Wednesday, 19 May 2021

Waziri Kalemani amsimamisha kazi Meneja TEHAMA TAESCO kisa ununuzi wa luku

...


Waziri wa Nishati Mh.Dkt.Medard Kalemani ameagiza kusimamishwa kazi kwa siku 10  watumishi watatu wa TANESCO akiwemo Meneja wa mfumo wa LUKU kwa kushindwa kutatua tatizo la LUKU lililojitokeza kwa siku tatu na kuleta  usumbufu kwa wananchi.

Waliosimamishwa kazi ni Meneja wa TEHAMA na huduma za biashara wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Lonus Feruzi na Wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Njau ili watoe maelezo kufuatia kuwepo kwa tatizo katika huduma ya manunuzi ya LUKU kupitia njia za kielektroniki na kusema endapo maelezo yao hayatojitosheleza wataondolewa kazini.

Kwa muda wa siku tatu, Wateja wa TANESCO wameshindwa kununua umeme wa LUKU kwa njia ya Kielekroniki hivyo kulilazimu Shirika hilo kuwaelekeza Wateja wake kununua umeme kwenye ofisi zake za Mikoa na Wilaya katika maeneo mbalimbali nchini.



Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger