Wednesday 19 July 2017

MPYA:JINSI YA KUOMBA CHUO MWAKA HUU WA MASOMO 2017/2018

...
Habari yako?

Kwanza kabisa naepnda kumshukuru Mungu kwa kuzidi kunipa nguvu na akili ya kuzidi kuwatumia kwa kuwapa vitu muhimu hasa kipindi hiki cha uombaji wa vyuo vikuu 2017.

Watu wengi wamekuwa wakiuliza na kujiuliza je mwaka huu tunaombaje vyuo?

Maswayetu blog itaongelea jinsi ya kutuma maombi.

Kwa muda mrefu wanafunzi wengi wamekua wakiomba vyuo kupitia TCU au NACTE.Lakini mwa ka huu hali imebadilika ambapo wanafunzi watatakiwa kufanya application direct chuoni kupitia mfumo wa online ambao utakuwa umeandaliwa na chuo husika.

Lakini baadhi ya vyuo vinapokea maombi kwa njia ya barua ambapo hadi sasa hivi kuna vyuo 14 vilivyotoa form za kutuma maombi ya kujiunga masomo mwaka huu 2017/2018.

JINSI YA KUOMBA CHUO

Ili uweze kutuma maombi tafadhali ingia katika tovuti ya chuo husika ,kwa mfano unataka kwenda chuo kikuu SUA ,ingia google andika chuo kikuu SUA ,then itakuja official website ya SUA then ingia hapo,angalia habari mpya za admission ambazo ukiingia tu katika website husika lazima utakua Taarifa na form ya maombi.

ADA YA KUOMBA CHUO

Hapo awali watu walikua wanalipa tshs 50000 TCU na unaruhusiwa kuomba vyuo 5 unavyopenda kwenda,lakini kwa mwaka huu hali ipo tofauti kwani kila chuo utakachotaka kuomba lazima ulipie pesa,ambapo pesa ya maombi ina range kuanzia 20000 hadi 50000 inategemea na chuo,mfano endapo utataka kuomba vyuo 5 lazima uwe na kiasi kisichopungua 150,000/=.

KOZI NGAPI UNARUHUSIWA KUOMBA KWA KILA CHUO?

hii inategema na chuo husika kuna baadhi ya vyuo wanaruhusu kuomba hadi kozi tatu tofauti lakini kuna vyuo vingine unaruhusiwa kuomba kozi moja tu.

JE,USIPOCHAGULIWA CHUO ULICHOOMBA UNAFANYAJE?

Hili swala lipo hasa kutokana na competition,mfano Chuoni SUA kozi ya BVM inahitaji wanafunzi 70 tu,ambao waeomba ni wanafunzi 870,wakati wakufanya selection huwa wanaangalia mwanafunzi mwenye sifa za juu kushinda wote.

Basi endapo utaomba usipopata Chuo kinatakiwa kiwasilishe majina TCU ya wanafunzi waliokosa ili TCU watayatangaza nini cha kufanya.

Maombi yanataanza tarehe 22.7 2017 na kuishia one month later.

NOTE:kwa wanafunzi waliokosa sifa za kwenda chuo kikuu hadi sasa application zilishaanza na mwisho ni august 20 2017,kama unataka kuomba vyuo vya serikali tafadhali utaomba kupitia tovuti ya nacte.go.tz kwa afya na ualimu.

MWISHO

MASWAYETU BLOG INAKUTAKIA APPLICATION NJEMA NA TUNAOMBA ENDELEA KUTEMBELEA BLOG YETU KWA HABARI ZAIDI KUHUSU VYUO VILIVYOANZA KUPOKEA MAOMBI.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger