Friday, 9 September 2016

Serikali yawaonya wahitimu elimu ya msingi



SERIKALI imewataka wahitimu wa darasa la saba waliomaliza mitihani yao jana nchini kote kutojihusisha na tabia au vitendo vyovyote vinavyohatarisha afya, usalama na maendeleo yao.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ametoa onyo hilo leo katika tamko maalum alilolitoa kwa wanafunzi hao waliohitimu elimu ya msingi nchini kote.
Takwimu zinaonyesha kuwa, wanafunzi 795,761 (wavulana 372,883 sawa na asilimia 46.86 na wasichana 422,878 sawa na asilimia 53.14) walisajiliwa na kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu.
“Hivyo ningependa kutumia fursa hii kuwaasa watoto waliomaliza darasa la saba kutojihusisha na tabia au vitendo vyovyote vinavyo hatarisha afya, usalama na maendeleo yao, kama vile kujihusisha kwenye masuala ya ngono, matumizi ya madawa ya kulevya na vileo katika kipindi hiki cha kusubiri matokeo ya mitihani yao,”amesema Ummy.
Amesema watoto wa Kike na Kiume wajitambue, na wajue kuwa wao ni hazina ya pekee katika maendeleo ya nchi.
Waziri Ummy amesema kipindi hiki wakitumie vizuri kwa kuwa waadilifu, waaminifu, wenye bidii na kuzingatia kanuni za nidhamu na tabia njema huku wakijiandaa kwa ajili ya kuendelea na elimu ya Sekondari.
Share:

Tangazo la Usaili wa Walimu Unguja 2016


image043
#TANGAZO #LA #USAILI #WIZARA #YA #ELIMU #NA #MAFUNZO #YA #AMALI #ZANZIBAR
Tume ya Utumishi Serikalini inawatangazia vijana ambao wameomba nafasi ya kazi ya Ualimu kwa upande wa Unguja tu! kufika katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini kwa ajili ya kufanyiwa usaili siku ya Jumamosi  saa 2:00 za asubuhi na pia wachukue vyeti vyao halisi vya kumalizia masomo, Cheti cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
#INDHARI: #Tangazo #hili #linawahusu #wale #waliomba #nafasi #hiyo #upande #wa #Unguja #tu!.
#VIJANA #WENYEWE #NI
Share:

MPYA:HALMASHAURI YA JIJI DAR YAMWAGA KAZI KWA WATANZANIA WENYE SIFA,DEADLINE NI SEP 30 2016


HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA YA
HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA KIPINDI
CHA MWAKA 2015 - 2020

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam anawatangazia wakazi wa Dar es Salaam wenye sifa, kutuma  maombi ya nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha Mwaka 2015 - 2020.
SIFA ZA MWOMBAJI:
1.  Awe Raia wa Tanzania, Mkazi wa kawaida wa Jiji la Dar es Salaam na mwenye umri usiopungua miaka  Arobaini na tano (45).
2. Awe na taaluma katika mojawapo ya fani zifuatazo:-
  • Menejimenti ya Rasilimali Watu (Human Resources Management), Utawala na Uongozi (Public Administration au Sheria (Law).
3. Asiwe Mwajiriwa wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
4. Awe na uzoefu mkubwa katika masuala ya Rasilimali Watu na Utawala.
5. Awe Mwadilifu.
MAELEKEZO
1. Waombaji wote watume barua zao za maombi zikiwa na viambatisho vifuatavyo:-
  • Cheti cha kuzaliwa.
  • Vivuli vya masomo na Taaluma (Certified).
  • Barua ya Utambulisho toka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa ikiwa na picha ndogo ya hivi karibuni.
  • Wasifu  (CV).
2. Barua toka kwa wadhamini wawili (2) zikiwa na anuani kamili
3. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Septemba, 2016
4.  Barua zote za maombi zitumwe kwa anuani ifuatavyo:-
  Mkurugenzi wa Jiji,
  Halmashauri ya Jiji,
  Ukumbi wa Jiji,
  1 Barabara ya Morogoro,
  S.L.P. 9084,
  11882 – DAR ES SALAAM.
Sipora J. Liana
MKURUGENZI WA JIJI,
HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA ST.JOHN UNIVERSITY CHETI NA DIPLOMA FROM NACTE 2016/2017-SECOND BACTH

Share:

Picha 17: JAMAA ANAYEDAIWA KUFANYA MAPENZI NA WAKE ZA WATU KICHAWI SHINYANGA AKAMATWA,ASHUSHIWA KIPIGO


Wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wamemshushia kichapo jamaa anayedaiwa kuwaingilia wanawake nyakati za usiku kisha kufanya nao mapenzi kwa njia za kishirikina.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa kumi jioni ambapo wakazi wa kitongoji cha Bugayambelele jirani na kijiji cha Nhelegani kilichokumbwa na taharuki ya kuwepo mtu anayefanya mapenzi na wake za watu kimazingara,walimshtukia jamaa huyo baada ya kuonekana akifanya vitendo walivyodai kuwa vya kishirikina katika familia mbili za kitongoji hicho.

Malunde1 blog baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo ilifika eneo la tukio haraka zaidi na kushuhudia umati mkubwa wa watu ukiwa umemzingira jamaa huyo huku askari polisi wakiwa eneo la tukio kuzuia wananchi wasiendelee kumshushia kipigo jamaa huyo.

Wakazi wa eneo hilo walisema mtu huyo aliingia kwenye nyumba mbili(kaya mbili) bila kupiga hodi huku akidai kuwa alikuwa anatafuta mke wake, akidai kuwa ametoka kwa mganga wa kienyeji kaelekezwa kuwa mke wake yupo eneo hilo.

Hata hivyo baada ya kumtilia mashaka jamaa huyo alianza kukimbia na kutupa simu zaidi ya tatu za mkononi alizokuwa nazo,wananchi wakafanikiwa kumkamata kisha kumpeleka kwenye mkutano wa sungusungu na walipompekua wakamkuta na dawa za kienyeji zinazodaiwa kuwa za mapenzi,zikisomoka kama ifuatavyo;

“Imala yose -kuchoma kuomba mke wako roho yake irudi kwako akupende” na nyingine maandishi yakisomeka kuoga na kuchoma kuomba mkeo akupende na arudi kwako”.
 
Wakazi wa eneo hilo walisema kutokana na maelezo yake,pia kuingia katika familia moja bila hodi huku akidaiwa kupotea kimiujiza eneo hilo na kuibukia katika familia nyingine pamoja na dawa za kienyeji alizokuwa nazo walimhusisha moja kwa moja na tukio la ubakaji kwa njia za kishirikina.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugayambelele Donald Francis alisema alipigiwa simu na kuelezwa kuwepo kwa mwanamme anayehusishwa na tukio la kubaka wanawake kishirikina katika kijiji jirani cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
 
Alisema mwanamme huyo alikutwa na dawa za kienyeji huku akitoa maelezo yasiyoeleweka ikiwemo kudai amefika hapo kwa ajili ya kutafuta kazi ya kufyatua matofali,kutafuta mke wake na anatoka kwa mganga wake wa kienyeji aliyemnyweshwa dawa za ajabu.
Tutawaletea taarifa kamili hivi punde....

Mwanamme aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Charles kutoka Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga anayedaiwa kujihusisha na vitendo vya kubaka wanawake kishirikina nyakati za usiku-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Polisi wakiwa eneo la tukio


Wananchi wakiwa eneo la tukio

Dawa za kienyeji alizokutwa nazo jamaa huyo

Dawa za kienyeji za jamaa pamoja simu yake

Dawa za kienyeji

Polisi na wananchi wakiwa wamemzunguka jamaa huyo

Mwandishi wa habari wa Radio Faraja Steve Kanyeph akifanya mahojiano na jamaa huyo

Wananchi wakiwa eneo la tukio

Wananchi wakiwa eneo la tukio

Gari la polisi likiwasili eneo la tukio


Jamaa akipanda kwenye gari la polisi

Baiskeli ya mtuhumiwa ikipandishwa kwenye gari la polisi


Polisi wakiondoka na mtuhumiwa

Wananchi wakiondoka eneo la tukio
Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugayambelele Donald Francis akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema alipigiwa simu na kuelezwa kuwepo kwa mwanamme anayehusishwa na tukio la kubaka wanawake kishirikina katika kijiji jirani cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO CHA TUMAINI MAKUMIRA ARUSHA SECOND SELECTION 2016/2017

Share:

MPYA:TANGAZO KWA WANAFUNZI WOTE MLIOCHAGULIWA CHUO CHA MAJI UBUNGO 2016/2017


ALL 2016-17 FIRST YEAR STUDENTS
Kindly be informed that, WDMI ACCCOMODATION APPLICATION FORMS (available on this website) must reach the office of DEAN OF STUDENTS not later than 30th September, 2016. No Accommodation service will be offered to student without completion of ACCCOMODATION APPLICATION FORMS.
Dean of Students
Water Development and Management Institute.
Share:

HII HAPA JOINING INSTRUCTION ZA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA DIT 2016/2017 UNDER-GOVERNMENT SPONSORSHIP

Joining Instruction letter for Government Sponsored Students

Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA (1ST & 2ND SELECTION) YA WANAFUNZI DIPLOMA NA CHETI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU CHA KAMPALA UNIVERSITY(KIU) 2016/2017


UPDATED NACTE FIRST AND SECOND SELECTION LIST 2016

 

Kampala International University-dar




Students whose names appear on the list should come to campus and pick their admission letter/Joining Instructions immediately as they are ready.
Share:

JE,WALIMU MNAOSUBIRIA AJIRA SASA KUANZA KUFANYIWA INTERVIEW? ONA HII HALAFU JIPE JIBU MWENYEWE

 Image result for SERIKALI YA TANZANIA
Katika pitapita yangu,Nimenusa sehemu na kufanikiwa kukutana na system ambayo  ni ya online kwa ajili ya walimu wote kuapply online kwa kusubmitt vyeti vyako vyote.
Nimejiuliza sana,je ni kweli walimu kuanza kufanyiwa interview kama kozi zingine?
Maswayetu blog bado tunalifuatilia hili ktk ofisi za TAMISEMI kukuletea taarifa kamili.
P.O.BOX 1923 Dodoma - Tanzania. Tel: 026 232 2848. Fax: Email: ps@tamisemi .go.tz. Website: www.tamisemi.go.tz.
Online Teachers Employment Application System-OTEAS
www.osaistz.com
ONLINE TEACHERS EMPLOYMENT APPLICATION SYSTEM,THIS IS THE COMPUTER SYSTEM FOR MONITORING
Share:

MPYA:HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA(ACSEE),UALIMU(GATCE&DSEE) 2016 MAPYA KWA WANAFUNZI WALIOKATA RUFAA

Share:

MPYA:HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA(ACSEE),UALIMU(GATCE&DSEE) 2016 MAPYA KWA WANAFUNZI WALIOKATA RUFAA

Share:

RAIS MAGUFULI ATEUA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA YA RUKWA NA MARA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Septemba, 2016 amemteua Bw. Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara. 

Bw. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu. 

Pia, Rais Magufuli amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. 

Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu. 

Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye. 


Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU 
Dar es Salaam 
09 Septemba, 2016
Share:

Tundu Lissu : Prof. Lipumba Hana Hoja, Anawavuruga CUF

MBUNGE wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Tundu Lissu, amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Iblahim Lipumba amekosa hoja ya kuzungumza na badala yake anawavuruga wanachama wa CUF.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema amesema Lipumba hakuwahi kuwa na idadi kubwa ya wabunge kama walivyo sasa tangu alipoanza kugombea urais zaidi ya kupata viti viwili tu lakini walipoungana mwaka jana katika umoja wao wa Ukawa wakaibuka  na viti 10.
1Mbunge wa Singida Mashariki ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheia Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari. (hawapo pichani).
Kauli hiyo ameisema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo aliongeza kuwa Lipumba aache kukiandama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai ya kuwa kinaivuruga CUF.
Aliongeza kuwa Lipumba kuendelea kutoa matamshi hayo kwa wanachama wa CUF ni chanzo cha yeye kuendelea kukivuruga chama hicho hivyo wanachama wampuuze kwani alikikimbia tokea walipoungana katika umoja wao wa Ukawa kabla ya mwezi mmoja kujiunga  aliyekuwa mgombe urais kupitia umoja huo, Edward Lowasa kupitia Chadema.
2Lissu akisikiliza kwa makini maswali aliyokuwa akiulizwa na wanahabari.
Kwa upande mwingine Lissu amesema viongozi wa Chadema wamepanga Jumanne wiki ijayo kupelekea malalamiko yao katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili wafuasi 10 wa Chadema waliokamatwa kwa madai ya kusambaza maneno ya uchochezi.
3Viongozi hao wakiendelea kusikiliza maswali ya wanahabari yaliyokuwa yakiulizwa.
Alisema wanapeleka hoja hiyo mahakamani ili mahakama iweze kuamuru waachiwe huru kwani hivi sasa wanateseka mahabusu.
4Mkutano ukiendelea na wanahabari.
Alisema mahakama ndiyo chombo kikuu chenye dhamana ya kuwahoji Mkuu Jeshi la Polisi, IGP Ernest  Mangu na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini DCI, Diwan Athumani ili watoe sababu ya jeshi la polisi kuwaweka mahabusu wanachama 10 wa chadema kwa zaidi ya wiki moja sasa bila kuwapeleka mahakamani.
Share:

Official VIDEO | TID Ft. Joh Makini - Confidance | Watch/Download


Share:

New AUDIO[SINGELI] | Manyo lee - Mwendo wa Pushap | Download

Share:

MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN WAPATA AJALI MKOANI MTWARA,WANNE WAJERUHIWA


Moja ya Gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Rais, Mama Samia Sukuhu Hassan,namna lilivyo haribika mara baada ya Kuacha njia na kupinduka.

 Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais ,mkoani Mtwara, umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu Rais.
Majeruhi wa ajali wakipata msaada wa  huduma ya kwanza mara baada ya gari walilokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger