Friday, 9 May 2014

MEZA YA MAGAZETI:SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA 09/MAY/2014

1_81498.jpg
2_26178.jpg
3_ef8c9.jpg
4_a89d6.jpg
5_16397.jpg
7_24f31.jpg
8_41148.jpg
9_dac4a.jpg
10_2995c.jpg
11_bc604.jpg
12_a211f.jpg
13_ada82.jpg
14_14681.jpg
15_ebff3.jpg
16_4149e.jpg
Share:

MAGARI ZAIDI YA MIA YAKWAMA ENEO LA MANZESE BARABARA YA DAR ES SALAAM MTWARA

 Malori na Mabasi yakiwa kwenye msururu mrefu mara baada ya kushindwa kuendelea na safari kwa takribani masaa zaidi ya nane katika eneo la Manzese lililopo Kilwa barabara ya Dar Es salaam kuelekea Mtwara hapo jana kutokana na eneo hilo kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama
Baadhi ya wasafiri kwenye mabasi yaendayo Dar Es Salaam kutoka Mtwara, Lindi na Kilwa na yale yatokayo Jijini Dar Es Salaam kuekelea mikoa ya Kusini wakiwa wamesimama kushuhudia juhudi zinazofanya na vijana wa eneo la Manzese na baadhi ya madereva wa malori na mabasi pamoja na abiria kuhakikisha wanasaidia magari kuvuka ili kuweza kuendelea na safari zao.
 Wasafiri na wakazi wa Eneo la Manzese wakishuhudia greda lililofika kwaajili ya kusaidia kusawazisha eneo hilo na kutoa magari yaliyonasa kutokana na eneo hilo kujaa maji na tope zito yaliyosababisha magari kukwama kwa takribani masaa zaidi ya nane hapo jana.
Mabasi yatokeayo Mikoa ya Kusini kuelekea Bara yakiwa yamekwama katika eneo la Manzese - Kilwa kutokana na barabara kuwa mbovu katika eneo hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kusababisha magari zaidi ya mia kunasa na kutoendelea na safari zao kwa zaidi ya masaa nane.
Greda likiondoa tope na kusawazisha eneo hilo ambalo lilileta usumbufu mkubwa sana kwa watumiaji wa barabara ya Dar Mtwara na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama katika eneo hilo lililoaharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha. 

--
Share:

SHOW YA OMMY DIMOZ ILIOWAPAGAWISHA WATOTO WA KIKE PANDE ZA MAMTONI,



Share:

LISTEN AND DOWNLOAD BRAND NEW AUDIO:: MUULIZE MENEJA BY SUMA G FT PROF JAY


SIKILIZA NYIMBO HAPO CHINI

CHANZO: www.bongosound.com
Share:

KIJANA ACHOMWA MOTO HADI KUFA KWA TUHUMA ZA WIZI...TUNAOMBA RADHI PICHA HIZI ZINATISHA




Share:

Kuelekea kombe la dunia: Vikosi vya Ujerumani na Brazil vyatangazwa SOMA HAPA

 
72781_04_lgHoma ya kombe la dunia imeanza kupanda na timu kadhaa zimeanza kutangaza vikosi vya wachezaji watakaoenda Brazil kushiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuanza June mwaka huu.
Jana usiku kocha wa timu ya taifa ya Brazil Luis Fellipe Scolari alitangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 wataowawakilisha wabrazil kwenye fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchi kwao – kikosi kilikuwa kama ifuatavyo: Goalkeepers: Jefferson (Botafogo), Julio Cesar (Toronto FC), Victor (Atletico MG).
Defenders: Dante (Bayern Munich) David Luiz (Chelsea), Henrique (Napoli), Thiago Silva (PSG) Dani Alves (Barcelona), Maicon (Roma) Marcelo (Real Madrid), Maxwell (PSG).
Midfielders: Fernandinho (Manchester City) Hernanes (Inter) Luiz Gustavo (Wolfsburg) Oscar (Chelsea) Paulinho (Tottenham Hotspur), Ramires (Chelsea), Willian (Chelsea).
Forwards: Bernard (Shakhtar Donetsk), Fred (Fluminense) Hulk (Zenit) Jo (Atletico MG), Neymar (Barcelona).
Leo hii kocha Joachim Loew wa Ujerumani nae ametangaza kikosi cha awamu ya kwanza cha wachezaji 30 ambao watachujwa na kubakia 23 watakaobeba dhamana ya wajerumani Brazil mwaka huu: Goalkeepers : Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Borussia Dortmund), Ron-Robert Zieler (Hannover)

Defenders : Jerome Boateng (Bayern Munich), Erik Durm (Borussia Dortmund), Kevin Grosskreutz (Borussia Dortmund), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Marcell Jansen (Hamburg), Philipp Lahm (Bayern Munich), Per Mertesacker (Arsenal), Shkodran Mustafi (Sampdoria), Marcel Schmelzer (Borussia Dortmund)
Midfielders : Lars Bender (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Schalke), Matthias Ginter (Freiburg), Leon Goretzka (Schalke), Mario Gotze (Bayern Munich), Andre Hahn (Augsburg), Sami Khedira (Real Madrid), Toni Kroos (Bayern Munich), Max Meyer (Schalke), Mesut Ozil (Arsenal), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich)
Attackers : Miroslav Klose (Lazio), Kevin Volland (Hoffenheim), Lukas Podolski (Arsenal), Marco Reus (Borussia Dortmund), Andre Schurrle (Chelsea), Thomas Muller (Bayern Munich)
Share:

MTANZANIA MWINGINE AKAMATWA AIRPORT NAIROBI AKIWA NA MZIGO WA DAWA ZA KULEVYA.

Mwanaume mmoja Mtanzania amekamwata katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi Kenya akiwa amebeba dawa za kulevya akiwa njiani kuelekea Antananarivo ambapo mzigo huo ulitokea Tanga kisha ukapita Mombasa na baadae kwa ndege mpaka Nairobi.
Mzigo wenyewe ni wa cocaine na Heroin ambazo zote zina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 24 za Kitanzania na dawa hizo alikua  ameziingiza katika njia ya haja kubwa.
Mkuu wa kitengo cha CID katika uwanja huo Joseph Ngisa amesema mshukiwa alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba cha uchunguzi na baadae akatoa tembe za cocain na tembe za Heroin na tayari ameshapelekwa Mahakamani.

Mwezi March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja huohuo walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 75 za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Wanawake watatu na mwanaume mmoja kila mmoja akishtakiwa kando kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya na walikua wameingia Kenya kupitia Namanga na walikamtwa wakiwa njiani kuelekea Hong Kong.
Kuanzia March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano wamekamatwa kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za kusafirisha dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.
Share:

SUGU AMCHANA WAZIRI MAGUFULI

Akichangia jioni hii Mhe Sugu amesema kuwa Mhe Magufuli hafanyi kazi kitaalamu bali anapiga siasa tuu ili kupumbaza watu. Amesema kuwa hizo barabara anazojisifia na zinazotumia mabilioni mbona baada ya miezi michache zinqumuka na kuhitaji matengenezo makubwa wakati kuna barabara za zamani kama Makambako -Songea ni za zamani na bado zinahimili zaidi ya hizi?
Pia amezungumzia makampuni ya kigeni kama Strabag kuwazulumu vibarua wazawa naye kukaa kimya kwa hilo zaidi ya kujisifia binafsi.
Kamaliza na kusema kama anajipigia debe la urais huko asahau bali mahali panapo msahili ni jela kwa kushiriki kwake ubadhilifu
Share:

NYIMBO MPYA YA MWANA FA FT G NAKO - MFALME

http://bongosound.com/admin/audio_images/mfalme.jpg  CHANZO: www.bongosound
Share:

RAY C ASIMULIA ALIVYOKICHUNGULIA KIFO


MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya Dengue.

Akifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa huo.
Alisema kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari lake na kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.
Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu.
“Huwezi kuamini baada ya madaktari kunipima na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue, walinishangaa sana hata namna nilipofika pale na kwamba sikutumia dawa yoyote ya kutuliza maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni lazima utatafuta tu dawa ya kukufanya upoze maumivu.
“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’ unaweza kupoteza maisha mara moja.
“Katika magonjwa ya ajabu na yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja basi huu ni ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa iwe macho sana maana haufai hata kidogo.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.
“Mateso niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa Mwananyamala ni elimu tosha kabisa na kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa nchi basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada za haraka kuhakikisha wanapata chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol tu!” alimalizia Ray C.
Share:

MAIMARTHA AWAUZIA MASTAA DAWA ZA KUKUZA MAKALIO


MTANGAZAJI aliyepata kuwika katika vituo mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha Jesse, amedaiwa kuwauzia mastaa wa mjini dawa za kuongeza makalio.Habari za moto kutoka kwa sosi wa kuaminika, zinasema kuwa Maimartha ambaye pia huitwa Mai amefikia hatua hiyo baada ya yeye kutumia na kufanikiwa.
Mtangazaji aliyepata kuwika katika vituo mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha Jesse.
“Hamshangai siku hizi kila staa anaonekana kuwa na makalio makubwa? Ni kazi ya Mai hiyo. Anafanya hiyo biashara muda mrefu sana. Ni za kunywa na kupaka.
“Mbona hata yeye ametumia dawa hizo muda mrefu sana? Ukimwangalia utagundua zamani hakuwa na hipsi za kiivyo. Ni kwa sababu ya dawa,”  alisema sosi huyo.
Akaongeza: “Hata Lulu Semagongo (Aunt Lulu)   ndiye aliyemsababishia kuwa na makalio makubwa kwani wakati wako karibu alikuwa akimpa dawa hizo.”
Waandishi wetu walifika dukani kwa Mai bila kujua kama ni waandishi na kuulizia bidhaa hizo ambapo zilitolewa, wakapiga picha bila kugundulika.
Mai akiwa hajui kuwa yupo mikononi mwa mapaparazi waliokuwa na njaa ya habari, aliwaambia: “Ni dawa nzuri, mara moja zinarekebisha umbo na unakuwa wa kuvutia. Kuna za shilingi 250,000 na 260,000 inategemea kama ni vidonge au losheni.”
Mapaparazi wetu walipompigia simu Mai baada ya kutoka dukani hapo na kumweleza kuhusu uuzaji wa dawa hizo dukani kwake, alisema duka lake linauza urembo wa aina zote kwa mastaa na wasio mastaa.
“Kama nimetumia dawa za kuongeza makalio, nyie inawahusu nini? Kifupi duka langu linadili na urembo wa aina zote,” alisema Mai akishindwa kufafanua zaidi.
Lulu alipovutiwa waya na kuulizwa kama makalio yake ni matokeo mazuri ya dawa za Mai alisema: “Sijawahi kutumia dawa za Mai kwa ajili ya kuongeza makalio.
Yangu ya asili lakini watu wakinipigia simu na kuniuliza dawa za kuongeza makalio huwa nawaelekeza kwa Mai.”
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger