Sunday, 4 September 2016
Rais Magufuli Azungumzia Tukio la Maalim Seif kukataa mkono wa Rais Shein
Rais John Magufuli
amemshangaa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kwa kuidhinisha fedha
za matibabu ya mpinzani wake wa kisiasa, Maalim Seif Sharif Hamad
wakati alikataa kumpa mkono wa salamu walipokutana kwenye mazishi wiki
mbili zilizopita.
“Mtu mmekutana kwenye msiba, mahali kwenye majonzi,
mnamsindikiza marehemu. Kwa unyenyekevu wako Dk Dhein ukatoa mkono wako
kumsalimia mtu fulani. Huyu mtu akakatalia mikono yake na bado asubuhi
yake ukasaini fomu zake za kwenda kutibiwa nje ya nchi?” alisema
Magufuli.
“Haya ni mapenzi makubwa sana. Amekataa mkono wako. Huyohuyo
akiugua unampeleka hospitali. Akitaka kusafiri nje, unasaini na unampa
na fedha na posho za kwenda nje. Mimi nisingeweza.”
Rais ametoa kauli
hiyo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani
Unguja ambako amekwenda kushukuru wananchi kwa kumchagua kwenye Uchaguzi
Mkuu uliopita.
Visiwani Zanzibar, uchaguzi wa Rais, wawakilishi na
madiwani uliingia dosari siku ya mwisho ya kutangaza matokeo. Mwenyekiti
wa Tume ya Ucha- guzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha alifuta matokeo
ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani Oktoba 28
mwaka jana, siku ambayo alitarajiwa kutangaza mshindi wa mbio za urais.
Alifuta wakati matokeo ya majimbo 31 yakiwa yameshatangazwa na kubakia
tisa ambayo yalishahakikiwa na kusubiri kutangazwa huku baadhi ya
washindi wa viti vya uwakilishi wakiwa wameshatangazwa na kupewa vyeti.
Jecha alisema kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi na
kutangaza uchaguzi mpya Machi 20, lakini chama kikuu cha upinzani
visiwani humo, CUF kikasusia na tangu wakati huo uhusiano baina ya
wafuasi wa vyama hivyo umeharibika.
Uhasama huo ulifikia kiwango cha juu
wakati Maalim Seif alipokataa kumpa mkono Dk Shein walipokutana kwenye
mazishi ya Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi kitendo
kilichomfanya Rais Magufuli aeleze yake ya moyoni jana.
Akishangiliwa na
wananchi, ambao wengi walivalia fulana za rangi za njano na kijani
ambazo hutumiwa na CCM, Rais Magufuli alisema Dk Shein ni mpole na kama
angekuwa na moyo kama wake, hali ingekuwa tofauti baada ya kufanyiwa
kitendo hicho cha Maalim Seif.
“Niutoe mkono wangu, uukatae halafu kesho
niende ofisini kukusainia wewe (akaongea kilugha). Ndiyo maana nasema
wewe ni special. Nafikiri wanapotoka malaika wewe ndiyo unafuata. Kama
mtu anaukataa mkono wako, na wewe kataa kufanya mambo yake, ajifunze
kwamba na wewe mkono wako una thamani.”
Alisema anaomba
Mungu amsaidie kumpa angalau nusu ya moyo wa Dk Shein na kuomba Mungu
ampe Dk Shein nusu ya roho na mawazo yake ili Zanzibar iende bila kelele
za aina yoyote.
“Jana nilikwambia angalau uongeze kaukali kidogo.
Umefanya mambo makubwa sana katika nchi hii. Tulishazungumza na wewe
umezungumza kwamba kwa mujibu wa Katiba, uchaguzi umekwisha,
ukisharudiwa umekwisha. Utarudiwa tena mwaka 2020, wazunguke waimbe
lakini wewe ndiye rais,” alisema.
Magufuli alisema upendo na unyenyekevu
alionao Dk Shein ni wa hali ya juu kwani licha ya mikikimikiki
aliyoipata kutoka kwa wapinzani, ameendelea kuwaingiza katika Serikali
yake, jambo ambalo yeye hawezi kulifanya.
“Mimi nilipata ushindi kwa asilimia 58, lakini hakuna mtu kutoka chama kingine atakayekanyaga mguu kwenye Serikali yangu.
“Mimi nilipata ushindi kwa asilimia 58, lakini hakuna mtu kutoka chama kingine atakayekanyaga mguu kwenye Serikali yangu.
"Mzee huyu ana moyo wa tofauti, namuomba
Mungu apate hata robo ya moyo wangu maana amekuwa mpole mno,” alisema Dk
Magufuli.
Rais Magufuli alisema licha ya maendeleo yaliyopo, bado wapo Wazanzibari (hakuwataja majina) wanaokwenda nje ya nchi na kuwazuia wageni na watalii kuacha kutembelea visiwa hivyo.
“Mwenyeji anakuja na kuwaambia wageni wasije hapa na wao wamempuuza. Bado wageni wanakuja. Ukigombea mwaka wa kwanza ukashindwa, mwingine ukashindwa, mwingine ukashindwa, huwezi kujifunza hata kwenda kuuza nyanya sokoni kwamba biashara hii imekataa kwako,” alisema na kuongeza:
“Kwani hakuna wengine ambao wanakuja? Kuna mtu alitegemea kwamba nitakuwa Rais, hata kuota.Lakini nimekuwa waziri kwa miaka 20 sikujaribu hata siku moja kugombea (urais).
“Unajua vyeo hivi vinaletwa na Mungu, hata uzunguke namna gani, hata ufuge ndevu namna gani hata unyoe. Kama kasema hapana ni hapana tu, ndiyo maana nasema watu, ni shetani kama sivyo, basi ana moyo wa kishetani na mtu anayefarakanisha mke na mume kwa itikadi za vyama vyao pia ni shetani.
Rais Magufuli alisema licha ya maendeleo yaliyopo, bado wapo Wazanzibari (hakuwataja majina) wanaokwenda nje ya nchi na kuwazuia wageni na watalii kuacha kutembelea visiwa hivyo.
“Mwenyeji anakuja na kuwaambia wageni wasije hapa na wao wamempuuza. Bado wageni wanakuja. Ukigombea mwaka wa kwanza ukashindwa, mwingine ukashindwa, mwingine ukashindwa, huwezi kujifunza hata kwenda kuuza nyanya sokoni kwamba biashara hii imekataa kwako,” alisema na kuongeza:
“Kwani hakuna wengine ambao wanakuja? Kuna mtu alitegemea kwamba nitakuwa Rais, hata kuota.Lakini nimekuwa waziri kwa miaka 20 sikujaribu hata siku moja kugombea (urais).
“Unajua vyeo hivi vinaletwa na Mungu, hata uzunguke namna gani, hata ufuge ndevu namna gani hata unyoe. Kama kasema hapana ni hapana tu, ndiyo maana nasema watu, ni shetani kama sivyo, basi ana moyo wa kishetani na mtu anayefarakanisha mke na mume kwa itikadi za vyama vyao pia ni shetani.
Rais Magufuli aahidi kulinda Muungano na kudumisha amani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amewahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa atasimamia kwa nguvu zote
masuala yote yanayohusu maendeleo, kudumisha Muungano wa Tanzania Bara
na Tanzania Zanzibar na kudumisha amani kwa faida ya wananchi.
Rais
Magufuli amesema hayo jana tarehe 03 Septemba, 2016 alipokuwa
akizungumza na wananchi wa Zanzibar katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika uwanja wa Kibandamaiti Mjini Unguja.
Dkt.
Magufuli ambaye aliongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli alisema ili
mambo hayo yafanikiwe Wananchi wa Zanzibar hawana budi kukataa
kujihusisha na vitendo vya vurugu na kuvunja amani na amewaonya watu
wanaochochea vitendo hivyo kuacha mara moja.
Aliwataka
wananchi wa Zanzibar kujihadhari dhidi ya wanasiasa ambao wanapandikiza
chuki, ubaguzi na fitina, kwani watu hao wanataka kubomoa misingi
mizuri ya umoja, upendo na mshikamano wa Taifa uliojengwa na waasisi wa
Taifa hili.
Rais
Magufuli alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein aliyehudhuria mkutano huo, kwa hatua
mbalimbali anazozichukua kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar huku
akibainisha kuwa tatizo la maji linalovikabili visiwa vya Zanzibar
litakwisha baada ya kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa maji utakaofadhiliwa
na Serikali ya India kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 92, na
mradi mwingine utakaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 21.
Aidha,
Rais Magufuli alivipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri
vinayofanya katika kusimamia amani visiwani humo huku akivihakikishia
kuwa yeye akiwa kiongozi wao anawaunga mkono.
Pamoja
na Rais Shein Mkutano huo ulihudhuriwa na Mke wa Rais wa Kwanza wa
Zanzibar Mama Fatma Karume, Mawaziri na Viongozi wa Siasa na Dini.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Unguja
Saturday, 3 September 2016
HVI HAPA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU TANZANIA KUTOKA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA -TFDA
Afikishwa Mahakamani Kwa Kumuita Rais Magufuli ni Kilaza
ELIZABETH
Asenga (40), mkazi wa jijini Dar es Salaam amepandishwa kortini jana
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuandika maneno ya
kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa What’s App.
Akisomewa
mashtaka yake na Leonard Chalu, wakili wa serikali, mbele ya Hakimu
Huruma Shahidi, mwanamama huyo, alidaiwa kufanya kitendo hicho kilicho
kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.
Wakili
Chalu alidai kuwa, mnamo tarehe 06 Agosti mwaka huu, mtuhumiwa huyo
aliandika kwenye mtandao wa what’s App ujumbe uliosomeka;
“….Rais
kilaza kama huyu wetu, angalia anampa Lissu umashaghuli… f****l** lile,
kwanza picha yake ukiweka ofisini ni nuksi tupu na ukiamka asubuhi
ukakutana na picha yake, siku yako inakuwa ina mkosi mwanzo mwisho.”
Hata
hivyo, mshitakiwa Elizabeth, alikana mashtaka hayo huku wakili wa
serikali akidai kuwa, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Mtuhumiwa
alipewa dhamana yenye masharti yanayohitaji wadhamini wawili huku kila
mmoja akitakiwa kusaini hati ya shilingi 3 millioni.
Kesi hiyo imeahirishwa na inatarajia kutajwa tena mnamo tarehe 22 Septemba, mwaka huu.
Waziri Mkuu aitaka Wizara ya Elimu kuongeza wataalamu wa Afya nchini.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi iweke mpango maalumu wa kuongeza wataalamu zaidi katika sekta ya
afya ndani ya nchi ili kuipunguzia Serikali gharama za kusomesha
wataalam hao nje ya nchi.
Ametoa
agizo hilo Ijumaa, Septemba 2, 2016 wakati alipokagua maendeleo ya
mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi
ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na Ujenzi wa Kituo cha Tiba cha Kimataifa cha
Muhimbili katika eneo la Mloganzila.
Amesema
Serikali zilizotangulia zimefanya kazi kubwa na nchi imefikia hatua
nzuri ya kuongeza wataalam ndani ya nchi ambao watakwenda kutatua
changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa kwenye hospitali za mikoa na
wilaya.
Waziri
Mkuu amesema ujenzi wa kituo hicho cha tiba cha kimataifa pia
utawapunguzia wananchi adha ya kutafuta fedha za kwenda kupata matibabu
nje ya nchi. Tayari upasuaji mkubwa wa magonjwa ya moyo umeanza
kufanyika nchini.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw.
Humphrey Polepole awasake watu wote waliohusika na wizi wa lita 1,000 za
mafuta ya kuendeshea mitambo katika karakana ya mkandarasi anayejenga
Kampasi hiyo.
“Wafanyakazi
waache wizi. Lita 1,000 zinaondokaje katika karakana ya mkandarasi? Hii
kampuni inayolinda kama imeshindwa kazi iondolewe na Mkuu wa wilaya
usimhurumie mwizi,” amesisitiza.
Kwa
upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce
Ndalichako amesema kukamilika kwa kampasi ya Mloganzila kutasaidia
upatikanaji wa madaktari bingwa wengi nchini ambao watapunguza gharama
za kupeleka wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Awali,
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Ephata Kaaya alisema kukamilika kwa
hospitali pamoja na kampasi yote ya chuo kutawezesha kupunguza kwa kiasi
kikubwa uhaba wa wataalamu wa afya nchini.
Amesema
hospitali hiyo itatumika kutoa huduma za afya za kitaalam zaidi kwa
magonjwa mbalimbali, hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje
ya nchi kwa matibabu. Pia itapunguza msongamano wa wagonjwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ujenzi
wa mradi huo umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali
imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni
43. Kukamilika kwa ujenzi wa kampasi hiyo ya Mloganzila kutawezesha
chuo kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa fani ya afya kutoka 4,010
hadi 15,000.
Prof.
Kaaya amesema mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo
ulisainiwa tarehe 12, Desemba, 2014 na ujenzi ulianza mwezi Julai, 2015
na unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2016.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Rais Magufuli ataka Jecha apewe Tuzo ya heshima .........Amtaka Dr Shein Apunguze Upole, Watakaomsumbua Awataje Washughulikiwe
RAIS
John Magufuli, amemtaka Dk. Ali Mohamed Shein, kumpa tuzo Jecha Salim,
mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kutokana na kile alichokiita
kazi nzuri aliyoifanya visiwani humo mwaka jana, kwa kufuta matokeo ya
uchaguzi mkuu.
Rais Magufuli aliyasema hayo jana
jioni, katika ziara yake ya kikazi visiwani Pemba. Wakati Rais Magufuli
akichaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Dk. Shein
alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kufuatia uchaguzi wa marudio
uliofanyika Machi mwaka huu.
“Nampongeza
sana Jecha kwa kazi nzuri aliyofanya kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar,
na kwa kweli Dk. Shein kama kuna tuzo zako utakazotoa, naomba usimsahau
kumpa na Jecha,” alisema Rais Magufuli.
Rai Magufuli pia alimtaka
Rais huyo wa Zanzibar kumtaarifu yeye ili awashughulikie watu wote
wanaomsumbua visiwani humo au wanaoonekana kumzidi nguvu.
“Rais
Shein kama kuna mtu unaona anakusumbua wewe au anakupa tabu nijulishe
mimi tu, hata dakika tano hazitapita nitamshughulikia,” ameeleza.
Kauli
hiyo inakuja, ikiwa ni zaidi ya miezi kumi sasa tangu hali ya mahusiano
baina ya wananchi wa Zanzibar iwe tete, tangu pale Jecha Salim Jecha,
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) alipotangaza kufuta
matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Mahusiano
hayo mabaya yamesababisha, wafuasi wa vyama vya CUF na CCM vyenye nguvu
zaidi visiwani humo, kufikia hatua ya kusitisha ushirikiano katika
shuguli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kutohudhuria misiba na kutonunua
bidhaa za mtu wasiyeendana naye kiitikadi.
“Niombe
vyombo vya ulinzi na usalama wafuatilie hao wanaokatakata na kuchoma
karafuu washughulikiwe bila huruma. Atakayejaribu kuichezea amani,
atacheza yeye tena mchezo asiojua kuucheza,” aling’aka Rais Magufuli.
Tangu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana visiwani Zanzibar, hali ya usalama imekuwa si ya kuridhisha.
Nyumba na mashamba ya karafuu yamekuwa yakichomwa moto, huku baadhi ya watu wakitiwa mbaroni na vyombo vya dola kwa tuhuma hizo