Saturday, 2 April 2016
MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WATANZANIA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JESHI LA MAGEREZA 2016
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TANGAZO LA KUITWA CHUONI
2.Picha (Passport size) za rangi 5 za hivi karibuni.
3.Chandarua cheupe cha duara ft 31/2, shuka nyeupe mbili, mto wenye foronya nyeupe zisizo na maua/maandishi.
4.Fedha taslimu Tshs.90,000/=.
5.Kalamu za wino, za risasi na madaftari ya kutosha.
6.Cheti cha afya kutoka kwa hospitali ya Serikali.
7.Nguo za kiraia za kutosha sweta, raba (Brown au nyeusi) na soksi
8.Kwa wale wenye kadi za Bima waje nazo na
9.Kila mwanafunzi atajitegemea kwa nauli ya kwenda.
<<<<<<<<BONYEZA HAPA KUONA MAJINA YOTE>>>>>>
<<<<<<BONYEZA HAPA KWA MAJINA YA NYONGEZA>>>>
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Jeshi la Magereza)
(Jeshi la Magereza)
TANGAZO LA KUITWA CHUONI
Kamishna
Jenerali wa Magereza Tanzania Bara anawatangazia wafuatao kuwa
wamechaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza baada ya Usaili kufanyika
katika kambi mbalimbali za JKT. Usaili huu ulihusu vijana waliohitimu
Shahada ya Kwanza, Stashahada, Astashahada, Kidato cha Sita na Kidato
cha Nne.
Wahusika
wote wanatakiwa kuripoti katika Ofisi za Wakuu wa Magereza Mikoa mara
wapatapo taarifa hii tayari kwa safari ya kwenda Chuo cha Mafunzo ya
Awali kilichopo Kiwira Tukuyu Mkoani Mbeya.
Mafunzo
yanategemewa kuanza tarehe 12 Machi, 2016 hivyo mwisho wa kuripoti
chuoni ni tarehe 14 Machi, 2016. Yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa
tarehe iliyotamkwa kwenye tangazo hili hatapokelewa.
Wahusika wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
1.Walete vyeti halisi vya masomo na vya kuzaliwa, vikiwa na pamoja na nakala 5 za kila cheti.2.Picha (Passport size) za rangi 5 za hivi karibuni.
3.Chandarua cheupe cha duara ft 31/2, shuka nyeupe mbili, mto wenye foronya nyeupe zisizo na maua/maandishi.
4.Fedha taslimu Tshs.90,000/=.
5.Kalamu za wino, za risasi na madaftari ya kutosha.
6.Cheti cha afya kutoka kwa hospitali ya Serikali.
7.Nguo za kiraia za kutosha sweta, raba (Brown au nyeusi) na soksi
8.Kwa wale wenye kadi za Bima waje nazo na
9.Kila mwanafunzi atajitegemea kwa nauli ya kwenda.
Tangazo
hili linapatikana kwenye mbao za matangazo zilizopo Ofisi za Magereza,
tovuti ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.go.tz sanjari na blog ya
Magereza kwa anwani ya www.magereza.blogspot.com
Imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza.
SIGNED
Dr. J. A. Malewa - CP
Kny: KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
<<<<<<BONYEZA HAPA KWA MAJINA YA NYONGEZA>>>>
SERIKALI KUPITIA WIZARA YA AFYA KUAJIRI WATUMISHI WA AFYA (AJIRA ZA AFYA 2015/16) 10000
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Serikali kuajiri watumishi wa afya 10,000
Serikali inatarajia kuajiri watumishi 10,000 wa sekta ya afya katika
mwaka ujao wa fedha ili kukabiliana na upungufu wa wataalamu wa fani
hiyo nchini.
Hayo yalisema jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla wakati akizindua majengo yatakayotumika kufundishia wakunga na wauguzi yaliyokarabatiwa na Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU).
Dk Kigwangalla alisema Serikali ina upungufu wa asilimia 51 ya wakunga na wauguzi na ili kukabiliana nao, imeamua kuongeza idadi ya wanafunzi katika vyuo vya afya.
“Nakipongeza Chuo Kikuu Cha Aga Khan kwa kuzalisha wataalamu wa fani ya ukunga na uuguzi kwa ngazi ya shahada na bado Serikali inahitaji kuwa na vyuo vingi vya afya ili kupunguza tatizo la uhaba wa wataalamu wa afya,” alisema.
Awali, Makamu wa Rais na Ofisa Mkuu wa Fedha wa AKU, Al-Karim Haji alisema chuo hicho kimepatiwa Sh2.9 bilioni na Benki ya Ujerumani (KFW) kwa ajili ya kukarabati vyumba na majengo ya kufundishia watalaamu hao.
“Lengo letu ni kuongeza ubora wa watumishi wa fani ya ukunga na uuguzi kwa sababu hapa nchini tumebaini kuwa kuna upungufu mkubwa wa vifaa na vyuo vya kisasa vyenye ubora wa kufundisha,” alisema Haji.
Alisema kupitia uboreshaji huo, AKU itachukua wauguzi na wakunga ambao wako kazini na kuwafundisha mara mbili kwa wiki ili waongeze ujuzi na kuwawezesha kupata shahada kwa wale wenye stashahada.
“Katika kipindi cha miaka 10, Chuo Kikuu Cha Aga Khan kimefanikiwa kuwafundisha manesi zaidi ya 600 katika ngazi ya stashahada na shahada,” alisema Haji.
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dk Gerd Muller alisema walitoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini.
Katibu Mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk Richard Sezibera alikipongeza chuo hicho kwa kuboresha sekta hiyo na mchango wake unaonyesha namna wataalamu wa afya watakavyopata elimu bora ambayo inakidhi viwango vya kimataifa.

Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa Naye Afikishwa Mahakamani Leo Kwa Tuhuma Za Rushwa
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa amepandishwa kizimbani mahakama ya Kisutu leo akituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni 30 akiwa kwenye Kamati za Bunge.
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa amepandishwa kizimbani mahakama ya Kisutu leo akituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni 30 akiwa kwenye Kamati za Bunge.
Ndasaa
anakuwa mbunge wa nne wa CCM kupandishwa mahakamani kwa tuhuma
za rushwa baada Mbunge wa Mwibala, Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero
Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa
kupandishwa mahakamani jana kwa tuhuma za kuomba rushwa ya milioni 30
toka kwa mkurugenzi wa Gairo ili taarifa yake ipitishwe bila
kujadiliwa.
Bosi wa Zamani wa TRA na Wafanyakazi wa StanBic Benki Wafikishwa Mahakamani
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Aliyekuwa
Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Harry Kitilya na wenzake Shose Sinare na Sioi
Solomoni wamefikishwa mahakamani (Kisutu DSM) leo kwa mashitaka 8
ikiwemo tuhuma za kujipatia fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6,
mwezi Machi mwaka 2013, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic
kwenda serikalini.
Watuhumiwa hao wamekana makosa na kurudishwa rumande hadi April 8, 2016
Watuhumiwa hao wamekana makosa na kurudishwa rumande hadi April 8, 2016
TAKUKURU Kuwafikisha Mahakamani Kamishna Mkuu wa Zamani wa TRA na Wafanyakazi Wawili wa Stanibic Benki
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016
imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA),
Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na
Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na
Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham
Solomon.
Washtakiwa
wote wanashtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa
udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16
R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha
Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu
kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha
Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.
Mashtaka
hayo yalisomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mhe.
Hakimu Emirius Mchauro. Kwa upande wa Jamhuri kesi hii inasimamiwa na
Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali Herman Tibabyekomia,
Christopher Msigwa na Mwendesha Mastaka wa TAKUKURU Stanley Luoga.
Washtakiwa wanatetewa na Wakili wa Kujitegemea Ringo Tenga, Rosai
Mbwambo, Semo na Nyaisa.
Washitakiwa
wote watatu wamepelekwa rumande, wamekosa dhamana kwani Kifungu Na.
148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Kinazuia utoaji
wa dhamana kwa washtakiwa wa Utakatishaji wa fedha haramu. Kesi hii
itatajwa tena tarehe 8/4/2016.
IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU
1 APRIL, 2016.
Bakwata Wakabidhi Msaada wa Madawati 500 kwa Serikali
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
BARAZA
Kuu la Waislaam nchini (Bakwata) kwa kushirikiana na Shia wamekabidhi
msaada wa madawati 500 kwa serikali ili kusaidia upungufu wa madawati
katika shule za msingi na sekondari.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi madawati, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania,
Abubakar Bin Zuberi amesema kuwa katika msaada hawaangalii suala la dini
kinachoangaliwa ni watakaolia madawati hayo ni watanzania.
Mufti
Zuberi amesema kuwa wamechangia katika kusaidia serikali kauli mbiu ya
elimu bure katika kuweza kusaidia watanzania wapate elimu.
Amesema
kuwa wataendelea kushawishi waislaam katika kuendelea kuchangia elimu
ili watoto wapate elimu iliyo bora kwa kuwa serikali pekee yake haiwezi
kutatua changamoto zote za elimu.
Mwenyekiti
wa SHIA, Azim Dewj amesema kuwa amepeleka msaada huo katika bakwata
ikiwa ni kuonyesha umoja na jinsi ya kusaidia serikali katika upande wa
elimu.
Amesema
kuwa ataendelea kushawishi matajiri wenzake kuangalia namna
watakavyosaidia katika sekta ya elimu upande wa madawati kuwa kila mwaka
kuweza kuchangia madawati 1000.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi akizungumza kwa
niaba ya Waziri Mkuu amesema kuwa msaada wa madawati hayo ni mkubwa
kutokana na changamoto iliyopo mbele yao.
Amesema
kuwa idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza kuandikishwa umeongezeka
kutokana na mpango wa elimu bure hivyo serikali kupata madawati ni
jambo la furaha na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia madawati
kutokana na mahitaji kuwa makubwa.
Rais Magufuli Amteua Hilda Nkanda Kuwa Kamishna Wa Kazi
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bi. Hilda Nkanda Kabisa kuwa Kamishna wa kazi.
Kabla
ya Uteuzi huo, Bi. Hilda Nkanda Kabisa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi,
Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Bi. Hilda Nkanda Kabisa, anachukua nafasi iliyoachwa na Bw. Sauli Kinemela ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amemteua Prof. Siza D. Tumbo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha
Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC).
Kabla
ya Uteuzi huo, Prof. Siza Tumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Sokoine (SUA) aliyebobea katika masuala ya Uhandisi Mitambo
ya Kilimo.
Prof. Siza Tumbo anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Evarist Ng'wandu ambaye alistaafu kwa mujibu wa sheria.
Uteuzi huu wa watendaji wakuu wa taasisi za serikali umeanza tarehe 26 Machi, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
01 April, 2016
MSHAHARA WA RAIS MAGUFULI NI MILION 9,500,000/=
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli jana alimpigia simu mtangazaji wa kipindi cha Clouds360 cha CloudsTv, Hudson Kamoga baada ya kusikia watu wanazungumzia kuhusu mshahara wa Rais.

Rais alisema mshahara alioukuta na ambao analipwa ni milioni 9 na laki 5 (9,500,000) na wala sio milioni 30 kama wanavyodai wapinzani. Amelazimika kuyasema hayo wakati wa uchambuzi wa magazeti kupitia Clouds360.
Aliahidi akirudi kutoka likizo yupo tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake.
Gazeti la Nipashe toleo la jana lilikuwa na habari iliyowanukuu Tundu Lissu na Zitto Kabwe wakitaka Rais Magufuli ataje Mshahara wake na aweke wazi kama anakatwa kodi ili kuondoa sintofahamu iliyopo .

Friday, 1 April 2016
EWURA-TANESCO YASHUSHA BEI YA UMEME 2016
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza
kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.
Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa.
Bei mpya kwa watumiaji wadogo ni sh.100 kwa uniti, watumiaji wa kati ni sh.292 toka 298 ya zamani.Wafanyabiashara wadogo ni sh. 195 toka sh. 200 ya hapo awali.
Bei mpya kwa wafanyabiashara wa kati ni sh.157 toka sh. 159. Wanaonunua kwa wingi (bulk) ni sh. 152 toka sh. 156 ya hapo awali

TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WALIOHAMISHIWA UDOM KUTOKA ST.JOSEPH 2016
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
IMPORTANT ANNOUNCEMENT
TRANSFERRED STUDENTS FROM ST. JOSEPH UNIVERSITY TO THE
UNIVERSITY OF DODOMA
This is to inform all students transferred from St. Joseph University in Tanzania to The University of Dodoma that, they are required to report to their respective Colleges (College of Education and College of Natural and Mathematical Sciences) at the University of Dodoma on Saturday 9th April 2016. effectively from 8.00am to 6.00pm.
All students are required to pay tuition fees and direct costs for academic year 2015/2016. Students who will fail to comply with this notice will not be allowed to join the university. Payment must be made before students reporting to the University as follows:
Transferred Students from St. Joseph University to The University of Dodoma
TRANSFERRED STUDENTS FROM ST. JOSEPH UNIVERSITY TO THE
UNIVERSITY OF DODOMA
This is to inform all students transferred from St. Joseph University in Tanzania to The University of Dodoma that, they are required to report to their respective Colleges (College of Education and College of Natural and Mathematical Sciences) at the University of Dodoma on Saturday 9th April 2016. effectively from 8.00am to 6.00pm.
All students are required to pay tuition fees and direct costs for academic year 2015/2016. Students who will fail to comply with this notice will not be allowed to join the university. Payment must be made before students reporting to the University as follows:
Mkazi wa Mwananyamala Apandishwa Mahakamani Kwa Kutishia Kumuua Rais Magufuli Kwa Kujitoa Mhanga
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Kondakta wa daladala, Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala
Ujiji, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli kwa maneno.
Seif
alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana mchana na kusomewa shtaka
hilo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kenneth Sekwao.
Mshtakiwa
huyo alikana shtaka hilo na Hakimu Mkazi, Hellen Liwa alisema kuwa
dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi na alitakiwa kuwa na wadhamini
wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambaye atasaini hati
ya dhamana ya Sh2 milioni.
Licha ya dhamana yake hiyo kuwa wazi,
mshtakiwa huyo alishindwa kukamilisha masharti hayo kwani baada ya
kusomewa mashtaka alipoulizwa kama alikuwa na wadhamini alishindwa
kuwapata.
Akimsomea shtaka linalomkabili, Wakili Sekwao alisema
kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya
Soweto, Makumbusho wilayani Kinondoni kinyume cha kifungu cha 89 (2) (a)
na kifungu cha 35 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu.
Wakili Sekwao
alisema akiwa katika baa hiyo, mshtakiwa alitishia kumuua Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa maneno kwa njia ya
kujitoa mhanga.
“Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli,
mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alisema
Wakili Sekwao akimnukuu mshtakiwa huyo.
Hata hivyo, Wakili
Sekwao alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na akaomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.