Saturday, 20 February 2016

Rais Magufuli Amteua Hebert Mrango kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
MKUTANO WA MHE. NAPE MOSSES NNAUYE, WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO NA WAANDISHI WA HABARI
 

TAREHE 20/02/2016
-------------
Dondoo Alizozungumza Waziri Nape Nnauye;
Napenda kuwafahamisha kuwa kufuatia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kumaliza Muda wake, uundwaji wa Bodi Mpya umekamilika. 
Ni vyema kuwafahamisha kuwa katika utaratibu wa kisheria wa kuunda Bodi ya TBC mwenye Mamlaka ya kisheria ya Kumteua Mwenyekiti wa Bodi ni Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.
 
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC iliyomaliza muda wake, Prof. Mwajabu Possi na wajumbe wake wote kwa kazi waliyoifanya kwa muda wote wa uhai wa bodi hiyo. 
Ninaamini Bodi Mpya itaendeleza yale mazuri yote yaliyofanyika na Baodi iliyopita na kubuni mambo mengine mapya ili kuongeza tija kwa Shirika.
 
Baada ya kutoa maelezo haya ya awali, sasa nichukue fursa hii kuwajulisha yafuatayo;
1.   Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Mhe. Balozi Herbert E. Mrango (pichani) kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya TBC. Uteuzi huu unaanza tarehe 19/02/2016 kwa kipindi cha miaka Mitatu.
 
Balozi Mrango kielimu ana shahada ya Uzamili katika uendelezaji wa Mifumo (MSc – Systems Development) aliyoisomea Chuo Kikuu cha Dublin Nchini Uingereza. Aidha amehitimu Shahada ya kwanza ya Takwimu za Kiuchumi katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Tanzania.
 
Balozi Mrango alishashika nyadhifa mbalimbali, zikiwemo kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara  ya Miundombinu Kuanzia Februari, 2011 hadi September, 2013.
 
Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Balozi Mrango kwa kuaminiwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huu muhimu. 
Aidha nimhakikishie Mwenyekiti huyu Mpya wa TBC kwamba kwa kuwa Shirika la TBC liko chini ya Wizara yangu, tutampa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika shirika letu la Utangazaji.

2.Kwa mujibu wa Sheria iliyounda TBC, baada ya Mhe. Rais kumteua Mwenyekiti wa Bodi, Waziri mwenye dhamana na shughuli za utangazaji,  anateua Wajumbe sita wa Bodi. 
Katika uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilishatupatia vigezo vya utaalamu wa wajumbe wakati wa uteuzi.

Hivyo basi, mimi Nape Moses Nnauye, nikiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kwa kufuata taratibu zingine za kufanya uteuzi, nimewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya TBC;

(i) Bw. William Steven Kallaghe; Mtaalamu wa Uchumi.  (M.A – Economics; Head of Public Policy: NBC Bank  Tanzania ).

(ii)Bw. Mustapha Kambona Ismail; Mtaalamu wa Sheria. (LLB - UDSM; Associate Director, Litigation & Investment – Bank of Tanzania; Advocate of the High Court of Tanzania).

(iii) Bi. Elimbora Abia Muro; Mtaalamu wa Uhasibu. (CPA, MBA: Senior Internal Auditor, Tanzania Investment Centre).

(iv) Bw. Mick Lutechura Kiliba; Mtaalamu wa Rasilimali watu. (MBA – Public Service Mgt; Director of Management: President’s Office – Public Service Management).

(v) Dkt. Ayub Rioba; Mtaalamu wa Sekta ya Utangazaji na Utangazaji.  (PhD – Mass Communication; Associate Dean: School of Journalism, University of Dar Es Salaam) na

6. Bw. Assah Andrew Mwambene; Mtaalamu wa Sekta ya Habari. ( MSc – Media Research and Analysis; Director of Information: Ministry of Information, Culture, Arts and Sports).

Uteuzi wa wajumbe hawa ni kuanzia tarehe 19/02/2016 kwa muda wa miaka mitatu.

3. Nimalizie kwa kuwapongeza tena wote waliopata uteuzi huu. Tuna matumaini makubwa toka kwao kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa TBC katika tasnia ya Utangazaji katika ulimwengu wa Teknolojia inayobadilika kwa kasi kubwa duniani.
Ni imani yangu kwamba Bodi hii mpya italeta msukumo mpya katika utendaji wa Shirika ili hata watumishi wanaofanya kazi katika shirika hili waendelee kujivunia kuwa ndani ya TBC lakini pia Umma wa Watanzania wajivunie viwango vya utendaji wa Shirika hili.
Share:

MPYA:WANAFUNZI WA SUA KOZI YA FOOD PROCESSING WAFANIKIWA KUPANDA MLIMA ULUGURU NA KUWEKA RECORD MPYA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Wanafunzi wa chuo kikuu SUA kozi ya food processing wamefanikiwa kupanda mlima uluguru,kwa mara ya kwanza,tangu wafike chuoni hapo.

Wakizungumza na reporter wa blog hii ya MASWAYETU ,mmoja wa walioshirikisafari hiyo bwana SHABANI MLISHIDI amesema kwamba safari hiyo ilianza mida ya saa moja kasoro asubuhi ambapo walifanikiwa kupanda mlima huo kupitia njia ya kwa mkuu wa mkoa wa MOROGORO. 
Zifuatazo ni picha mbalimbali wakati wa TOUR hiyo iliyofanyika mapema leo hii,
Kutoka kulia ni mwa picha hii ni(bi halima,prisca,angle,bazila,tete,lilian,mlishidi,sabuni,cos,jaq,kato,tina,da froza,isaya,na mr,innocent

hawa ni wanafunzi wa SUA mwaka wa tatu wakiwa mlimani

hapa katika picha ni vijana wakiwa wanapanda mlima,(tete,eddy,neville)

hapa ni moja ya picha wakiwa wanapanda mlima huo  wakiongozwa na bi halima

waliopo ktk picha ni pamoja na mchizi wa dar-ibra,kato,dada fathiya,valence,bazilla,shadrack,tete,prisca,angle,innocent na  christina

wanafunzi hao wakiwa mlimani ktk moja ya vyanzo vinavyotirisha maji mkoani morogoro

hapa ni brother neville na brother eddy wakiwa njiani wakipanda mlima huo



Share:

MATOKEO LIGI KUU TANZANIA BARA,YANGA 2 SIMBA 0

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

TUNAIANGAZIA YANGA SC DHIDI YA SIMBA SC.
Kabla ya Yanga SC inaanza kurehesha imani kwa mashabiki wake baada ya kutandikwa na Simba bao 5-1 katika mchezo wa mtani jembe na kibao hicho sasa kimegeuzwa upande wa pili baada ya Yanga ikipata ushindi waa bao 2-0 katika mzunguko wa kwanza na kurudiaa ushindi kama huo wa bao 2-0 katika ligi kuu Tanzania bara katika msimu wa mwaka 2015/2016.

Mshambuliaji wa Yanga SC raiaa wa Zimbambwe Donald Ngoma ndiye aliyeresha furaha hiyo kwa mabashki wa Yanga kwa kuwasahaulisha kipigo cha bao 5-1 baada ya kufunga bao dakika ya 40 kufuatia kuunasa mpira na kuwalamba chenga beki na kipa wa Simba mpira ambao ulirudishwa golini mwa Simba SC.

Yanga waliongoza bao la pili kupitia kwa mshambuliaji Amis Tamwe akifunga dakika ya 72 baada ya kazi nzuri kutoka kwa Geofrey Mwashiuya na kumfunga kipa wa Simba Vicent Agban.

Kutokana na matokeo hayo Yanga SC wanakwea hadi kileleni kwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara kwa kufikisha pointi 46.

Mlinzi wa Simba SC, Abdi Banda ameonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 25 baada ya kufanya faulo ndani ya dakika 3 katika mchezo huo.

Yanga na Simba zimekutana mara 91.
Yanga imeshinda mara 34, imefunga magoli 99.
Simba imeshinda mara 25,imefunga magoli 88.
Wababe hawa wa soka la Tanzania wametoka sare mara 32.
Share:

MA-DC WAPATA KIWEWE,KILA MMOJA NA VIOJA VYAKE,WANANCHI WAPONDA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

MWENENDO wa utendaji kazi wa baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya sasa umeanza kuonyesha dalili za kukumbwa na kiwewe cha kutoteuliwa tena katika safu mpya inayotarajiwa kutangazwa wakati wowote na Rais John Magufuli.


Hali hiyo imebainika wiki iliyopita baada ya Rais Magufuli kulitaja hadharani jina la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuwa mmoja wa watu waliojihakikishia nafasi katika Serikali yake kutokana na utendaji kazi wake.



Rais Magufuli aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wazee wa Dar es Salaam ambapo pamoja na kusifia utendaji kazi wa Makonda, alisema umma usishangae iwapo atampandisha cheo.



Makonda anatajwa kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kuhamasisha uchangiaji wa elimu na kusimamia shughuli za maendeleo.

“Najua watu wanauliza sana ni lini nitateua wakuu wa mikoa na wilaya. Wala hawatajua, lakini ninaendelea kuwachambua, angalau mheshimiwa Makonda umeshajihakikishia angalau kupata. Lakini na wewe sasa usianze kulala,” alisema Rais Magufuli.

Kauli hiyo ya Magufuli imeonekana kuwaibua baadhi ya wakuu wa wilaya ambao kwa zaidi ya wiki moja sasa wamekuwa wakisambaza wenyewe au mawakala wao picha za utendaji kazi wao kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.



Picha ambazo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii zinawaonyesha viongozi hao wakijishughulisha na kazi za kutatua migogoro ya ardhi, kupanda miti, kufanya usafi wa mazingira, kuhamasisha uchangiaji wa vifaa vya elimu na hata kushiriki shughuli za uokoaji wa majanga.



Mmoja wa viongozi hao ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ambaye tayari picha zake zimezua mjadala mkubwa katika mitandao ya Whatsap, facebook na Jamii Forum.



Katika mitandao hiyo, picha za Kasesela zinamuonyesha akiwa anawaokoa baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mboliboli, Tarafa ya Pawaga wilayani humo ambao kijiji chao kimezingirwa na maji baada ya kukumbwa na mafuriko.



Picha iliyozua gumzo zaidi ni ile inayomuonesha Kasesela akiwa amembeba mgongoni mtu aliyedaiwa kuwa ni mpiga picha. Katika picha hiyo, maoni mbalimbali yametolewa kwenye mitandao ambako wachangiaji wengi wameeleza kuwa anafanya kazi kwa kujionyesha ili Rais Magufuli amkumbuke wakati wa uteuzi.



Mmoja wa wanasiasa ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, aliweka picha hiyo katika akaunti yake ya facebook na kuandika kuwa; “Hizi ndizo siasa za Tanzania, Mkuu wa Wilaya anapombeba mpiga picha!”



Kasesela alipoulizwa na MTANZANIA Jumamosi kupitia simu yake ya kiganjani iwapo anafanya kazi ili Rais Magufuli amuone au la, kwanza alikiri kuwa picha iliyotumwa na Msigwa ni yake na kwamba tangu alipofika katika wilaya hiyo amekuwa akijishughulisha na uokoaji watu katika mafuriko hayo.



“Toka naingia niko kazini, toka nimefika ni mafuriko, mafuriko hata sasa niko huku porini nafyeka ili kutengeneza mahali pa kuwahifadhi watu waliookolewa, tuko tunafanya kazi,” alisema Kasesela.



Alisema hata picha iliyozua gumzo mtandaoni inayomuonyesha akiwa amembeba mpigapicha badala ya kuokoa watoto inatafasiriwa vibaya lakini lengo lake lilikuwa ni kumwokoa asiharibu vifaa vyake vya kufanyia kazi.



“Kuokoa watu 399 sio mchezo, yule mpiga picha kwenye ile picha iliyozua gumzo mtandaoni alikuwa ameshika chombo nami nilikuwa nimekwishavua viatu, kuna watu wanapotosha kauli ya Rais Magufuli,” alisema Kasesela.



Picha nyingine katika mitandao ya kijamii inamwonyesha Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mrisho Gambo, akila chakula na wananchi eneo ambalo linaonekana kuwa ni shamba huku nyingine ikimwonyesha akiwa amejitwisha mawe kichwani.



Alipoulizwa Gambo kupitia simu yake ya kiganjani ili kujua iwapo picha ile ni yake na kwamba alikuwa katika tukio lipi, alipokea na kusikiliza kisha akaomba apewe muda kidogo amalizane na watu aliokuwa nao.



Hata hivyo, Gambo alipotafutwa baadaye hakupokea simu.



Mwingine aliyezua gumzo ni Mkuu wa Wilaya ya Hai, Antony Mtaka ambaye picha zake katika mitandao ya kijamii zinamuonyesha akiwa amekaa chini akizungumza na wananchi ambao wamesimama.



Mtaka alipoulizwa kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu tukio hilo, aling’aka kwa ukali huku akidai kuwa waandishi wa habari wanamfuatilia na kumsakama na kwamba wengi wana chuki na Serikali.



Akizungumza kwa sauti ya ukali, ya juu huku akitamka maneno machafu ambayo hatuwezi kuyaandika gazetini, Mtaka alisema hafanyi kazi na vyombo vya habari kwa sababu hahitaji kuonekana utendaji wake na mtu yeyote na kwamba yeyote anayemuhoji kuhusu hilo ni upumbavu.



“Mimi sifanyi biashara ya kuonekana ili ifanyeje? Muulize aliyenipiga picha kuwa ilikuwa wapi, sifanyi kazi na media mimi, hatufanyi kazi ya kuonekana kwenye media, mimi upumbavu huo sifanyi,” aling’aka Mtaka.



Alipobanwa kuwa ni kwanini anaruhusu picha zake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii kama hataki kuonekana, aling’aka tena kwa ukali huku akieleza tuhuma za moja kwa moja kwa gazeti hili kuwa limefanya kazi ya kuichafua Serikali kwa muda wa miaka minane mfululizo hivyo ni ajabu sasa kuanza kuisifia Serikali ya Rais Magufuli.



“Mmefanya kazi ya kuichafua Serikali kwa miaka nane leo hii Serikali ya Magufuli imekuwa nzuri,” alihoji kwa sauti ya ukali Mtaka.



Tangu Rais Magufuli alipotangaza Baraza la Mawaziri Desemba mwaka jana, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wameripotiwa kuishi kwa hofu ya kutemwa katika uteuzi utakaofanywa.

Tayari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amekwishawaaga baadhi ya watumishi wa umma mkoani Mwanza, hatua inayoelezwa na wachambuzi na wafuatiliaji wa siasa za hapa nyumbani kuwa inatokana na kutokuwa na uhakika wa kuteuliwa.
Share:

KIKOSI MECHI YA LEO SIMBA VS YANGA HIKI HAPA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

YANGA

Kocha Hans van der Pluijm amelazimika kufanya mabadiliko katika kikosi chake upande wa ulinzi kutokana na pengo la wachezaji wawili.

Kelvin Yondani ana kadi nyekundu, nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' ni majeruhi. Hivyo Pluijm amewapanga Bossou na Pato Ngonyani kuongoza safu ya ulinzi huku mkongwe Mbuyu Twite akiongoza kiungo cha ukabaji.

1. Ally Mustapha ‘Barthez’
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Pato Ngonyani
5. Vicent Bossou
6. Mbuyu Twite
7. Deus Kaseke
8. Thabani Kamusoko
9. Amissi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Haruna Niyonzima

SUB
Deo Munish
Malimi Busungu
Nadir Harub
Geofrey Mwashiuya
Oscar joshua
Issofou Boubacar
Simon Msuva

SIMBA
1. Vicent Agbani
2. Hassan Kessy
3. Mohammed Hussein ‘Tshabalala’
4. Juuko Murshid 
5. Abdi Bhanda
6. Justuce Majabvi
7. Mwinyi Kazimoto
8. Jonas Mkude
9. Hamisi Kiiza
10. Ibrahim Ajibu
11. Said Ndemla

SUB:
Peter Manyika
Emry Nimubona
Lufungo
Awadh Juma
Dani Lyanga
Mussa Mgosi

Brian Majwega
 
Share:

LIVE UPDATES:TAZAMA MECHI YA SIMBA VS YANGA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

SIMBA WATUA TAIFA, WACHEZAJI WAKE WAKIKWEPA CHUMBA CHA YANGA, WAINGIA CHUMBA CHA WAANDISHI WA HABARI



Vikosi vyote vya Yanga na Simba, tayari vimewasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi yao ya leo.

Lakini wachezaji wa Simba, ambao walitua uwanjani ahapo baada ya Yanga. Hawajaingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo ambacho kawaida hutumiwa na Yanga.

Badala yake wameingia kwenye chumba ambacho hutumiwa na waandishi wa habari wakati wa mikutano yao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa Simba waliingia kwenye chumba cha waandishi wa habari na mara moja kuanza maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itaanza hivi punde.

Hivi karibuni, TFF ilitoa adhabu kwa timu zilizotumia vyumba vya waandishi wa habari au kugoma kuingia vyumbani.

Share:

BODABODA KIAMA KIMEFIKA,IGP MANGU ATANGAZA OPERESHENI KAMATA BODABODA NCHI NZIMA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewaagiza makamanda wa Polisi kote nchini, kuendesha oparesheni kali ya kuwachukulia hatua za kisheria, waendesha bodaboda wasiotii sheria za usalama barabarani.

Ametaja makosa yatakayosababisha waendesha bodaboda hao kukamatwa kuwa ni pamoja na kubeba abiria zaidi ya mmoja, kupita katika taa nyekundu na kutovaa kofia ngumu.

IGP Mangu alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na maofisa wakuu wa Polisi, wakiwemo makamanda wa Polisi wa mikoa, vikosi na makao makuu katika kikao kazi kilichofanyika Dar es Salaam hivi karibuni ambacho kilifunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.

Alisema waendesha bodaboda wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za usalama barabarani, lakini sasa mwisho wao umefika na kuwataka makamanda wa Polisi wa mikoa kote nchini, kutekeleza maelekezo hayo, ili kuleta nidhamu kwa bodaboda katika kufuata sheria za usalama barabarani.

IGP Mangu alisema suala la kufuata sheria za usalama barabarani kwa bodaboda halina mjadala na kila Kamanda ahakikishe kuwa wote wasiofuata sheria na kukaidi, wanakamatwa bila kuoneana muhali kwa kuwa wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuzuilika.

“Pamoja na kuendelea kudhibiti uhalifu wa aina zote, natoa maelekezo kwa kila mkoa kuhakikisha unaendesha oparesheni kali dhidi ya bodaboda, ili kupunguza ajali zinazosababishwa na bodaboda.
 “Wengi wao hawataki kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani, tusiwaonee muhali maana maisha ya watu ni muhimu sana na jambo la msingi ni kusimamia sheria tu,” alisema IGP Mangu.

Awali akifungua kikaokazi hicho Waziri Kitwanga alilitaka Jeshi la Polisi kuendelea na mapambano yake dhidi ya uhalifu na wahalifu, ili usalama wa raia na mali zao uendelee kuimarika na Watanzania waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo bila hofu ya kutendewa uhalifu.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARY 20 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

HIZI NDIZO SABABU ZA KUSHINDWA VIBAYA SHULE ZA VIPAJI MAALUM MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Anguko la shule za sekondari za Serikali zikiwamo za vipaji maalumu katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, limedaiwa kusababishwa na walimu kukata tamaa, miundombinu duni na mazingira magumu ya kufundishia na kusomea.

Shule za vipaji maalumu, zinazochukua wanafunzi wanaofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba, hazimo kwenye orodha ya shule 50 bora, na kati yao ya kwanza inashika nafasi ya 53.

Orodha hiyo imetawaliwa na shule binafsi na za taasisi zisizo za serikali, hasa za kidini wakati za Serikali zinapambana kuanzia nafasi ya 53.

Kukata tamaa kwa walimu na mazingira magumu ya kufundishia ndiko kumeelezwa na wachambuzi mbalimbali kuwa ndiyo sababu kuu ya kuporomoka kwa kiwango cha ufaulu kwa shule hizo.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alitaja shule 10 bora juzi kuwa ni Kaizirege ya Kagera, Alliance Girls (Mwanza), St Francis Girls (Mbeya), Alliance Boys (Mwanza), Canossa (Dar es Salaam), na Marian Boys (Pwani).

Nyingine ni Alliance Rock Army (Mwanza), Fedha Girls (Dar es Salaam), Feza Boys (Dar es Salaam) na Uru Seminary (Kilimanjaro).

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa Kaizirege kuongoza katika mitihani ya kitaifa huku Alliance Boy na Girls zikiwamo pia katika 10 bora kwa miaka mitatu mfululizo.
 Anguko la shule za Serikali 
Kuanguka kwa shule hizo kumedhihirika juzi mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne ambayo sehemu kubwa hazikufanya vizuri.

Dk Msonde alizitaja baadhi ya shule za sekondari za vipaji maalumu kuwa ni Ilboru ambayo imeshika nafasi ya 53, Kibaha (69), Kilakala (94), Mzumbe (71), Tabora Boys (124), Tabora Girls (128) na Msalato (148).

Akizungumzia hatua hiyo, Meneja wa Utafiti na Sera wa Taasisi ya Hakielimu, Godfrey Boniventure alisema anguko hilo linaonyesha wazi kuwapo kwa tabaka kubwa kati ya walionacho na wasio nacho.

“Shule zote 10 za mwisho ni za Serikali ambazo wanasoma watoto wa maskini. Kibaya zaidi hata za vipaji maalumu zilizokuwa zikitegemewa zipo hoi. Hii ni hatari kwa Taifa,” alisema.

Alisema tabaka hilo litawafanya watoto wanaotoka kwenye familia zenye uwezo kupata nafasi za juu kwenye soko la ajira, huku maskini wakishindwa kuingia kwenye ushindani huo.

Profesa wa Chuo Kikuu Ruaha (RUCU), Gaudence Mpangala alisema anguko hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kukata tamaa kwa walimu.

Alisema walimu hawana moyo wa kuendelea kufanya kazi hiyo na utafiti kwenye baadhi ya shule unaonyesha wengi wao wanaingia darasani kukamilisha ratiba na si kufundisha.

Profesa Mpangala alisema sababu iliyowafanya kufikia hatua hiyo ni Serikali kutowalipa stahiki zao kama mishahara, motisha, makato na mazingira magumu ya kufundishia.

“Ilitokea kwangu. Niliamua kumhamisha mwanangu aliyekuwa akisoma shule ya vipaji maalumu kwa sababu walikuwa hawaingii darasani, sikuwalaumu hata kidogo, niliona wazi mazingira yao ya kazi ni magumu.”

Alisema sera ya elimu bure itachangia anguko kubwa zaidi kutokana na hali ya shule hizo kuendelea kuwa mbaya. “Majengo ya shule za vipaji maalumu yamechoka, Serikali haipeleki pesa na wazazi hawachangii. Kitakachotokea hapo ni kufeli zaidi,” alisema.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kitila Mkumbo alisema kukata tamaa kwa walimu kunachangia shule hizo kufanya vibaya.

Aliitaka Serikali kurejesha hadhi ya shule zake ili ziendelee kuwa kimbilio la wanyonge.

“Ari ya walimu kufundisha imeshuka kwa kiwango kikubwa, Serikali isipotoa kipaumbele kwa kundi hili, itakuwa hatari zaidi,” alisema.

Ilboru wanena 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ilboru, Julius Shura alikiri kuwa hali ya shule hiyo ni taabani kutokana na kuchakaa kwa miundombinu.

“Hata hivyo, tumejitahidi kutoa wanafunzi wawili bora ambao wametokana na jitihada zetu walimu licha ya kuwa mazingira ya kufundishia ni magumu. Tunaomba Serikali itupie jicho shule hizi ambazo zilikuwa taa kwa watoto wa Kitanzania wenye vipaji maalumu,” alisema.

“Hali ni ngumu zaidi kwa watoto wenye ulemavu, hakuna mazingira rafiki hata kidogo. Piga picha bajeti ya Sh1,500 kwa mtoto anayesoma sayansi ni ndogo sana kwa siku, usitegemee kwamba atafanya maajabu,” alisema.

Siri ya shule binafsi kuongoza 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Visivyo Vya Serikali (Tamangsco), Benjamin Nkonya alisema siri ya shule zao kuongoza ni kuwekeza kwa walimu.

“Tunawasikiliza walimu, kuwapa heshima wanayostahili na kuhakikisha wanapatiwa kila wanachohitaji kama mikopo ya magari na nyumba, ukimjali mwalimu mengine yote yatakwenda vizuri,” alisema.
Share:

Friday, 19 February 2016

New AUDIO | ROMA Ft. WALTER CHILAMBO - MTOTO WA KIGOGO | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
https://mkito.com/song/mtoto-wa-kigogo-ft-walter-chilambo/18921/bwi-1-36866
Share:

MPYA:BAADA YA KUFUTWA KWA ST.JOSEPH SONGEA,SUA KUPOKEA WANAFUNZI ZAIDI YA 800 KUTOKA SONGEA,HIZI NDIZO KOZI ZINAZOHAMISHIWA SUA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY




Kozi zitakazohamishiwa SUA ni pamoja na zifuatazo;
1. BACHELOR OF SCIENCE IN COMPUTER SCIENCE
2. BACHELOR OF SCIENCE IN EDUCATION WITH
    COMPUTER SCIENCE


3. BACHELOR OF TECHNOLOGY IN AGRICULTURE
4. BACHELOR OF TECHNOLOGY IN HORTICULTURE
5. BACHELOR OF TECHNOLOGY IN AGRICULTURAL
    ENGINEERING

6. BACHELOR OF TECHNOLOGY IN FOOD PROCESS
    ENGINEERING


Share:

BREAKING NEWS:TCU YAFUTA VYUO VIKUU VYA ST.JOSEPH SONGEA-VIDEO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

>>>>>VIDEO <<<<

MG1Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof Yunus Mgaya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Kuhusu uamuzi wa Tume kufuta usajili wa vyuo vikuu vishiriki vya Mtakatifu Joseph tawi la Songea. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

……………………………………………………………………………………..
Na Nyakongo Manyama MAELEZO
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeamua kufuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Tume hiyo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof Yunus Mgaya amesema kutokana na mapungufu yaliyobainishwa na Tume ambayo ni matatizo ya ubora wa elimu na ukiukwaji wa Sheria za uendeshaji wa Chuo Kikuu kama ulivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu hii  imepelekea Tume kuchukua hatua ya kufuta usajili wa vyuo hivyo.
“ kutokana na yaliyobainishwa hapo awali tunapenda kutaarifu umma kwamba ,Tume imejiridhisha kuwa hivi vyuo vikuu vishiriki viwili havitoi elimu ya Chuo kikuu ya viwango stahiki na ukizingatia wanafunzi katika Vyuo hivi ndio waathirika wakubwa wa matatizo yaliyopo”Alisema Prof Mgaya.
“Napenda kufafanua kwamba Vyuo vikuu vishiriki tuliyovifutia usajili ni tawi la Songea na Vyuo vingine vishiriki vya Mtakatifu Joseph vilivyopo Dar es Salaam na Arusha vitaendelea kufanya kazi kama kawaida”Alisema Prof Mgaya.
Prof Yunus Mgaya amesema wanafunzi wote wanaosoma katika vyuo vishiriki vilivyofutwa usajili wanaarifiwa kuwa watahamishiwa kwenye vyuo vikuu vingine vinavyofundisha programu za masomo zinazofanana na masomo wanayosoma hivi sasa chini ya utaratibu uliopangwa.
Amevitaja vyuo ambavyo watapelekwa wanafunzi walipo katika vyuo vishiriki vilivyofutwa usajili kuwa ni Chuo Kikuu cha kilimo Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Chuo Kikuu cha  Kikatoliki cha Mwenge(MWECAU) na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha(RUCU).

Amesisitiza kuwa orodha ya majina ya wanafunzi na vyuo watavyohamishiwa yatawekwa kwenye tovuti ya Tume hivi karibuni na wale wote wanaonufaika na Mikopo toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, mikopo yao itahamishiwa katika vyuo watakavyokuwa wamehamishiwa.
Vyuo vikuu vyote chini vinakumbushwa kufata Sheria na kuzingatia utoaji wa elimu inayokidhi viwango vya ubora vinavyokubalika kitaifa na kimataifa, hivyo Tume haitasita kuchukua hatua stahiki kwa chuo kikuu chochote kitakachobainika kutoa elimu isiyokubalika.

BARUA HII HAPA 



 
Share:

LINK MPYA YA KUANGALIA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2015,ANGALIA HAPA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 Image result for TANZANIA

 KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CSEE 2015


KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE QT 2015

<<<<  BONYEZA HAPA>>>>>>
Share:

Waziri Mbarawa Awakamua MAJIPU Wakurugenzi TCRA na TEMESA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waziri wa Ujenzi wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, kusitisha mara moja mkataba wa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nzagi, kwa kushindwa kusimamia ufungwaji wa kifaa cha kufuatilia mapato ya simu ya ndani katika mitambo ya kuchunguza mapato katika mitandao ya simu (TTMS).

Waziri Mbarawa amesema kutokufungwa kwa kifaa hicho kumeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 400/= hivyo ameiagiza pia bodi hiyo ya TCRA kuwasimamisha kazi mara moja, Kaimu Mkurugenzi anayesimamia mfumo wa uhakiki na usimamiaji huduma za mawasiliano, mhandisi Sunday Richard na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Modestus Ndunguru ili kupisha uchugnuzi dhidi ya uhusika wao katika kusababisha kifaa hicho kutokufungwa.

Aidha, Waziri Mbarawa ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRCA, Ally Simba kwa kutokuwa makini katika utendaji huo huku akimwagiza kuhakikisha kuwa kifaa hicho kinafungwa ndani ya siku saba. 
Profesa  Mbarawa  pia  ametengua  uteuzi  wa  Mtendaji  mkuu  wa  Wakala  wa  Umeme  na  Ufundi  Tanzania  (Temesa),Mhandisi  Marcellin Magesa  kwa  kushindwa  kusimamia  matengenezo  ya  magari  ya  serikali, mitambo  na  vivuko.
Kadhalika, ametengua  uteuzi  wa  Mkurugenzi  wa  matengenezo  ya  magari  ya  serikali,Prisca  Mukama  na  Meneja  wa  Karakana   ya   magari  ya  Serikali  John Mushina  ambao  watapangiwa  majukumu mengine.
Share:

Jeshi la Polisi Latua Bandarini Kuimarisha Ulinzi.....Waziri Kitwanga Atoa Onyo Kwa Polisi Wanaowabambika Kesi Wananchi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Jeshi la Polisi limeweka ulinzi katika Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kuwa ilindwe na vyombo vya dola badala ya kampuni binafsi za ulinzi.

Akizungumza kwenye kikao cha kazi kilichowahusisha makamanda wa mikoa na vikosi vya polisi nchini, Mkuu wa jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu, alisema tayari  wamepeleka askari bandarini ambao wanafanya kazi kwa muda wakishirikiana na walinzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Mangu alisema askari hao wanakwenda kulinda kwa muda wakitokea Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.

Alisema amewaomba TPA wajenge kituo cha polisi bandarini hapo, ili askari wawepo muda wote.

“Tumetekeleza agizo la waziri, kwa sasa bado tunamalizia logistics fulani ili tuwe pale bandarini permanently (muda wote). Tunahitaji ushirikiano wa watendaji wote ili kuimarisha ulinzi wa mali za wananchi,” alisema Mangu.

Alisema polisi wamejipanga vyema kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kurudisha nidhamu ya utendaji, kupambana na uhalifu, dawa za kulevya, ujangili na ujambazi.

Mkuu huyo wa polisi alisisitiza kwamba, kuanzia Juni Mosi, mwaka huu wataanza utaratibu mpya wa utendaji chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ili kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kulinda mali na maisha yao.

“Kaulimbiu yetu ni ‘badilika kifikra, acha kufanya kazi kwa mazoea’. Kaulimbiu hii ni kielelezo cha jinsi tulivyodhamiria kubadilika kiutendaji,” alisema.

Awali, akifungua kikao hicho, Waziri Kitwanga aliwapongeza makamanda hao kuandaa kikao ili kuelekezana nini cha kufanya kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na Taifa.

“Serikali haitafumbia macho askari au ofisa yeyote atakayeomba na kupokea rushwa, kuchelewesha upepelezi, kutowajali wateja, kubambikia wananchi kesi na mambo mengineyo. Tutachukua hatua bila kujali cheo chake,” alisisitiza.

Kitwanga alisema Serikali imejipanga kuboresha maisha ya askari na mazingira yao ya kazi.

Alisema Serikali imeagiza magari na kupanga kujenga nyumba 3,500 kwa ajili ya makazi ya askari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker ambayo pia imedhamini kikao hicho alipendekeza matumizi ya fedha kielektroniki kwa kuwa ndiyo njia salama ya kutumia huduma za kibenki.
Share:

Kambi ya Upinzani bungeni Yaendelea Kumgomea Spika Ndugai

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu amesema kambi hiyo haitaongoza kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac) hadi ofisi ya Spika itakapobadilisha uteuzi wa wajumbe wa kamati hizo.

Kwa mujibu wa mabunge ya Jumuiya za Madola, kamati hizo huongozwa na wapinzani, lakini tangu Spika wa Bunge, Job Ndugai afanye uteuzi wa wajumbe, kambi hiyo imesusia kushiriki uchaguzi kwa kile wanachokiita “kupangiwa wajumbe”.

Jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema mazungumzo kati ya ofisi ya spika na kambi hiyo bado yanaendelea na kusisitiza kwamba uteuzi huo unaweza kutenguliwa au kuachwa kama ulivyo. 
Katika maelezo yake, Lissu alisema licha ya kambi hiyo kuwa katika mazungumzo na ofisi ya spika, suluhisho halijapatikana na kusisitiza kuwa msimamo wao upo palepale. 
“Hatujafika popote. Msimamo wetu uko palepale na hatutakubali kuchaguliwa viongozi wa hizo kamati na CCM, kama wanafikiria ni lazima iwe wanavyotaka sisi hatutakubali,” alisema.

Joel aliwahi kunukuliwa na na vyombo vya habari  akisema kuwa kama kambi hiyo itasusia uchaguzi, shughuli za kamati zitafanywa na makamu wenyeviti ambao wanatokea CCM.

“Ni bora tusiziongoze kabisa kamati hizi. Ukifuatilia utabaini kuwa katika PAC na Laac tuna wajumbe sita kila kamati kati ya wajumbe 23, wakati huohuo kamati ya Ukimwi tumepewa wajumbe 12 kati ya wote 23,” alisema Lissu.

Alisema wajumbe sita waliopo katika kamati ya Laac na PAC wameteuliwa na CCM na kama kamati hizo zinaongozwa na upinzani ni lazima wapinzani wajichagulie wajumbe wao, wakiwamo watakaochaguliwa kuwa wenyeviti. Alisema wabunge wana haki sawa, lakini hawana uwezo sawa.

Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alisema uamuzi wa spika kuwapangia wajumbe katika kamati hizo hauna nia nzuri na kwamba, huenda ni mkakati wa ofisi hiyo kuifanya Serikali iwe inapitisha mambo yasiyofaa bungeni.

Februari Mosi mwaka huu, Kambi ya Upinzani bungeni ilisusia uchaguzi wa viongozi wa kamati hizo kwa maelezo kuwa Spika Ndugai alifanya uteuzi ‘kiholela’ na kuahidi kutoshiriki mpaka pale watakapopewa idhini ya kupendekeza wenyeviti.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger