Thursday 29 December 2022

KASI YA UKUAJI MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA NA UCHUMI KATI YA TANZANIA NA CHINA, DKT SAMIA ANASTAHILI PONGEZI


Tunapoelekea kufunga mwaka 2022, ubalozi unatoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali kwa ushirikiano wao uliowezesha utekelezaji wa Majukumu ya Ubalozi. Katika Mwaka 2022 mambo mbalimbali yenye tija na manufaa kwa wananchi yamefanyika kufuatia mwongozo na maelekezo ya Mwanadiplomasia No 1 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyofanyika:


MOSI
Tarehe 2-4 Novemba 2022 Ilifanyika Ziara ya Kihistoria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk Samia Suluhu Hassan-nchini China. Kupitia ziara hiyo Tanzania na China zilipandisha hadi ya mahusiano kuwa ya Kimkakati katika nyanja zote.


PILI
Kwa upande wa biashara, Mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la China yaliongezeka kutoka Dola za Kimarekani Milioni 409 hadi kufikia Dola za Kimarekani Milioni 605.5. Inatarajiwa katika mwaka 2023 mauzo yataongezeka kwa asilimia 20 kutokana na Tanzania kufunguliwa soko jipya la bidhaa wakati wa ziara ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan nchini China.


TATU
Wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania wanaoshughulika na zao la Parachichi walifunguliwa soko jipya la China Mwezi Novemba 2022. Kuanzia msimo ujao wa 2023 mauzo ya parachichi katika soko la China yataanza.

NNE
Wavuvi wa Tanzania walifunguliwa soko Jipya la kuuza mabondo ya Samaki na samaki aina sangara nchini China Mwezi Novemba 2022. Inatarajiwa mwaka 2023 mauzo ya bidhaa za uvuvi yataongezeka.


TANO
Bidhaa za Tanzania zilizoongezewa thamani zilianza kuuzwa katika soko la China kupitia Mtandao Maarufu wa Biashara wa JD.COM wenye watumiaji milioni 600- Mei 2022.


SITA
Watanzania walianza kufanya shughuli za usafirishaji wa mizigo yao moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China kwa kutumia Shirika la Ndege la Air Tanzania- Mei 2022. Inatarajiwa mwaka 2023 baada ya China kufunguka shughuli zitaongezeka.

SABA
Usafiri wa abiria wa ndege wa moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Guangzhou ulianza Mwezi Julai 2022. Kuanzia Mwezi Januari 2023 Wafanyabiashara,wanafunzi & watalii watanufaika na huduma hiyo baada ya hatua ya China kufungua mipaka na kuondoa masharti ya udhibiti wa UVIKO19


NANE
Kufuatia maelekezo ya Mhe Rais @SuluhuSamia Ubalozi Mdogo wa Tanzania katika jijini la Biashara la China- Guangzhou ulifunguliwa rasmi mwezi Mei 2022. Watanzania wameanza kupata huduma mbalimbali za kufanikisha shughuli zao za biashara na Ubalozi mdogo umeanza kufungua fursa mpya za masoko ya bidhaa.


TISA
Filamu ya Tanzania Royal Tour ilioneshwa katika Televisheni ya Hainan Mwezi Oktoba 2022 na kutizamwa na watu milioni 60. Aidha filamu hiyo iliyotafsiriwa kwa lugha ya kichina imeoneshwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ya China ikiwemo Bilibili m.bilibili.com/video/BV1jB4y1…

KUMI
Wanafunzi wa kitanzania watanufaika kwa kupata shahada na stashahada kufuatia kusainiwa kwa Makubaliano Mwezi December 2022 kati ya Tasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), na Taasisi ya Chongqing Vocation Institute of Engineering (CQVIE) ya China ya kuendesha mafunzo ya pamoja


KUMI NA MOJA
Vijana wa kitanzania wataanza kunufaika na mafunzo ya ufundi kufuatia hatua ya ufunguzi rasmi wa Chuo cha Ufundi cha VETA mkoani Kagera kilichojengwa kwa msaada kutoka China na kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk @SuluhuSamia Mwezi Oktoba 2022


KUMI NA MBILI
Watanzania 122 wamepata ufadhili (scholarships) wa masomo ya Elimu ya Juu katika Vyuo Vikuu nchini China katika fani mbalimbali. Mwaka 2023 watanzania wataendelea kupata fursa za masomo ikiwa ni sehemu ya matokeo ya ziara ya Mheshimiwa Rais @SuluhuSamia nchini China


KUMI NA TATU
Katika mwaka 2022 Wafanyabiashara wa Tanzania wamepatiwa elimu kwa umma kuhusu fursa za biashara zilizopo nchini China pamoja na ushauri juu ya hatua za kuchukua ili kuepuka kuangukia mikononi mwa wafanyabiashara wasio waaminifu.

KUMI NA NNE
Katika Mwaka 2022 Vipindi vya Elimu kwa Umma vilianzishwa ili kuwapa wananchi ufahamu juu ya fursa za upatikanaji wa teknolojia mbalimbali za bei nafuu kwa ajili ya uzalishaji/usindikaji wa malighafi zinazopatikana nchini




Share:

BAADA YA KUIKACHA YANGA , FEI TOTO KUMBE KAJIFICHA JKU...ANASWA AKIGONGA MECHI YA KIRAFIKI NA MLANDEGE



Kiungo wa Yanga Feisal Salum Abdallah (Fei toto) asubuhi ya leo Alhamis Disemba 29, 2022 ameichezea Timu yake ya zamani JKU kwenye mchezo wa Kirafiki dhidi ya Mlandege kwenye Uwanja wa Mao Zedong, Zanzibar ambapo JKU walifanikiwa kupata ushindi wa Mabao 4-2 .

Katika mchezo huo Fei alicheza dakika 45 za kipindi cha pili ambapo wakati anaingia Fei JKU walikuwa tayari wapo nyuma kwa Mabao 2-0, lakini baada ya kuingia wakafanikiwa kusawazisha Mabao hayo na kuongeza mengine mawili huku Fei akifunga moja kati ya Mabao hayo 4 na akiwa na msaada mkubwa wa kupatikana Mabao hayo.

Mwandishi wa Habari hii alifanya jitihada ya kuzungumza na Fei mara baada ya kumalizika mchezo huo lakini Fei aliomba kutozungumza chochote.


“Naomba nisiongee chochote, naomba sana, ikifika siku ya kuongea nitaongea “. Alisema Fei.

Si mara ya kwanza Fei kuonekana kucheza JKU kwani ndio Timu yake ya zamani aliyoondoka mwaka 2018 kabla ya kujiunga na Yanga.

Jumamosi ya Disemba 24, 2022 kupitia mitandao yake ya Kijamii Fei aliwaaga Wanayanga huku timu yake hiyo siku hiyo hiyo ikitoa taarifa yakuwa bado Fei ana mkataba na Yanga mpaka Mei 30, 2024.

Hivi karibuni ziliibuka taarifa ya kuwa Fei huenda akajiunga na Azam FC kutokana na dau nono aliloahidiwa ambapo yeye binafsi aliwahi kusema hachezi mpira kufurahisha Watu bali anacheza Soka kwa kuangalia wapi kuna maslahi.
Share:

JENERALI MSTAAFU GEORGE MWITA WAITARA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA UWANJA WA GOFU 'SERENGETI NATIONAL PARK GOLF COURSE'

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Jenerali (Mstaafu) George Mwita Waitara ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa gofu ambao umebeba jina la SERENGETI NATIONAL PARK GOLF COURSE wa kipekee duniani katika eneo la Fort Ikoma Wilayani Serengeti Mkoa wa Mara.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi na uzinduzi wa kampuni ya uwekezaji ya TANAPA – Tanapa Investment Ltd, Waitara ambaye ni mtaalam na mbobevu katika mchezo huo alisema dhumuni kubwa la kuanzisha zao hili la utalii ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni tano na mapato ya dola za kimarekani kufikia bilioni sita ifikapo mwaka 2025.

“Ni Dhahiri kwamba kutokana na umaarufu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti tuna kila sababu ya kuamini kwamba zao hili jipya la utalii litakuwa kivutio kikubwa na chachu ya kuongeza mapato yatokanayo na utalii katika shirika letu na Taifa kwa ujumla”, alisema Waitara.

Akifafanua zaidi, Mwenyekiti wa Bodi hiyo alisema kwamba sehemu ya kwanza ya mradi huo imekamailika ambapo mashimo mawili na sehemu ya mazoezi (range) yamekamilika na kwamba mtandao wa mashimo mengine 16 pia umekamilika.

Aidha, Waitara ametoa wito kwa wawekezaji na wafanyabiashara ya utalii kutambua uwepo wa zao hili, kulitangaza na hatimaye kuleta wachezaji wa golf ambao pia watatalii katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Akizungumza katika taarifa yake juu ya mradi huu, Kamishna wa Uhifadhi, William Mwakilma wa TANAPA amebainisha kuwa mradi huu unatekelezwa na kampuni ya Uwekezaji ya shirika TANAPA INVESTMENT LIMITED ambayo imeanzishwa kwa maelekezo ya Serikali ili kutekeleza shughuli mbalimbali za ujenzi ndani nan je ya Shirika.

“Kukamilika kwa mradi huu kunategemea kuwavutia wacheza golf zaidi ya 3,000 kwa mwaka kutoka ndani nan je na shirikila linatarajia kupata TZs bilioni 2 kwa mwaka.” Alisema Kamishna Mwakilema.

Akiwasilisha salamu za kihandisi, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa wahandisi (ERB), Mhandisi Wakili, Menye Manga aliahidi kufanya kazi kwa karibu na kampuni ya TANAPA Investment Ltd na kupongeza uanzishwaji wa kampuni hiyo ambayo ina wataalam wa kutosha na vifaa vya kutekeleza kazi mbalimbali za kihandisi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha gofu nchini, Gilman Kasiga aliishukuru TANAPA na hasa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA kwa kuendeleza michezo nchini hususan mchezo huu wa gofu na kuahidi kuleta mashindano makubwa ya kimataifa katika kiwanja hicho kwani kinakidhi viwango vya kimataifa.

Ujenzi wa uwanja huu wa golf unatarajiwa kugharimu jumla ya shilling bilioni 7.5 mpaka kitakapokamilika.




Share:

Wednesday 28 December 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DESEMBA 29,2022




Share:

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AWASILI MAKAO MAKUU YA WIZARA JIJINI DODOMA, NAIBU KATIBU MKUU AONGOZA MAPOKEZI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akipokea maua kutoka kwa mtumishi wa wizara hiyo,Aisha Juma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katikati ni Naibu Katibu Mkuu,Dkt.Maduhu Kazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo,Amani Mashaka wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na Mkaguzi Mkuu wa Ndani,Martina Nguluma wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na mtumishi wa wizara hiyo,Mariamu Omary wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na mtumishi wa wizara hiyo,Juma Mnyanile wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger