Friday 29 September 2017

MKUU WA WILAYA BUSEGA DC TANO MWERA, AZINDUA RASMI ZOEZI LA UANDIKISHAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA KATA YA MWAMANYILI-BUSEGA

...

Mkuu wa wilaya ya Busega Bi Tano Mwera azindua rasmi zoezi la kuandikisha vitambulisho vya taifa, katika kata ya Mwamanyili wilayani Busega. 













Akizundua zoezi hilo Mkuu wa Wilaya amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kuja kuandikisha. Vile vile mkuu wa wilaya ameeleza faida ya wananchi  kuwa na kitambulisho cha taifa ni pamoja na kusaidia serikali kujua idadi kamili ya raia wake ili iweze kupanga maendeleo ya nchi vizuri. 

 
Vitambulisho hivyo vya Taifa pia vitasaadia kutoa wafanyakazi hewa katika mfumo wa malipo ya serikali,Vitasaidia pia kwa mtu binafsi kutumika kama kitambulisho chake anapoenda sehemu mbali mbali za kupata huduma kama vile Banki. Na kama serikali vitambulisho vitasaidia kuwabana wakwepa kodi. Kwa ujumla vitambulisho vinafaida nyingi. 
 
"Ndugu wananchi nawasihi msambaze habari hii kwa wote ambao hawakufanikiwa kuwa hapa leo waje wajiandikishe. Zoezi hili ni endelevu ila kwa sasa limezogezwa karibu na wananchi. Ni vizuri mkatumia nafasi hii." Alimalizia Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya

Baadhi ya wananchi wakifatilia mkutano wa ufunguzi chini ya DC TANO S.MWERA

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger