Sunday, 28 March 2021

Picha : TGNP, UNFPA WAUNDA NGUVU YA PAMOJA NA WASAIDIZI WA KISHERIA, VIONGOZI WA VIJIJI NA KATA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

...

Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee akifungua kikao cha Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala. Kushoto ni Mratibu wa Huduma za Msaada wa Kisheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) mkoa wa Shinyanga, John Shija.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na la shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) wamekutana na Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa, ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa ajili ya kujadili na kupanga mikakati kuhusu njia za kuondoa Ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake na watoto.

Kikao hicho kimefanyika leo Jumapili Machi 28,2021 katika kijiji cha Shilela ambacho ni sehemu ya vijiji vitano vinavyounda kata ya Shilela ambapo vingine ni Nyikoboko, Malito, Ndala na Ilelema.

Akifungua kikao hicho, Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee amesema lengo ni kuongeza ushirikiano zaidi baina ya viongozi kata na wa serikai za mitaa wakiwemo wenyeviti wa vijiji na vitongoji, Wasaidizi wa Kisheria na Vituo vya taarifa na maarifa katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia.

“Endapo makundi haya yatashirikiana kwa ukaribu matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yatapungua. Naomba makundi haya na wadau wengine waendelee kushirikiana ili kuondoa ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kumaliza changamoto ya utoro wa rejareja kwa wanafunzi katika shule za sekondari na msingi”,alisema Mwanaidi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Huduma za Msaada wa Kisheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) mkoa wa Shinyanga, John Shija alisema matukio ya ukatili wa kijinsia yanaendelea kujitokeza kutokana na uwepo wa mila na desturi kandamizi zinazokandamiza mwanamke na mtoto lakini pia ukosefu wa elimu ya sheria hali inayochangia waathirika wa matukio ya ukatili kukosa haki zao.

“Ushirikiano huu tuliouanzisha katika kata ya Shilela na Lunguya katika halmashauri ya wilaya ya Msalala kwa ufadhili wa TGNP na UNFPA utawezesha kukuza ustawi wa jamii. Tukipigana vita hii kwa pamoja naamini kabisa hakuna vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vitaonekana majumbani wala mtaani. Wanawake na watoto watakuwa salama kuanzia nyumbani hadi mtaani”,alisema Shija.

Aidha aliwataka washiriki wa kikao hicho kuongeza uwajibikaji kila mmoja kwenye eneo lake na kama viongozi wa vijiji na kata watashindwa kushughulikia mashauri wanayoona yapo juu ya uwezo wao basi wayapeleke ngazi za juu zaidi.

Katika kikao hicho kilichojikita katika kufanya mapitio ya mipango kazi baina ya makundi hayo katika kutokomeza ukatili wa kijinsia suala la utoro kwa wanafunzi shuleni pia limejadiliwa na kuweka mikakati ya kuwarudisha shuleni wanafunzi watoro.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Malito, Furaha Mashamba alisema suala la utoro wa wanafunzi shuleni linasababishwa na wazazi na walezi kutotimiza vyema majukumu yao ikiwemo kuwapatia mahitaji muhimu kama vile madaftari na sare za shule hali inayosababisha watoto wachukie shule.

Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ilelema, Prisca Leonard Lunyili alisema bado kuna baadhi ya wazazi wana tamaa ya kupata mali hivyo wanarubuni watoto wafeli kwenye mitihani ili wawaozeshe lakini pia watoto kutumia muda mwingi wakichunga ng’ombe hali inayosababisha wasihudhurie masomo.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Shilela, Daniel Paul aliwataka wazazi kushirikiana na walimu na kuhamasisha wanafunzi kwenda shule badala ya kuwapa kazi za nyumbani na kuchunga ng’ombe na kusababisha utoro wa reja reja matokeo yake wanapoteza vipindi darasani.

Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela kinachosimamiwa na TGNP , Joseph Samwel Mbunge alieleza kuwa wanaendelea kufuatilia wanafunzi watoro na kuwarudisha shuleni pamoja na kutoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia kwa jamii.

Naye Msaidizi wa Kisheria Hawa Hashim kutoka kata ya Bulyanhulu alisema wasaidizi wa kisheria wanaendelea kutoa elimu ya masuala ya kisheria katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee akifungua kikao cha Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala ambapo alisema lengo ni kuongeza ushirikiano zaidi baina ya viongozi kata na wa serikai za mitaa wakiwemo wenyeviti wa vijiji na vitongoji, Wasaidizi wa Kisheria na Vituo vya taarifa na maarifa katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee akifungua kikao cha Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala
Mratibu wa Huduma za Msaada wa Kisheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakijadili namna ya kuweka nguvu katika kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo mila na desturi kandamizi.
Mratibu wa Huduma za Msaada wa Kisheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) mkoa wa Shinyanga, John Shija akiwasisitiza Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala kuweka nguvu katika kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo mila na desturi kandamizi.
Mratibu wa Huduma za Msaada wa Kisheria Kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala

Msaidizi wa Kisheria Hawa Hashim kutoka kata ya Bulyanhulu akiwasilisha mpango kazi wa wasaidizi wa kisheria katika halmashauri ya wilaya ya Msalala katika kutokomeza ukatili wa kijinsia
Katibu msaidizi wa Kituo cha taarifa na maarifa kata ya Shilela, Joseph Samwel Mbunge akiwasilisha mpango kazi wa kituo hicho katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia
Wakili Jesca Makalwe akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kisheria kwenye kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia
Wakili Jesca Makalwe akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kisheria kwenye kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia
Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiendelea na kikao
Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye kikao

Afisa Mtendaji kijiji cha Shilela, Shemenzi Ngeleji akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Shilela, Daniel Paul akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Malito, Furaha Mashamba akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyikoboko, Godfrey Masiku akichangia hoja kwenye kikao hicho
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ilelema, Prisca Leonard Lunyili akichangia hoja namna ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiendelea na kikao
Mwana kituo cha taarifa na maarifa kata ya Shilela Maulid Ibrahim akichangia hoja katika kikao hicho
Makamu Mwenyekiti wa kituo cha taarifa na maarifa kata ya Shilela,Lameck Masolwa Manyesha akichangia hoja kwenye kikao hicho
Kikao kinaendelea
Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’, Viongozi wa serikali za mitaa,ngazi ya kata na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiendelea na kikao.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger