Saturday 23 January 2016

Apiga chini shule, aondoka kwao, aanza harakati za muziki

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


BELAChristian Bella ‘Obama’
Wiki iliyopita ndipo tulianza na Christian Bella ‘Obama’ kwenye kolamu hii akisimulia juu ya maisha yake, aliishia kusimulia pale ambapo hali ya kiuchumi kwenye familia yao ilipobadilika kutoka ya ‘kishua’ na kuwa ya kifukara, akalazimika kuingia mitaani kujitafutia kipato, akajifunza pia kutengeneza mikate kwenye kiwanda-bubu kilichokuwa nyumbani kwao na rafiki yake Junion Kumbukumbu.
Tambaa nayo…
“Enhee, baada ya kuanza kujifunza kutengeneza mikate nini kiliendelea?” nilimuuliza Bella huku nikikaa sawa kwenye kiti, aliendelea kusimulia baada ya kupiga mafunda mawili matatu ya kinywaji chake fulani hivi bariiidi.
Anasema kuwa baada ya kufahamu vizuri kutengeneza mikate na kuanza kuingiza mkwanja wa kueleweka kwa ‘level’ yake kiasi kwamba akawa hategemei tena kupata pesa ndogondogo kutoka nyumbani kwao, alijikuta akipiga chini kwenda shule na kujikita zaidi kwenye masuala ya kutafuta pesa na kuhudhuria kwenye vikundi vya uimbaji pamoja na rafiki zake.
“Nilipoachana na shule baba aliumia sana maana alichoamini urithi wa mtoto ulikuwa ni kwenye elimu tu, aliniita mara kadhaa na kunionya juu ya uamuzi wangu lakini wakati huo sikuhitaji kumsikiliza mtu yeyote zaidi ya sauti niliyokuwa naisikia ndani yangu,” alisema Bella.
“Ni sauti gani hiyo uliyokuwa unaisikia?” nilimuuliza huku nikimtazama kwa makini.
“Niache shule, nitafute pesa na kufanya muziki,” alijibu.
“Mama vipi, yeye aliupokeaje uamuzi wako huo wa kuacha shule?”
“Ulionekana kumshangaza, hakuamini kama ningeweza kufanya hivyo, pia kama mzazi alijaribu kunisihi lakini sikuhitaji kurudi nyuma.”
“Enhee, nini kikaendelea?”
“Basi bwana; baada ya kukacha skuli sikupenda kuishi tena nyumbani maana tayari mimi na wazazi wangu zilikuwa haziungi tena freshi, kwa hiyo nilichoamua kufanya ilikuwa ni kuondoka nyumbani na kwenda kuishi magetoni kwa washkaji zangu.”
“Nikiwa huko mishemishe za muziki ndiyo zikaanza rasmi maana nao walikuwa katika harakati hizohizo, sasa kule kwetu Kongo kipindi cha nyuma kwa vijana wadogo ambao wanafanya ishu za muziki walikuwa wanatunga nyimbo wakishazikariri wanatengeneza bendi na kuanza kufanyia mazoezi kwenye majumba mabovu huku ala za muziki zikiwa madebe.”
“Kwa hiyo na nyie mlifanya hivyo?”
“Ndiyo, tulifanya hivyo na kila jioni tulikuwa kwenye jumba bovu f’lani hivi karibu na nyumbani kwao na mshkaji wangu Bosei Junioh tukifanya yetu, huwezi amini watu walikuwa wanajaa kinoma kila waliposikia tunaimba, baada ya muda tukaanza kuwa vizuri na kuwa kivutio mtaani.”
Bella anaendelea kuwa matumaini na mwanga juu ya kufanikiwa kimuziki alianza kuvipata kutokana na kukubalika huko kwenye mitaa ya kwao, anasema kilichomfurahisha zaidi kwa wakati huo ilikuwa ni wasichana wengi wa mtaani kwao kuanza kuhitaji kuwa naye kimapenzi.
“Kutokana na umri ilikuwa ni vigumu kujizuia kuruka na baadhi yao waliokuwa wananivutia na kunihitaji, hata hivyo nilikuwa na msichana f’lani ambaye nilikuwa nina mpenda sana, huyo alikuwa kila kitu kwangu, lakini tofauti na wengine yeye hakuwa anataka kabisa tufanye mapenzi.”
“Alikuwa ana umri gani?” nilimuuliza.
“Miaka kumi na sita.”
“Wewe?”
“Wakati huo kumi na nane na ndiyo umri nilioanza kufanya mapenzi.”
“Mkh…”
“Siku zikasonga mbele, kila kitu kuhusu masuala yangu na wasichana wengine yalikuwa ni siri kubwa kwa huyo niliyempenda, nikazidi kustrago kwenye ishu zangu za muziki nilipofikisha miaka kumi na tisa ikabidi niende kuomba kujiunga kwenye Bendi ya Chateau du Soleil.”
“Baada ya kupeleka maombi yangu kwenye bendi hiyo ambayo ilikuwa inamilikiwa na tajiri mmoja aitwaye Frank Isekya rafikiye mkubwa na Papa Wemba nikapangiwa siku ya kufanyiwa usaili kabla ya kunikubali au kunibwaga kwenye bendi yao.”
Baada ya maneno hayo Bella anachukua glasi yenye kinywaji akipendacho mezani na kubugia mafunda matatu, kisha anairudisha mezani na kunitazama huku akitabasamu, macho yake yalinifanya nipate swali la haraka la kumuuliza.
“Bila shaka kumbukumbu za usaili ndizo zinakufurahisha?”
“Asikwambie mtu, siku hiyo nakumbuka usiku wake sikupata usingizi kabisa, akili yangu yote ilikuwa kwenye usaili ambao ningeufanya kesho yake, lakini kikubwa nilikuwa nimepania kujikamua sawasawa nipate nafasi na nilimuomba Mungu hilo liwezekane.”
Je, nini kitaendelea? Bella atafanikiwa kupita kwenye usaili huo? Vipi kuhusu mpenzi wake anayempenda sana, wataishia wapi? Usikose wiki
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger