Saturday 23 January 2016

Ostaz Juma: Miaka 10 na wanamuziki ilitaka kunivunjia ndoa

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
_MG_4483
Meneja wa muziki hapa Bongo, Ostaz Juma Namusoma.
Musa mateja
UKIANZA kutaja majina ya mameneja mbalimbali wa muziki hapa Bongo, baadhi ya majina makubwa yasiyoisha miongoni mwao huwezi kulikosa jina la Ostaz Juma Namusoma.
_MG_4486 Kwa mujibu wa kinywa chake mwenyewe Ostaz Juma Namusoma, juzikati nilipata nafasi ya kumbana na kunieleza kiunagaubaga namna alivyoweza kujipenyeza hadi kupata jina kupitia muziki wa Bongo.
Kwa kinywa chake aliniambia kwamba, muziki kwake ni sehemu ya maisha ambayo ameishi kwa kipindi kirefu sana, kwani tangu alipokuwa mdogo alipenda muziki kushinda kitu chochote, msikie mwenyewe.
OSTAZ JUMA: Mimi ni miongoni mwa vijana wa kipindi hicho ninayetokea Musoma mkoani Mara. Nilianza kupenda muziki tangu nasoma shule ya msingi tena mapema kabisa nikiwa darasa la tatu.
Nikiwa shuleni nilikuwa napenda sana kuimba nyimbo mbalimbali za wasanii wa Kongo hadi nikafikia hatua ya kununua redio na kuwarekodi watoto wenzangu wakiimba kisha nazitunza nyimbo walizokuwa wakishindana kuimba hasa za Boringo za Wazaire.
_MG_4506
Nimefanya hivyo hadi nikawa nagombezwa na wazazi wangu lakini sikukoma hadi nilipokuwa mtu mzima na kuanza kujifanyia mambo yangu ambapo wazazi hawakuweza kuniingilia.
Kwa jinsi hii ndiyo utaweza kugundua kuwa nina kipaji cha kusimamia watu ndiyo maana nimeweza kuwasaidia wanamuziki wengi tu kwenye dansi ambapo kabla ya kujiingiza katika Bongo Fleva niliwahi kuwasaidia wanamuziki wa dansi kama Ally Chocky, Super Nyamwela, Jose Mara, Kalala Junior, Nyoshi El-Saadat, Mwinjuma Muumini na Mulemule.
Tabia za wanamuziki kiukweli hazipishani sana hivyo ukiona meneja yeyote analalamika juu ya wanamuziki basi ujue matatizo yao mara kadhaa yamekuwa hayapishani sana, ila wanaopishana tabia na namna ya kuongoza ni mameneja tu.
_MG_4516
Namna ya kuongoza na kummeneji mtu kunategemeana na uwezo wa kifedha na akili pia, nasema hivyo kwa sababu muziki wetu umekuwa ukiyumba mara kadhaa kutokana na baadhi ya mameneja kuwa wasimamizi wabovu na wengine wanasimamia wakiwa hawana fedha ya kuweza kuwaongoza wasanii.
Meneja ninayeweza kumpa saluti hapa Bongo ni Saidi Fella kwani ameonesha njia kubwa ya kuimarisha Muziki wa Dansi na sasa umeanza kuwa juu kiasi cha watu kuanza kuupenda tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ulianza kupoteza dira.
ALIANZAJE KUSIMAMIA BONGO FLEVA?
Ostaz Juma: Kwenye Bongo Fleva niliingia baada ya kuanza kumsimamia shemeji yangu aitwaye Abdallah David aliyekuwa akijiita Fil David, huyu nilijikuta namsimamia baada ya kumuona ana kipaji kizuri na baadaye nikaanzisha rasmi kampuni yangu ya Mtanashati.
Mtanashati ilipoanza tu nikapunguza kuwasaidia wanamuziki wa dansi hivyo nikajikita kwenye Bongo Fleva ambapo nilianza kumsimamia marehemu Sharo Milionea aliyemleta Kitale, lakini kabla sijaingia mkataba na Sharo akafariki dunia.
Baada ya kufariki kwa Sharo Milionea ambaye ndiye msanii naweza kujisifia katika upande wa Bongo Fleva kwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana, nilimchukua PNC, Dogo Janja na Happy Balis ambao nilifanyanao project kibao kiasi ilifikia hatua nikawa nakosana hadi na mke wangu kisa muziki huu.
Nimekuwa nikiwasaidia wasanii hawa kwa muda lakini nilichoweza kujifunza ni kwamba wasanii wengi hawana adabu kabisa, kwani kuna siku niliwahi kukosana na mke wangu kwa kushindwa kumpeleka hospitali kisa kumpeleka Dogo Janja kwenye interview jambo ambalo mke wangu amekuwa akinikumbusha kila mara nami huwa halitoki kichwani hadi leo.
Fedha niliyowahi kutumia hadi leo kwa ajili ya Dogo Janja na PNC naweza kujenga hata ghorofa tatu hapa mjini, lakini kwa kuwa nilikuwa naupenda muziki ndiyo maana leo utaona inafikia muda sasa nimeamua kuachana na hawa Bongo Fleva maana hawana nidhamu hata tone ila ukilinganisha na wanamuziki wa dansi utagundua ni bora dansi kuliko Bongo Fleva.
Nasema wanamuziki wa dansi ni bora kuliko wa Bongo Fleva kwa sababu wakati nadili na wanamuziki wa dansi walikuwa wanaonesha nidhamu ya hali ya juu jambo ambalo wanalifanya hadi sasa.
Ujue nilikuwa nikiwapatia fedha za kodi za nyumba, mara nyingine kama Christian Bella na Chocky hawa niliwahi hata kuwalipia studio mara kadhaa kwa ajili ya kurekodi nyimbo zao binafsi.
Christian Bella yeye aliwahi hadi kunitungia wimbo ambao unaitwa Ubinadamu ambao hata yeye ukimuuliza leo anaujua na ninao mimi mwenyewe.
Wasanii wakijua kuwa muziki ni kazi na sehemu ya maisha yao basi hakuna Bongo Fleva atakuja kushindwa kufanya mambo makubwa kama anavyofanya Diamond kwani kinachomfanya kuheshimika na kufanikiwa ni nidhamu yake tu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger