Tuesday 18 July 2017

USHAURI KWA FORM SIX WALIOKOSA SIFA ZA KWENDA CHUO KIKUU KUHUSU NINI CHA KUFANYA

...


USHAURI NINI CHA KUFANYA KWA FORM SIX AMBAO HAWAJAPATA VIGEZO VYA KWENDA CHUO KIKUU 2017/2018

Habari yako?
Kama tulivyokuahidi kuhusu kutoa ushauri na mwongozo kwa wanafunzi wa kidato cha sita ambao hawakufikisa vigezo vya kwenda chuo kikuu mwaka huu 2017.
Ili uende chuo kikuu lazima uwe na minimum points of 4(D D) AU 4(C E) katika masomo yako mawili uliyosoma.


Wanafunzi wengi mwaka hawatweza kwenda chuo kikuu hasa sayansi kutokana na wengi kuwa na D E ambapo ukijumlisha unapata 3 pts badala ya pts 4 zinazohitajika.

Kawaida yangu Blogger boy ni kukupa kitu roho inapenda ili ukawaeleweshe wenzako wote.
NINI UFANYE BAADA YA KUTOKUPATA POINTS ZA KWENDA CHUO KIKUU
Kitu cha kwanza ninachopenda kukushauri kwanza usisumbuke kuomba chuo kikuu kama haujafikisha points kwani utapoteza pesa yako bure,ukiangalia mwaka jana kuna watu hawakua na points za kwenda chuo kikuu wakajaribu kuomba lakini mwisho wa siku walishindwa kwenda chuo kutokana na kutokuchaguliwa.

Kama wewe ni mwanafunzi uliesoma sayansi advanced level kati ya combination zifuatazo PCB,PCM,CBG,CBN,PGM ninaimani kwamba o level ulisoma masomo ya sayansi.

Basi kama jibu ni ndio ,cha kwanza ninachokushauri TUMIA CHETI CHAKO CHA FORM FOUR kufanya application katika vyuo vya afya na uombe kozi za afya kama pharmacy,nursing au clinical officer.

Unapotumia cheti cha form 4 kumbuka kuambatanisha na RESULT SELEEP yako ya ACSEE hii itaupa uzito ktk kufanya application yako iweze kukubaliwa kwa uharaka zaidi.

TIMIZA NDOTO YAKO
Kutokwenda chuo kikuu kusikufanye ukate tamaa na kuamua kuolewa au kuoa,soma kitu unachokipenda maishani kwa mfano;
“assume unataka kua mwalimu na unapenda kufundisha ualimu nenda kasomee ualimu” hii inamaana kwamba ukifanya kitu unachokipenda maishani lazima ufanikiwe tu,”DO YOUR PASSION”.

Watu wengi wamekuwa wakishindwa kufanikiwa maishani mwao kutokana na kusoma kitu ilimradi upate mshahara mkubwa au uajiriwe,hii sio sahihi hata kidogo,kwani endapo usipopata kazi itakufanya ujutie elimu yako.

Sasa hivi kuna vyuo vingi sana ambavyo vinapokea maombi kwa wanafunzi wanaotaka kusoma diploma,ninakusihi tumia nafasi hii kabla deadline haijafika,kwa sababu unaweza ukasema mwaka huu huendi chuo mwakani ukakuta hata vigezo vya kwenda diploma hauna.

Kwa watu waliosoma combinations tajwa hapo juu,wanaweza pia wakaomba vyuo kama DIT,ATC au MBEYA UNIVERSITY kozi mabalimbali ambazo ni nzuri sana.

Mfano;wewe malengo yako yalikuwa kusomea CIVIL ENGINEERING chuo kikuu lakini baada ya matokeo umekosa points za kukufanya kwenda chuo kikuu,usikate tama omba diploma ya civil engineering chuo cha DIT,MBEYA AU ATC,one day utafikia malengo yako.

KOZI GANI NZURI UOMBE?

 (i)Ordinary Diploma in Civil Engineering

(ii)Ordinary Diploma in Computer Engineering

(iii)Ordinary Diploma in Electrical Engineering

(iv)Ordinary Diploma in Electronics &Telecommunications Engineering

(v)Ordinary Diploma in Mechanical Engineering

(vi)Ordinary Diploma in Mining Engineering

(vii)Ordinary Diploma in Science &Laboratory Technology (Main Campus)

(viii)Ordinary Diploma in Science &Laboratory Technology (Mwanza Campus)

(ix)Ordinary Diploma in Biomedical Equipment Engineering

(x)Ordinary Diploma in Information Technology

(xi)Ordinary Diploma in Multimediaand Film Technology

(xii)Ordinary Diploma in Communication Systems Technology

(xiii)Ordinary Diploma in Renewable Energy Technology

(xiv)Ordinary Diploma in Food Science and Technology
(xv)Ordinary Diploma in Biotechnology

(xvi) Water Supply and Sanitation Engineering
(xvii)Hydrology and meterology
(xviii)
Hydrogeology and Water Well Drilling
(xix)
Irrigation Engineering
(xx) Water Quality Laboratory Technology
(xxi) Diploma in Veterinary Laboratory Technology DVLT
(xxii)
Veterinary Laboratory technology
(xxiii)
Animal Health and Production
(xxiv)
Diploma in Range Management and Tsetse Control-DRMTC

Kozi nyingi tajwa hapo juu zinahitaji sifa ndogo sana,tafadhali nakuomba usikate tama mda bado unao.

KUHUSU MKOPO
Pia baadhi ya kozi hapo juu watakusomesha bure endapo utachaguliwa ,kozi wanazotoa mikopo ni irrigation engineering-diploma ambayo ipo chuo cha maji.

ADA YA APPLICATION
Kila chuo kina da yake lakini vingi ada yake ni tshs 20000 hadi 30000 amabyo ninaimnai unweza ukaafford.

MWISHO KABISA NINAKARIBISHA MASWALI NA MAONI
Wako;
Innocent(blogger boy)
MASWAYETU BLOG DIRECTOR




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger