Thursday 29 June 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 29 2023






Share:

Wednesday 28 June 2023

AJERUHIWA VIBAYA KWA KUMWAGIWA TINDIKALI NA WASIOJULIKANA





Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani 


Na Walter Mguluchuma -Malunde 1 blog - Katavi

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Ernest Lyoba (61) Mkazi wa Kijiji cha Namanyere Kata ya Majimoto Wilaya ya Mlele amejeruhiwa vibaya katika sehemu yake ya uso na mgongoni baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana wakati akiwa njiani anaelekea nyumbani kwake .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo la kikatili la kusikitisha limetokea June 25,2023 huko katika eneo la Kijiji cha Namanyere.

Amebainisha kuwa siku ya tukio Ernest alikuwa yuko njiani akiwa anaelekea nyumbani kwake majira ya saa tisa alasiri mara baada ya kuwa amemaliza shughuli zake za kujitafutia riziki ndipo watu wasiojulikana walimmwagia tindikali sehemu za usoni na mgongoni na kumjeruhi vibaya na kisha watu hao walitokomea mahali pasipojulikana.

Kamanda Ngonyani amesema baada ya muathirika wa tukio hilo kumwagiwa tindikali hiyo alipiga kelele za kuomba msaada na baada ya muda mfupi watu walifika kwenye eneo hilo na kumkuta Ernest Lyoba akiwa amejeruhiwa vibaya .

Ameeleza kuwa wasamaria  wema hao walimchukua muathirika wa tukio hilo na kumkimbiza kwa haraka hadi kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe kwa ajiri ya matibabu hata hivyo kutokana na kuwa amejeruhiwa vibaya mhanga alipewa rufaa ya kwenda kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

Hata hivyo baada ya kuwa amefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi alipewa tena ya kwenda kupatiwa matibabu zaidi kwenye Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Mkoani Kilimanjaro ambako amelazwa hadi sasa.

Kamanda Ngonyani amesema juhudi za kuwanasa watuhumiwa hao zinaendelea kufanywa na jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ili kuhakikisha linawakamata na kuwatia nguvuni na kuwafikisha mara moja Mahakamani ili wakajibu mashitaka ya tuhuma zitakazokuwa zinawakabili .


Share:

WATOTO WAFARIKI DUNIA KWA KUPONDWA MAWE


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Watoto wawili wa familia moja wamekutwa wamefariki dunia  baada ya kufukiwa/kupondwa na mawe wakati wakichimba mchanga katika eneo la Marahara kijiji cha magata kata ya Karutanga wilayani Muleba mkoani Kagera .

Diwani wa Kata ya Magata Karutanga  Alhaji Yakubu Mahamudu amesema kuwa watoto hao  walipotea  Juni 26 ,2023 na walitafutwa maeneo yote hawakuweza kupatikana na June 27 watoto hao walipatikana wakiwa tayari wamefariki dunia baada ya kufukiwa  na mawe wakati wakichimba mchanga.

Alhaji Yakubu amewataja watoto hao kuwa ni Samsoni Eliud mwenye umri wa miaka 13 na Emmanuel Eliud mwenye umri wa miaka 10 ambapo wote walikuwa wanafunzi wa shule ya Msingi Magata   na kuongeza kuwa watoto hao waliterekezwa na baba yao  mzazi na kubaki na mama yao pekee .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga  amefika katika eneo hilo ambapo amepiga marufuku na kuzuia mtu yoyote yule kufanya shughuli za uchimbaji wa mchanga kwani eneo hilo sio salama na kuagiza kukaguliwa maeneo yote ya uchimbaji wa mchanga katika wilaya hiyo ili kudhibiti maafa yasiendelee kutokea.

Nao baadhi ya wananchi ambao ni Ashimu Salimu na Godfrey Joel wamesikitishwa na tukio hilo na kuwahimiza wazazi kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema na kuwahimiza wanaume kutowatelekeza watoto.

Share:

HATUA ZA KUSHINDA JACKPOTI YA MERIDIANBET



Shinda Jackpoti

 

Watu wengi sana hujiuliza inakuaje mtu Fulani anashinda Jackpoti je huwa vigezo gani vinatumika, haswa katika kampuni nambari moja kwa ubashiri na kasino ya mtandaoni Meridianbet, Leo nakupitisha hatua kwa hatua namna ya kushinda Jackpoti.

 

Hatua za Kufanya Kushinda Jackpoti za Meridianbet

 

Promosheni ya Jackpoti huwa ipo kwenye aina mbili upande wa Jackpoti ya Soka yaani kubeti soka, na Jackpoti ya michezo ya kasino ya mtandaoni, hapa kuna utofauti mdogo unapaswa kufahamu.

 

Jackpoti ya kubeti soka mfano ile Jackpoti ya Meridianbet kubashiri na kitochi ya Tsh Mil 80, hii ni ngumu kidogo kwakuwa unahitaji kusuka jamvi lako kwa utulivu huku ukifanya tafiti ya timu unazozipa ushindi.

 

Lakini ukicheza Jackpoti ya kasino ya mtandaoni huhitaji kutumia akili sana bali, unachotakiwa kukifanya kuchagua michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni unaweka dau lako kisha unacheza, kadiri unavyocheza ndio unajiweka kwenye nafasi kubwa ya kushinda Jackpoti ya Meridianbet.

 

Vigezo na masharti kwa kila jackpot hutegemea, lakini Jackpoti ya Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet ndiyo jackpot pekee ambayo inakuwa rahisi zaidi. Usikae mbali na kurasa za Meridianbet ya ofa na promosheni kuona kapu la jackpot linapokuwa hewani.

 

Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet huratibu jackpot nyingi za kasino kwa nyakati tofauti ambazo huhusisha waandaaji wa michezo ya kasino, michezo ya Sloti, na Meridianbet wenyewe. Wachezaji wa kasino ya mtandaoni Meridianbet wanakuwa na nafasi sawa ya kupata ushindi mkubwa wa jackpot ya kasino.

 

Nini ufanye kushinda Jackpot ya kasino kwa Meridianbet?

 

Hili ni swali rahisi, ambalo unaweza kujibiwa na nguli wa ubashiri wa Meridianbet na wale wanaofuatilia promosheni mbali mbali za kasino za Meridianbet. Siri ni kufuatilia kwa ukaribu ukurasa wa promosheni wa Meridianbet, na kucheza zaidi michezo ya kasino ya Meridianbet kujiweka kwenye nafasi ya kushinda jackpot ya kasino.

 

Pia, una nafasi ya kufanya bashiri za kawaida na Meridianbet, pale kunapokuwa na matukio yanayokuvutia zaidi ya kimichezo. Unaweza kubashiri kwa tovuti, App ya simu au kwa kupiga *149*10# ukiwa na Tigo au Airtel kubashiri.

 


Share:

AMPONYA MJOMBA KICHAA KILICHO MUANZA GHAFLA

Tunaishi kwenye famila ya pamoja na baadhi ya ngugu zake mama wa kiume ambao wao hawakuwa wameoa tayari, ni wajomba wawili na shangazi mmoja dada yake baba naye pia bado hakuwa ameolewa. Mimi ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto watano ambapo wamwisho ni mapacha mmoja wa kike na mmoja wa kiume.


Familia yetu siyo yenye uwezo sana lakini tunakula milo yote mitatu kwa wakati na pamoja kuwa na ndugu baadhi wa pande zote mbili hatukuwahi kuona mafarakano ndani ya nyumba baina ya baba, mama wala hao ndugu zao ambao tuko kuishi nao pale nyumbani.


Siku mbili kabla ya sherehe ya sikukuu ya kikristu ya Christmas ya mwaka 2020 ndio mara ya kwanza kuona changamoto kubuwa imetukumba pale nyumbani ule usiku ghafla mama alipigiwa simu na marafiki zake wa mitaani wakimwambia kuwa mjomba wangu ambaye ni mdogo wake wa pili wa kiume yuko barabarani ameshikwa na kichaa ghafla analala barabarani tena kwenye ‘traffic lights’.


Kwa kweli isingekuwa msaada wa daktari BAKONGWA ambaye tulichelewa sana kumjuwa kabla ya wageni wa kikundi cha vikoba kumfahamisha mama na kumpa nambari zake daktari huyo za whatsapp +243990627777 na tovuti zake https://bakongwadoctors.com tungeishia kumlea mjomba ndani kwa kuogopa kichaa ambacho kilimshika.

Mjomba alikuwa amekuja mjini kujiendeleza kielimu tu hakuwa na jjambo lolote lile ambalo kwa kweli alilifanya kwa siri sisi tusilijue, taarifa zilipotufikia haraka tukakodi bajaji na kumchukuwa tukijuwa ni homa ya ghafla au maralaria kali tukamuwaisha hospitali mara moja.


Hospitali pale alikaa kwa muda wa miezi mitatu bila ya mafanikio hakukuwa na dalili yoyote ile ya mjomba kuamka, hali yake ilikuwa mbaya zaidi hakuwa anamjuwa yoyote katika sisi kila aliyemsogelea kumpa pole mjomba alikuwa akitukana na kutishia kusema nitakuua mimi, tuliamua kufanya mbadala tukaleta masheikh kulingana na imani yetu wao wakafanya dua na dua wiki nzima masheikh walizunguka hospitalini pale lakini kichaa cha ghafla cha mjomba hakikupona.


Hospitali wakasema tumtowe pale au tuwe tayari apelekwe wodi ya vichaa jambo ambalo mama hakulikubali kabisa ni mwezi wa tisa sasa ya mwka 2021 ni miezi kumi toka kichaa cha ghafla kimshike mjomba na kila msaada wa maombi na wa hospitali haukuwa umemponya changamoto yake.


Kikundi cha kina mamakikawa kinakaa kikoba kikafayikia nyumbani kwa wakati huwo tayari mjomba alikuwa amerudi nyumbani tumemfungia ndani asitoke kwa kuogopa madhara ambayo tungeyapata au angeyafanya kwa watu, kwa bahati rafiki wa mama ndiye aliyemuona na kumwambia mama amtafute daktari Bakongwa atatusaidia.


Baada ya kikundi kuisha mama aliniita akanikabidhi nambari zile alizopewa na mwenzake kisha nikampigia daktari ambaye tulifanya naye mazungumzo kwa kipindi kirefu mama akamuelekeza haliyote ilivyoanza mpaka mwisho, daktari akataka majina mawili ya mgonjwa pesa ya kumuangalizaia kisha akasema atatupigia.


Alipotupigia alitowa taarifa kuwa kuna alikuwa anamchezea ambaye aliona nyota ya mjomba na kuamuwa kuitumia kwa kumfanya awe kichaa na ndiyo sababu kichaa chake kilianza ghafla mara mmoja akatutumia dawa ambayo ilikuwa na kikaratasi kilichotaka mjomba anywe ile dawana kupga kwa siku tatu mchana na asubuhi.


Baada ya siku hizo tatu maajabu tuliyaona mjomba alianza kubadilika na kurudi kwenye hali yake ileile hakuwa tena mchafu , wa kudondosha mate, kutukana watu wala kuwafokea akaanza kututambua sote mpaka kichaa chake cha ghafla kikakoma kabisa , asante sana daktari kwa tiba zako nzuri na za muda mfupi.


Share:

NIMEPOTEZA HAMU YA TENDO NAJILAZA TU KAMA GUNIA KITANDANI

 

Kwa masikitiko makubwa, niliweza kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mume wangu miaka tatu tu baada ya kufunga ndoa naye, waweza kushangaa hilo lakini lipo kwa wengi ila hawajaweza kujitokeza na kulieleza au kutaka kupata usaidizi.


Mimi nimeamua kueleza niliyoyapitia na jinsi nilivyoweza kupata msaada kupitia African Doctors, ni matumaini yangu haya nitakayoeleza hapa yanaweza kuwasaidia na wengine kutafuta usaidizi wa changamoto hiyo.

Jina langu ni Wanjiku, ni mwanamke ambaye umri wangu umeenda kidogo ila sio sana, nilifunga ndoa miaka mitano iliyopita, tulipofunga ndoa na mpenzi wangu tulitumaini kuishi maisha ya furaha nyakati zote ila mwaka wa tatu tu baada ya ndoa mambo yalianza kuenda mrama.

Nilikosa na kuipoteza furaha niliyokuwa nayo mwanzoni mwa ndoa, nilipoteza hamu ya kushiriki tendo na mume wangu, kwa vile nilimpenda kwa dhati na nilikua na mapenzi yasiyo na kifani kwake, wakati wote tungeshiriki tendo la ndoa ningejifanya kufurahia lakini haikuwa hivyo.

Nilijilaza kama gunia la mahindi na kumpa mume wangu alichohitaji, upande wake alineokana mwenye kufurahishwa lakini hakuwai kujua kuwa mkewe sijisikii raha kabisa wakati wa kufanya tendo hilo.

Maji yalipozidi unga niliamua kuanza kutafuta suluhu kwa kuwa nilikua najihisi kukosa maana ya kuwa kwenye ndoa, kamwe singeweza kumuacha mume wangu kwa kuwa nilimpenda sana.

Niliamua kuomba ushauri kutoka kwa wasikilizaji wa redio moja maarufu nchini Kenya, Radio Jambo kupitia kipindi chao cha Mahusiano na Ndoa kiitwacho Mahaba, niliweza kuwapigia simu watangazaji wa kipindi hicho na kuwaeleza yote niliyokuwa napitia katika ndoa.

Nilisikiliza kwa umakini maoni ya wasikilizaji wao, na kuamua kutumia ushauri wao lakini sikupata suluhu, bado niliendelea kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mume wangu.

Hata hivyo, baada ya kupita huku na kule, niliamua kwenda kumuona Daktari wa uzazi katika Hospitali moja Jijini Nairobi, alinipa tembe, nilizomeza kwa miezi mitatu ila bado sikupata suluhisho lolote.

Wakati mmoja nilipokuwa na safari zangu Nairobi nilikutana na tangazo la African Doctors kuhusu huduma zao, miongoni mwa mambo waliyokuwa wanatibu ni pamoja na tatizo langu la kukosa hamu ya tendo la ndoa.

Bila kusita nilichukua namba yao na kuwapigia simu na kuwaeleza nahitaji kuonana nao ili niweze kupata huduma yao, basi siku iliyofuata niliweza kukutana na African Doctors, alinipa matumaini kuwa naweza kupona tatizo langu kwa asilimia 100.

Alinipatia madawa ya miti shamba na kunieleza ningeyaona mabadiliko kwa siku chache zijazo, siku tatu baadaye hamu ya kushiriki tendo la mdoa ilirejea, na mara kwa mara nilikua na hamu ya kutaka kushiriki tendo hilo, shukrani za dhati kwa African Doctors.

Pia kumbuka African Doctors anatibu magonjwa kama Saratani ya mapafu, Kisonono na mengine mengi, pia wanatatua matatizo kama kulinda boma, kulirejesha penzi lililopotea na mengine mengi.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.



Share:

Tuesday 27 June 2023

WAZIRI AWESO AHAIDI KUMALIZA TATIZO LA MAJI JIMBO LA ULANGA

 

Mbunge wa Jimbo la Ulanga (CCM) Mhe Salim Alaudin kulia akizungumza na Waziri wa Maji Jumaa Aweso


Waziri wa Maji Jumaa Aweso(Mb) amemuahidi Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe.Salim Alaudin Hasham kuwa atatoa ushirikiano wa kina yeye na ofisi yake katika mapambano ya kuhakikisha wilaya ya Ulanga inamaliza Changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.


Waziri Aweso ameyasema hayo wakati alipotembelewa Ofisini kwake Dodoma na Mbunge Salim akiwa na wafadhili kutoka Nchini Uswisi ambao wamekuja kwa lengo la kuangalia Changamoto ya maji wilayani Ulanga ili kuona namna bora ya kuisaidia kuondokana na shida hiyo.


Naye mfadhili wa maswala ya maji kutoka nchini Uswisi Bi. Rubab Jawad Aziz amesema kilichomvutia kusaidia wilaya ya Ulanga kuondokana na tatizo la maji ni kwasababu wazazi wake waliishi hapo na yeye alilelewa hapo hivyo anajua Changamoto hizo tangu akiwa mtoto mdogo kabla ya kwenda nje ya nchi kutafuta maisha.


Kwa upande wake Mbunge Salim amesema lengo la kutafuta wafadhili kwa wingi ni kuona namna bora ya kuisaidia Serikali katika kutatua Changamoto mbalimbali.


Jimbo la Ulanga linazalisha kiasi cha lita 8000 hadi 9000 wakati mahitaji ya maji ikiwa ni lita 1,600,000.






Share:

WAJASIRIAMALI NA WAFANYABIASHARA WANAOTOA HUDUMA KATIKA MIGODI WALIA MALIPO KUCHELEWA

Imeelezwa kuwa  kuchelewesha malipo Kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wanaotoa Huduma katika migodi kunachangia kuzorotesha mzunguko wa Biashara za wajasiriamali pamoja na kuishiwa mitaji ya kuendeleza biashara zao.

Hayo yamebainika leo katika warsha ya kutoa matokeo ya ripoti ya Utafiti wa ushirikikishwaji wa wazawa Kwenye sekta madini Tanzania iliyofanyika katika mkoa wa Mara na Geita.

Akitoa taarifa ya Utafiti huo Afisa ufuatiliaji,Tathimini na mafunzo Kutoka Hakirasilimali Francis Mkasiwa amesema kuhusu Hali ya ajira kwa wazawa Utafiti unaonyesha kuwa wazawa wanapewa kazi za kuuza mbogamboga,Huduma za usafiri,malazi,kuuza Chakula na kuuza vifaa vya ujenzi.

Francis ameongeza kuwa tafiti waliofanya inaonyesha watoa Huduma hawalipwi fedha zao Kwa wakati Hali inayokwamisha mzunguko wa Biashara zao pamoja na kuishiwa mitaji Yao.

Sambambam na hayo ripoti inaonyesha kuwa Hali ya kuhamisha maarifa Kwa wazawa ni ndogo kwani elimu na mafunzo hutolewa Kwa Watu wachache na yasiyo ya kudumu Kwa wazawa hao.

Awali akifungua warsha hiyo mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi mtandao wa mashirika yanayofanya kazi katika sekta ya madini na Gesi (Hakirasilimali) Jimmy Luhende amependekeza kuendelea kufanyika tafiti nyingi za kisayansi katika migodi inayozunguka wananchi ili kunufaisha pande zote  za wawekezaji na wananchi.

Nao baadhi ya washiriki wa warsha hiyo Bonny Matto Kutoka tarime na Asia Hussein Kutoka Gieta wamewashauri viongozi hususa wenyeviti na madiwani kutetea na kusimamia sheria ndogo Ili kuwe na manufaa ya pamoja kati ya wananchi na wawekezaji.

Akitoa ufafanuzi kuhusu ucheleweshaji wa malipo Kwa watoa Huduma Meneja mahusiano wa AKO GROUP LTD Waisile Bairi amesema utaratibu wa malipo Huwa unafanyika ndani ya siku thelathini baada ya mtoa Huduma Kupeleka Ankra (Invoice) Kwa mwekezaji.

Warsha hiyo ya Siku moja iliyofanyika Mkoani Geita  ya uzinduzi wa ripoti ya Utafiti wa Ushirikikishwaji wa wazawa Kwenye sekta ya madini iliyoandaliwa na Hakirasilimali na Policy Forum imejumuisha wadau wa madini Kutoka mkoa wa Mara,Shinyanga na Geita.
Share:

BARRICK BULYANHULU NA GGML WAONYESHANA UBABE MCHEZO WA KIRAFIKI WA BASKET BALL

Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya kutoka Barrick Bulyahulu na GGML wakiwania mpira wakati wa mchezo huo wa kirafiki
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya kutoka Barrick Bulyahulu na GGML wakiwania mpira wakati wa mchezo huo wa kirafiki
Wachezaji wa GGML katika picha ya pamoja baada ya mechi hiyo ya kirafiki kumalizika
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya kutoka Barrick Bulyahulu na GGML wakiwania mpira wakati wa mchezo huo wa kirafiki
Wachezaji wa GGML wakipata mawaidha kutoka kwa kocha wao
Wachezaji wa Barrick Bulyanhulu wakipata mawaidha kutoka kwa kocha wao
Baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wakifuatilia mchezo huo
 ****

Timu za mchezo wa kikapu za wafanyakazi kutoka migodi mikubwa ya dhahabu nchini ya Barrick Bulyanhulu na Geita Gold Mine Ltd. (GGML) zilionyeshana umwamba katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika viwanja vya michezo vya mgodi wa Bulyanhulu.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali GGML ilibuka na ushindi wa magoli 85 dhidi ya magoli 81 yaliyofungwa na timu ya Barrick Bulyanhulu.

Mchezo huo mbali na kudumisha urafiki na kuleta furaha ni mwendelezo wa programu za makampuni hayo ya kuhakikisha wafanyakazi wake wanafanya mazoezi ya kujenga afya zao.

Kampuni ya Barrick nchini imekuwa na program za mazoezi kwa ajili ya kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa na nguvu na afya bora.

Kila mwaka kampuni imekuwa ikiwezesha wafanyakazi wake kushiriki mashindano mbalimbali ya michezo ikiwemo mashindano ya mbio za kilomita 42 ya Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon,
yanayofanyika kila mwaka.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger