Monday 31 August 2020

TIC, Serikali ya Lindi Waanzisha Dawati la Uwekezaji kushughulikia Changamoto

Na Mwandishi Wetu, Lindi.
Serikali Mkoani Lindi kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC wameanzisha Dawati maalum la uwekezaji ambapo masuala yote yanayohusu uwekezaji sasa yanashughulikiwa  kupitia katika dawati hilo ambalo lengo lake ni kuwaweka karibu na kuwahudumia kwa upekee Wawekezaji wa Mkoa huo pamoja na kutangaza fursa zilizopo.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga amesema uamuzi wa Serikali wa kuanzisha dawati hilo Mkoani Lindi umekuja kufuatia kuwepo kwa fursa nyingi za Uwekezaji ambapo kwa kushirikiana na TIC wameweza kuzitangaza.

Mhe. Ndemanga aliyasema hayo wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC Dkt. Maduhu Kazi Mkoani Lindi, ambapo alisema kufuatia Kongamano la Uwekezaji lililofanyika mwaka jana waliweza kubaini masuala kadhaa ambayo yatasaidia kuongeza Wawekezaji.

“ Hapa Lindi tumeanzisha Dawati la Uwekezaji ambalo linatuweka karibu sisi na Wawekezaji wetu. Pia Ofisi ya TIC katika Kanda ya Kusini inafanya kazi nzuri ya kuhamasisha uwekezaji hivyo kwa kushirikiana nao tumepanga mambo makubwa na tutafanikiwa sana” alisema Mhe. Ndemanga.

Alisema Wawekezaji wengi wanafika Mkoani humo ambapo sasa kupitia dawati hilo wataweza kuwa karibu na kuwahudumia ipasavyo ambapo pia alizitaja baadhi ya Taasisi zilizoonesha nia ya kuwekeza ikiwepo Chuo Kikuu cha Dar es Salaama (UDSM) wanaotaka kujenga Chuo cha Utafiti wa Mazao, Chuo cha Usafirishaji na Chuo Kikuu cha Kiisilamu cha Morogoro; ambavyo vyote vimepata maeneo kwa ajili ya ujenzi wa vyuo husika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC Dkt. Maduhu Kazi alisema hatua ya Mkoa wa Lindi ya kutenga maeneo yenye miundombinu ya uwekezaji pamoja na kuwa na kuanzisha Dawati la Uwekezaji ni ya kupongezwa na kuiomba Mikoa mingine kuiga mfano wao.

“Mkoa wa Lindi mnafanya kazi nzuri kwa kutenga maeneo, kuweka miundombinu na kuanzisha Dawati la Uwekezaji, mmerahisisha kazi hizi kwa sababu sisi wote nia yetu ni moja katika mbinu za kuvutia uwekezaji” Alisema Dkt. Kazi.

Aidha aliuomba Mkoa huo kuwa na taarifa za maendeleo ya miradi na kufuatilia endapo Mwekezaji aliyeweka nia ya kuwekeza na hajawekeza, ili kujua ni changamoto gani alizokumbana nazo ili zisiweze kujirudia ambapo pia aliwashauri kufuatilia kwa karibu miradi iliyo mbioni kuanza ili iweze kuendelea na hivyo kukuza uchumi wa Mkoa na Nchi kwa ujumla.

Mwisho.


Share:

Shule ya Mivumoni Islamic Yaungua kwa Mara ya 3

Shule ya Sekondari ya Mivumoni Islamic, iliyopo katika eneo la Msikiti wa Mtambani Kinondoni Dar es Salaam, imeteketea kwa moto Alafajiri ya leo Agosti 31, 2020, na kuelezwa kuwa hii ni mara ya tatu shule hiyo kuungua ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Kamishina Msaidizi Mwanadamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni Salum Mohamed, amesema kuwa taarifa ya chanzo cha moto huo itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge.

"Kwa kipindi cha miezi miwili hili ni tukio la tatu katika shule hii, Julai 18 tulipata tukio la moto la muundo huu na tulizima, Julai 23 tukio la moto tena lilitokea hili ni tukio la tatu mfululizo ndani ya eneo moja, ni matukio ambayo yanaendelea kutokea ndani ya hizi Shule za Kiislamu za Jijini Dar es Salaam, uchunguzi umefanyika na Msemaji wa hili ili kujua chanzo ni nini ataitoa Mkuu wa Mkoa " amesema Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto.


Share:

MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI AFARIKI DUNIA KWA KULIPUKIWA NA BOMU


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi James Manyama
**
Mtoto mwenye mwenye umri wa miaka 9 katika kijiji cha Kasumo kata ya Kajana wilayani Buhigwe mkoani Kigoma amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu Agosti 28, 2020.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi James Manyama amesema,

''Mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Abas Jeras mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Lemba kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana alipatwa na mkasa huo tarehe 28 mwezi wa nane mwaka huu baada ya kuokota Bomu bila kujua na kuanza kulichezea kisha bomu hilo kuripuka na kusababisha apoteze maisha'',amesema Kamanda Manyama.

Polisi inahusisha uwepo wa Bomu hilo katika kijiji hicho huenda ni kilikuwa kikitumiwa kama njia na makundi ya waasi waliokuwa wakitoka nchi ya Burundi kwenda kambi ya wakimbizi ya Mtabila hivyo kudhaniwa huenda liliangushwa na watu hao.

Jeshi la polisi imetoa rai kwa wananchi wote wanaoishi vijiji vinavyopakana na nchi ya Burundi kuwakataza watoto kuokota vitu na kuvichezea ili kuepusha madhara kama yaliyotokea.
CHANZO - EATV
Share:

Tangazo La Nafasi Za Masomo Chuo Kikuu Kishiriki Cha Kumbukumbu Ya Stefano Moshi (SMMUCo)

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO
Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) kilichopo Moshi pamoja na Taasisi yake tanzu ya Masoka Professionals Training Institute (MPTI) kinatangaza nafasi za masomo kwa mwaka 2020/2021 katika ngazi ya:-

SHAHADA
1. Bachelor of Arts in Community Development
2. Bachelor of Accounting and Finance
3. Bachelor of Arts with Education
 
ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA)
1. Law
2. Information Technology
3. Accounting and Finance
4. Mass Communication
5. Community Development
6. Business Administration
7. Human Resource Management
8. Procurement and Supply
9. Tour guiding and Tourism
10. Office Management and Secretarial
11. Journalism
12. Records and Archives Management
13. Theology
 
SIFA ZA MWOMBAJI
Kozi za Cheti: Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne ufaulu wa alama D nne na kuendelea isipokuwa somo la Dini.
 
Stashahada (Diploma): Mwombaji awe amemaliza kidato cha sita na awe na Principal Pass moja na subsidiary moja isipokuwa somo la dini AU awe amehitimu Astashahada kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.
 
Shahada: Mwombaji awe amehitimu kidato cha sita na ufaulu wa alama nne na kuendelea katika masomo mawili isipokua masomo ya dini AU Awe amehitimu Stashahada kwa ufaulu wa G.P.A ya 3.0 na kuendelea kutoka chuo kilichosajiliwa na serikali na atume maombi yake kupitia mtandao wa chuo www.smmuco.ac.tz Bofya neno ONLINE APPLICATION, KWA MSAADA 0756 512 757, 0755 807199
 
FOMU ZA MAOMBI: Zinapatikana kwenye website ya Chuo www.smmuco.ac.tz
 
Kwa maelezo zaidi fika ofisi za udahili zilizopo Moshi Mjini au wasiliana nasi kwa namba; 0653-422 928, 0756-029 652, 0786 862 089,
0755 319 082,
+255 756 302 743,
+255 755 553 970,
068 726 3623,
+255 65 319 3550,
+255 67 278 7155.

 
MAOMBI YOTE YA KUJIUNGA NA CHUO NI BURE


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu August 31

















Share:

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Akabidhi Ramani Ya Tanzania Inayoonyesha Afya Ya Udongo Kwa Taha

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya jana (30.08.2020) amefanya kikao na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuendeleza Mazao ya Bustani (TAHA) Dkt.Jacquline  Mkindi jijini Arusha cha kujadili mikakati na mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya tasnia ya mboga mboga na matunda (horticulture) nchini.

Sambamba na kikao hicho, Katibu Mkuu Kusaya ameikabidhi TAHA zawadi ya Ramani ya Tanzania inayoonesha viwango vya pH na Afya ya Udongo kwa nchi nzima na imepokelewa na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Dr. Jacqueline Mkindi.

Kusaya ameitaka TAHA kuendelea kuelimisha wakulima wengi zaidi kuzingatia kilimo cha kitaalam kwa kutambua aina ya udongo unaofaa kwa zao husika na mbolea gani itumike, ndio maana amekabidhi ramani hiyo kuwezesha utambuzi wa maeneo yanayofaa kwa mazao ya horticulture nchini.

“Tunaendelea kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano mkubwa na wa muda wote inaotupatia wadau wa sekta ya horticulture ” Dr Mkindi alisema.

Katibu Mkuu Kusaya alikuwa mkoani Arusha Kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kutembelea taasisi zinazojihusisha na kilimo vikiwemo viwanda vya kuzalisha mbolea kwa matumizi ya kilimo.


Share:

Sunday 30 August 2020

VIGOGO YANGA SC YAWACHAPA AIGLE NOIR 2-0 KILELE CHA WIKI YA MWANANCHI


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Vigogo wa soka Tanzania, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Burundi, Aigle Noir katika mchezo wa kirafiki usiku wa leo Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais mstaafu wa awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete – Aigle Noir iliwaruhusu Yanga kupata mabao baada ya kiungo wake, Mghana Koffi Kouassi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29 kufuatia kuonyeshwa kadi ya njano ya pili na refa Martin Saanya wa Morogoro. 

Baada ya hapo Yanga SC wakapata bao la kwanza dakika ya 39 likifungwa na winga wake mpya, Tuisila Kisinda aliyemchambua kipa Mtanzania wa Aigle Noir, Erick Johola kufuatia pasi nzuri ya Feisal Salum ‘Fei Toto’. 

Mshambulaji mpya, Mghana Michael Sarpong akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 59 kwa kichwa kikali kutoka umbali wa mita sita kufuatia krosi maridhawa ya Ditram Nchimbi.

Na ikashuhudiwa kipindi cha pili kocha mpya wa Yanga SC, Mserbia Zlatko Krmpotic akibadili kikosi kizima.

Mchezo huo ulitanguliwa na burudani ya muziki iliyoongozwa na msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ aliyeingia uwanjani kwa kushuka na kamba mithili ya Komandoo.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata/Farouk Shikhalo dk60, Kibwana Shomari/Paul Godfrey ‘Boxer’ dk81, Yassin Mustafa/Adeyoum Ahmed dk67, Abdallah Shaibu ‘Ninja’/Carlos Carlinhos dk81, Bakari Mwamnyeto/Said Juma ‘Makapu’ dk67, Mukoko Tonombe/Zawadi Mauya dk54, Tuisila Kisinda/Waziri Junior dk54, Feisal Salum ‘Fei Toto’/Haruna Niyonzima dk54, Michael Sarpong/Abdulaziz Makame dk67, Ditram Nchimbi/Farid Mussa dk54 na Deus Kaseke/Juma Mahadhi dk67.

Aigle Noir; Erick Johola, Ndikumana Desire, Hitimana Hamza, Yanick Nkurunziza, Masoud Marcsse, Koffi Kouassi, Ndikumana Asman, Ngabonziza Blanchare, Christ Attegbe na Nzojibwami Frank.

CHANZO- BINZUBEIRY BLOG
Share:

MADHEHEBU YA SHIA YAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUOMBOLEZA KIFO CHA MJUKUU WA MTUME MUHAMMAD (SAAW), IMAM HUSSAIN


Sehemu ya waandamanaji wa madhehebu ya Shia wakiwa katika maandamano ya amani ya kuadhimisha mwezi mtukufu wa Muharram sambamba na kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain.
Mmoja wa viongozi wa madhebu ya Shia ambae pia ni kiongozi Mkuu wa Chuo cha Dini ya Kiislam kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam, Sheikh. Hemed Jalala akizungumza na waandishi wa habari katika maandamano ya amani ya kuadhimisha mwezi mtukufu wa Muharram sambamba na kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain
Sehemu ya waandamanaji wa madhehebu ya Shia wakiwa katika maandamano ya amani ya kuadhimisha mwezi mtukufu wa Muharram sambamba na kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain.

Dar es Salaam, Tanzania, Jumamosi 29/08/2020 – Wiki moja baada Jumuiya ya Khoja ShiaIthnasheri kupitia programu yake ya “Hussain Blood Drive” kufanikisha zoezi la uchangiaji damu kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama na Hospitali ya Ebrahim Haji, jumuiya hiyo kwa kushirikiana na madhebu yote ya Shia imefanya maandamano ya amani katika kukumbuka kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad, (SAAW), Imam Hussain. Maandamano hayo ni muendelezo wa kuadhimisha mwezi mtukufu wa Muharram sambamba na kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain.

Akizungumza katika zoezi hilo, mmoja wa viongozi wa madhebu ya Shia ambae pia ni kiongozi Mkuu wa Chuo cha Dini ya Kiislam kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam, Sheikh. Hemed Jalala alisema “Matembezi haya ya amani ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain ambae aliuawa zaidi ya miaka 1300 iliyopita huku akiamini katika uhuru na mshikamano ambao hata sisi leo tunauhitaji kwa ajili ya maendeleo na mafanikio ya nchi yetu”.

Sheikh Jalala amesema pamoja na uhuru na mshikamano, Imam Hussain aliamini katika kutunza amani na utulivu jambo ambalo Watanzania wanalihitaji sana hususan kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ili kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kubaki kuwa kisiwa cha amani na utulivu. “Lengo la kutoka kwa matembezi haya kwa ajili ya Imam Hussain (as) ni kutaka kupaza sauti kwamba amani, utulivu na upendo ni mambo muhimu ambayo yanapaswa kuenziwa na kutazamwa kwa umakini” alisema Sheikh Jalala.
Maandamano hayo yamefanyika kukumbuka siku ya Ashura ambayo ni siku ya kumi ya mwezi mtukufu wa Muharram. Zaidi ya Miaka 1300 iliopita, Katika siku hii ya Ashura mjukuu wa Mtume yaani Imam Hussain (as) aliuawa katika tambarare za mji wa Karbala, Iraq. Siku hii huadhimishwa kila mwaka, ili kutunza thamani ya mafundisho ya Imam Hussain (as) ambae alisimamia katika kuamrisha mema na kukataza mabaya. “Amr bil Marouf na Nahy anil Munkar”

Pamoja na maandamano hayo, Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri imekua ikifanya matukio yanayolenga kusaidia jamii kumuenzi mjukuu huyo wa Mtume. Mambo hayo ni pamoja na zoezi la kuchangia damu huku pia ikiratajia kufanya zoezi la kuendesha uchunguzi na upasuaji wa mtoto wa jicho kwa wenye uhitaji bila malipo yoyote.

Kwa maelezo zaidi:
Tovuti  http://www.KSIJDar.org


Share:

MSITU WA MINYUGHE ULIOPO IKUNGI MKOANI SINGIDA UPO HATARINI KUTOWEKA


Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo, viongozi wa Kata ya Mwaru pamoja na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, wakati akikagua Msitu wa Minyughe ambao umevamiwa na kufanyika uharibifu mkubwa wa mazingira.
Miti ikiwa imekatwa kwenye msitu huo.
Miti ikiwa imekatwa kwenye msitu huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo (katikati) na wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa Kata ya Mwaru wakiangalia mkaa uliotelekezwa na wavamizi katika msitu huo.Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo (katikati) akiwaonesha wajumbe wa kamati hiyo mkaa uliotaifishwa na Serikali baada ya kutelekezwa na wavamizi katika Msitu wa Minyughe wilayani humo mwishoni mwa wiki wakati akikagua msitu huo. Kulia ni Mshauri wa Jeshi la Akiba wa wilaya hiyo, Capteni Gabriel Chabimia na Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Ikungi, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Stephano Chaula.
Miti ikiwa imekatwa kwenye msitu huo.
Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Mwaru, Mohamed Mrisho (katikati) akielezea uharibifu wa msitu huo.
Ulinzi ukiimarishwa wakati wa ukaguzi wa msitu huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo (kushoto) akizungumza na mtoto Soud Seme anayeishi na wazazi wake ndani ya msitu huo.
Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Mwaru,wakimwaga mkaa uliohifadhiwa kwenye viroba na wavamizi wa msitu huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo (kushoto) na wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa Kata ya Mwaru wakiangalia mkaa uliotelekezwa na wavamizi katika msitu huo.
Mhifadhi Misitu Wilaya ya Ikungi (DFC), Wilson Pikoloti akizungumzia uharibifu wa msitu huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwaru, Mwinyimvua Midelo , akizungumzia uharibifu wa msitu huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango na Fedha wa Kijiji cha Mwaru, Shabani Nyombe akizungumzia uharibifu wa msitu huo.
Mjumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Kijiji cha Mwaru, Johari Haji, akielezea uharibifu wa msitu huo.
Safari ya ukaguzi wa msitu huo ikiendelea.

Na Dotto Mwaibale, Singida.

HALI ya Msitu wa Minyughe uliopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida imeendelea kuwa mbaya kutokana na wakazi wanaouzunguka kuuvamia kwa kukata miti hovyo na kuingiza mifugo bila ya kufuata taratibu.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo mwishoni mwa wiki ilitembelea na kujionea hali halisi na namna uvunaji wa mazao ya msitu huo ikiwemo ukataji wa miti na uchomaji wa mkaa ukifanyika bila ya kufuata utaratibu wimbi kubwa la wahamiaji kutoka mikoa ya jirani wakihusishwa na uharibifu huo.

Msitu huo wenye ukubwa wa takribani hekta 230,000 upo katika Tarafa za Sepuka, Ihanja na Ikungi na kuundwa na vijiji 26 wilayani Ikungi.

Msitu huo ulianzishwa chini ya mradi wa LAMP (Land Management Programme) ukifadhiliwa na Shirika la Sida la Uswisi mwaka 2002.

Msitu huo una uoto wa asili wa miti jamii ya miombo na maeneo kidogo ya mbuga na uoto adimu wa vichaka vya Itigi (Itigi Thickets) huku ukiwa na wanyamapori na viumbe wengine wa aina mbalimbali ambao walifanya makazi ndani ya msitu huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya, Edward Mpogolo akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo, viongozi wa Kata ya Mwaru pamoja na waandishi wa habari wakati akikagua msitu huo alisema lengo la kuuanzisha ilikuwa ni kutunza uoto wa asili na bioanuwai zilizokuwa hatarini kutoweka ikiwemo wanyamapori

Alitaja lengo lingine kuwa ni kutunza mazingira kwa ujumla na kupambana na hali ya kuenea kwa jangwa, kutunza rasilimali asili kwa kizazi kilichopo na kijacho pamoja na jamii kunufaika moja kwa moja na rasilimali misitu zilizopo.

Mpogolo alisema msitu huo ni nguzo ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi ukiungana na msitu wa mikoa ya Tabora, Rukwa na Katavi katika kuimarisha mvua zitokazo misitu ya Kongo.

"Msitu huu ni chanzo cha maji ya Ruaha Mkuu ( Internal Drainage) ukiunga pori la akiba la Rungwa, Muhesi na Kizigo lililopo Manyoni", alisema Mpogolo.

Alisema msitu huo ni kidaka maji ( Catchment Forest) kwa bonde la Wembere linaloweka uhai wa Ziwa Kitangiri na Eyasi.

Mpogolo alitoa maagizo ya kuwachukulia hatua watu wote waliovamia msitu huo kwa kujenga na kuingiza mifugo yao ambapo alitaka orodha yao ikiwa na kuondoka mara moja ndani ya msitu ndipo wafanye utaratibu wa kuomba upya kwa serikali ya kijiji.

"Haiwezekani kuingia kwenye hifadhi bila ya kufuata taratibu na kufanya uharibifu huu mkubwa, Serikali ya kijiji na kamati yangu ya ulinzi na usalama ni lazima tuhakikishe uhalibifu huu wa msitu haujirudii tena", alisema Mpogolo.

Alisema hali hiyo ikiachwa eneo hilo litakuwa jangwa na jamii inayoishi humo itapata matatizo ya maisha kwani hata madawa yatokanayo na miti ya asili hayata patikana.

Mpogolo alitumia nafasi hiyo kuwaagiza viongozi wa halmashauri ya kijiji katika eneo hilo kuitisha mkutano utakaowakutanisha wavamizi hao na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ili kujua walipateje kibali cha kuingia kwenye hifadhi hiyo kwani yamekuwepo madai ya watu kuwa kuna baadhi ya viongozi wasio waaminifu wa vijiji vinavyozunguka msitu huo kuchukua fedha au ng'ombe kutoka kwa wafugaji hao na kuwagawia ardhi katika hifadhi.

Alisema kupitia mkutano huo watawabaini viongozi waliojihusisha kwa namna moja au nyingine kutoa maeneo kwenye hifadhi hiyo nao watachukuliwa hatua za kisheria huku wavamizi hao wakifanyiwa utaratibu na halmashauri wa kutafutiwa maeneo mengine ya kuishi na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji nje ya hifadhi. 

Aidha Mpogolo alisema mvamizi atakaye kahidi hatua hizo za awali za mazungumzo na kuwasikiliza atachukuliwa hatua kali ikiwemo kuondolewa kwa nguvu ndani ya hifadhi hiyo.

Share:

Simba Bingwa Ngao Ya Hisani, Yainyuka Namungo Mabao 2:0

Klabu ya simba, leo Agosti 30 imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Namungo FC na kufanikiwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Mabao ya Simba yalifungwa na nahodha wa timu hiyo, John Bocco kwa mkwaju wa penalti dakika ya saba baada ya Bernard Morrison kuchezewa faulo ndani ya 18.

Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 59 ambapo Morrison alipachika bao la pili kipindi cha pili ndani ya 18 kwa pasi ya Clatous Chama.

Ushindi huo unaifanya Simba kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwa kushinda mbele ya Namungo FC inayonolewa na Hitimana Thiery.


Share:

WAZIRI UMMY ASHIRIKI HARAMBEE KANISA LA ANGLIKANA CHUMBAGENI TANGA,ATOA NENO KWA VIONGOZI WA DINI

 

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati alipoongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Augustino wa Hippo Chumbageni Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Canon Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga 
Canon Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga  akizungumza wakati wa harambee hiyo

MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa Katibu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mt.Augustino wa Hippo Chumbageni Tanga

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea mchango wa mtoto Nicolaus Galula wakati wa harambee hiyo
MENEJA wa Hotel ya Tanga Beach ya Jijini Tanga Joseph Ngoyo akizungumza jambo wakati wa harambee hiyo
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea mchango kutoka kwa Catherine Kitandula wakati wa harambee hiyo
Kwaya ikitumbuiza wakati wa harambee hiyo


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka viongozi wa dini kote nchini kuendelea kuliombea Taifa amani, umoja na mshikamano kuelekea uchaguzi mkuu.

Ummy aliyasema hayo leo wakati alipoongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Augustino wa Hippo Chumbageni Tanga.

 

Katika harambee hiyo walifanikiwa kukusanya fedha taslimu milioni 13.7 papo hapo na ahadi ikiwa ni milioni 47.2.huku mwisho wa kukusanya michango hiyo ikiwa ni Septemba 20 mwaka huu. 

Katika harambee hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na viongozi wa dini wakiwemo waumini huku kwaya mbalimbali zikitumbuikza

“Lakini pia tunawashukuru viongozi wa dini kwa jinsi walivyotuunga mkono kwa sala za kila siku katika mapambano dhidi ya Corona na mungu akatuepusha na janga hili hivyo niwaombe hata wakati huu nchi ikielekea kwenye uchaguzi mkuu tuendelee kuiombea nchi”Alisema Waziri Ummy

“Nimekuwa nikipata ujumbe kutoka kwa mawaziri wa nchi nyengine Afrika tumefanya kitu gani mpaka hakuna Corona nisema kwamba ugonjwa huo umetoweka kutokana na Mungu ameipenda Tanzania”.

 Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu wa Kanisa hilo Cyprian Mtweve alisema lengo la harambee ya leo katika kuadhimisha sikukuu ya Mt.Agustino wa Hippo ni kupata kiasi cha sh.milioni 125 kwa ajili ya kuezeka kanisa.

 Alisema wanaamini kiasi hicho sio kikubwa kwa Mungu cha kushindwa kupatikana huku wakimshukuru mgeni rasmi kuwaongozea zoezi la harambee hiyo na kushiriki kwa moyo na kwa ukamilifu.

 Aidha alisema upanuzi wa jengo la kanisa hilo umekuwa ukifanywa kwa kulirefusha kwa kiwango ambacho mawasiliano baina ya kasisi anayeongoza ibada madhabahuni na waumini wanaokaa viti vya mwishoni nyuma ya kanisa yanakuwa hafifu sababu ya umbali.

“Jengo hili limejengwa kwa kutumia teknologia ya zamani isiyohimili uwekwaji wa mifumo mbalimbali ya kisasa ikiwemo ile itakayoboresha ibada”Alisema

Miongoni mwa viongozi ambao wamechangia kwenye harambee hiyo ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Profesa Palamagamba Kabudi wakiwemo wakuu wa wilaya .

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger