 asubuhi walikuta Kamanda Matei akishuka
kwenye gari na alipanda tena akasogea kando kuzungumza na baadhi ya
askari wake.
Pili,
baada ya hakimu kumaliza kusikiliza kesi hiyo, Mkumbo hakurudishwa
mahabusu mahakamani hapo kama ilivyo ada ili kusubiri utaratibu mwingine
badala yake mshtakiwa huyo alihamishiwa chumba cha hakimu ambacho
hakikuwa na kesi inayoendelea.
Humo
ndugu zake walimpelekea koti kubwa jeusi na kofia aina ya pama, hivyo
alitoka akiwa tofauti na alivyoingia akiwa na fulana yenye rangi nyeupe,
bluu na nyeusi. Baada ya kuvaa alitoka akiwa amezingirwa na polisi,
huku ndugu wakiwazuia wanahabari kumpiga picha.
Mashtaka dhidi yake
Mkumbo
ambaye ni mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam alipandishwa kizimbani
kujibu mashtaka sita, la kwanza likiwa la kutishia kuua kwa bastola na
la pili ni la usalama barabarani lenye makosa matano.
Alisomewa
mashtaka hayo na mawakili wa Serikali Sunday Hyera na Edgar Bantulaki.
Katika shtaka la kwanza, mbele ya hakimu Agripina Kimaze anadaiwa Oktoba
15, saa 10:30 jioni alitenda kosa la kutishia kuua eneo la Mkambarani,
Manispaa ya Morogoro.
Anadaiwa
katika shtaka hilo la jinai namba 226 la mwaka 2016, alitishia kumuua
kwa bastola askari namba 5057, Koplo Tuti Ndaga wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Mkoa wa Morogoro, kinyume na kifungu namba 89 (1),(2),(a) cha
Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba16.
Katika
shtaka la pili la ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani lenye
makosa matano, ilidaiwa kuwa; kwanza, siku na muda huo eneo la Mbuyuni
Mkambalani, mshtakiwa alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Prado lenye
rangi ya kijivu bila kuwa na leseni.
Pili,
ilidaiwa alikuwa akiendesha gari hilo ambalo halikuwa na bima; tatu,
alikutwa akiendesha kwa mwendo kasi; na nne, alikataa kupeleka gari
Kituo cha Polisi cha Kingoluwira kama alivyoamriwa na askari, WP namba
5392 Sajenti Anna.
Ilidaiwa
katika shtaka la tano kwamba, wakati akiendesha alisimamisha gari
katikati ya barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam kwa uzembe, bila
uangalifu wala kuzingatia watumiaji wengine wa barabara. Mkurugenzi huyo
alikana mashtaka yote yanayomkabili.
Hakimu
Kimaze alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kwamba awe na mdhamini
mmoja kwa kila shtaka, yaani shtaka la jinai na la usalama barabarani
lenye makosa matano, wote wawe wakazi wa Morogoro na mmoja akitakiwa
kuweka dhamana ya Sh500,000 kwa kosa la kwanza na Sh1 milioni kwa kosa
la pili.
Mshtakiwa
alikidhi masharti ya dhamana na kuachiwa huru, huku gari likiendelea
kushikiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro.
Hakimu
Kimaze aliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 31, usikilizwaji wa awali
utakapoanza baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi umekamilika.
Watu
10 wamefariki dunia na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni
ya Barcelona walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kwenda
mkoani Lindi kupata ajali eneo na Miteja mkoani Lindi.
Taarifa
iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga imesema
kuwa chanzo cha ajali hiyo kimetokana na tairi ya gari ya upande wa
kushoto kupasuka na kutokana na mwendo wa kasi wa basi hilo, dereva
alipoteza uelekeo ndipo likapinduka.
Pia
Kamanda Mzinga amesema kuwa wamechunguza na kugundua kua licha ya kuwa
basi hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 48, wakati basi hilo
linapata ajali kulikuwa na abiria 54 kitu ambacho ni kosa kisheria.
Aidha,
Kamanda Mzinga amesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi kuweza
kubaini alipo dereva ili kuweza kufahamu ni kipi hasa kilichotokea. Hadi
sasa wanamshikilia kondakta wa basi hilo lakini bado hajaweza kuelezea
tukio halisi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Devis Deogratius akiongea na mawakala na wageni waalikwa
MfanyabiasharaJuliusMasalu
mkazi wa Mwanza (katikati) akipokea funguo za gari alilojishindia
katika droo ya promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha
mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL)
kutoka kwa Meneja wa Chapa ya Konyagi,Martha Bangu (Kulia),anayeshuhudia
kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TDL,Devis Deogratius.Droo ya pili ya promosheni hiyo ilifanyikamwishoni
mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi mwishoni
mwa wiki ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na
kanda ya ziwa
Baadhi ya maofisa wa TDL na mawakala katika picha ya pamoja
Mawakala wa Konyagi wakiserebuka wakati wa hafla hiyo
Meneja Masoko wa TDL,George Kavishe akiwashukuru mawakala walioshiriki kwenye promosheni hiyo
MfanyabiasharaJuliusMasalu (58) mkazi wa Mwanza ameibuka mshidi wa gari aina ya Eicher lenye thamani ya shilingi milioni56katika mzunguko wa pili wa bahati nasibu ya Promosheni yaNunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL).
Droo ya pili ya promosheni hiyo ilifanyikakatika
viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi mwihoni mwa wiki ikihusisha
washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa na
kusimamiwa na afisa wa Bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha Humudi
Abdul Hussein.
Akiongea
kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Masalu alisema ametoka
Mwanza akiamini kuwa atajishindia gari hilo na kwamba bahati nasibu hiyo
imeendeshwa kwa uwazi na hakuna upendeleo unaoweza kufanyika.
“Katika bahati nasibu hii hakunalongo
longo,shindano limeendeshwa kwa uwazi mkubwa sana na namshukuru Mungu
kwa kuweza kupata zawadi hii ya gari itanisaidia sana katika kusambaza
bidhaa zakampuniya konyagi kwa wateja wangu,” alisema Masalu.
Kaimu MenejaMkuu wa Konyagi, DevisDeogratius alisema dhumuni ya promosheni hiyo nikukuza
uhusiano wa kibiashara na wasambazaji wa bidhaa za TDL pamoja na
kuwapatia kifaa kitakachosaidia katika kupanua masoko ,kusambaza na
kuongeza ufanisi.
“Safari
ilianza mwezi wa saba hadi mwezi wa tisa ,kumekuwa na usawa katika
mchakato huu wa kumpata mshindi na hakuna upendeleo wowote ,wale ambao
wamefikia malengo wamefika katika promosheni hiina kuwepo hali ya usawa katika kushinda zawadi ya gari”alisema Deogratius.Alisema mbali na mshindi huyo wa garikatika droo hii ya kwanza washirikiwatano walibahatikakujishindia katoni 10 za Konyagi kila mmoja.
Baadhi ya washiriki katika droo hiyo, Mkamba Zephania na Joas Muganyiziwalisema wameridhishwa na mchakato mzima ulivyofanyika katika kuchezesha droo na wala hapakuwa na kasoro ama udanganyifu wowote.
“Kampuni ya TDL kupitia bidhaa yake ya Konyagi katika promosheni ya NunuaUza,Shinda
na Konyagi imesaidia kuwakutanisha wafanyabiashara wa maeneo mengine ya
kanda ya Kaskazini na kanda ya ziwa hali inayochangia kuongeza wigo
katika kufanya biashara”.Alisema Muganyizi.
Washindi
wengine waliojinyakulia katoni 10 kila mmoja za bidhaa ya Konyagi na
maeneo wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Linus Mathew (Kagera) Msemo
Enterprises (Arusha) ,Joace Muganyizi(Bukoba) Mkamba Zephania (Bariadi)
na Yohana Masunga (Geita).
Huu
ni mzunguko wa pili wa droo ya bahati nasibu ya Promosheni ya Nunua
Uza,shinda na Konyagi ambapo katika droo ya kwanza mfanyabiashara Grace
Oroki,mkazi
wa Jijini Dar es salaam, alijinyakulia gari kwa mawakala wa kuuza
bidhaa za kampuni ya TDL wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini na Pwani.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Bw. Bakari Mohammed kuhakikisha
hospitali ya wilaya hiyo inakusanya mapato kwa kutumia mfumo wa
kielektroniki.
Ametoa
agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati alipotembelea
hospitali ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya
siku tatu mkoani Lindi.
Waziri
Mkuu amesema Serikali ilishaagiza taasisi zote za umma kutumia mfumo wa
kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kudhibiti mianya
ya upotevu wa fedha za umma.
Amesema
taasisi ambazo tayari ziameanza kutumia mfuko huo katika ukusanyaji wa
mapato zimeweza kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka sh. 300,000 hadi
milioni nne kwa siku.
Pia
aliwaagiza viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwahamasisha wananchi
kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao utawawezesha kupata
huduma ya matibabu bure katika kipindi cha mwaka mzima.
Akizungumzia
kuhusu matibabu kwa wazee, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Mohammed
kuhakikisha anafungua dirisha la kuwahudumia wazee ili kuwarahisishia
upatikanaji wa huduma wanapofika hospitalini hapo.
“Mkurugenzi
hakikisha watendaji wako wa kata na vijiji wamebaini wazee wote katika
maeneo yao na kuwatengenezea vitambulisho vitakavyowawezesha kupatibiwa
bure,” amesema.
Naye
Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Samwel Laizer amesema muamko mdogo wa
jamii kujiunga na CHF ni moja kati ya changamoto zinazowakabili katika
utoaji wa huduma za afya.
Dk. Laizer amasema kati ya kaya 30,000 zilizoko wilayani Nachingwea ni kaya 7,133 tu ndizo zilizojiunga na mfuko wa CHF.
Awali
Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa
Chuo Cha Walimu na kuwataka wabadilike ili waweze kuwatumikia wananchi
kwa uadilifu bila ya kujali itikadi zao za kidini na kisiasa.
Amesema
Serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu
wake wa kuwatumikia wananchi. “Serikali haitaridhika kuona wananchi
wakizagaa kwenye ofisi za halmashauri hiyo bila ya kusikilizwa,”
amesema.
ACDI/VOCA, an
International NGO with Headquarters based in Washington, D.C., is
currently advertising for the position outlined below for the Cereals
Market System Development (CMSD) Activity. CMSD is a four-year project
funded by The United States Age, for International Development (USAID),
which promotes economic growth by facilitating the competitiveness of
the smallholder-based rice and maize value chains, especially in rural
areas. Position:Grants Assistant Location:lringa Job Summary: The Grants
Assistant is a member of the CMSD Grants team. The primary role of the
Grants Assistant is to work with the Gran. Manager to ensure that grants
are executed in an efficient and timely manner, in full compliance with
ACD/VOCA grants policies and procedures, as well as USAID rules and
regulations. The Grant& Assistant works with the Grants Manager on
ensuring the integrity and transparency of the process of identifying
grantees and the procedures used to award them. S/he ensures that
processes and procedures are clear and clearly communicated to staff,
applicants, grantees and subcontractors. Key Responsibilities: • Participate
in improving/clarifying processes and procedures for awarding and
administering grants, and propose corrective action when these are
unclear or causing unnecessary delays • Collect and
safely store received prequalification applications and submit to Grants
Manager for processing Distribute grant applications to evaluation
committee and with collaboration with Grants Manager, perform Pre-Award
Assessments • Coordinate approval of milestones/deliverabies and payments to grantees • Ensure that all grants files are well filed and property documented according to the grant documentation checklist requirement • Ensure and Make proper filing and documentation of Grantees files with respect to the grant documentation check list • In the absence of Grants Manager, serve as a non-voting member of the grant application evaluation committee • Identify and
document any problems or shortcomings of grantee performance, recommend
corrective actions, and communicate these to the Grants Manager and
appropriate personnel in timely fashion • Review and
analyze grantee budget estimates for allow ability and reasonableness,
and consistency and routinely spot check visit grantees to ensure that
funds allocated are used for specified purposes • In close
collaboration with Grants Manager, conduct internal training sessions on
CMSD grants Processes including the preparation of grant applications,
financial management and reporting requirements • In close
collaboration with Grants Manager, conduct mandatory training for all
grantees regarding administration and technical reporting requirements • Engage and
facilitate interaction with our technical team to ensure that roles and
responsibilities in the granting ()MGM are clear and clearly
communicated Qualifications and Experience: • University
Degree in Accounting, Finance, Business Administration, Economics or
related field with at least 1.2 years of work experience in Grants
Management, Accounting, or Finance • Proven knowledge of USAID rules and regulations, preferred with International NGO experience. • High level of English, both spoken and written English,strong communication and interpersonal skills Application Instructions: To apply for
this position, qualified candidates should submit an application letter
describing why he/she is the best fit for this position, and a
curriculum vitae detailing relevant work experience with three referees
to hr@nafaka-tz.org. Closing date for applications is 21st October 2016 (Only shortlisted candidates will be contacted) ========
============
Are you
disappointed by fruitless job applications and never get shortlisted?
The problem is not you, its your CV. This comes to an end, Now for
outstanding CV and Jobs professional advice, contact Bright
Professionals Tanzania and grab your dream job. We also prepare social
science business researches and proposals.