Saturday 24 February 2024

WAZIRI MAVUNDE ASHUHUDIA URUSHWAJI NDEGE NYUKI ANGANI





*Kusini kuchele, Utafiti wa Miamba na Madini wahamia Mtwara

*GST kufanya tafiti madini mkakati Mtwara

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameshuhudia jaribio la urushwaji wa Ndege Nyuki (Drone) angani kwa ajili ya utafiti wa miamba na madini hususan madini ya Kinywe, Nikeli, chuma na titanium katika Kijiji cha Utimbe kata ya Lupaso wilayani ya Masasi mkoa wa Mtwara.

Waziri Mavunde ameshudia jaribio hilo leo Februari 23, 2024 baada ya kutembelea eneo linalofanyika utafiti huo kwa lengo la kukagua shughuli za utafiti zinazo endelea katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa Vision 2030 "Madini ni Maisha na Utajiri".

Akizunguza katika eneo la utafiti, Waziri Mavunde amesema mpaka sasa Tanzania ina taarifa za kina za tafiti wa miamba na madini kwa asilimia 16 ambazo zimepelekea uwepo wa migodi mikubwa, ya kati na midogo hivyo amesisitiza kwamba nchi hiyo ikifanyiwa utafiti wa kina wa High Resolution Airborne Geophysical Survey wa angalau asilimia 50 ifikapo 2030  itasaidia ongezeko kubwa la uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Aidha, Waziri Mavunde amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayo ongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa dhati kuhakikisha inawasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwapatia maeneo yenye taarifa za jiolojia ili wachimbe kwa faida na kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha.

Awali, Waziri Mavunde alitembelea ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa lengo la kupata taarifa za shughuli za madini zinazoendelea mkoani humo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, ameipongeza Wizara ya Madini kwa kurusha Ndege Nyuki kwa ajili ya utafiti katika eneo lake na pia, amemuomba Waziri Mavunde kusaidia upatikanaji wa soko la madini ya Chumvi sambamba na kujengwa  Kiwanda cha kuchakata madini hayo mkoani humo.

Naye, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba amemshukuru Waziri Mavunde kwa kukubari kushiriki na kushuhudia jaribio la urushwaji wa Ndege Nyuki kwa lengo la kutafiti miamba na madini kwa kutumia teknolojia ya high resolution airborne geophysical survey katika kijiji cha Utimbe wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.

Sambamba na hayo, Dkt. Budeba amesema GST inashirikiana na Kampuni za Tukutech Company Ltd kutoka Tanzania, Zanifi Enterprise Ltd kutoka Zambia na Radai OY kutoka nchini Finland kufanya tafiti za miamba na madini katika maeneo mbalimbali nchini kwa kurusha Ndege Nyuki angani kwa kutumia teknolojia ya High Resolution Airborne Geophysical Survey.

Katika hatua nyingine, Dkt. Budeba amesema Ndege Nyuki inauwezo wa kufanya uchunguzi wa madini na miamba katika eneo kubwa kwa haraka ambapo hupelekea kupungua kwa muda na gharama zinazohitajika katika tafiti ikilinganishwa na njia nyingine za utafiti.

Mpaka sasa majaribio ya utafiti wa high resolution airborne geophysical survey unaoendelea kufanyika mkoani Mtwara tayari umefanyika katika mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Geita, Manyara na Lindi kwa lengo la kutekeleza dhana ya Vision 2030.

*#Vision2030MadininiMaishanaUtajir#*

*#UtafitiTanzania#*

*#GeologicalSurveyofTanzania#*


Share:

Friday 23 February 2024

WAZIRI KIJAJI AZITAKA TBS, BRELA NA WMA KUFANYA UKAGUZI KWENYE VIWANDA VYA MABATI NCHINI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt, Ashatu Kijaji (MB) amezitaka Taasisi zinazohusika na utoaji Leseni(BRELA) Shirika la Viwango Tansania (TBS) na wakala wa vipimo sahihi (WMA)kupita kwenye viwanda vyote nchini vinavyozalisha bidhaa za mabati na bidhaa nyingine kukagua na kujiridhisha kama bidhaa zinazozalishwa na viwanda nchini zinakidhi vigezo vilivyo vilivyoainishwa na kukubalika na Serikali.

Waziri Kijaji ameyasema hayo leo 22 Febriari ,2024 jijini Dodoma wakati alipofanya ziara katika Viwanda vya kuzalisha mabati vya ALAF na Herosean Interprises inayozalisha mabati ya DRAGON ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na Viwanda hapa nchini zinanoreshwa.

Aidha Mhe. Waziri akiwa kwenye kiwanda cha Herosean Interprises kinachozalisha mabati ya DRAGON ameweza kubaini uwepo wa bidhaa nyingine ambazo haziusiani na malengo halisi ya leseni iliyotolewa na BRELA.

"Leo nimetembelea Viwanda hivi viwili lakini cha kusikitisha hiki Kiwanda cha kuzalisha mabati ya DRAGONI kinajihusisha na biashara ya kuuza bidhaa nyingine ikiwemo Friji, PVC, Vigae na Gypsum bord ,

"Nimewataka wanioneshe vielelezo vya usajili wa bidhaa hizo tofauti na bidhaa za mabati kiwandani hapa,sikupata majibu sahihi , naziagiza taasisi zinazohusika na hili suala zilishughurikie ili kupata ukweli wake. Amesema Kijaji

Vile vile Waziri Dkt.Kijaji ametoa wito kwa Viwanda vinavyozalisha bidhaa za mabati hapa nchini kuuzwa kwa bei rafiki ili kunufaisha wanunuaji kwa makundi yote.

" Jambo lingine ninalotaka kuwaambia watanzania kwa bidhaa nilizotembelea leo ,ukilinganisha kwa nchi za Afrika mashariki kwa bidhaa hii ya mabati sisi Tanzania bei yetu ipo chini kuliko nchi yoyote ile ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo niwatake msisikilize kelele za mtaani endeleeni kujenga kwa wingi na sisi kama Serikali tunaendelea kutekeleza miradi yetu"Ameongeza Dkt. Kijaji.

Kwa nyakati tofauti, wazalishaji wa viwanda hivyo Herry Jailos afsa huduma kwa wateja kiwanda cha mabati ya Alaf na Boniface Lekwasa Afsa Masoko Kiwanda cha kuzalisha mabati Dragon

wameishukuru Serikali kufanya ziara na kubaini changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa masoko kutokana na wazalishaji wa bidhaa hizo kuwa wengi nchini.
Share:

BYABATO AKUTANA NA WANANCHI, WAFANYABIASHARA BAKOBA


Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Stephen Byabato ambaye pia ni Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki

Na Mariam Kagenda _ Bukoba

Mbunge wa Jimbo  la Bukoba Mjini  Adv Stephen Byabato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  leo Februali 23  2024 amefika  kata ya  Bakoba na kuzungumza na wananchi wa kata hiyo.

Licha ya kuzungumza na wananchi hao pia  amekagua shughuli za wafanyabiashara wadogo na kupitia eneo la mradi wa TACTIC katika  barabara ya Shabridin kuangalia maandalizi ya mapokezi ya mradi huo mkubwa. 
                         Mhe. Adv. Byabato alipata fursa ya kuzungumza na wananchi wanaopatikana katika maeneo hayo na kuwaeleza juu ya miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  ndani ya manispaa ya Bukoba pamoja na kuwaomba wananchi hao kuendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi waliopo kuanzia kwa wenyeviti, madiwani na yeye mbunge ili mambo mazuri yaendelee kutekelezwa kama ilivyoahidiwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM  2020-2025.  

Kwa upande wake  diwani wa kata Bakoba Mhe Shabani Rashidi wakati akimkaribisha Mhe Mbunge baada ya kufika katika kata hiyo   amesema kuwa  wanabakoba wanajivunia  uongozi wa Mhe Rais   Samia Suluhu Hassan pamoja na  mbunge wa jimbo la Bukoba Mhe Stephen Byabato  kwani kila sehemu kuna mradi wa maendeleo  unaoendelea  hivyo wanaamini  miradi vipolo ikikamilika watakuwa hawana deni kwa wananchi.

Aidha Mhe. Shabani amesema kuwa wanaendelea kushirikiana  kushirikiana na wananchi katika maeneo tofauti tofauti katika kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za  serikali za kutatua kero za wananchi.

 Mhe.Adv Byabato  aliambatana na diwani kata Bakoba Mhe. Shabani Rashidi pamoja na viongozi wa mtaa.







Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini akiambatana na Mhe diwani wa kata ya Bakoba na wananchi wa kata hiyo wakati wa kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa

Share:

NAIBU KATIBU MKUU WA AFYA DKT. GRACE MAGEMBE AKAGUA HUDUMA NA MIRADI YA AFYA SHINYANGA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amefanya ziara mkoani Shinyanga ambapo ametembelea Kituo cha Afya Kambarage kujionea namna huduma za afya zinavyotolewa, pia amekagua huduma zinazotolewa katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura na ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Katika ziara hiyo ya kukagua huduma na miradi ya afya aliyoifanya leo Ijumaa Februari 23,2024 Dkt. Magembe pia amekagua miradi ya ujenzi na utoaji huduma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

PICHA na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (katikati aliyesimama) akiangalia kwenye mtandao huduma zinazotolewa katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (katikati aliyesimama) akiangalia kwenye mtandao huduma zinazotolewa katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembea akitembelea Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (katikati) akikagua ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia) akikagua ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia) akikagua ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Robert Elisha akimwelezea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe kuhusu ujenzi unaoendelea wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia) akisalimiana na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Robert Elisha baada ya kuwasili katika Kituo cha Afya Kambarage
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (katikati) akisalimiana na wananchi waliofika kupata huduma za afya katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Mmoja wa wananchi akimwelezea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe kuhusu huduma za afya katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza na wananchi katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza na wananchi katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia katikati) akiwa katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia katikati) akiwa katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

DKT MPANGO ATOA AGIZO KWA HAZINA ,TAMISEMI KUTUMIA HATI FUNGANI KATIKA KUHARAKISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO



Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango akizindua mradi wa kuongeza upatikanaji wa maji kwa wastani wa lita 60 katika Jiji la Tanga na wilaya jirani za Muheza na Mkinga baada ya lita 45 za awali, mradi huo umeanza baada ya uzinduzi wa hati fungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji Tanga katika eneo la Mabayani Jijini Tanga ukiwa na lengo la uboreshaji wa upatikanaji wa maji ambapo unagharama ya zaidi ya Bilioni 53 ambao utazalisha lita milioni 60, kushoto ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba


Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango akizindua mradi wa kuongeza upatikanaji wa maji kwa wastani wa lita 60 katika Jiji la Tanga na wilaya jirani za Muheza na Mkinga baada ya lita 45 za awali, mradi huo umeanza baada ya uzinduzi wa hati fungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji Tanga katika eneo la Mabayani Jijini Tanga ukiwa na lengo la uboreshaji wa upatikanaji wa maji ambapo unagharama ya zaidi ya Bilioni 53 ambao utazalisha lita milioni 60, kushoto ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba

Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango akizindua mradi wa kuongeza upatikanaji wa maji kwa wastani wa lita 60 katika Jiji la Tanga na wilaya jirani za Muheza na Mkinga baada ya lita 45 za awali, mradi huo umeanza baada ya uzinduzi wa hati fungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji Tanga katika eneo la Mabayani Jijini Tanga ukiwa na lengo la uboreshaji wa upatikanaji wa maji ambapo unagharama ya zaidi ya Bilioni 53 ambao utazalisha lita milioni 60, kushoto ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba
Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango akizindua mradi wa kuongeza upatikanaji wa maji kwa wastani wa lita 60 katika Jiji la Tanga na wilaya jirani za Muheza na Mkinga baada ya lita 45 za awali, mradi huo umeanza baada ya uzinduzi wa hati fungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji Tanga katika eneo la Mabayani Jijini Tanga jana ukiwa na lengo la uboreshaji wa upatikanaji wa maji ambapo unagharama ya zaidi ya Bilioni 53 ambao utazalisha lita milioni 60, kushoto ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba


Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally FungoNa Mwandishi wetu.


MAKAMU wa Rais Mhe,Dkt Philip Mpango ameiagiza Ofisi ya usajili wa hazina kama msimamizi wa taasisi na mashirika ya umma nchini wakishirikiana na Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kuhakikisha wanasimamia Halmashauri nchini kutumia dirisha la hati fungani katika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Dkt Mpango aliyasema hayo wakati wa ghafla ya uzinduzi wa hatifungani ya kijani ya Mamlaka ya Maji Tanga(Tanga uwasa) na kusema Halmshauri zoye Nchini zitumie dirisha la hati fungani kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutoa nafasi kwa Serikali kujikita kwenye madai mengine ya vipaumbele ambayo hakuna uwezeshwaji wa kifedha.


"Nakuona bwana makopa na ukamwambie bosi wako na Waziri wa Tamisemi hakikisheni mnasimami vizuri taasisi hizo na Halmashauri zote"Alisema Dkt Mpango.



Mbali na agizo hilo pia Dkt Mpango ameiagiza Bodi ya wakurugenzi wa Tanga Uwasa,Menejimenti na Wafanyakazi wote kusimamia vizuri matumizi ya fedha zitakazopatikana kupitia hatifungani ambayo imezinduliwa leo na mapato mengine mtakayokusanya baada ya kukamilisha mradi huo


Aidha alisema nidhamu ya fedha na usimamizi thabiti ndio utakaowezesha kurejesha kwa wakati fedha za wawekezaji wa hatifungani hiyo na Serikali na haitavumilia uzembe wa aina yoyote utakaonekana kukwamisha jitihada za Rais Samia.


"Kwa maneno ya Waziri wa Maji Jumaa aweso kwamba ukimzingua Mama nanyeye atakuzingua sasa shauri yanu"Alisema Dkt Mpango.


Alisema kuwa anatambua kwamba mamlaka za maji kwa kiwango kikubwa zinafanya vzuri na ipo haja ya kuwakumbusha watu wa Tanga Uwasa waongeze ufanisi katika uendeshaji ili urejeshaji wa hatifungani hiyo usiwe sababu ya kuzorota kwa huduma au ongezeko la bei za maji kwa Tanga na Mikoa mingine ambayo itapata nafasi ya kuwa na mradi kama huo.


Makamu huyo wa Rais pia ameiagiza Mamlaka ya Masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na wizara ya maji wekeni utararibu na mfumo wa tahadhari ili kufuatilia na kubaini mapema vihatarishi vitakavyoweza kujitokeza baada ya kuzinduliwa kwa hatifungani hiyi.


Dkt Mpango alikwenda mbali zaidi na kusema kwa kuwa urejeshwaji wa fedha hizo ni wa mkupuo baada ya kuiva kwa hatifungani inaweza kuleta changamoto wakati wa kulipa hivyo basi ni vema mjipange mapema na ikiwezekana mfungue mfuko maalumu wa kukusanya kidogo kidogo fedha za marejesho.


"Tuwe na wazo la kibunifu la dira za maji na ninaamini kwa dhati hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa kusanayaji wa mapato na hivyo kuongeza uwezo wa kulipa"Alisema.


Hata hivyo Dkt Philip Mpango alisema hatifungani ambayo imezinduliwa leo ikawe chachu na motisha kwa taasisi na halmashauri nyingine Nchini kutumia njia hiyo kwa ajili ya kupata fedha za miradi ya maendeleo.


Kwaupande wake waziri wa Maji Jumaa Aweso aliishukuru wizara ya Fedha na Mipango kwakufanikisha kupata mradi huo wa hati fungani ambao utasaidia kuongeza ufanisi na upatikanaji wa maji katika jiji la Tanga pamoja na wilaya za Muheza,Pangani na Mkinga,


" Hati fungani itasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Wilaya za Tanga jiji,Muheza ,Pangani na mkinga ambapo ,hali ya upatikanaji wa huduma ya maji itapanda ifikapo 2025 hadi asilimia 100 kutoka asilimia 96" alisema Aweso


Alisema wamepata uzoefu wakusimamia miradi mingi ya maji hivyo wanaamini mradi huu wa Hati fungani utatekerezwa na wananchi watapata fursa yakushiriki kwa kiwango kikubwa

Naye Afisa mtendaji wa mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ( CMSA) Nicodemus Mkama alisema mfumo wa Hatifungani ni sehemu ya Masoko ya mitaji katika Sekta ya fedha inayowezesha upatikanaji wa fedha kwa muda mrefu.

"Fedha za kugharamia shughuli za maendeleo huweza kupatikana kwa kuuza hisa za kampuni ( Shares),hatifungani za kampuni ( corporate Bond) ,hati fungani za Serikali ( Government Bond)na vipande katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja ( collective investment scheme) "alisema Mkama

Aliongeza kuwa Taasisi hiyo imepata mafanikio zaidi kwa kipindi cha miaka minne iliyopita ambapo thamani ya uwekezaji katika masoko na mitaji imeongezeka kwa asilimia 31.2 na kufukia shilingi Tirioni 37 .3 katika kipindi kilichoishia January 2024 ikilinganishw na Tirioni 28.4 ya kipindi kilichoishia January 2021,


"Jumla ya mauzo ya hisa na hati fungani katika soko la hisa yameongezeka kwa asilimia 61 .6 na kufikia shilingi tirioni 9.3 kutoka trioni 5.8,vilevile thamani ya mfuko ya uwekezaji wa pamoja imeongezeka kwa asilimia 291.6 na kufikia tirioni 1.9" alisisitiza Mkama
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger