TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la
Kujenga Taifa linakanusha taarifa zinazosambazwa kupitia ujumbe mfupi wa
maandishi kwenye simu za kiganjani na baadhi ya mitandao ya kijamii
kuwa “Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ametoa nafasi maalum kwa
wahitimu wa taaluma ya Uandishi wa Habari wenye elimu ya stashahada na
shahada wanaopenda kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea”.
Habari
hizo siyo sahihi kwani mchakato wa nafasi zote za vijana wanaotaka
kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Kujitolea zimepelekwa
kwenye mamlaka za Serikali za mikoa yote, ambapo kwa sasa zoezi hilo
linaendelea katika ngazi za wilaya.
Aidha
Makao Makuu ya JKT yanaendelea kusisitiza kuwa hayapokei na wala
hayatapokea maombi yoyote ya kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea
kwa mwaka 2016.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 02 Mei 2016