Wednesday, 11 May 2016

Rais Magufuli: Huyu Shetani Aliyetulaani Watanzania kwanini Asife? Hivi Hatuhurumii hata Kidogo?

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) limetakiwa kuingia ubia na kampuni za madini nchini ili kutengeneza ajira kwa vijana wa Kitanzania ambao wengi wao wako vijiweni.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Rais John Magufuli wakati akizindua majengo ya mifuko ya pensheni ya NSSF na PPF yaliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 60 yaliyojengwa jijini hapa.

Rais Magufuli alisema wakati umefika kwa NSSF kujikita katika biashara ya kupata faida kwa haraka kama vile ya madini ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kukata madini hayo na kusanifu ili vijana wafundishwe na hatimaye kuajiriwa katika viwanda hivyo.

Alisema suala la Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa kuuza madini ya tanzanite wakati madini hayo yanapatikana hapa hapa tu na kuziacha nchi za India na Kenya zikiongoza, ni suala la kushangaza sana.

Alisema NSSF sasa inapaswa kujipanga na kuingia katika biashara ya madini hususan tanzanite kwa kuingia ubia na kampuni kama hiyo ya Signature inayomilikiwa na mzawa Sailesh Pandit ili ifanye biashara na wanachama wa mfuko huo wapate faida haraka haraka na kuachana na uwekezaji wa majengo.

"Siku nyingine hakuna ubaya hata NSSF mkawa ndio wawekezaji wakubwa wa Tanzanite mkawa mnanunua Tanzanite kutoka kwa vijana hawa badala ya kuwa inavushwa mpaka Kenya na kwenda Kenya, badala ya Tanzania kuwa ya kwanza kuuza Tanzanite duniani inajitokeza India alafu inafata Kenya

"Unajua saa nyingine watu wanatuona Watanzania sijui tukoje,
huyu shetani aliyetulaani sisi Watanzania kwanini asife? hata hatuhurumii kidogo? basi kama ni kuswali na kusali tusali sana ili tubadilike, tuthamini mali yetu kwa ajili ya vizazi vyetu." Alisema RAais Magufuli

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema kampuni ya madini ya Signature iliyopanga katika jengo la mfuko huo la Mafao House imeajiri vijana zaidi ya 47 wa kuchonga tanzanite na watashirikiana katika kuanza biashara hiyo.

Profesa Kahyarara alisema kauli ya Rais ya shirika hilo kujikitaka katika biashara ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kuchonga madini hayo wataifanyia kazi haraka iwezekanavyo bila ya wasiwasi wowote.

Hata hivyo, serikali ilishapiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi na kutaka madini yote kuchongwa nchini na wazawa kuanzisha viwanda vya kuchonga madini hayo.
Share:

Mambo Ambayo Wanaume Wanakosea Wakati wa Kutongoza Mwanamke

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
1.PAPARA
Wanaume wengi tumekuwa na haraka sana tunapokuwa tukitaka kuaproach hali inayomfanya mwanamke akuwekee ugumu.mfano umekutana na dada mzuri mmesalimiana hapo hapo unamuomba namba yake.mjomba hata akikupa ujue utasumbuka sana kumpata coz atakufikiria sana juu ya uharaka wako.

2.KUJIFAKE
Wanaume wengi tumekuwa tukijipandisha au kujionyesha tofauti na hali zetu.ukiwa unaaproach jaribu kuwa real.huwezi kumwambia mdada unafanya kazi benki afu uko na techno

3.KUTOSOMA MOOD YA MWANAMKE
unapomuaproach mwanamke lazma usome mood yake coz sometime unaweza kutoswa coz hujamsoma mwanamke unamtongozaje mwanamke asubuhi?

4.KUMPONDA UR EX LOVER
Mwanamke anakuuliza kwanini uko single,unaanza kumponda ex wako kwa maneno ya kashfa hali kama hii inaweza kumtisha kisaikolojia umtongozae.

5.KULALAMIKA
Unamtongoza mwanamke huku unalalamika juu ya mapenzi oooh mara sijawahi kupendwa mjomba hapo unaonyesha udhaifu wako.

UKITULIA NA KUMTONGOZA MWANAMKE BILA KUYATENDA HAYA MBONA UTAMPATA KILA UMTAKAE
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MAY TAREHE 11.5.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Tuesday, 10 May 2016

SUKARI:KILO 622,000 ZAKAMATWA MOROGORO,RC DODOMA AAGIZA TANI 154 ZIUZWE KWA WANANCHI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Suala la uhaba bandia wa sukari limeendelea kuitikisa nchi, lakini vyombo vya ulinzi na usalama vikifanya kazi nzuri baada ya kuwatia nguvuni wafanyabiashara wengine, waliohodhi bidhaa hiyo kinyume cha sheria huku ikiwamo kukamata kilo 622,000 za mfanyabiashara Haruni Zakaria mkoani Morogoro.

Mwishoni mwa wiki, mfanyabiashara huyo anayemiliki Kampuni ya Al Naeem, alikutwa akiwa ‘ameficha’ tani 4,579.2 za bidhaa hiyo katika maghala yake yaliyoko Tabata, Dar es Salaam. 
Kwa mujibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), wachunguzi wa taasisi hiyo na wa Jeshi la Polisi, walifanya ukachero wao katika maghala ya kampuni hiyo yaliyopo Mbagala na Tabata, Mei 5, mwaka huu.

Lakini siku chache baada ya kunasa sukari hiyo, kikosi kazi cha Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoa wa Morogoro kilichoundwa na Mkuu wa Mkoa huo, Dk Kebwe Steven Kebwe kufuatilia wafanyabiashara walioficha sukari, kimebaini kiasi cha kilo 622,000 za sukari zilizofichwa katika maghala mbalimbali yaliyomo mkoani humo. 
Dk Kebwe amemwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei kuweka ulinzi kwenye maghala hayo yaliyokutwa yameficha sukari hiyo na kuhakikisha inauzwa kwa bei elekezi, iliyowekwa na serikali kwa wananchi.

Pia alimwagiza kuwafikisha wafanyabiashara walioficha sukari hiyo mahakamani mara moja na kumsaka mfanyabiashara Sadick Yassin ambaye alifunga duka lake wakati wa ukaguzi na kutokomea kusipojulikana.

Mali ya Zakaria wa Dar
Akizungumza jana, Dk Kebwe alisema sukari hiyo imebainika kuwa ni mali ya mfanyabiashara mmiliki wa Kampuni ya Al Naeem Enterprises na kuhifadhiwa katika maghala mbalimbali ya Kiwanda cha Sukari Kilombero (K1) tani 429, Kiwanda cha Sukari Kilombero (K2) tani 135 na katika Manispaa ya Morogoro tani 58.4, jumla kuwa ni tani 622.4

“Nimeunda kikosi kazi cha kufuatilia wafanyabiashara walioficha sukari katika maghala yao katika ukaguzi wa awali, jumla ya tani 622.4 za sukari zimebainika kwenye maghala mbalimbali na sukari yote iliyobainika ni mali ya Al-Naeem Enterprises na tayari maghala hayo yenye sukari yapo chini ya ulinzi wa vyombo vya dola,” alisema.

Licha ya kumwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa kuweka ulinzi katika maghala hayo na kusimamia sukari hiyo inauzwa kwa bei elekezi ya serikali, pia alimwagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakiki iwapo sukari hiyo imelipiwa kodi ya serikali.

Dk Kebwe pia aliwataka wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani humo, kutoa taarifa za wafanyabiashara au watu walioficha sukari ili hatua zichukuliwe mara moja dhidi yao. 
Kabla ya kuweka msimamo wa Serikali ya Mkoa dhidi ya wafanyabiashara dhalimu, Dk Kebwe na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa walifanya ziara ya kushtukiza ya kuhakiki upya maghala ya wafanyabiashara wa maduka ya jumla katika Manispaa ya Morogoro.

Katika ghala la Kampuni ya Sukari Kilombero lililipo mjini Morogoro lilikuwa na tani 58.4 za sukari ambayo ni mali ya Al Naeem Enterprises.
Msimamizi wa ghala hilo, Robert Charles alimfahamisha Mkuu wa Mkoa na timu yake kuwa sukari hiyo ipo kwa muda wa mwezi mmoja sasa baada ya kununuliwa na mfanyabiashara huyo kutoka kiwandani Kilombero.

Alisema sukari tani 58.4 iliyokutwa ndani ya ghala hilo ni mali ya mfanyabiashara Zakaria aliyeinunua kutoka kiwandani Kilombero na kuihifadhi hapo akisubiri kusafirishwa na kuwauzia wanunuzi wa jumla. 
Baadhi ya wauzaji wa maduka ya jumla waliokaguliwa na timu ya Mkuu wa Mkoa, Thabit Islam na Hassan Binzoo walisema hali ya upatikanaji wa sukari katika kipindi hiki ni mgumu kutokana na kuadimika ghafla.

Dar yanaswa nyingine
Katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, zimekamatwa tani 2,700 za sukari zikiwa zimefichwa katika ghala moja eneo la Mbagala. 
Akitoa taarifa hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana, Paul Makonda, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Photidas Kagimbo alisema sukari hiyo imekamatwa baada ya Rais kutoa agizo la kuwabaini wale wote walioficha sukari na kusababisha wananchi kuteseka kupata bidhaa hiyo.

Kagimbo alisema licha ya kukamatwa kwa sukari hiyo Manispaa hiyo bado inaendelea na msako ili kuwabaini na wafanyabiashara wengine waliohodhi bidhaa hiyo.

Msako mkali Kahama
Wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Polisi imefanya upekuzi katika baadhi ya maghala ya kuhifadhia sukari na kuwabaini baadhi ya wafanyabiashara wanne wanaojihusisha na kazi hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Michael Nyange alisema wamefanya ukaguzi katika maghala ya wafanyabiashara wakubwa wa sukari, ambayo ni ya wafanyabiashara John Hango (walikuta mifuko miwili ya kilo 50), Nyorobi Kisabu (hakuna kilichokutwa), Mshaka Kaziro (hakuna kilichopatikana) na Alex Magina (mifuko 40, yenye kilo 50 kila mfuko). Alisema kazi hiyo itakuwa endelevu.

RC Dodoma aagiza iuzwe
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ameagiza tani 154 kuuzwa kwa wananchi kwa bei elekezi, huku akiwataka wafanyabiashara ambao bado wameficha sukari kuitoa mara moja kabla rungu halijawashukia.

Takukuru kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani hapa walikamata na kuzifungia tani 154 za sukari katika ghala la mfanyabiashara Haidary Gulamali na sasa Rugimbana ametoa agizo la kufunguliwa kwa ghala hilo ili litoe huduma kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa akiwa amefuatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa alisema wameamua kufungua ghala na kuanza kutoa huduma kwa wananchi ambao wanauhitaji mkubwa kwa sasa wa sukari.
Share:

PATA HABARI FASTER KUPITIA SIMU YAKO KUHUSU AJIRA ZA UALIMU 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari zenu,
Je wewe ni mwalimu unaesubilia ajira za ualimu mwaka huu wa 2016 ,basi MASWAYETU BLOG TEAM tunakuletea huduma ya watsup bure itakayokuwa inakupa taarifa kuhusu ajira za walimu faster na kwa wakati sahihi.
ili uweze kupata habari kwa njia ya watsup ,fanya yafuatayo,
1.save hii namba 0652740927 (MASWAYETU BLOG)
2.nitext watsup kwa jina lako mfano.John-UPDATES KUHUSU AJIRA ZA UALIMU
3.nitakuunganisha kwenye huduma hii mara moja na utapokea updaes zote kuhusu ajira za ualimu na habari
   mbalimbali.


NOTE;USISAHAU KUISAVE ,KWA USIPOSAVE TAARIFA HAZITAKUFIKIA,MWAMBIE NA
            RAFIKIA AKO.



IMETOLEWA NA UONGOZI WA MASWAYETU BLOG TEAM
Share:

MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO ULIOFANYIKA TAREHE 7 MEI 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

MUHIMU
Wasailiwa wote waliochaguliwa kuendelea na usaili wanatakiwa kufika katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira zilizopo maktaba complex, Barabara ya Bibi Titi Mohamed saa moja asubuhi siku iliyoonyeshwa kwenye matokeo wakiwa na vyeti vyao halisi (original certificates).
KADA:  SUPPLIES OFFICER GRADE II 
MWAJIRI:  THE TANZANIA BUILDINGS AGENCY (TBA)
EXAMINATION NUMBER MARKS REMARKS
SUPPLIES OFF II - 0395 72 SELECTED FOR INTERVIEW ON 9 MAY 2016
SUPPLIES OFF II - 0438 70 SELECTED FOR INTERVIEW ON 9 MAY 2016
SUPPLIES OFF II - 0373 68 SELECTED FOR INTERVIEW ON 9 MAY 2016
Read more...
 
Share:

NAFASI ZA MASOMO VYUO VYA UVUVI TANZANIA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA 2016/2017

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


WAKALA WA ELIMU NA MAFUNZO YA UVUVI - FETA
             S. L. P.  83, BAGAMOYO. TANZANIA

UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) unatangaza kozi zifuatazo kwa ngazi ya Certificate na Diploma
KAMPASI YA MBEGANI - BAGAMOYO
1.   Uvuvi na Ubaharia  (Masterfisherman)
2.    Uchakataji Samaki, Udhibiti wa Ubora na Masoko (Fish Processing, Quality Assurance and Marketing)
3.    Menejiment ya Mazingira na Rasilimali za Pwani
(Environment and Coastal Resources Management)
4.    Uhandisi Mitambo Baharini (Marine Engineering)
5.    Ufugaji Samaki (Aquaculture)
KAMPASI YA NYEZI MWANZA
1.    Menejimenti na Tekinolojia ya Uvuvi (Fisheries Management and Technology)
2.   Sayansi na Tekinolojia ya Uvuvi (Fisheries Science and Technology)
3.   Ufugaji Viumbe Kwenye Maji (Aquaculture)
KAMPASI YA KIGOMA
1.   Ufugaji Viumbe Kwenye Maji (Aquaculture)
KAMPASI YA GABIMORI
1.    Ufugaji viumbe kwenye maji
Kozi Zote za Certificate ni kwa Mwaka Mmoja, na Diploma ni Miaka Miwili.
Sifa za Jumla kwa Waombaji wa Kozi za Stashahadi ni Walau Principla Pass Moja na Subsijary Pass Moja kwa waliomaliza kidato cha sita au Aliyehitimu Cheti Katika Ngazi ya Astashahada (NTA Level IV)
Sifa za Ujumla Kwa Waombaji wa Kozi za Astashahada ni Walau Pass Kwa Kiwango cha D Nne Katika Mchangajiko Wowote wa Masomo, Waombaji Wenye Kiwango cha Pass Katika Masomo ya Sayansi Watapewa Kipaumbele
Maombi yatumwe kupitia mfumo wa uombaji wa pamoja (Central Admission System) wa NACTE www.nacte.go.tz Pia fomu za maombi zinapatikana kwenye kampasi zote za FETA na kwenye tovuti Tovuti ya Wakala www.feta.ac.tz au www.anfts.org au tembelea Kampasi Yoyote Iliyo Karibu Nawe na Pia kwa Maofisa Uvuvi wa Wilaya.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na;
Mtendaji Mkuu,
Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi – FETA
S. L. P. 83
Bagamoyo.


AU

Piga simu; 0732 -928166


IMETOLEWA NA OFISI YA MTENDAJI MKUU – FETA MAKAO MAKUU

 
Share:

New AUDIO | Shilole Ft. Barnaba Classic - Say My Name | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
DOWNLOAD via MKITO
https://mkito.com/song?idx=11439&referrer=b0c32f4ffb36e425688f50f13bf0b685ec77d943
Share:

VIDEO:Mr. Nay TRUE BOY - Saka Hela

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

https://youtu.be/_xPahWe8BvY
Share:

New AUDIO | Mr. Nay TRUE BOY - Saka Hela | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

DOWNLOAD via HULKSHARE
http://old.hulkshare.com/dl/kb152qefzhts/Mr._Nay_-_Saka_Hela.mp3?d=1
Share:

Kigwangalla Amtaka Gardner Aombe Radhi kwa Kumdhalilisha Lady Jaydee

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla, amemtaka mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G Habash kumuomba radhi aliyekuwa mke wake, Lady Jaydee kwa ‘kile alichokiita’ kama udhalilishaji kwake na kwa wanawake wote.

Wikiendi iliyoisha imesambaa video mtandaoni ikimuonesha mtangazaji huyo akiongea kwenye tamasha alilokuwa mshereheshaji: "My name is Captain Gardner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana. Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi.”

Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Jaydee na watu wengi kwa ujumla.

“Ndg. Gardner amefanya udhalilishaji mkubwa si tu Kwa @JideJaydee bali ametukana wanawake wote. Mimi #BaloziWaWanawake namtaka aombe radhi,” ameandika mheshimiwa Kigwangalla kwenye Twitter.

“Natoa rai kwa uongozi wa @cloudsfm kumtaka Ndg. Gardner afute kauli yake na aombe radhi kwa @JideJaydee na kwa umma ili kulinda heshima yao,” ameongeza.

“Jamani, sijui ugomvi wao wala sina interest ya kujua, sema alichokisema G na nikasikia ni katika tusiyosemaga hadharani kwa heshima ya mama,” amefafanua.

“Sina maana wamchukulie hatua. Watambue tu kosa lake na wamtake kwa heshima kwa mama aombe radhi. Mimi ni mtumishi namba 2 kwenye Wizara inayosimamia ‘mambo ya wanawake’! I know what I am talking about hapa.”

==>Video Hii Hapa

Share:

SUMATRA Yatangaza Nauli Za Usafiri Wa Mabasi Yaendayo Haraka.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Hatimaye  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetangaza nauli zitakazo tumika kwa mabasi yaendayo kasi kuwa ni 400, 650 na 800 kwa safari za Mbezi mwisho hadi Kivukoni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Giliard Ngewe amesema nauli kutoka Mbezi mwisho hadi Kimara Sh400, na nauli ya Sh650 itatumika maeneo ya  Kimara  kwenda  Kivukoni, Kimara –Kariakoo, Kimara – Morocco, Kariakoo - Kivukoni.

Amesema nauli ya Sh800 ni Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho.

“Chombo chochote cha usafiri hakitaruhusiwa kutumia barabara za mwendo kasi kuanzia kesho, watakao kiuka agizo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni za biashara zao” amesema.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu nauli zitakazotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka unaotarajiwa kuanza rasmi Mei 10, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi kutoka SUMATRA Bw. Nahson Sigala.
Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Nahson Sigala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu viwango vipya vya nauli baada ya SUMATRA kufanya tathmini ya viwango vya nauli iliyopendekezwa awali na Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT na kubaini kuwa gharama zilizopendekezwa ni kubwa mno. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe (Kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu DART Bw. Ronald Lwakatare wakimkabidhi leseni ya usafirishaji Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Katikati)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe baada ya kupokea leseni ya usafirishaji kutoka SUMATRA.
Share:

Songas Yazima Mitambo Yao kwa Kuidai Tanesco Sh Blioni 194

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Kampuni ya kufua umeme kwa njia ya gesi asilia, Songas Limited imezima mitambo yake, baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kushindwa kulipa deni la Dola 90 milioni za Marekani sawa na Sh193.5 bilioni, jambo linalotishia ukosefu wa nishati hiyo muhimu nchini.

Hata hivyo, Tanesco imepinga uamuzi huo na kueleza kuwa ni vitisho kwa wananchi na inakiuka vifungu namba 4.4 , 4.6 na 17 vya mkataba ulioingiwa na Songas. 

Mkurugenzi Mkuu wa Songas, Nigel Whittaker alisema jana kuwa wameamua kuchukua hatua ya kuzima mitambo hiyo baada ya kuzidiwa na gharama za uendeshaji kutokana na deni hilo.

“Mtambo huo uliopo Ubungo unazalisha Megawati 189, tumefikia hatua ya kuzima kidogo kidogo kuanzia Aprili 29 mwaka huu kutokana na deni hilo, Tanesco imekuwa ikisuasua katika kulipa,” alisema Whittaker.

Alisisitiza kuwa mradi huo wa Songas, ulioanzishwa tangu mwaka 2004 , ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania na umekuwa ukizalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kutoka Songosongo na kuuingiza katika gridi ya taifa.

Whittaker alieleza kuwa kiasi cha umeme wanaozalisha ni takriban asilimia 20 ya nishati inayozalishwa nchini.

“Ilikuwa tuifunge mitambo hii tangu mwaka jana, lakini Serikali ilituomba tuendelee wakati ikisimamia hatua ya kulipwa, tunaendelea lakini hatimaye tumekwama kwa kuwa kuna mahitaji ya msingi ambayo yanategemea fedha ikiwamo matengenezo ya mitambo hiyo,”alisema.

Alisema pia wamejikuta katika hali ngumu kwa kudaiwa na taasisi kadhaa za Serikali ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), na Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC), hivyo wanaendelea kujadiliana na Tanesco na Serikali ili kuangalia jinsi ya kushughulikia jambo hilo kwa kutambua umuhimu wa mradi huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba, alisema Songas wamevunja makubaliano ya mkataba hususan kifungu cha 4.4 ambacho kinaitaka Songas kutoa siku 90 ya kuwa na majadiliano.

Aliwatoa wananchi hofu kwa nchi haitaingia gizani kwa kuwa licha ya Songas kutangaza kuzima kabisa mitambo yote Mei 11.

"Tayari walikwisha kuwa wameanza kuizima na haututokea mgawo. Ingawa ni kweli wanatudai, lakini siwezi kusema kiasi gani nami nitakuwa nimekiuka huo mkataba, kwa hili walilofanya tutachukua hatua hatukubaliani nao,” alisema.

Songas ambao taarifa ya hivi karibuni ya Serikali inaonyesha kuwa wanauzia umeme Tanesco kwa senti za 2.4 za Marekani kwa uniti, wanalipwa capacity charge ya Dola za Marekani 5.2 milioni kwa mwezi ambazo ni sawa na wastani wa Sh11.4 bilioni.

Kulingana na hesabu hizo, kila mwaka kampuni hiyo inalipwa Sh136.9 bilioni tangu 2001 walivyoingia mkataba na Tanesco.

Mahitaji makubwa ya umeme Tanzania mara ya mwisho yalirekodiwa kuwa megawati 898.5.
Share:

Makonda Awasimamisha Kazi Vigogo wawili wa Manispaa Kwa Tuhuma za Kushindwa kutoa Maelezo kuhusu Watumishi Hewa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewasimamisha kazi wakuu wawili wa idara katika manispaa mbili kwa tuhuma za kushindwa kutoa maelezo kuhusu watumishi hewa katika idara zao, huku wakiendelea kuidhinisha mishahara yao kwa miaka mingi.

Makonda aliwataja watumishi hao waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkuu wa Idara ya Utumishi wa Manispaa ya Ilala, Francis Kilawe na Mkuu wa Idara ya Afya Temeke, Syrivia Mamkwe na kuagiza uchunguzi dhidi ya tuhuma zao ufanyike haraka.

Kiongozi huyo alichukua uamuzi huo baada ya hivi karibuni kuwaapisha wakuu wa idara kutoka manispaa tatu ili kusema ukweli na kuwapa wiki moja kuhakiki watumishi hewa katika maeneo yao ya kazi.

Makonda alisema hadi kufikia jana, jumla ya watumishi hewa 39 waligundulika na kufikisha 248 kutoka 209 wa takwimu za awali. 
Kati yao, 26 wanatoka Ilala, wawili (Kinondoni) na 11 (Temeke) na kulisababishia jiji hilo kupata hasara ya zaidi Sh3 bilioni.

“Kilawe ameshindwa kujieleza kuhusu watumishi hewa 11 ambao hajui wako wapi, lakini wanapokea mishahara tangu mwaka 2010.Huku yeye akisaini mishahara yao,” alisema Makonda.

Makonda ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliongeza kuwa Mamkwe alishindwa kujieleza walipo watumishi hewa wawili ambao bado wanaendelea kupata mishahara huku akiwa kiongozi wa idara husika.

Kutokana na hali hiyo, Makonda amewaongezea wiki mbili maofisa wanaochunguza suala hilo ili kuwabaini zaidi watumishi hewa kwa madai kuwa bado wanaonekana katika mfumo wa kupokea malipo kutoka Hazina kwenda katika manispaa. 
“Huu ndiyo mkutano wangu wa mwisho kwenu.Wiki hizi mbili zikiisha tutaanza uchunguzi dhidi yenu na tukibaini watumishi hewa katika idara yako utawajibishwa ,” alisema Makonda ambaye pia ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger