Tuesday, 13 May 2014

UKATILI WA KUPINDUKIA! KICHANGA CHATUPWA ENEO LA MTO NG'OMBE MWANANYAMALA, DAR


Kichanga kikiwa kimetupwa eneo la mto Ng'ombe Tandale jijini Dar.
Wakazi wa Tandale wakiwa eneo la mto Ng'ombe kushuhudia tukio hilo.
MWILI wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na miezi kati ya saba au nane umeokotwa ukiwa umetupwa eneo la mto Ng'ombe jirani na Alasco, Mwananyamala jijini Dar.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kichanga hicho cha kiume kimekutwa eneo hilo leo asubuhi kikiwa kwenye mfuko wa Rambo. 
Mtandao huu ulifanikiwa kuongea na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Bi. Husna aliyetoa rai kwa wananchi wa eneo lake kutojihusisha na vitendo viovu kama hiki, huku akiwasihi kutumia njia za uzazi wa mpango kujikinga na matatizo kama hayo.

"Nina masikitiko makubwa kwa kitendo hiki, ni bora kichanga hiki kingeletwa serikalini tukilee kuliko kutupwa eneo hili. Kama wananchi mkishindwa kuvumilia bora mtumie uzazi wa mpango," alisema Bi. Husna huku akiahidi kufanya uchunguzi wa kina kumtafuta muhusika!
Share:

MWANAFUNZI WA CHUO AWEKA PICHA ZA UTUPU MTANDAONI(18+)

Share:

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MATOKEO YA RUFAA - AWAMU YA III



BILAL ISLAMIC SEMINARY, P.O.BOX 760, ZANZIBAR
P1360-0176

Kumb. MTS.2/54/LXXXIX/29 Tarehe ya Rufaa: 16-Apr-2014
Maoni
011 CIVICS F F Haijabadilika
013 GEOGRAPHY F F Haijabadilika
015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU E E Haijabadilika
021 KISWAHILI F F Haijabadilika
025 ARABIC LANGUAGE E E Haijabadilika
 

Na. Somo Jina la Somo Gredi ya Awali Gredi ya Sasa
S.L.P 78382 DAR ES SALAAM
P3548-0076

Kumb. MTS.2/54/LXXXIX/36 Tarehe ya Rufaa: 07-May-2014
Maoni
022 ENGLISH LANGUAGE E E Haijabadilika
024 LITERATURE IN ENGLISH E E Haijabadilika
 

Na. Somo Jina la Somo Gredi ya Awali Gredi ya Sasa
CHIEF SARWAT SECONDARY SECONDARY SCHOOL, P.O.BOX 25 KARATU
S0533-0032

Kumb. MTS.2/54/LXXXIX/28 Tarehe ya Rufaa: 16-Apr-2014
Maoni
012 HISTORY E E Haijabadilika
013 GEOGRAPHY E E Haijabadilika
031 PHYSICS F F Haijabadilika
032 CHEMISTRY E E Haijabadilika
033 BIOLOGY D D Haijabadilika
034 AGRICULTURAL SCIENCE E E Haijabadilika
041 BASIC MATHEMATICS F F Haijabadilika
 

Na. Somo Jina la Somo Gredi ya Awali Gredi ya Sasa
S.L.P 23 MONDULI
S0949-0155

Kumb. MTS.2/54/LXXXIX/34 Tarehe ya Rufaa: 05-May-2014
Maoni
011 CIVICS F F Haijabadilika
012 HISTORY F F Haijabadilika
013 GEOGRAPHY F F Haijabadilika
021 KISWAHILI E E Haijabadilika
022 ENGLISH LANGUAGE F F Haijabadilika
033 BIOLOGY F F Haijabadilika
041 BASIC MATHEMATICS F F Haijabadilika
Thursday, May 8, 2014 Page 1 of 2
061 COMMERCE F F Haijabadilika
062 BOOK KEEPING F F Haijabadilika
Share:

MH.KAWAMBWA KATIKA UTOAJI WA TUZO KWA WANAFUNZI BORA KIDATO CHA NNE 2013


Ministry of Education and Vocational Training


Ministry of Education and Vocational Training






















HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. SHUKURU KAWAMBWA (MB) KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU
HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA (MB) YA KUMKARIBISHA MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU KITAIFA UWANJA WA JAMHURI, DODOMA. JUMAMOSI TAREHE 10 MEI, 2014
Read more...
 
Share:

RIDHIWAN KIKWETE:AKICHANGINA BUNGE LA KATIBA DODOMA

Share:

BREAKING NEWS:KIDATO CHA SITA WOTE MNAKUMBUSHWA KUOMBA MKOPO KABLA YA KWENDA JESHI(JKT)


Mojawapo ya eneo linalolalamikiwa  na wanafunzi wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuhusu Bodi ya Mikopo ( HESLB), ni eneo la madaraja wanayopangiwa na bodi hiyo kwa ajili ya kupata mkopo wa  masomo ya kozi wanazochukua.

Kuna malalamiko kwamba, bodi ya mikopo imekuwa ikipanga madaraja kwa upendeleo kwa kuwa ile dhana ya kumkopesha mwanafunzi anayetoka katika familia maskini kwa kiwango cha asilimia 100,haionekani kufanya kazi kwa wanafunzi walio wengi.
Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko  kwamba,katika upangaji wa madaraja unaofanywa na bodi,wanafunzi wanaotoka katika familia zenye uwezo mkubwa au wa kati, ndio wamekuwa wakipata asilimia 100 na wale wanaotoka katika familia maskini wakiishia kuambulia asilimia 60 mpaka 40. 
April mwaka huu, bodi ya mikopo nchini ilianzisha  utaratibu mpya wa kuomba mikopo kwa wanafunzi wapya na wale wanaoendelea kwa njia ya mtandao.
Mfumo huu unatarajiwa  kuchukua nafasi ya ule wa zamani, ambapo mhusika alikuwa anatakiwa kujaza fomu  kisha kuziwasilisha HESLB. 
Fomu hizo zilijazwa taarifa mbalimbali za muombaji zilizokuwa zinahitajika na bodi ili ziisaidie kumpangia muombaji daraja la fedha alizostahili kupewa kama mkopo kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali anazopaswa atika chuo au taasisi aliyokuwa anachukua kozi yake.

Wanafunzi wote wakidato cha sita mnatakiwa kuomba mkopo kwa kutumia utaratibu wa kulipia MPESA kabla ya kwenda jeshi kuepuka usumbufu.
KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA :www.heslb.go.tz au olas.heslb.go.tz 
Share:

MASWAYETU:SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE

Share:

TUNDU LISSU: Walipotelea wapi waasisi wa Muungano



tundu-lissu_81984.jpg

Serikali imetakiwa kutoa maelezo bungeni, kuhusu sababu za kuuawa kwa waasisi sita wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wanaodaiwa kuzikwa katika handaki moja Zanzibar.
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), msemaji wake, Tundu Lissu aliitaka Serikali kueleza waasisi hao walifanya makosa gani.
Aliwataja waasisi hao kuwa ni Abdallah Kassim Hanga aliyekuwa Waziri Mkuu, Abdulaziz Twala aliyekuwa Waziri wa Fedha na Saleh Akida aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na viongozi waandamizi wa Serikali ya Mapinduzi, Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha Ubwa ambao alisema waliuawa na kuzikwa handaki moja eneo la Kama, Zanzibar.
Lissu alisema hayo huku akinukuu kitabu cha 'Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru' kilichoandikwa na Harith Ghassany alichosema kilionyesha jinsi viongozi hao walivyouawa na kuzikwa katika kaburi moja.
"Sisi wa kizazi cha Muungano tunataka kujua ukweli juu ya makosa waliyoyafanya hawa waasisi wa Muungano hadi wakauawa na kuzikwa katika kaburi au handaki moja," alisema Lissu huku wabunge wakiwa kimya kumsikiliza.
Mgawo wa Zanzibar
Lissu pia aliibua mambo mazito kuhusu mgawanyo wa fedha za misaada na mikopo ya kibajeti kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Alisema Muungano ni kielelezo cha unyonyaji na ukandamizaji ambao nchi kubwa imeifanyia nchi ndogo ya Zanzibar kwa miaka mingi.
Alikwenda mbali na kuitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Wazanzibari kwa umoja wao, kufungua kesi Mahakama za kimataifa kudai fedha zote ambazo nchi yao imeibiwa kwa kivuli cha Muungano.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alisema hadi Machi mwaka huu, Zanzibar ilikuwa imepata gawio la Sh27.1 bilioni badala ya Sh32.6 bilioni zilizoidhinishwa na Bunge, sawa na asilimia 83.
Hata hivyo, alisema hilo linaweza lisiwe tatizo, kwani kwa mwelekeo wa takwimu hizo, hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wa fedha, gawio lililoidhinishwa linaweza kuwa limelipwa lote.
Haya hivyo, alisema tatizo kubwa na la msingi ni kwamba, gawio lililoidhinishwa na Bunge si halali kwa Zanzibar, kwa mujibu wa hotuba ya Waziri wa Fedha, Saada Mkuya ya Aprili 30, mwaka huu.
Chanzo: www.mwananchi.co.tz
SOMA ZAIDI>>>>>
Share:

KASHFA NZITO HOSPITALI YA OCEAN ROAD DAR

ocean_c4007.jpg
Dar es Salaam. Kashfa imeikumba Hospitali ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) kutokana na tuhuma za mmoja wa wauguzi wake kumuuzia dawa 'feki' mgonjwa ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika taasisi hiyo ya Serikali.
Mtumishi wa ORCI katika kitengo cha dawa, Almasi Matola anatuhumiwa kudai fedha kwa mmoja wa wagonjwa wa satarani (jina tunalihifadhi kwa sasa), lakini akampa dawa feki baada ya kupewa fedha.
Mgonjwa huyo alipewa rufaa kwenda Ocean Road Novemba mwaka jana akitokea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kubainika kwamba alikuwa na saratani ya titi.
Baada ya kufika ORCI, ilibainika kwamba mgonjwa huyo alikuwa akihitaji tiba ya kuua vijidudu vya saratani inayojulikana kitaalamu kwa jina la chemotherapy au chemo kwa kifupi na ndipo alipokutana na Matola.
"Huyu Almasi (Matola) alisema anahitaji apewe fedha za dawa moja kwa moja kupitia akaunti yake ya NMB yenye namba zinazoanzia 206016024** (namba mbili za mwisho tumehifadhi), ambako tuliweka kiasi cha Sh340,000," alisema mgonjwa huyo.
Almasi alikiri kuwekewa fedha katika akaunti yake, lakini akakanusha kuomba fedha hizo kama ujira wa kumpa mgonjwa huyo dawa.
"Huyo mgonjwa unayemsema ninamkumbuka ijapokuwa jina lake limenitoka. Lakini ni kweli sijawahi kuonana naye uso kwa uso isipokuwa nilikuwa nawasiliana naye kupitia kwa mfanyakazi mwenzangu ambaye ni ndugu yake. Huyo ndiye alikuja kwangu na kutaka nimsaidie ndugu yake," alisema Matola.
Kwa mujibu wa taratibu za OCRI, wagonjwa wanaokwenda hospitalini hapo kwa rufaa kutoka hospitali nyingine hawapaswi kutozwa fedha zozote kwa ajili ya matibabu.
Mmoja wa madaktari wa OCRI, Dk Steven Shadrack alisema utaratibu wa wagonjwa wengi waliogundulika na saratani, kwa kawaida hutokea Muhimbili ambako huwa wamefanyiwa uchunguzi.
Dk Shadrack alisema mgonjwa anapopewa rufaa kwenda OCRI, hatakiwi kulipia hata senti tano na kama kuna kifaa kilichoharibika ndipo hutakiwa kupimwa nje ya hospitali hiyo.
Kwa mujibu wa madaktari, mgonjwa wa saratani anayehitaji tiba ya chemo, hutakiwa kupewa dozi hiyo kulingana na hatua ya saratani na aina ya dawa aliyoandikiwa.
Ilikuwaje
Mgonjwa huyo alisema Matola alimwambia kuwa tiba yake inahitaji dozi sita za dawa ambazo gharama yake ni zaidi ya Sh2 milioni kwa maana kwamba kila dozi inagharimu Sh340,000.
Alisema kabla ya kuanza kupewa tiba, alielekezwa atoe damu kwanza, ambayo ingepimwa na majibu kutoka siku inayofuata, hivyo angeanza kupewa tiba siku ya tatu.
"Siku ya kwanza ilikuwa Novemba 3, 2013 nilipotolewa damu na nikaenda siku ya tatu kupewa tiba ya chemo," alisema mgonjwa huyo. Alisema alipokwenda kwa ajili ya kupewa dozi ya pili, Matola alimchukua damu na hapohapo akamwekea dripu ya dawa.
Alisema licha ya kupewa tiba hiyo, alikuwa akisikia maumivu makali kwenye titi lililoathirika huku sehemu ya uvimbe ikitoka damu na maji kwa wingi na uvimbe huo ambao ulikuwa mdogo, uliendelea kusambaa kuelekea mabegani, chini ya kwapa hadi kwenye tumbo. "Nilikuwa kwenye maumivu makali sana. Halafu, ndani ya dakika 10, nguo yangu ilikuwa inalowa kwa maji kutoka kwenye titi," alisema mgonjwa huyo.
Katika awamu ya pili na ya tatu ya tiba, mgonjwa alisema alikuwa akimpatia Matola mkononi Sh340,000 kwa kila awamu na kwamba alikuwa akiweka fedha hizo mfukoni, taarifa ambazo hata hivyo, Matola alizikanusha.
Wasiwasi wa tiba
Kwa maelezo ya Dk Shadrack, kwa kawaida dawa za saratani hasa chemotherapy zina madhara mbalimbali kwa watumiaji wake.
"Kwa mfano, mgonjwa baada ya kupata chemo, anaweza kuharisha, kutapika, damu kupungua na wakati mwingine kupata kizunguzungu," alisema Dk Steven na kwamba dalili kubwa kwa wanaopata tiba hiyo huwa ni nywele kunyonyoka.
Lakini, licha ya mgonjwa huyo kupewa dozi tatu za chemo, hakuwahi kupata athari zozote kama hizo.
Mgonjwa huyo alisema ulipofi ka awamu ya nne ya kupewa dawa hiyo Januari 15 mwaka huu, alimwambia Matola kwamba hali yake inazidi kuwa mbaya hivyo alitaka kwenda kwa daktari bingwa, lakini alimkataza akisema hiyo ni hali ya kawaida tu.
"Baada ya kuniambia hivyo alisema kwa dozi ya nne na kuendelea atanipunguzia bei ya dawa na sasa nitakuwa nikilipa Sh320,000 kwa dozi na kama kawaida nilimkabidhi na akaziweka mfukoni kwake."
Alisema alikwenda kwa daktari bingwa, Dk Dominista Kombe na kumwelezea hali yake. "Ni kama alishtuka hivi na alisema inashangaza kama nilikuwa nimepata dozi nne lakini nywele zangu zilikuwa hazijanyonyoka," alisema
Alisema daktari huyo alionekana kushangazwa na kiasi kikubwa cha fedha alizokuwa akitozwa na kumwagiza amwite Matola.
"Wakati tukielekea kwa daktari, Matola alikuwa akilalamika kwamba 'nimeshaharibu mambo'. Hata hivyo, sikuruhusiwa kuwepo wakati wa mazungumzo kati ya daktari na Matola," alisema.
Alisema baadaye Dk Kombe alimwambia ni vyema aanze tiba upya kwani dawa alizopewa ni feki.
Daktari huyo alimwandikia dawa nyingine na kumwelekeza aende katika duka la dawa ambako alizinunua kwa Sh26,000.
Alisema baada ya dozi ya kwanza tu, aliona dalili zote za kufanya kazi kwa tiba hiyo ukiwamo uvimbe kuanza kunywea, damu na maji kukauka.
Utetezi wa Matola
Lakini Matola alidai kuwa mgonjwa huyo alitoa fedha kama asante.
"Baada ya kuwa nimewapatia dawa, yule mfanyakazi mwenzangu aliniambia kwamba mgonjwa anataka namba yangu ya simu au akaunti ya benki ili anipe asante na mimi niliwapa ila sikujua waliweka shilingi ngapi," alisema Matola.
"Nilipokwenda benki nilikuta fedha zimeongezeka, lakini sikujua ni shilingi ngapi ila yule mgonjwa aliwahi kunipigia simu akaniambia kwamba aliniwekea asante, sijui Sh300,000 au 330,000 au sijui 340,000..."
Matola alisema hakuwahi kumwomba fedha mgonjwa huyo na kwamba hakuwahi kuchukua fedha mkononi kama anavyodai.
Dk Kombe anena
Dk Kombe alikiri kukutana na tukio hilo na kusema baada ya kuona hali ilivyo kwa mgonjwa, alimwandikia dawa nyingine ili aendelee na matibabu.
"Nakumbuka hiyo kesi lakini simkumbuki mtu mwenyewe, ila ninachojua ni kuwa, yeye mwenyewe (mgonjwa) alimpa mtu hela mkononi. Yalikuwa ni makosa yake kwa upande mwingine, dawa hazinunuliwi sasa utampaje mtu hela mkononi?" alihoji daktari huyo.
Dk Kombe, ambaye alisema hakumbuki ni mhudumu gani aliyefanya hivyo, alionyesha kuhofia maisha ya mgonjwa au wagonjwa ikiwa taarifa hizo zitatolewa gazetini.
"Unajua wataendelea kupata tiba kwa muda mrefu hapa na hii ni hatari kubwa kwao, huwezi kujua nini kinaweza kuwapata. Cha muhimu wameandikiwa dawa nyingine na wanaendelea nazo, ni bora wangekaa kimya," Dk Kombe.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Ocean Road, Dk Twalib Ngoma alisema mgonjwa aliyefanyiwa hayo aende kushtaki kwenye vyombo vya sheria badala ya vyombo vya habari.
"Anakuja kwako kulalamika wewe umsaidie nini? Anatakiwa kwenda katika vyombo vya sheria ili apewe haki yake, wewe utamsaidiaje?" alihoji Dk Ngoma.
Alisema kama mgonjwa amefanyiwa unyama kama huo, anatakiwa alipwe fidia na hakuhitaji maswali zaidi ya hapo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Mussa Wambura alisema watashughulikia suala hilo kwa kupata vithibitisho vyote
Share:

MAUAJI YA KUTISHA!! KIONGOZI CCM AUAWA KWA SHOKA!

KIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Shina Namba 30, Kigamboni Kisiwani jijini Dar, Bernadetha Shabani (53) amefariki dunia baada ya kupigwa shoka la kichwa na anayedaiwa kuwa ni mpangaji wake aliyefahamika kwa jina la Shija Ng’waya (33).
Bernadetha Shabani enzi za uhai wake.
Tukio hilo la kikatili lilijiri Mei 5, mwaka huu nyumbani kwa marehemu, Kigamboni jijini Dar es Salaam na marehemu alizikwa Mei 6.
Akizungumza na Uwazi kwa uchungu katika msiba wa marehemu huyo mwishoni mwa wiki iliyopita,  mtoto wa marehemu, Ester Shija (hakuna undugu na mtuhumiwa) alisema mlalamikiwa huyo alikuwa mpangaji wao kwa mwaka mmoja akahama.
lisema baada ya muda, mtuhumiwa alirudi kwa marehemu mama yake na kudai kuna vitu vyake aliviacha kwenye chumba.
“Mama alimuuliza ni vitu gani akasema mwiko, tambi za jiko la Mchina, tochi na redio ndogo. Mama alimwambia hakuviona pengine watoto walivichezea. Shija akasema yeye anachotaka ni vitu vyake, akaondoka na kuahidi kurudi siku nyingine.
Ndugu jamaa na marafiki wakijiandaa kwenda kuuzika mwili wa marehemu.
“Kweli, alirudi tena siku nyingine na kumdai mama vitu vyake na akasema vikikosekana atamuua kisha akaondoka.
“Mama alikwenda kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa (hakumtaja jina). Shija akaitwa na kuulizwa ni vitu gani? Akavitaja na  kusisitiza kama asingevipata  angemfanyia kitu kibaya mama. Mwenyekiti aliripoti polisi kutokana na vitisho hivyo.
“Awamu nyingine, Shija  alikuja nyumbani akiwa uchi wa mnyama na kudai vitu vyake. Siku hiyo akasema kama hatavipata lazima aue, mwenyekiti akaenda tena polisi, wakaja kumchukua lakini haukupita muda alikuja akamwambia mama, ‘nimetoka na ni lazima nitakuua.’
“Siku nyingine tena Shija akaja. Hii ni mara ya nne, tena alikuwa uchi. Akasema amefuata vitu vyake, mama akampigia simu mwenyekiti na kumtaarifu, akaja na wajumbe wengine wa serikali na kamati ya ulinzi ya kijiji wakamchukua Shija mpaka ofisini kwao, wakamuuliza kama alikuwa tayari kulipwa fedha akavinunue vitu hivyo, akasema yuko tayari kama atapewa shilingi milioni 3.
...Mazishi.
“Mama alimwambia kutokana na maisha yake yalivyo anamuomba amlipe shilingi elfu sabini, Shija akanyanyuka na kuuambia uongozi, ‘mnaona mama huyu alivyo na dharau, hiyo hela haitoshi thamani ya vitu hivyo, nitamuua tu,’’ alisema mtoto huyo akimkariri mtuhumiwa na kulia.
Naye mtoto wa pili wa marehemu, Sofia Mabula alisema: “Shija alifungwa kifungo cha nje cha miezi sita kutokana na makosa yake lakini cha ajabu ndani ya mwezi mmoja akatimiza lengo lake la kumuua mama.
“Sidhani kama mahakama ilistahili kumfunga kifungo cha nje maana alimtishia mama zaidi ya mara nne mwisho wa siku akamuua kweli, inauma sana.”
Mwenyekiti wa serikali ya  mtaa aliyejitambulisha kwa jina moja la Zakaria ‘Waiti’ alisema aliposikia kwa mara ya kwanza kuhusu madai ya vitu hivyo. Alijiuliza vilikuwa na nini cha zaidi!
...Waombolezaji.
“Niliwahi kumuuliza mtuhumiwa kwa nini aling’ang’ania vitu hivyo, akasema alipewa na babu yake ambaye kwa sasa ni marehemu na vifaa hivyo vilikuwa vinamsaidia katika maisha yake kwani vina nguvu ya ziada ndani yake,” alisema mwenyekiti huyo.
Akaongeza: “Alisema tochi kazi yake ilikuwa kuwatibu watoto wadogo wenye mtoto wa jicho, mwiko ulikuwa wa mti wa Mkula ambapo alikuwa akipikia chakula unampa nguvu za kulima. Kuhusu redio ilikuwa ikimsaidia kusikiliza matatizo ya watu.
Askari wa JWTZ aliyejitambulisha kwa jina la Koplo Deus wa Kikosi cha Wanamaji, Kigamboni ndiye  aliyemkamata mtuhumiwa wakati akikimbia kwa kujitumbukiza kwenye Bahari ya Hindi.
Kamanda wa Mkoa wa  Kipolisi Temeke, SACP Alibert Kiondo alithibitisha kutokea  kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa yuko mikononi  mwa polisi, uchunguzi  unaendelea ili kujua utimamu  wa akili yake.
Share:

Avunja Ndoa yake kwa kutamani maisha ya Wema Sepetu.....



Kuiga  ni  kawaida  kwa  wengi.Wapo  walioiga  mambo  fulani  na   hatimaye  wakafanikiwa, na  pia  wapo  walioiga  vitu  flani  wakaharibikiwa.Huyu  aliiga  na  akaharibu  kila  kitu...

Ni  msanii  wa  siku  nyingi  katika  fani.Alitamba  zaidi  akiwa  Kaole, na  hata  mwanzoni  mwa  ujio  wa  filamu  za  Kanumba  alizidi  tu  kashaini....

Kiasili  ni  mweusi  japo  siku  hizi  kuna  weupe  fulani  katika  ngozi  yake  nyororo.Ana  sura  nzuri  yenye  mvuto,umbo  aslia  la  kibantu,meno  yake  meupe  yamepambwa  na  mwanya  mdogo  na  kufanya  iwe  fahari  kumuona  akitabasamu...

Hana  kashfa  ya  kuvaa  nguo  fupi  sana  ila  aliwahi  kukumbwa  na  skendo  kubwa  zaidi.Mkumbuke  vizuri.Mrefu  wa  wastani,anajua  kutembea,anaongea  kwa  mapozi  huku  akipenda  kulamba  papi  ya  midomo  yake. Umemjua???....Hapana, siyo  huyo...!!

Huyu  ni  mpole  kiasili  na  anapendwa  sana  na  mama  yake.Katika  maigizo  ana  uwezo  wa  kukufanya  uamini  unachoangalia  ni  kitu  halisi.Japo  huwezi  kumtaja, ila  ndani  ya  wasanii  kumi  anapaswa  kuwamo...

Na  ingawa  mvuto  wake  umepungua  kiasi,ila  bado  mrembo  sana.Lakini  wakati  anaigiza  Kaole  alikuwa  mrembo  zaidi.Kwa  uzuri  wake ,  alivuma  na  kila  habari  inayohusu  mwanaume  maarufu  na  mwenye  pesa

Habari  ya  kutakiwa  na  kila  mwanaume , wenye  rangi  na    vipato  tofauti  zilisikika  kila  kona.Baadhi  alitoka  nao  na  wengine  haikuwa  bahati  yao....

Toka  kitambo  almanusura  aolewe, ila  ni  miaka  ya  juzi juzi  ndipo  aliolewa.Uzuri  wake  si  wa  kutafuta, kila  mwenye  macho  na  ngozi  ya  kuhisi  atautambua....

Mbali  na  majanga  yote  aliyopitia  katika  maisha  yake,mengine  yakibaki  kumchafua  na  watu  kudhani  hawezi  kuolewa  na  mwanaume  yeyote  kabla  ya  ile  bahati  ya  mtende  akaolewa; yeye  aliamua  kuachana  na  ndoa  yake  kwa  kuona  aishi  katika  umaarufu  wake....

Mara  kadhaa  alikuwa  akiwaambia marafiki  zake  kuwa, mwenye  hadhi  na  anayetakiwa  kuishi  kama  Wema  Sepetu  sio  Wema  bali  ni  yeye  na  wakongwe wengine  waliosotea  sanaa  na  kuipigania  kama  roho  zao  na  kuilinda  kama  mboni  ya  jicho  lao.....

Akaona  ndoa  sio  mahala  pake,bila  sababu  za  msngi  akaamua  kumwambia  mumewe  watengane....Japo  haikuwa  rahisi ,lakini  walitengana!!

Cha  kufurahisha  ni  kwamba  bado  Wema  anaishi  kama  Wema  na  bado  yeye  haishi  kama  Wema  Sepetu  na  ndoa  haipo  tena...Umemjua  ninayemzungumzia?
Share:

DAKTARI JIJINI MWANZA AFIA GESTI JIJINI DAR

MTU mmoja aliyedaiwa kuwa ni daktari wa jijini Mwanza, Raymond Simion (36) amekutwa amekufa ndani ya chumba kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti’ ijulikanayo kwa jina la Nesta iliyopo Ubungo NHC wilayani Kinondoni jijini Dar.
Mwili wa Dk. Raymond Simion ukitolewa kwenye chumba cha kulala wageni na polisi.
Taarifa kutoka katika gesti hiyo zinasema marehemu alijiorodhesha kwenye kitabu cha wageni kuwa ni daktari wa Hosptali ya Nyamagana jijini Mwanza na alikuja  Dar kikazi kwa muda wa wiki moja. Mauti yalimkuta akiwa na siku mbili tu tangu alipowasili.
Mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kuwa, daktari huyo alifika katika gesti hiyo Jumapili ya Mei 4, mwaka huu na kuchukua chumba namba 102.
Alisema Jumatatu ya Mei 5, marehemu aliomba abadilishiwe chumba, akapewa namba 105 ambamo mauti yalimkutia.
Mwili wa Dk. Raymond Simion ukipakizwa kwenye gari la polisi.
Uwazi lilifanikiwa kufika katika eneo la tukio na kufanya mahojiano na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ubungo NHC, Amani Sizian ambaye alisema taarifa ya kifo cha daktari huyo aliipokea saa 9: 03 alasiri ya siku ya tukio ambapo mhudumu wa gesti hiyo ndiye aliyempigia simu kumjulisha.
Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa mhudumu huyo alimweleza kwamba marehemu baada ya kuchukua chumba Jumapili alitoka na kurudi saa 3:00 usiku ambapo alilala, lakini kesho yake hakuonekana kutoka.
Nje ya eneo la tukio.
“Mhudumu aliniambia kuwa baada ya kutomwona asubuhi, hawakumfuatilia hadi ilipofika saa 9:00 alasiri ambapo walikwenda kumchungulia chumbani kwake na kumwona katika hali ya kutokuwa hai.
“Ilibidi niende. Nilipofika tukakuta mlango umefungwa kwa ndani.
Katika kumchungulia tulimwona mtu huyo akiwa amekaa kitandani bila kujigeuza jambo lililonifanya nipige simu polisi ambao walifika na kuvunja mlango na kumkuta akiwa amefariki dunia,” alisema mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa, katika chumba hicho alichofia mteja huyo, kulikutwa mabomba mawili ya sindano ambapo moja lilikwishatumika, pia kulikuwa na mifuko miwili yenye nguo na begi moja.
Polisi waliuchukua mwili na kuupeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili. Hata hivyo, ndugu wa marehemu walipatikana na mwili kufanyiwa uchunguzi na daktari kisha kuuchukua na kuusafirisha kwenda Mwanza kwa mazishi.
Chumba alipokuwa amelala marehemu Raymond Simion.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema: “Marehemu alikutwa na mabomba mawili ya sindano, moja lilishatumika na lilikuwa na masalia ya damu. Pia kulikuwa na kete moja ya vitu vinavyodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.
Share:

MASKINI DAVINA WA BONGO MOVIE APONZWA NA BIRTHDAY...!

Msanii wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’.
SHEREHE ya bethidei ya msanii wa filamu Vivian Minza ambaye ni shosti wa Halima Yahya ‘Davina’ iliyofanyika Mei 1, mwaka huu imedaiwa kuwa ndiyo chanzo cha kuvunja urafiki wa wawili hao. 
 Imeelezwa kuwa kutofautiana kwao ni Davina kutokwenda katika sherehe hiyo, ili kujiridhisha na madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Davina, akafunguka: 

“Mwenzangu kweli kanichunia lakini najua yataisha tu, sababu ni kutokwenda kwenye sherehe yake ya kuzaliwa kwani yeye huwa anajitoa sana kwangu, siku hiyo nilikuwa naumwa sana,” alisema Davina.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger