Saturday, 27 December 2025

MAPACHA WA ARUSHA: KUTOKA MAADUI WAKUBWA HADI MARAFIKI WA DAMU


 Huu ni ushuhuda wa kweli kutoka jijini Arusha, kuhusu familia ya Mzee Abdulah na mkewe. Maisha yao yalianza kwa furaha tele walipowapata watoto wao mapacha, Baraka na Faraji. Tangu utotoni, walikuwa kama pete na kidole; walivaa sare, walisoma shule moja, na hata mmoja akiumwa, basi mwingine naye aliishiwa nguvu.

Matatizo yalianza baada ya kumaliza elimu ya msingi. Baraka alichaguliwa kujiunga na shule ya kutwa ya kawaida, huku Faraji akifanikiwa kwenda Shule ya Kitaifa (National School). Tangu siku hiyo, ule uzi uliowaunganisha ulikatika. Chuki ilitanda, dharau ikaingia, na mapacha hawa wakawa kama paka na panya. Nyumba ya Mzee Abdulah ilijaa huzuni na simanzi.Baada ya jitihada za kifamilia kushindikana, Mzee Abdulah alimshirikisha rafiki yake wa karibu ambaye alimuelekeza kwa mtaalamu mashuhuri, Dr. Magongo. Ingawa Mzee Abdulah alikuwa na kusitasita awali, upendo kwa wanawe ulimfanya apige hatua hiyo ya kishujaa kutafuta suluhu kwa Dr. Magongo.

Dr. Magongo alimpokea Mzee Abdulah kwa ukarimu na busara. Hakutumia nguvu, bali alitumia tiba asilia na maarifa ya kale ya kurekebisha mahusiano yaliyovunjika:
• Dawa ya ‘Muungano wa Damu’: Dr. Magongo alimpa Mzee Abdulah dawa ya asili ya kupaka na kunyunyizia kwenye nguo za vijana hao, iliyolenga kuamsha ile hali yao ya asili ya kuzaliwa pamoja.
• Maelekezo ya Kiroho: Dr. Magongo alifanya tambiko maalumu la kuondoa roho ya husuda na mashindano iliyoingia kati ya Baraka na Faraji baada ya kutengana shule.
• Maneno ya Busara: Alimshauri Mzee Abdulah jinsi ya kuzungumza nao kwa namna ambayo haitaonyesha upendeleo kwa mmoja.

Baada ya Mzee Abdulah kufuata maelekezo yote ya Dr. Magongo, anga la nyumba yake lilianza kubadilika. Siku ya kwanza ya kukutana kwao ilikuwa ya kipekee na haitasahaulika.Baraka alikuwa ameketi nje, kwenye kile kiti cha mbao ambacho mapacha hao walipenda kukaa zamani kabla ya chuki kuingia. Faraji alitoka ndani, na badala ya kupita kwa dharau kama ilivyokuwa desturi yake, alisimama ghafla na kumtazama ndugu yake. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, macho yao hayakujawa na hasira, bali yalijawa na shauku na majonzi ya kupotezana.

Faraji alikuwa wa kwanza kuvunja ukimya. Alimsogelea Baraka na kumuwekea mkono begani, ishara ambayo ilimfanya Mzee Abdulah, aliyekuwa akichungulia dirishani, kutokwa na machozi ya furaha.”Ndugu yangu Baraka, nimekukumbuka. Shule na madaraja vilitutenganisha, lakini damu yetu ni moja.”Fariji alisema (Akisimama na kumkumbatia ndugu yake kwa nguvu) Baraka alinena na kusema “Nilidhani umenisahau kwa sababu ya mafanikio yako, lakini moyo wangu ulikuwa unakuita kila siku.”

Walikaa hapo kwa saa kadhaa, wakisimuliana mambo ya shuleni na kucheka kama walivyofanya walipokuwa watoto wadogo. Ile hali ya mmoja kuhisi maumivu ya mwingine ilirejea papo hapo; Baraka alipokuwa akisimulia changamoto za shule yake, Faraji aliahidi kumsaidia kwa vifaa na maarifa aliyopata kwenye shule ya kitaifa.Tangu siku hiyo, ile kuta ya chuki ilibomoka kabisa.

Dr. Magongo hakurudisha tu maelewano, bali alirudisha roho ya pacha mmoja ndani ya miili miwili. Leo hii, Arusha nzima inawajua Baraka na Faraji kama mfano wa kuigwa wa upendo wa ndugu. Mzee Abdulah sasa anatembea kifua mbele, akijua kuwa familia yake imepona na itabaki imara milele.Mzee Abdulah sasa anaishi kwa amani, akimshukuru Dr. Magongo kwa kuirudisha furaha iliyokuwa imepotea nyumbani kwake. Wasiliana na Dr. MAGONGO Leo.Usikubali kutaabika na matatizo kama haya. Dr. MAGONGO yuko hapa kukusaidia popote ulipo.
• Simu (Kenya): +254 720899984
• Simu (Tanzania): +255 740700621
• Barua Pepe: info@magongodoctors.com

Share:

Friday, 26 December 2025

DKT HOMERA AKABIDHI MABOMBA YA SHILINGI MILIONI 30 KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA MAJI NAMTUMBO

Mwalimu Saidi Homera akikabidhi mabomba kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Dkt Juma Zuberi Homera na Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania 

Na Mwandishi Wetu Malunde 1-Blog 

Mbunge wa Jimbo la Namtumbo ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, amekabidhi mabomba yenye thamani ya shilingi milioni 30 kama hatua za dharura za kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji katika jimbo hilo. 

Msaada huo umetolewa kabla ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji ya Serikali, ukiwa na lengo la kupunguza kero ya maji kwa wananchi wa Namtumbo.

Akikabidhi mabomba hayo kwa niaba ya Mbunge,  Mwalimu Saidi Homera amesema msaada huo umetokana na juhudi binafsi za Dkt. Homera, kama sehemu ya dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama. 

Ameeleza kuwa hatua hiyo inaonesha uwajibikaji na ukaribu wa mbunge kwa wananchi wake.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo, David Mkondya, amesema mabomba hayo yatatumika kukamilisha uchimbaji wa visima 10 katika vijiji 10. 

Baada ya uchimbaji, visima hivyo vitawekewa mifumo ya pampu za umeme na matenki ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita 20,000 hadi 50,000 kulingana na idadi ya watu, hatua itakayoongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 74 hadi kufikia asilimia 76.

 Baadhi ya wakazi wa Namtumbo, akiwemo Diwani wa Kata ya Namtumbo Rajab Uhonde, wamempongeza na kumshukuru Dkt. Juma Homera kwa jitihada zake za kutatua changamoto za wananchi. 

Wamesema msaada huo unaonesha mbunge yupo karibu na wananchi na anashughulikia kero zao, huku wakimpongeza pia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za Serikali katika ujenzi wa miradi mikubwa ya maji katika mji wa Namtumbo.



Share:

DC NKINDA AKUTANA NA VIJANA KAHAMA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA XMAS, ASIKILIZA KERO NA KUWAHIMIZA KULINDA AMANI

 



Na Neema Nkumbi, Kahama



MKUU wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda, amekutana na makundi mbalimbali ya vijana wilayani humo katika hafla ya pamoja ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi, iliyolenga kuimarisha mshikamano kwa kula chakula cha pamoja sambamba na kusikiliza changamoto zinazowakabili vijana wa Kahama.

Akizungumza katika mkutano huo, Mchungaji wa Kanisa la Kalvari Lango la Ushindi, Mchungaji Flora Mwanri, amempongeza Mhe. Nkinda pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya Glory Absalum kwa hatua ya kuwakutanisha wananchi wa Kahama bila kujali dini au itikadi za kisiasa kwani tukio hilo limeonesha mfano wa uongozi unaojali umoja na mshikamano wa jamii, akibainisha kuwa kiongozi huyo amewaunganisha wananchi wote kwa pamoja.

Kwa upande wake, kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wilayani Kahama, Abas Omari, amewasilisha kero kadhaa ikiwemo ombi la kuwekwa taa za barabarani katika eneo la Shunu ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kibiashara nyakati za usiku, Pia ameeleza changamoto ya barabara ya kuelekea makaburini ya Shunu ambayo huwa haipitiki wakati wa mvua kutokana na tope, hali inayowalazimu baadhi ya wananchi, wakiwemo waliovaa kanzu, kuzikunja ili kupita.

Aidha, ameeleza kuwa barabara ya eneo la Msikiti wa Shunu Lugela imekatika kabisa, jambo linalowalazimu watoto wanaotoka upande wa pili kuzunguka milimani kufika Shule ya Msingi Shunu.

Akitoa nasaha zake, Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kahama (OCD), Mtaju, amewataka wananchi na vijana kutokuwa na hofu ya kufikisha changamoto zao polisi wakati wowote amesema ofisi yake iko wazi muda wote na endapo changamoto itahitaji utatuzi wa ngazi za juu, atalifikisha kwa mamlaka husika.

Pia, amewahimiza vijana kutumia hekima katika kutatua changamoto, akisisitiza kuwa vijana ni nguvu kazi na tegemeo la taifa, hivyo wanapaswa kuepuka kujihusisha na shughuli zisizo halali zinazoweza kukatiza ndoto zao.

Akijibu hoja na kero zilizowasilishwa, Mhe. Nkinda amesema kuhusu barabara ya makaburini Shunu, amemtaka aliyetoa changamoto hiyo kufika ofisini kwake kufikia Jumatatu ili yeye na timu ya wataalamu wa wilaya waende eneo husika kujionea ukubwa wa tatizo na kulifanyia kazi kwa haraka.

Kutokana na vijana wengi kuwa na changamoto amesema wataandaa kongamano maalum la vijana, litakalowapa fursa ya kuwasilisha changamoto zao kwa kina ili zipatiwe ufumbuzi.

Mhe. Nkinda amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ina utaratibu wa kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi, iwe ni kwa makundi au mtu mmoja mmoja, akibainisha kuwa milango ya ofisi yake iko wazi kwa wananchi wote.

Katika hitimisho lake, Mkuu wa Wilaya aliwataka vijana wa Kahama kuendelea kuwa watulivu, kulinda amani na mshikamano, akisisitiza kuwa uongozi wa wilaya uko pamoja nao katika kuhakikisha maendeleo na ustawi wa wananchi wa Kahama yanaendelea kupatikana.

 
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 26,2025

Magazeti








Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger