INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Thursday, 26 May 2016
Wednesday, 25 May 2016
Rais Magufuli amteua Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria(OUT)
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,IKULU Dar es salaam
25 Mei, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,IKULU Dar es salaam
25 Mei, 2016
Breaking News : Serikali yavunja Bodi ya TCU,yawasimamisha kazi vigogo
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Prof. Joyce Ndalichako amevunja Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini Tanzania(TCU ) kufuatia Tume hiyo kupitisha majina ya wanafunzi 486 wasio na sifa kusomea Shahada ya Elimu.
Pia,Waziri Ndalichako amewasimamisha kazi Maafisa kadhaa waandamizi wa TCU kwa kushindwa kusimamia na kutekeleza vyema wajibu wa TCU. Waziri Ndalichako amewateua Makaimu wa nafasi za waliosimamishwa.
Sababu kuu ni kupitisha majina 486 ya wanafunzi wasio na sifa, kusoma ST JOSEPH UNIVERSITY.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Prof. Joyce Ndalichako amevunja Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini Tanzania(TCU ) kufuatia Tume hiyo kupitisha majina ya wanafunzi 486 wasio na sifa kusomea Shahada ya Elimu.
Pia,Waziri Ndalichako amewasimamisha kazi Maafisa kadhaa waandamizi wa TCU kwa kushindwa kusimamia na kutekeleza vyema wajibu wa TCU. Waziri Ndalichako amewateua Makaimu wa nafasi za waliosimamishwa.
Sababu kuu ni kupitisha majina 486 ya wanafunzi wasio na sifa, kusoma ST JOSEPH UNIVERSITY.
Mkoa wa Mwanza Unategemea Kupokea Tani 500 za Sukari
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mkoa wa Mwanza unategemea
kupokea Tani 500 za Sukari zitakazo ingia katika mkoa huu zikitokea
kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar tarehe 24, Mei, 2016, ambazo
zinaingizwa mkoani hapo na muagizaji na Msambazaji P.H Shah.
Hata
hivyo mkuu wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na bei
elekezi kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja nakufikishwa
katika vyombo vya dola.
Mongella
amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari
wametoa maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la
sukari na kwamba wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie
maelekezo bila kuvunja utaratibu utakao wekwa.
Mahitaji
ya sukari katika mkoa wa Mwanza ni Tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi ya
kawaida kwa wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 itasaidia
kupunguza uhaba wa sukari unao ukabili mkoa huu kwa sasa..
Hata
hivyo mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema,
tayari viwanda vya hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na
kwamba muda si mrefu tatizo la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.
Imetolewa na Atley J. Kuni
Afisa habari na Mahusiano, Ofisi ya mkuu wa Mkoa
MWANZA -24, Mei 2016
Waziri Mkuu: Serikali Kuiuzia Umeme Zambia
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya
umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la
umeme linaloikabili nchi hiyo.
“Serikali
ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka Iringa –
Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme
unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.
Amesema
upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya
umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta
fedha kwa ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa
ya Zambia.
Waziri
Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk.
John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo jana mchana (Jumanne, Mei 24,
2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali
uliohusu Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano
cha kimataifa wa Mulungushi.
Alisema
ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za bara
hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na
wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu
kulikamilisha kila nchi peke yake.
Alisema
ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania inafanyia
marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo.
Akizungumzia
kuhusu hali ya nishati Tanzania, Waziri Mkuu alisema Tanzania
imebarikiwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 57.25
(tcf), makaa ya mawe yenye uhjazo wa tani bilioni 1.9 (asilimia 25
imevumbuliwa), umeme wa nguvu ya maji wa gigawati 4.7 ambazo ni asilimia
12 tu ndiyo inatumika. Pia alisema Tanzania ina deposits za urani yenye
ujazo wa ratili milioni 200 (200 million pounds), joto la ardhini
(geothermal) linaloweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 5,000.
“Hivyo ni mbali na vyanzo vya umeme utokanao ua upepo na jua,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu alisema Tanzania
kupitia REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye asilimia 52 ya vijiji
vyote na inatarajia kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.
Akishiriki
mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara
la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli
linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.
“Hatuwezi
kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua
peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka
mitambo,” alisema.
Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário
Akishiriki
mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara
la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli
linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.
“Hatuwezi
kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua
peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka
mitambo,” alisema.
Naye
Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema
masuala ya nishati yanahitaji uwekezaji mkubwa kwa hiyo akashauri
makampuni kuungana kwenye uwekezaji na kuibua miradi ambayo ina tija
(feasible and viable).
Waziri
Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji,
wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.
14 Wakamatwa Mauaji ya watu Watatu Msikitini Jijini Mwanza
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Jeshi
la Polisi Nchini linawashikilia watuhumiwa 14 kufuatia tukio la mauaji
ya watu watatu lililotokea katika msikiti wa Rahman eneo la Ibanda
relini mkaoni Mwanza, Mei 18 mwaka huu.
Akiongea
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la
Polisi nchini Kamishna Msaidizi Advera Bulimba alisema kuwa msako wa
kuwakamata watuhumiwa wengine unaendelea katika maeneo mbalimbali
nchini.
Hivyo
amewaomba wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi hilo ili
kufanikisha kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.
“Nitoe
wito kwa wananchi kushirikiana kikamilifu na vyombo vya usalama katika
kufichua wahalifu kwa kuwa ni watu tunaoishi nao, hivyo hakuna budi
kutoa taarifa zao ili usalama na mali zetu uendelee kuimarika”, aliongeza Kamishna Msaidizi Bulimba.
Hata
hivyo, alieleza kuwa hali ya usalama nchini iko shwari na kuwatoa hofu
wananchi kwamba jeshi hilo limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha
hali ya usalama inaendelea kuwepo.
“Niwaombe
wananchi kuondoa hofu juu ya hali ya usalama na wasiwasi na watoe
ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kuhakikisha kwamba wote
wanaojihusisha na uhalifu wanakamatwa haraka”, alisema Kamishna Msaidizi Bulimba.
Aliongeza
kuwa uchunguzi zaidi wa matukio ya uhalifu nchini unaendelea ikiwemo
matukio ya mkoani Tanga, Dar es Salaam na mikoa mingine ili kubaini na
kuwakamata wahusika na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Hivi
karibuni kumeripotia matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani katika
mikoa mbalimbali ikiwemo mauaji ya watu watatu waliouawa wakiwa
msikitini jijini Mwanza.
Wamiliki wa silaha watakiwa kuhakiki silaha zao kabla ya Juni 30
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Jeshi
la Polisi nchini limetoa wito kwa wamiliki wa silahi kujitokeza na
kuhakiki silaha zao katika Wilaya wanazoishi kabla ya kumalizika kwa
zoezi hilo mnamo Juni 30 mwaka huu.
Hayo
yalisemwa na Msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Advera Bulimba
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
“Serikali
imetoa muda wa miezi mitatu kukamilisha zoezi hili muhimu na tayari
miezi miwili imepita hivyo wale ambao bado hawajahakiki silaha zao
kuzikakiki sasa kabla ya Juni 30 ili kuepukana na usumbufu” alisema
Kamshna Msaidizi Bulimba na kuongeza kuwa:
“Natoa
wito kwa watu wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria kusalimisha
silaha hizo katika vituo vya polisi, ofisi za serikali na kwenye nyumba
za ibada na watakaofanya hivyo ndani ya muda ulipangwa hawatachukuliwa
hatua zozote za kisheria”.
Aliongeza
kuwa baada ya muda ulipangwa na Serikali kupita na wamiliki
hawajahakiki silaha zao Jeshi la Polisi nchini litaendesha operesheni
kali kuwakamata wale ambao hawakujitokeza katika zoezi la uhakiki na
hatua kali zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa leseni na silaha zao
kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Aliwaomba
ndugu wa wale walikuwa wakimiliki silaha ambao wamefariki au ni
wagonjwa wasalimishe silaha hizo katika vituo vya Polisi kwa niaba ya
ndugu zao ndani ya kipindi cha uhakiki wa silaha.
Zoezi
la uhakiki wa silaha lilianza Machi 21 mwaka huu kufuatana na sheria ya
usimamizi wa silaha na risasi ya mwaka 2015, ambapo kifungu cha 66 cha
sheria hiyo kinamtaka kila mmiliki kuhakiki kumbukumbu za silaha yake au
risasi pale anapoamriwa na mamlaka.
Lengo
la kuhakiki kumbukumbu za wamiliki wa silaha ni kupata taarifa sahihi
za wamiliki hao zitakazosaidia kubaini wale wote wanaomiliki kinyume na
sheria, kuwafahamu wamiliki waliohama na kuhamia makazi mapya,
kuwafahamu wamiliki waliofariki ili kuzuia vitendo vya uhalifu na
uvunjwaji wa amani nchini.
Tuesday, 24 May 2016
MPYA:AJIRA ZA KILIMO SERIKALINI KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA SUA DIGRII ZIFUATAZO,DEADLINE KESHO
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
1.BLS
2.FORESTRY
3.AFISA NYUKI
4.MFUGAJI NYUKI
1.BLS
2.FORESTRY
3.AFISA NYUKI
4.MFUGAJI NYUKI
FUNDI SANIFU MAABARA MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY LABORATORY TECHNICIAN II)- - 5 POSTEmployer: MDAs & LGAs |
2016-05-25 Login to Apply |
|
000663 | AFISA MISITU DARAJA LA II (FORESTRY OFFICER GRADE II)- - 4 POSTEmployer: MDAs & LGAs |
2016-05-25 Login to Apply |
000667 | AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER II) - 5 POSTEmployer: MDAs & LGAs |
2016-05-25 Login to Apply |
000670 | MFUGAJI NYUKI MSAIDIZI DARAJI LA II- - 5 POSTEmployer: MDAs & LGAs |
2016-05-25 Login to Apply |