Thursday, 30 May 2024

MWANAFUNZI WA DUCE AIBUKA NA MFUMO WA KUZUIA UPOTEVU WA MAJI NA KULINDÀ UHARIBIFU WA PAMPU

...


Bw. Kalua Polikarpo, Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu (BSc. Ed) kutoka katika Idara ya Fizikia, Hisabati na Infomatiki ( PMI ) iliyo chini ya Kitivo cha Sayansi ( FoS ) abuni mfumo wa kudhibiti mtiririko wa maji unaotokea pindi maji yanapojaa kwenye matanki na kuzuia uharibifu wa pampu.

Hayo yamedhihirika katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 yanayoendelea hapa jijini Tanga

DUCE tunayo furaha kubwa kuujulisha Umma kuwa Bw. Kalua Polikarpo, Mwanafunzi wetu wa Mwaka wa Tatu anayesoma _Shahada ya Sayansi ( Hisabati na Fizikia) na Elimu_, ameonesha ujuzi wa hali ya juu kwa kubuni mfumo wa kuzuia upotevu wa maji na kupunguza uwezekano wa kuungua kwa pampu kutokana na kuvuta upepo kwa muda mrefu. 

Akifafanua hayo, Bw. Kalua amesema mfumo huo utasaidia kuratibu matumizi bora ya maji. 

Zaidi amesema kuwa mfumo huo mpya utaokoa gharama za matengenezo na ununuzi wa pampu mpya. 

Kimsingi, mradi huu utaleta suluhisho muhimu kutokana na changamoto zinazoikabili jamii yetu. Aidha, ubunifu huu unadhihirisha uwezo wa wanafunzi wetu katika nyanja za elimu, sayansi, na teknolojia.

 Kwa dhati, tunampongeza na tunajivunia ubunifu huu ambao ni chachu kwa maendeleo ya jamii na Taifa. 

Karibuni katika viwanja vya Popatlal jijini Tanga, kushuhudia na kujifunza zaidi kuhusu maonesho ya miradi mbalimbali yenye ubunifu wa hali ya huu kama huu kutoka kwenye Chuo chetu. Hii inadhihirisha kuwa DUCE ni zaidi ya ualimu.

#DUCE #WikiYaElimu2024 #Ubunifu #Ujuzi #ElimuNaSayansi #ProudlyDUCE #Kalua #SaveWater #SustainableLiving #DUCEnizaidiyaualimu


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger