Tuesday 2 March 2021

TCRA YAPATA DAWA YA MALALAMIKO YA VIFURUSHI 'BANDO'...MATAPELI MTANDAONI NAO KUNYOOSHWA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,) Mhandisi. James Kilaba

***

 *Kanuni zaruhusu watumiaji kuhamishiana 'uniti' za vifurushi


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,) imeandaa kanuni ndogo ambazo zitawezesha kutatua kero za watumiaji wa huduma na kuongeza ustawi wa sekta ya mawasiliano ikiwemo ya mtoa huduma kuweka utaratibu au mfumo wa kumwezesha mtumiaji wa huduma kuhamisha uniti za kifurushi kwenda kwa mtumiaji mwingine ndani ya mtandao wake kwa masharti mawili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,) Mhandisi. James Kilaba amesema  TCRA imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikihusisha watoa huduma ili kushusha bei ya simu za kawaida ambazo ni bei ya nje ya vifurushi, na kanuni hizo zitaanza kutumia Aprili 2, mwaka huu.

Mhandisi Kilaba amesema, Februari 5 mwaka huu TCRA ilitoa matangazo ya kukaribisha maoni ya wadau wote wakiwemo watoa huduma, watumiaji na Serikali kuhusu huduma za vifurushi vinavyouzwa na watoa huduma kwa wateja ili kuhakikisha ufanisi na kuwezesha upatikanaji wa huduma bora kulingana na thamani ya fedha ya malipo yaliyofanywa na wanaojiunga na vifurushi husika na jumla ya maoni 3,278 yalikusanywa.

"Moja ya kanuni ya ni mtoa huduma kuweka utaratibu au mfumo wa kumwezesha mtumiaji wa huduma kuhamisha uniti za kifurushi kwenda wa mtumiaji mwingine ndani ya mtandao wake kwa masharti kwamba.....kiasi cha chini cha kuhamisha kitakua 250 Mb na mtumiaji anaweza kuwahamishia watumiaji wasiozidi wawili na mtumiaji aliyehamishiwa kifurushi hataruhusiwa kumhamishia mtumiaji mwingine uniti hizo au sehemu ya uniti alizohamishiwa." Ameeleza Mhandisi Kilaba.

Akieleza kanuni nyingine ambazo watoa huduma watatakiwa kuzifuata Kilaba amesema mtoa huduma hatatoa huduma bila kibali maalumu cha Mamlaka hiyo.

Aidha mtoa huduma atahakikisha kwamba bei za vifurushi zinazingatia bei husika ya chini na juu zilizowekwa na Mamlaka hiyo pamoja na mtoa huduma kutumia lugha rahisi na vigezo na masharti yaliyo wazi kuhusu vifurushi vinavyotolewa.

Aidha amesema, mtoa huduma anatakiwa kutoa fursa kwa mtumiaji wa huduma za mawasiliano kuchagua na kujiunga na vifurushi visivyokuwa na ukomo wa muda wa matumizi vitakavyopatikana kwenye Menu kuu, na watoa huduma wote watatumia jina linaalofanana kwa vifurushi hivyo ili vitambulike kwa wepesi na hiyo ni pamoja na kutoondolewa, kurekebishwa au kubadilishwa kwa vifurushi ndani ya siku 90 tangu kuidhinishwa kwake.

Vilevile kanuni hizo zinawataka watoa huduma kutoa taarifa pindi matumizi ya kifurushi yatakapofikia asilimia 75 na 100 kwa vifurushi vya muda wa maongezi, data na ujumbe mfupi (Sms) Pamoja na kutopunguza kasi ya mtandao katika kifurushi na hilo ni sambamba na watoa huduma kuweka programu Rununu ili kuwawezesha watumia huduma wenye simu janja kufuatilia matumizi yao ya data kwa kupakua Programu Rununu hiyo kutoka kwa mtoa huduma.

Kanuni nyingine iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo ni kwa watoa huduma kuweka utaratibu unaowawezesha watumiaji wanaojiunga na huduma za vifurushi kuchagua na kukubali kutozwa gharama zisizokuwa kwenye vifurushi mara muda wa vifurushi wanavyojiunga au uniti za kifurushi husika kumalizika.

"Utaratibu huu wa kuchagua na kukubali utakuwa chaguo msingi mpaka pale anayejiunga achague na kukubali kutumia gharama nje ya kifurushi pindi kifurushi husika kinachoisha muda wa matumizi" Amesisitiza Kilaba.

Pia Kilaba amesema, watoa huduma waweka utaratibu wa kumwezesha aliyejiunga na kifurushi chochote kuendelea kutumia muda au uniti za kifurushi ambazo zitakuwa zimesalia ndani ya muda wa matumizi uliowekwa kwa kununua tena kifurushi hicho hicho kabla ya kumalizika muda wake.

Kilaba ametumia wasaa huo kuwakumbusha watanzania juu ya mapambano ya utapeli mtandao kwa kutokubali kutapeliwa kwa kutekeleza maelekezo yanayohusu miamala yoyote ya kifedha katika simu zao kwa kupigiwa simu kwa wanaojifanya ni wafanyakaziwa Kampuni yoyote ya simu na kuwataka kutuma namba za wanaopiga kwenda namba 15040 bure, na kwa wanaotumiwa jumbe fupi za utapeli wasitekeleze bali watume (Forward) jumbe hizo na namba za waliowatumia kwenda namba 15040.

Pia amewahimiza Watanzania kuhakiki namba zao walizosajili kwa kitambulisho cha Taifa kwa kubonyeza *106# kisha kuchagua namba 2 na kuangalia namba zilizosajiliwa kwa vitambulisho vyao na kuchukua hatua za kuzifuta kwa alama ya vidole kwa watoa huduma endapo watakuta namba ngeni zilizosajiliwa kwa vitambulisho vyao.

CHANZO - MICHUZI BLOG
Share:

WAZIRI AWESO : MSIFANYE KAZI KWA MAZOEA, BADILIKENI KIFIKRA


Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na wafanyakazi walio chini ya Wizara hiyo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Bonde la Kati mjini Singida
Wafanyakazi wa Bonde la Kati, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida Mjini (SUWASA) na Wakala wa Usambazaji maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wakiwa kwenye mazunguzo na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida Mjini (SUWASA), Patrick Nzamba akimkaribisha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso aweze kuzungumza na Wafanyakazi
****

 

Na Abby Nkungu, Singida
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewataka wafanyakazi wa Wizara hiyo kubadilika kifikra kwa kuanza kuchapa kazi kwa nguvu zaidi badala ya kuendelea kufanya kazi kwa mazoea.

Alitoa rai hiyo mjini Singida wakati akiongea na wafanyakazi wa Bonde la Kati, Mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira Singida mjini (SUWASA) pamoja na Wakala wa usambazaji maji na Usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Singida.

Waziri Aweso alisema kuwa kwa kipindi kirefu sasa, Wizara hiyo imekuwa ikinyooshewa vidole kutokana na baadhi ya watumishi wake kukosa uaminifu na uadilifu; hivyo kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

"Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Ili kutimiza azma ya kumtua mama ndoo kichwani, lazima kila mfanyakazi aondokane na uvivu, afanye kazi kwa kutumia taaluma yake na kwa kuiheshimu taaluma hiyo naamini fedha nyingi zitolewazo na Serikali zitatumika vizuri kwa manufaa ya wananchi" alisema na kuongeza;

Hii itarejesha heshima ya Wizara yetu.....Nataka zikitajwa Wizara tatu zinazofanya kazi vizuri, sisi Wizara ya Maji tuwemo".

Alisema kuwa kutokana na ukweli kwamba maji hayahitaji porojo, ngojangoja wala hakuna mbadala wake, wafanyakazi wote wa Wizara hiyo hawana budi kushikamana na kufanya kazi kwa pamoja kwa kuwa wote ni familia moja.

"Ili tuijenge Wizara yetu tushikamane, tujiepushe na majungu na fitina lakini pia pale mnapofanya kazi nzuri ionesheni na kuitangaza kwa umma ili mtambulike".

Adha, alitoa mwito kwa Menejimenti zote kuhakiksha zinajali maslahi ya wafanyakazi wake kwa kuwa maslahi duni humnyong'onyesha mtumishi lakini maslahi bora humtia nguvu na kumjaza ari ya kufanya kazi zaidi.
Share:

Picha : DC MBONEKO ATEMBELEA KIWANDA CHA CHAKI 'SHINYANGA STANDARD CHALK' ...AAGIZA KILA SHULE IZINUNUE


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa amebeba maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ametembelea Kiwanda cha Kutengeneza Chaki cha ‘Shinyanga Standard Chalk’kilichopo Mjini Shinyanga na kujionea jinsi uzalishaji wa chaki unavyofanyika na kutoa agizo kwa Wakuu wa Shule katika wilaya hiyo kununua chaki hizo.

Mboneko amefanya ziara katika kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga leo Jumatatu Machi 2,2021.

Akizungumza kiwandani hapo, Mboneko amewapongeza vijana walioanzisha kiwanda hicho kwa kutengeneza chaki mzuri na bora na kutoa agizo kwa Wakuu wa shule zilizopo katika wilaya ya Shinyanga na kuahidi kutafuta masoko zaidi kwenye wilaya zingine.

“Natoa agizo kwa wakuu wa shule zote watumie chaki zinazozalishwa katika kiwanda chetu cha Shinyanga, kuna chaki za kutosha nataka chaki hizi zinunuliwe. Hatuwezi kununua chaki nje ya Shinyanga wakati tunazo hapa kwetu kwenye kiwanda chetu,tena ni chaki nzuri sana na wazalishaji wanafuata taratibu zote za uzalishaji”,amesema Mboneko.

“Nataka kila shule inunue Boksi moja hadi mawili. Mzigo upo wa kutosha na vijana hawa wapo tayari kuwasambazia chaki hadi kwenye shule zenu”,ameongeza Mboneko.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana walioanzisha Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa Hashim amesema walianza uzalishaji wa chaki mwezi Aprili 2020 na sasa wana uwezo wa kuzalisha katoni 102 kwa siku.

Amesema licha ya uzalishaji mkubwa wanaofanya bado changamoto kubwa ni ukosefu wa masoko kutokana na soko la ndani kusuasua akibainisha kuwa endapo soko la ndani likiwa zuri basi wataweza kuuza chaki hizo nje ya wilaya ya Shinyanga ambapo amemshukuru Mkuu wa wilaya hiyo, Jasinta Mboneko kuwaunga mkono kwa kuhamasisha wakuu wa shule kununua chaki katika kiwanda hicho.

Hashim amewaomba wenye uhitaji wa Chaki nzuri zenye ubora wa hali ya juu za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk wafike katika kiwanda hicho kilichopo mtaa wa Miti Mrefu karibu na Ofisi za Ally's Bus  Mjini Shinyanga au wapige simu namba  0713 332 609 au 0747 844 341 au Email shystandard1@gmail.com

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia chaki muda mfupi baada ya chaki hizo kutolewa katika mitambo ya uzalishaji katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga leo Jumanne Machi 2,2021. Katikati ni Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa, kulia ni Mhandisi mkuu wa kiwanda hicho Amani Daniel. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia namna uzalishaji wa chaki unavyofanyika katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia namna uzalishaji unavyofanyika katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard  Chalk Hassim Issa akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) kuhusu uzalishaji wa chaki kwenye Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya mitambo katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia namna uzalishaji wa chaki unavyofanayia kwenye Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia chaki zilizoanikwa juani muda mfupi baada ya chaki hizo kutolewa katika mitambo ya uzalishaji katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia chaki zilizoanikwa juani muda mfupi baada ya chaki hizo kutolewa katika mitambo ya uzalishaji katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Muonekano wa chaki zikiwa zimeanikwa juani
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiangalia Boksi la kuhifadhia chaki katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akizungumza katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) changamoto wanazokutana nazo wakati wa uzalishaji wa chaki ikiwa ni pamoja na kukosa masoko
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pilikushoto) akizungumza katika Stoo ya kuhifadhia chaki kwenye Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akizungumza katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia maboksi ya ndani ya chumba cha kuhifadhia chaki katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa, kushoto ni Mhandisi mkuu wa kiwanda hicho Amani Daniel wakiwa wameshikilia maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) na viongozi mbalimbali wakiwa wameshikilia maboksi ya chaki
Muonekano wa chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk
Muonekano wa maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk

 Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

BABU WA MIAKA 77 AFARIKI DUNIA KWA KUTUMBUKIA KISIMANI



Mzee mmoja aliyefahamika kwa majina ya Joseph Rutabana mwenye umri wa miaka 77 mkazi wa kijiji cha Butairuka amepoteza maisha, baada ya kutumbukia katika kisima cha maji, kilichochimbwa katika eneo la Kanisa Katoliki Parokia ya Maruku, katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera.

Kaimu Mkuu wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika wilaya ya Bukoba, Mkaguzi Msaidizi Abrahman Ngaugia, amesema kuwa walipata taarifa za kwenda kufanya Uokozi saa kumi mchana, na kwamba walipofika eneo la tukio askari wa jeshi hilo Sajenti Karata Ramadhan ndiye aliyeingia katika shimo hilo na kufanikiwa kuutoa mwili wa mzee huyo kwa kushirikiana na askari wenzake.

Kwa upande wao baadhi ya ndugu, majirani na viongozi wa eneo hilo wamesema kuwa siku tatu kabla ya tukio, mzee huyo alionekana kama amechanganyikiwa na kuwa wakati akiondoka nyumbani aliaga kwamba anakwenda kuoga.
Share:

Finance Assistant – East Africa Youth Inclusion at Heifer International

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Description Heifer International is an equal opportunity employer. All qualified applicants will receive consideration for employment without regard to race, religion, color, national origin, gender, gender identify, sexual orientation, age, status as a protected veteran, among other things, or status as a qualified individual with disability. FUNCTION Under the guidance and leadership of EAYIP Accountant […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Program Assistant – Ending Violence Against Women and Girls at UNV – United Nations Volunteers

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Eligibility criteriaCandidate age: between 18 and 29 throughout the entire duration of their assignment. Applicants must be nationals of or legal residents in the country of assignment.  Description of taskReporting to EVAW/G Program Specialist (Team Leader), the Programme Analyst provides programme support to the effective management of UN Women programmes in the Tanzania by contributing […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Head, Treasury Risk at NBC Bank

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services.   Job Summary Ensure that all activities and duties are carried out in full compliance with regulatory requirements , Enterprise Risk Management Framework .Understand and […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Research Officer at Ifakara Health Institute

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Summary Position:                    Research Officer – 1 post Reports To:               Project Leader/ Principal Investigator (PI) Work station:                      Ifakara Institute Overview Ifakara Health Institute (IHI) is a leading research organization in Africa with a strong track record in developing, testing and validating innovations for health. Driven by a core strategic mandate for research, training and services, the […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Roving Budget Manager – Great Lakes at International Rescue Committee

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Requisition ID: req12483 Job Title: Roving Budget Manager – Great Lakes Sector: Grants Employment Category: Regular Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: Yes Location: Kinshasa, Democratic Republic of the Congo Job Description   This job can be located in DRC, Burundi, CAR, Tanzania or Kenya. In the Great Lakes region (Burundi, Central African Republic, Democratic Republic of the Congo, Tanzania) IRC responds […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

PRINTER GRADE II at TIE

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST PRINTER GRADE II – 1 POST POST CATEGORY(S) CREATIVE AND DESIGN EMPLOYER TANZANIA INSTITUTE OF EDUCATION (TIE) APPLICATION TIMELINE: 2021-03-01 2021-03-14 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To prepare work schedule; ii. To prepare working tools and equipment; iii. To assign work to staffs under him/her; iv. To make follow-up on on-going activities […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

LABOTATORY TECHNICIAN II at MUHAS

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST LABOTATORY TECHNICIAN II – 1 POST POST CATEGORY(S) HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) APPLICATION TIMELINE: 2021-03-01 2021-03-14 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To carry out specified tasks connected with research, laboratory practical/tests, students’ projects, consultancy and services under supervision; ii. To carry out specified tasks […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

ARTISAN II at MUHAS

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST ARTISAN II – 1 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) APPLICATION TIMELINE: 2021-03-01 2021-03-14 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To perform specified craft jobs under supervision; ii. To perform routine technical cleaning of the work environment; iii. To take care of tools and […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

HEALTH LABORATORY SCIENTIST at TAMISEMI

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST HEALTH LABORATORY SCIENTIST – 1 POST POST CATEGORY(S) HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) APPLICATION TIMELINE: 2021-03-01 2021-03-14 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To coordinate different laboratory tests in Health Laboratories and research; ii.To coordinate different samples which require special expertise and samples for […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

VECTOR CONTROL OFFICER at TAMISEMI

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST VECTOR CONTROL OFFICER – 1 POST POST CATEGORY(S) HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) APPLICATION TIMELINE: 2021-03-01 2021-03-14 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To coordinate and evaluate resistance of disease vectors against pesticides for the program; ii.To carry out studies on control of livestock […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

AHADI YA RAIS MAGUFULI KUPELEKA MAJI KEMONDO YATEKELEZWA KWA VITENDO

Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) na Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imeanza kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika mji wa Kemondo mkoani Kagera. 

Mradi wa maji wa Kemondo unatekelezwa kufuatia ahadi aliyoitoa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati akiomba kura mwezi Oktoba, mwaka 2020 kwa wananchi wa Kemondo. 

Akizungumza na wananchi wa Kemondo katika mwendelezo wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ameipongeza Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira kwa utekelezaji wa haraka wa miradi huo.

“Ni matumaini yangu kuona wananchi wa Kemondo wanapata huduma ya majisafi na salama mapema iwezekanavyo, hivyo tuna kila sababu ya kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huu kwa wakati”, alisisitiza Mhandisi Mahundi.

Alisema mradi huo unaotekelezwa kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account) ukikamilika utahudumia kata sita zenye vijiji 17  kwa awamu 3 ambapo awamu ya kwanza itakuwa kata ya Kemondo yenye vijiji viwili hivyo litajengwa tenki la lita milioni 3, mtandao wa mabomba, (raising main) kwa gharama ya shilingi bilioni 6.8 na mpaka sasa wameshapokea shilingi milioni 600.

Awamu ya pili itagharimu shilingi bilioni 7 na itahusisha kata nne za Maruku, Kanyangereko, Bujugo na Katerero na awamu ya mwisho itahusisha Kata ya Muhutwe ambayo kazi zake zitagharimu shilingi bilioni 3. 

Aidha, Naibu Waziri aliagiza ufanyike utaratibu wa kuongeza nguvu kazi ili vifaa vilivyopo katika eneo la mradi viweze kufanyiwa kazi kwa haraka na ikiwezekana kazi zifanyike usiku na mchana ili mradi ukamilike kwa wakati na wananchi wapate huduma ya majisafi na salama. 

Pamoja na hayo, Mhandisi Mahundi alikagua mradi wa maji wa Kyaka Bunazi uliopo katika Wilaya ya Misenyi ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 48 na ukikamilika utahudumia wananchi wapatao 65,000 kwa gharama ya shilingi bilioni 15.5, mradi huu unatekelezwa kufuatia agizo alilolitoa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11 Julai, 2019 ambapo aliagiza wananchi wa Bunazi wapate maji kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja.


Share:

GARI YATUMBUKIA MTONI NA KUUA WATU WANNE NJOMBE


Watu wanne akiwemo Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Lugarawa, Steven Mtega (39), wamefariki dunia kwa kuzama kwenye mto Lupali wakiwa kwenye gari waliyokuwa wakisafiria katika Kata ya Lugarawa wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Akizungumza kwa njia ya simu Mganga Mkuu wa wilaya ya Ludewa Dkt Stanley Mlay, amesema tukio hilo limetokea Febuari 27 majira ya usiku marehemu hao walikuwa kwenye gari aina ya Toyota Harrier ambapo walikuwa Lugarawa kwenye mambo yao ya mapumziko.

"Walipata ajali kwenye mto Lupali huu mto sasa hivi una maji mengi kwa sababu ya mvua zinavyonyesha, walikuwa watu wanne kwenye mambo yao ya mapumziko Lugarawa na dereva alikuwa huyo mkuu wa chuo wakasema wabadilishe maeneo waende Mundindi sasa walivyofika maeneo hayo ndio wakaingia mtoni," ameeleza Mganga Mkuu Dkt. Mlay.

Dkt. Mlay amewataja marehemu wengine kuwa ni Marko Mpete, fundi umeme wa Lugarawa, Merk Mwalongo (35) mjasiriamali na Rukia Mfaume (28), ambaye alikuwa mhasibu wa mradi wa umeme wa Akra Lugarawa, na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Lugarawa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Lugarawa Erasto Mhagama, akizungumzia kutokea kwa tukio hilo amesema tukio hilo limetokea mpakani mwa kijiji cha Shaurimoyo na kijiji cha Amani.

Via>>EATV
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 2,2021

































Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger