Saturday, 25 May 2024

SERIKALI YADHAMIRIA KUKAMILISHA MIPANGO SITA YA USALAMA WA CHAKULA NCHINI

...
Mkurugenzi wa masoko na Usalama wa chakula kutoa wizara ya kilimo Gungu Mibavu akizungumzia jambo wenye mkutano huo

Na Christina Cosmas, Morogoro

SERIKALI imedhamiria kukamilisha mipango sita ya malengo endelevu ya suala la usalama wa chakula nchini kupitia Maendeleo ya Milenia (SDG) ya mwaka 2021/30 kabla ya mwaka 2030.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa masoko na usalama wa chakula kutoka Wizara ya Kilimo Gungu Mibavu wakati akifungua mkutano wa wadau wa masuala ya kilimo ulioandaliwa na Shirika la Kilimo na chakula (FAO) na kufadhiliwa na UN na kufanyika mkoani Morogoro.

Mibavu ameitaja baadhi ya mipango hiyo sita ya usalama wa chakula nchini kuwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula, mifugo na uvuvi na kuongeza uhakika na ziada ya chakula nchini.

Mibavu anasema asilimia kubwa ya mipango ya usalama wa chakula nchini imeshakamilika.

Mratibu wa uhimilivu wa mifumo na chakula kutoka Zanzibar Sihaba Vuai amesema serikali katika Kufanya mageuzi ya chakula imeweka kipaumbele kwenye mazao ya kilimo sambamba na kushirikisha  wadau wa kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Washiriki wakimsikiliza mtoa mada hayupo pichani
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger