Saturday, 3 September 2016

Waziri Mkuu aitaka Wizara ya Elimu kuongeza wataalamu wa Afya nchini.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi iweke mpango maalumu wa kuongeza wataalamu zaidi katika sekta ya afya ndani ya nchi ili kuipunguzia Serikali gharama za kusomesha wataalam hao nje ya nchi.

Ametoa agizo hilo Ijumaa, Septemba 2, 2016  wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na Ujenzi wa Kituo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili katika eneo la Mloganzila.

Amesema Serikali zilizotangulia zimefanya kazi kubwa na nchi imefikia hatua nzuri ya kuongeza wataalam ndani ya nchi ambao watakwenda kutatua changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kituo hicho cha tiba cha kimataifa pia utawapunguzia wananchi adha ya kutafuta fedha za kwenda kupata matibabu nje ya nchi. Tayari upasuaji mkubwa wa magonjwa ya moyo umeanza kufanyika nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Humphrey Polepole awasake watu wote waliohusika na wizi wa lita 1,000 za mafuta ya kuendeshea mitambo katika karakana ya mkandarasi anayejenga Kampasi hiyo.

“Wafanyakazi waache wizi. Lita 1,000 zinaondokaje katika karakana ya mkandarasi? Hii kampuni inayolinda kama imeshindwa kazi iondolewe na Mkuu wa wilaya usimhurumie mwizi,” amesisitiza.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema kukamilika kwa kampasi ya Mloganzila kutasaidia upatikanaji wa madaktari bingwa wengi nchini ambao watapunguza gharama za kupeleka wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Awali, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Ephata Kaaya alisema kukamilika kwa hospitali pamoja na kampasi yote ya chuo kutawezesha kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa wataalamu wa afya nchini.

Amesema hospitali hiyo itatumika kutoa huduma za afya za kitaalam zaidi kwa magonjwa mbalimbali, hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Pia itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ujenzi wa mradi huo umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni 43. Kukamilika kwa ujenzi wa kampasi hiyo ya Mloganzila kutawezesha chuo kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa fani ya afya kutoka 4,010 hadi 15,000.

Prof. Kaaya amesema mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo ulisainiwa tarehe 12, Desemba, 2014 na ujenzi ulianza mwezi Julai, 2015 na unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2016.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Share:

Rais Magufuli ataka Jecha apewe Tuzo ya heshima .........Amtaka Dr Shein Apunguze Upole, Watakaomsumbua Awataje Washughulikiwe

RAIS John Magufuli, amemtaka Dk. Ali Mohamed Shein, kumpa tuzo Jecha Salim, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kutokana na kile alichokiita kazi nzuri aliyoifanya visiwani humo mwaka jana, kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana  jioni, katika ziara yake ya kikazi visiwani Pemba. Wakati Rais Magufuli akichaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Dk. Shein alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kufuatia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi mwaka huu.

“Nampongeza sana Jecha kwa kazi nzuri aliyofanya kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, na kwa kweli Dk. Shein kama kuna  tuzo zako utakazotoa, naomba usimsahau kumpa na Jecha,” alisema Rais Magufuli.

Rai Magufuli pia alimtaka Rais huyo wa Zanzibar kumtaarifu yeye ili awashughulikie watu wote wanaomsumbua visiwani humo au wanaoonekana kumzidi nguvu.

“Rais Shein kama kuna mtu unaona anakusumbua wewe au anakupa tabu nijulishe mimi tu, hata dakika tano hazitapita nitamshughulikia,” ameeleza.

Kauli hiyo inakuja, ikiwa ni zaidi ya miezi kumi sasa tangu hali ya mahusiano baina ya wananchi wa Zanzibar iwe tete, tangu pale Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) alipotangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mahusiano hayo mabaya yamesababisha, wafuasi wa vyama vya CUF na CCM vyenye nguvu zaidi visiwani humo, kufikia hatua ya kusitisha ushirikiano katika shuguli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kutohudhuria misiba na kutonunua bidhaa za mtu wasiyeendana naye kiitikadi.

“Niombe vyombo vya ulinzi na usalama wafuatilie hao wanaokatakata na kuchoma karafuu washughulikiwe bila huruma. Atakayejaribu kuichezea amani, atacheza yeye tena mchezo asiojua kuucheza,” aling’aka Rais Magufuli.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana visiwani Zanzibar, hali ya usalama imekuwa si ya kuridhisha.

Nyumba na mashamba ya karafuu yamekuwa yakichomwa moto, huku baadhi ya watu wakitiwa mbaroni  na vyombo vya dola kwa tuhuma hizo
Share:

Friday, 2 September 2016

New AUDIO | Chadala X Ney Wamitego - Niweje | Download

Share:

MPYA NACTE:MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VYA UALIMU,AFYA,KILIMO,MIFUGO NK. CHETI NA DIPLOMA AWAMU YA PILI 2016/2017 KUTANGAZWA RASMI TAREHE 5 SEPTEMBER 2016

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA PILI NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na Umma kwa ujumla kuwa lilifunga dirisha la maombi mnamo tarehe 13 Agosti 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma ulitarajiwa kutangazwa tarehe 31 Agosti 2016 lakini kwa sababu zilizo nje wa uwezo wetu umesogezwa mbele mpaka tarehe 5 Septemba 2016.

Baraza pia linapenda kutoa taarifa  kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) kwa waombaji wa cheti na diploma utafunguliwa tena tarehe 5 Septemba 2016 hadi tarehe 15 Septemba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zitakazokuwa wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na  kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuomba udahili hapo awali.

Baraza linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 02 September, 2016
Share:

MPYA:SCHORALSHIP KWA FORM SIX KWENDA OMAN 2016/2017

Share:

MPYA:SCHORALSHIP KWA FORM SIX KWENDA EGYPT 2016/17

Share:

HIZI HAPA FORM FIVE JOINING INSTRUCTION 2016/2017 PDF - Joining Instruction Kidato cha Tano 2016/2017 -SECOND SELECTION

FORM FIVE JOINING INSTRUCTION 2016/2017 PDF - Joining Instruction Kidato cha Tano 2016/2017

PATA JOINING INSTRUCTION FORM FIVE 2016/2017


DOWNLOAD JOINING INSTRUCTION  FORM FIVE 2016/2017/MAELEKEZO YA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO 2016/2017


JOINING INSTRUCTION FORM FIVE 2016/2017 1ST SELECTION


SECOND SELECTION FORM FIVE 2016/2017 JOINING INSTRUCTIONS


MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI KIDATO CHA TANO 2016


Chagua Mkoa
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI SECOND SELECTION KIDATO CHA 5 2016 ,WANAFUNZI WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 25 HAKUNA KUINGIA FORM 5


ndalichako 




TANGAZO MUHIMU!


MUDA WA KURIPOTI (REPORTING TIME) KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili (31-AUG-2016.) atakuwa amepoteza nafasi h

>>bonyeza hapa kuona majina ya Waliochaguliwa kidato cha tano awamu ya pili 2016, Form Five Second Selection 2016 - TAMISEMI - New Update


ii.
Share:

breaking news:haya hapa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga form 5 awamu ya pili (second selection) 2016

 Image result for serikali ya tanzania

TAARIFA KWA UMMA





OR-TAMISEMI inatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya Pili (Second Selection) kwa mwaka 2016. Jumla ya wanafunzi 3,918 wakiwemo wasichana 2,413 na wavulana 1,505 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza.
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 1,864 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana 765 sawa na asilimia 47.58 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 2,054 wakiwemo wasichana 1,314 na wavulana 740 sawa na asilimia 52.42 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2015 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI


>>bonyeza hapa kuona majina ya Waliochaguliwa kidato cha tano awamu ya pili 2016, Form Five Second Selection 2016 - TAMISEMI - New Update

Tumia link hii kupata matokeo : >> Waliochaguliwa kidato cha tano awamu ya pili 2016
Link ya Matokeo ya awali : >> Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016
Share:

Rais Magufuli amuapisha Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  tarehe 01 Septemba, 2016 amemuapisha Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 
Bw. Doto M. James aliteuliwa kushika wadhifa huo jana tarehe 31 Agosti, 2016 na amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Servacius Likwelile ambaye atapangiwa kazi nyingine.
 
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).
 
Hafla ya kuapishwa kwa Bw. Doto M. James imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
 
Aidha, Bw. Doto M. James amekula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma, zoezi ambalo limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.

 Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es salaam
01 Septemba, 2016
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger