Saturday, 17 July 2021

AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMFUNGIA NDANI KISHA KUCHOMA MOTO NYUMBA DAR

...

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro Jumanne,

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia Grace Mushi (25) kwa tuhuma za kumuua aliyekuwa mpenzi wake Khamis Abdallah (25), mkazi wa Mbezi Makabe baada ya kumfungia ndani ya nyumba na kuimwagia mafuta ya petroli na kisha kuichoma moto nyumba hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Muliro Jumanne, na kusema kuwa tukio hilo limetokea Julai 16, 2021, majira ya saa 8:30 usiku na uchunguzi umebaini kwamba wapenzi hao walikuwa na mgogoro mkubwa wa mapenzi.

"Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alijaribu kutoroka lakini kwa kushirikiana na wananchi alikamatwa na uchunguzi wa awali umeonesha kwamba ulikuwepo mgogoro mkubwa wa kimpenzi kabla ya kufanyika kwa tukio hili la mauaji ya kikatili," ameeleza Kamanda Muliro.

CHANZO - EATV
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger