Thursday 28 September 2017

BUSEGA YAPATA NEEMA ,SASA KESI ZOTE KUSIKILIZWA BUSEGA BADALA YA BARIADI MJINI

...
 





Kilio cha muda mrefu cha wilaya ya Busega kimepata majibu. Tarehe 26/ 09/ 2017 Jopo la Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Tanzania kanda ya Shinyanga Mhe Richard M. Kibella lilitembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega Bi Tano S. Mwera na kumhakikishia kuwa, kuanzia sasa kesi zote za mahakama ya wilaya zitakuwa zinasikilizwa katika mahakama wa mwanzo Nyashimo badala ya Bariadi kama ilivyokuwa hapo awali. 
 
Hatua hii inasaidia wilaya ya Busega kuokoa takribani shillingi milioni moja na laki sita ya Kitanzania iliyokuwa inatumika kila mwezi kwa ajiri ya kusafirisha watuhumiwa, mashahidi na Askari wa upelelezi Bariadi pamoja na usumbufu mwingine waliokuwa wakiupata. 
 
Kwa upande wake Jaji mfawidhi amesema "lengo ni kusogeza huduma kwa wananchi na akaongeza kwa kusema kuwa muhimili wa mahakama umetengwa na inaonyesha raia hawauelewi vizuri, wananchi wanaweza kuchangia ujenzi wa shule, zahanati, kituo cha polisi n.k. Lakini hawawezi kufanya hivyo kwa mahakama.
 
 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Busega alimshukuru sana Jaji Mfawidhi kwa maamuzi hayo yenye tija kwa wilaya ya Busega kwani muda mlefu wamekuwa wakiomba kutokana na changamoto za wavuvi haramu na kadhalika. Na kuahidi kulifanyia kazi ombi la Jaji mfawidhi la kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa mahakama na mchango wake katika maendeleo ya taifa. Akaongeza kwa kusema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe Rais John Pombe Magufuli ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha tunamaliza kero zote za wananchi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger