Saturday 24 July 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 24,2021








































Share:

Friday 23 July 2021

ALIYEIBA GARI NA KUTAMBA NALO MTAANI AGONGA NA KUUA WANAWAKE WANNE

Wanawake waliofariki dunia kwa kugongwa na gari
**
 Wakazi wa Kiharu katika huko Murang'a nchini Kenya wanaomboleza kifo cha wanawake wanne waliofariki dunia walipokuwa wakirudi nyumbani kutoka kanisani na gari lililokuwa limepoteza mwelekeo likiendesha na kijana mdogo aliyeiba gari hilo nyumbani kwao bila idhini ya wazazi wake.

Tukio hilo la kusikitisha ambalo lilipelekea kifo cha Jane Waiego, Mary Njeri, Margret Karura Waithaka na Mary Waithera limetokea Jumapili, Julai 18,2021.

 Ripoti ya NTV ilionyesha kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa kundi la vijana ambao walitoweka pindi tu baada ya kutokea kwa ajaili hiyo kwenye ya barabara ya Murang'a- Kangema.

 Ripoti hiyo pia ilionesha kwamba mvulana aliyekuwa mdogo zaidi kati ya wenzake alikuwa amelichukua gari hilo kwao bila idhini ya wazazi wake.

Wanawake watatu walifariki dunia papo hapo naye mmoja alipoteza maisha yake akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Murang'a. 

Gari hilo lilipelekewa katika kituo cha polisi cha Murang'a huku uchunguzi ukianza rasmi.

 Familia zao zinaomba msaada wa kuandaa mazishi ya wanne hao.

 Tukio hilo linajiri takriban mwezi mmoja baada ya maafisa wa polisi kumkamata jamaa ambaye mtoto wake alinaswa kwenye kamera akiendesha gari la Toyota Prado TX katika eneo la Delview Park huko Thika.

 Kwenye video iliyosamba Jumapili, Juni 13, kijana huyo wa miaka saba alionekana akiendesha gari hilo la kifahari bila wasiwasi wowote huku akibadilisha gia kama mtaalamu.

 Kulingana na ripoti ya polisi, Ayub Kinyanjui Muigai alikamatwa katika eneo la Gatanga na maafisa wa trafiki kutoka Kikwara wakishirikiana na makachero wa DCI.

Chanzo - Tuko News
Share:

TANGA UWASA YAKUTANA NA WADAU KUPATA MAONI YA MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

 

MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa kikao cha wadau kilichofanyika leo kwenye ofisi zao za  Mwakidila  Jijini Tanga kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Alawi Ahmed  kushoto Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Chumbageni (CCM) Jijini Tanga  Saumu Bendera

 

Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Chumbageni (CCM) Jijini Tanga  Saumu Bendera akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akifuatiwa na  Meneja wa Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Alawi Ahmed
Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu Tanga Uwasa CPA Hussein Ubbena akizungumza wakati wa mkutano huo
Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala akizungumza wakati wa kikao hicho
Sehemu ya watendaji na madiwani wa Viti Maalumu (CCM) wakifuatilia kikao hicho


MKUTANO wa Wadau wa Tanga Uwasa kwa ajili ya kupata maoni kuhusu mkataba wa huduma kwa mteja ambao umefanyiwa marejeo mwaka 2021 umefanyika leo Jijini Tanga kwa kuwashirikisha Madiwani wa viti Maalumu,Maafisa Tarafa wa Jiji la Tanga na Maafisa Watendaji wa Kata.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema wameamua kukutana na viongozi hao kwa sababu wana watu wengi ambao wanawawakilisha na maoni yao ni kwa ajili ya wananchi wote na sio yao tu.

Alisema kwa sababu wao ndio viongozi waliopo kwenye maeneo hayo hivyo wajitahidi kuhakikisha ushiriki wao kwenye mkutano huo unakuwa na tija kubwa na sio bora mambo yaende hivyo hakikisheni mnatumia vizuri uwepo wenu.

“Tunazungumzia mkataba wa huduma kwa mteja amesema mwenyekiti hapa ni utawala bora lazima mnapokuwa mnapeana huduma muwe na kitu ambacho kinawaunganisha na kitu kinatuunganisha ni huu mkataba haki na wajibu wa pande zote mbili mtoa huduma na mpokeaji wa huduma “Alisema

Alisema wawasilishaji wa mada watawapitisha ili iwe rahisi kwenu kueleza muundo wa mkataba upoje?haki na wajibu upoje,zawadi na adhabu zipoje na mwisho wa siku ukikiuka mkataba tunakufanyaje hayo mambo yote inabidi tuyajadili kwa pamoja leo hapa“Alisema

Aidha alisema huo mkataba ni kwa wale watu ambao wana huduma na wale ambao bado hawana maana mwisho wa siku wataomba kwa ajili ya kuunganishiwa maji kwa sababu kuna vitu ambavyo anapaswa kufanya yeye na mtoa huduma na ukishafahamu hivyo itakuwa rahisi.

“Hiki ni kikao cha wadau tunakaa kwa ajili ya kupitia kwa sababu ni zoezi shirikishi na watakapomaliza hapo wataenda kukutana na wadau wengine halafu baada ya maoni yao yakishafanyiwa kazi yatapelekwa kwa mdhibiti Ewura kwa ajili ya kupitishwa rasmi na baadae watatengeneza vitabu watavigawa kwa wadau wao kwenye ofisi mbalimbali ikiwemo za Kata na watatoa nakala za kutosha ili kila mmoja aweze kupata.

Awali akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Chumbageni (CCM) Jijini Tanga Saumu Bendera alisema madhubuti ya mkutano huo ni kupitia maboresho ya mkataba kwa wateja .

Alisema kama wanavyojua maboresho mkataba ni kwamba mteja kuna haki na wajibu na pia vilevile mtoa huduma hivyo ni jambo jema ambalo linawapa wigo mpaka wa kutambua mambo mbalimbali.

Alisema kama wanavyojua Serikali imekuwa ikifanya maboresho ya kila siku na huo maana yake ni utawala bora kwa hiyo wamefika kama wadau kuweza kusikiliza maboresho hayo na wao wajue haki zao na wajibu wao na pia mtoa huduma na baadae watapitia na kuchangia.

Naye kwa upande wake,Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala akizungumza katika mkutano huo wakati akiwasilisha mada ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Tanga Uwasa.

Alisema kwamba mkataba wa huduma kwa mteja unatakiwa kufanyiwa maboresho kila baada ya miaka mitatu na maboresho hayo yanapofanyika lazima wadau wahusishwe kuhusiana na nini ambacho kinajiri.

Alisema watawapitisha kwenye mkataba wote ili wapate kufahamu na kuona huo mkataba umehusisha nini na nini na maeneo gani ambayo yamefanyiwa maboresho.

Awali akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu Haki na Wajibu wa Mteja Tanga Uwasa Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu Tanga Uwasa CPA Hussein Ubbena alisema lengo la mkutano huo ni matakwa ya sheria kwamba serikali inataka Taasisi zake zote zinazotoa huduma ziwe zinaingia mikataba ya huduma bora na wateja wake hivyo leo walikuwa wanatimiza takwa hilo la kisheria.

Alisema kwamba Mamlaka iliandaa mkataba wao wa kutoa huduma na leo wamefanya wasilisho kwa wadau ambao ni watendaji wa serikali za mitaa na madiwani viti waliwasilisha mkataba ambao waliitengeza kama drafti ili waweze kupata maoni yao jinsi ya kuuboresha na hatimaye uweze kutumika.


Share:

Picha : MATUKIO KUTOKA TUME YA UTUMISHI WA UMMA –JIJINI DAR ES SALAAM LEO JULAI 23 2021


Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa baadhi ya Wanachama wa TUGHE Tawi la Tume ya Utumishi wa Umma, Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na PSC).
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (mstaafu) Mheshimiwa Dkt. Steven J. Bwana (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi Hodari wa Tume baada ya kuwakabidhi Hati zao za Mfanyakazi Hodari wa Tume ya Utumishi wa Umma kutoka TUGHE kwa mwaka 2020/2021. Kushoto ni Bw. Nyakimura Muhoji, Katibu wa Tume. Hafla ya kuwakabidhi Hati hizo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji (Mstaafu) Mheshimiwa Dkt. Steven J. Bwana (kushoto) akizungumza na Wafanyakazi Hodari wa Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam baada ya kuwakabidhi Hati zao za Ufanyakazi Hodari kwa mwaka 2020/2021 zilizotolewa na TUGHE, pamoja naye ni Bw. Nyakimura Muhoji (wa pili kushoto) Katibu wa Tume, Bw. Gift Lyimo (Afisa Utumishi) na Bw. Charles Mulamula, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume. 
Bw. Nyakimura Muhoji, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma akiwashukuru baadhi ya Wanachama wa TUGHE Tawi la Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) waliofika Ofisini kwake leo kutoa shukrani kwa kuwa mwanachama wa TUGHE na kwa kutambua mchango wake alioutoa kwa Tume.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana (kushoto) akimpongeza baada ya kumkabidhi Hati ya Mfanyakazi Hodari iliyotolewa na TUGHE, Bi. Nuru Abdallah Hanti (kulia) Afisa Utumishi (Idara ya Rufaa na Malalamiko) Tume ya Utumishi wa Umma aliyechaguliwa kuwa mfanyakazi bora na hodari wa Tume kwa mwaka 2020/2021, hafla imefanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
Dkt. Garvin Kweka (wa kwanza kushoto) kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kitengo cha Figo akifafanua jambo kwa Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Umma leo wakati wa mafunzo kuhusu UKIMWI/VVU mahali pa kazi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
Dkt. Garvin Kweka kutoka Kitengo cha Figo, Hospitali ya Taifa Muhimbili akifafanua jambo kwa Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) wakati wa mafunzo kuhusu UKIMWI/VVU kwa Wafanyakazi wa Tume leo Jijini Dar es Salaam.
Bi. Celina Maongezi (kulia) Katibu Msaidizi, Tume ya Utumishi wa Umma akipima afya na VVU kwa hiari wakati wa mafunzo kuhusu UKIMWI yaliyotolewa leo kwa Watumishi wa Tume, kushoto ni Dkt. Hamdani Kanaya kutoka Maabara ya TAMISEMI.  (Picha na PSC).
Share:

MBUNGE WA CHALINZE ATEMBELEA SHULE YA KIWANGWA ILIYOUNGUA MOTO


Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mkoani Pwani Ridhiwan Kikwete akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Hajat Mwanaasha Tumbo leo Julai 23,2021 wamefika katika Shule ya Sekondari Kiwangwa na kujionea athari zilizotokana na moto ulioteketeza bweni la wasichana shuleni hapo ambapo wameazimia kurejesha mazingira katika hali yake ya kawaida ili watoto waendelee na masomo.

"Nimefika eneo la Shule ya Sekondari ya Kiwangwa kushuhudia uharibifu uliotokana na Moto uliounguza Bweni la Wasichana shuleni hapo. Shuleni hapo nimekutana na Katibu Tawala wa Mkoa Pwani Hajat Mwanaasha Tumbo. Tumejipanga kudhibiti na kuhakikisha hali inarudi vizuri kimasomo",alisema Mbunge wa Chalinze, Kikwete.

Bweni la wasichana Shule ya Sekondari Kiwangwa, lilishika moto na kuteketea kabisa usiku wa kuamkia leo Julai 23,2021 na hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo.
Jengo la Bweni lililivyoteketea
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akizungumza na uongozi wa shule na mkoa
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akizungumza na uongozi wa shule na mkoa
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akitembezwa.
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akizungumza
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Hajat Mwanaasha Tumbo (mwenye babibui nyeusi) akizungumza.
Share:

Mfanyabiashara Tabora Atiwa Mbaroni Kwa Kukutwa Akiuza Vifaa Tiba na Dawa Ambazo ni Mali ya Serikali


Na Lucas Raphael,Tabora  -TDMA
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba kanda ya magharibi imefanikiwa kumkamata mfanyabiashara Zakayo Bagomwa aneyemiliki Duka la Dawa  muhumu ilinaloitwa Maliza na Yesu  akiuuza dawa za kifua kikuu TB ,kadi za kliniki za Kina mama Wajawazito, kutoa huduma za matibabu ndani ya duka , vifaa tiba mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kenya vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 4,869,900.

Akizugumza na waandishi wa habari leo Kaimu meneja wa Mamlaka ya hiyo kanda ya magharibi Christopher Migoha alisema kwamba tukio hilo litokea julai 20 mwaka huu mara baada ukaguzi maalumu wa duka la dawa katika Kijiji cha Kanindo, Kata ya Kanindo, Tarafa ya Ulyankulu, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora.

Alisema kwamba katika duka hilo  walikuta  Dawa za Serikali ya Tanzania zikiwa zimetunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuuzwa kinyume cha Kifungu cha 312(1) cha Kanuni ya Adhabu Sura 16.

Alisema kuwa walikuta Vitendanishi vya kupima UKIMWI pamoja na Vitendanishi vya kupima Malaria ambavyo ni Mali ya Serikali ya Tanzania vikiwa vimehifadhiwa na kutunzwa kwa ajili ya kuuzwa kinyume cha Sheria.

Aidha kaimu meneja huyo alisema kwamba kwenye duka hilo kulikuwa na  Dawa zisizosajiliwa kutumika nchini zikiwa zimehifadhiwa na kuuzwa kinyume cha Sheria 

Migoha aliendelea kusema kwamba ndani duka  walikuta dawa mali ya Serikali ya Kenya zikiwa zimetunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuuzwa  .

Alisema kwamba ndani ya duka hilo walikuta dawa zisizoruhusiwa kuuzwa katika maduka ya dawa muhimu na kukuta  dawa zikiwa zimetunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuuzwa kinyume cha kanuni ya 63 ya Makundi ya Dawa ya Mwaka 2015.

Hata hivyo meneja huyo wa kanda ya magharibu alisema kwamba walikuta  dawa zilizokwisha muda wake wa matumizi zikiwa zimetunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuuzwa kinyume cha Kifungu cha 75(1) cha Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba Sura 219.

Alisema kwamba mmiliki hyo hakuweza kuwasilisha risiti za manunuzi wala mauzo ya dawa zote alizokutwa nazo kinyume cha  Kanuni za Uendeshaji wa Biashara ya Dawa za Binadamu.

Migoha aliendelea kusema kwamba kulikutwa Vifaa Tiba ambavyo ni Seti ya  kufanyia tohara vikiwa vimetunzwa kinyume cha Sheria pamoja na dawa za wangojwa wa kifuu kikuu ambazo hazikustahili kuwepo ndani ya duka hilo wala kuunzwa kwenye maduka ya dawa muhimu.

Aidha aliwataka wadau  wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) na  Wafanyabiashara wote wa bidhaa za Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi kufanya biashara zao kwa kuzingatia Sheria ya Dawa na Vifaa tiba Sura 219 pamoja na Sheria zingine    .


Share:

Wakulima 99,468 Bariadi kunufaika na mfumo mpya wa kilimo cha pamba


Samirah Yusuph.
Bariadi. Bodi ya pamba Tanzania (TCB)  imewafikia wakulima 99,468 waliopo wilaya ya Bariadi katika kampeni ya kitaifa ya kuongeza tija ya kilimo cha pamba nchini .

Kampeni hiyo iliyozinduliwa wilayani hapo juma lililopita ikilenga kuwawezesha wakulima kupata uelewa wa vipimo sahihi na vyenye tija katika maandalizi ya kilimo cha pamba pamoja na upandaji wa mbegu.

Akizungumza na watendaji wa vijiji,kata, maafisa kilimo na ugani pamoja na wakuu wa idara katika wilaya ya Bariadi baada ya kukamilisha mafunzo barozi wa kilimo cha pamba nchini Agrey Mwanri amesisitiza kuendelea kutoa mafunzo ya mfumo bora wa kilimo cha pamba kwa wakati ili msimu wa kilimo unapo anza kila mkulima awe na uelewa wa kutosha.

Mwanri amesema kuwa ili kila mkulima tumie mfumo wa kisasa wa sentimita 60 kwa 30 ni lazima viongozi wote katika wilaya washiriki kikamilifu katika kutoa elimu kwa kuonyesha tija iliyopo iwapo mkulima atatumia mfumo huu wa vipimo pamoja na manufaa yake katika uzalishaji.

"Shirikiana na mkulima tangu hatua za awali muelimishe namna ya kuweka mbolea msimamie hadi mavuno na yeye akiwa anaona shamba lako la lake yote yapo sawa sio unaenda kumpangia masharti tayari anakaribia mavuno, tuanze nao tangu mwanzo".

Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha mkulima anajikwamua kiuchumi na kuona thamani ya kilimo, hivyo kwa watendaji watakaokuwa wazembe na kufanya kinyume itakuwa ni ukaidi wa sera ya kitaifa katika kilimo.

Kwa upande wake Renatus Luneja Mkaguzi wa kutoka bodi ya  Pamba alieleza kuwa pamoja na kuhamasisha matumizi ya samadi na mbolea za viwandani pia viongozi wananwajibu wa kuhakikisha wakulima wote wanakuwa katika vyama vya ushirika.
 

"Ni rahisi kuwafikia wakulima wanapokuwa Katika vyama vya ushirika hamasisheni wajiunge katika ushirika huku mkiendelea kuwapa elimu ili tija ya kilimo ionekane".
 
Kampeni ya kuongeza tija ya kilimo cha pamba nchini imelenga kuwafikia wakulima zaidi ya laki tano katika mkoa wa Simiyu ambapo hadi sasa zaidi ya wakulima laki moja wa wilaya ya Busega na Bariadi tayari wamefikiwa.



Share:

KUTANA NA FAMILIA YA AJABU YA WATU 9, WOTE WAMEZALIWA TAREHE MOJA



Mwalimu mmoja nchini Pakistan kwa jina Amir Ali, amevunja rekodi ya dunia kwa kuwa na familia yenye watu wengi waliozaliwa katika tarehe moja –ya Agost mosi baada ya watu tisa wa familia moja kuzaliwa tarehe hiyo.

Rekodi ya awali ilikuwa imeshikiliwa na familia kutoka Caymans kwa miaka tisa ambapo watoto watano walikuwa wamezaliwa tarehe 5 mwezi Februari lakini miaka tofauti.

Amir, mkazi wa Larakana , alisema alizaliwa tarehe 1 mwezi Agosti ,Mke wake alizaliwa tarehe moja mwezi Agosti , Binti yake wa kwanza Sindh alizaliwa mwanawe wa kiume wa pili Amber na wanae pacha Ammar na Ahmar, wote walizaliwa tarehe 1 Agosti.

Amir Ali anaamini katika elimu ya nyota- nyota yake ni Asad au Zmarai na inaelezwa kuwa namba ya kwanza ya bahati, wakati alipoanza kazi tarehe 1 mwezi Agosti na kuoa tarehe 1 mwezi Agosti.

Amir anasema familia yake yote inasheherekea siku ya kuzaliwa kwao siku moja. Bw. Amir pia anaamini katika unajimu na kuandika ushairi. Ana shahada ya uzamili kwenye masomo kadhaa, ikiwemo sayansi ya jamii, mahusiano ya kimataifa na uchumi.

Tarehe 1 mwezi Agosti, familia yote husheherekea kwa pamoja, Bw. Amiri anasema. Anaongeza kuwa watoto wote wamezaliwa nyumbani kisha wakasajiliwa na mamlaka za manispaa. Aliongeza kuwa kwa ushauri wa rafiki yake, alituma maombi ya usajili kwa ajili ya kuwekwa rekodi kwenye Guiness Book of World Records.
Share:

TRENI YENYE KASI ZAIDI DUNIANI YAZINDULIWA




Treni yenye uwezo wa kusafiri kwa kasi ya kilomita 600 kwa saa imezinduliwa katika eneo la Qingdao nchini China. Treni hiyo ya mfumo wa Magliev iliotengenezwa na shirika la reli nchini China ndiyo treni yenye kasi zaidi duniani CRRC kwa sasa.

‘’Magliev ni neno kwa ufupi lenye maana ya Magnetic Levitation’’. Treni hiyo inaonekana kuelea angani kutokana na nguvu za umeme zinazoifanya kuonekana kuwa juu ya barabara ya reli.
Liang Jianying, naibu meneja na muhandisi mkuu wa shirika la CRRC Sifang, aliambia vyombo vya habari nchini humo kwamba mbali na kasi yake , treni hiyo haina kelele na inahitaji uangalizi mdogo ikilinganishwa na treni zengine zenye kasi ya juu. Mfano wa treni kama hiyo ulifichuliwa kwa vyombo vya habari mwaka 2019.

Mwaka huohuo, China ilitangaza mipango yake ya kuanzisha uchukuzi wa saa 3 katika katika miji yake mikuu. Reli yenye kasi ya juu nchini China ni kipaumbele , ikiwa na lengo la kuunganisha miji yake mikuu kwa treni ili kupunguza muda na gharama za usafiri ndani ya taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu duniani.
Kwa sasa , wastani wa kasi ya treni nchini humo ni kilomita 350 kwa saa, huku ndege zikiendeshwa katika kasi ya kati ya kilomita 800 hadi 900 kwa saa. Treni kama hiyo iliozinduliwa Qingdao inaweza kujaza pengo muhimu lililopo katikati. Hatahivyo kuna kitu kimoja muhimu ambacho ni kizuizi katika ufanisi wake ukosefu wa reli za magliev ambazo hazijakamilishwa.

Kwa sasa China ina reli moja pekee ya mfumo wa Magliev inayotumika kibiashara, na inaunganisha uwanja wa ndege wa Pudong huko Shanghai na kituo cha barabarani cha Longyang mjini humo. Safari hiyo ya kilomita 30 huchukua takriban dakika saba na nusu huku treni hiyo ikisafiri kwa kasi ya kilomita 430 kwa saa moja.
Share:

CORONA YAUA WATU 29 TANZANIA, WAZIRI ASEMA "UGONJWA UPO NA WATU WANAKUFA..WATU WACHUKUE TAHADHARI"

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amesema hadi sasa jumla ya watu 29 wamefariki dunia kutokana na wimbi la tatu la Covid-19 huku jana Julai 22,2021 pekee kulikuwa na jumla ya wagonjwa wapya 176.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 23,2021 Dkt. Dorothy amesema takwimu hizo ni alizopata jana hivyo upo uwezekano vifo zaidi vikawa vimetokea.

“Itoshe kuwaambia kuwa ugonjwa upo na watu wanakufa, tusingependa kupeana hizi taarifa za vifo tuchukue tahadhari, kila mmoja wetu ajiulize unapofanya mambo kinyume na kuchukua tahadhari unalenga kumtesa nani,” amesema Dkt. Gwajima.

Idadi hiyo inafikisha Tanzania kuwa na jumla ya wagonjwa 858 wa Covid-19.
Share:

SPIKA JOB NDUGAI : TOZO ZA MIAMALA YA SIMU NI HALALI, FEDHA ZITACHAGIZA MAENDELEO


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai

Na Dotto Kwilasa, Dodoma.

Baada ya mijadala mingi kuhusiana na tozo ya miamala ya simu hususani kwenye mitandao ya kijamii ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameibuka na kudai kuwa tozo hizo ni halali na kwamba fedha hizo zitachagiza masuala ya maendeleo ikiwemo huduma za kijamii kama vile shule,hospitali na maji.

Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kwamba kumekuwa na tozo kubwa katika miamala ya simu huku akipigilia msumari kwenye tozo hizo kwa kudai kuwa Bunge ndio limepitisha na kwamba wanaopinga wanatakiwa kutoa mawazo mbadala nini kifanyike huku akisisitiza lengo ni ifikapo 2025 Tanzania iwe Taifa tofauti katika suala la Maendeleo.

Akizungumza mapema leo Julai 23,2021,katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,Spika Ndugai amesema "Sisi kama Bunge tulikaa kwa pamoja na kujadiliana kisha tukaamua kuwa na tozo katika miamala ya simu kwa sababu fedha zitakakazopatikana zitaenda katika mfuko Maalum ambao utawasaidia wananchi,"amesema na kuongeza;


"Tumepitisha na tukatunga sheria , tunataka kuliona hilo,sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofaut,CCM hoyee,nimemaliza,"amesema Spika huyo.


Pamoja na hayo amezungumzia kuhusu maendeleo ya mkoa wa Dodoma na kuwataka watendaji wa mkoa wa huu kujitathimini katika utekelezaji wa majukumu yao kwani serikali imekuwa ikitimiza wajibu wake kwa kuleta fedha kwa wakati lakini tatizo lipo kwa watendaji.

"Naomba nitolee mfano kwa mkuu wa mkoa wa huu Antony Mtaka ,alimetoka Simuyu kule alifanya kazi nzuri, hivyo hapa akishindwa kufanya vizuri tujue kabisa tatizo lipo kwetu na sio kwake,tukishirikiana nae vizuri ataacha alama kubwa kwenye Mkoa wetu,"amesisitiza Ndugai.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amebainisha vipaumbele vinne ambavyo atavisimamia katika mkoa wa Dodoma na kusema kuwa kama watafanikiwa, Jiji la Dodoma litakuwa la kiuchúmi zaidi.

Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na Elimu, migigoro ya Ardhi, kilimo na ufugaji venye tija na huduma bora za sekta za afya huku akitangaza alizeti kuwa zao la biashara katika mkoa huo.

Akizungumzia katika kikao hicho ametaja lengo la kikao hicho kuwa ni kuweka mikakati ya pamoja ili kwenda pamoja kama timu katika kutekeleza mambo yanayohusu maendeleo.

"Ukitaka kufanikiwa nenda na wenzako,nawasii tuwe na lugha ya pamoja yapo Mambo mazuri wenzetu wameyafanya hivyo lazima tuyaendeleze, sisi Dodoma tunautofauti tunabeba haiba ya makao makuu ya nchi hivyo ni lazima tuwe na matarajio makubwa,"amesema.

Licha ya hayo Mtaka amezungumzia kiwango cha elimu Mkoa wa Dodoma kuwa kipo katika hali mbaya, katika ngazi zote ikiwemo mitihani ya mock kwa mkoa haujafanya vizuri hivyo zinahitajika nguvu za ziada kuhakikisha mkoa unafanya vizuri katika sekta ya elimu na kuondokana na aibu iliyopo.

"Halmashauri zote nane za mkoa wa Dodoma mnatakiwa kuwa na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitatuingizia fedha za kutosha kuendesha miradi mbalimbali,na kuufanya Mkoa wetu kuwa wa mfano,"amesisitiza Mtaka.

Amesema Jiji la Dodoma limekusanya sh.bilioni 70 kutokana na mauzo ya viwanja sasa wapo kiwango cha sh.bilioni 30 hivyo lazima watafute vyanzo vipya vya mapato na anatamani kuona ubunifu katika suala hilo.

"Natamani kuona kila kaya zikipanda miti mingi kwa ajili ya Utunzaji wa mazingira pamoja na kuweka Mipango mizuri ya Utunzaji wa mazingira katika mkoa huu,"amesemà.

Mtaka pia amesisitiza kuwa "Lazima niseme ukweli kwamba ili tufanikiwe Katika yote haya tuukatae uchonganishi na unafki,Wapo Watumishi waongo na wachonganishi siwapendi, watu wanachonganisha watu, hasa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, tumekutanishwa na kazi tufanye kazi tuheshimiane kiongozi haongozwi,".

Akitilia mkazo suala hilo amesemà ikitikea watumishe waongo na wachonganishi wakiendelwa kumtumia meseji atawataja hadharani ili kuepusha maneno na vikwazo katika uongozi wake.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger