Sunday, 17 November 2024

WANANCHI KATA YA KILIMANI WATAKIWA KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA




Na Dotto Kwilasa,Dodoma,Nov,17, 2024.

Mjumbe wa kamati ya siasa kata ya kilimani wilayani Dodoma amewataka wanachama wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani na mitaa yote minne kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wa kata ya kilimani kujitokeza kwa wengi ifikapo November 27 mwaka ili kuhakikisha wanatumia haki yao ya kikatiba kushiriki zoezi la kupiga kura kwa viongozi wao wa mitaa yote minne ya kata ya kilimani

Mjumbe huyo wa kamati ya siasa Comredi Barnabas kisengi ameyasema hayo wakati akizungimza na kituohichi kuelekea kuanza kwa kampeni ya vyama vya siasa kabla ya kufikia November 27 mwaka siku ya Uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa.

"Tunakumbushana sisi kama wanachama wa chama cha Mapinduzi kuwa ifikapo November 20 hadi 26 vyama vyote tutakuwa kwenye mchakato wa kampeni za kuwanadi wagombea wetu waliteuliwa kuwania nafasi za Viongozi wa serikali za mitaa kwa nafasi ya wenyeviti na wajumbe wao watano katika mitaa yatu minne ya kilimani, Nyerere, chinyoyo na Image iliyopo katkika kata ya kilimani Jijini Dodoma '

Comredi Kisengi amesema kama wanachama wa CCM wakishikana kwa pamoja na kuhakikisha wanawanadi wagombea wao vizuri katika kampeni kueleza utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi katika miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika mitaa yote minne kwa kipindi cha mwaka 2019 hadi 2024 hakika ilani ya CCM imetekelezeka kwa asilimia kubwa.

"Tunapaswa kuyasema yote mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi na kwa yaliyobaki basi wananchi watupe ridhaa yao tuweze kuyamalizia kwa kipindi hichi cha miaka mitano ijayo yani 2025 hadi 2030"amesema Comredi Kisengi

Aidha Comredi Kisengi amewataka wanacha kuhakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu ambazo zitaleta tija ya ushindi wa kishindo kwa viongozi wao November 27 mwaka huu.

Amewasisitiza wanachama kuhakikisha wanajitokeza kuwahamasisha wanachi na wakereketwa wote waliojiandikisha kwenye daftari la makazi katika mitaa yao yote minne wajitokeze kwa wingi siku ya November 27 mwaka huu kupiga kura kwa kuwachagua Viongozi wetu wanapitia kutokana na chama cha Mapinduzi.

Aidha Comredi Kisengi amesema kuto kujitokeza kwenda kupiga kura ni kujikoseshea haki yako ya Msingi kumpata kiongozi wa mtaa wako hivyo wanachama na wananchi hakikisheni mnajitokeza siku hiyo ili uweze kumchagua kiongozi bora umtakaye atakayekusimamia maendeleo ya mtaa wako.




Share:

SERIKALI YASISISITIZA HAKUNA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU MGODI WA NORTH MARA

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesisitiza kwamba hali ya usalama na haki za binadamu katika sekta ya madini hususani katika mgodi wa North Mara hapa nchini ni shwari na hiyo iimethibitiswa na ripoti iliyotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania (THBUB) hivi karibuni kuhusu hali ya usalama na haki za binadamu kwenye mgodi huo unaomilikwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya DW ,Waziri Mavunde, alisema Tanzania ina vyombo vyake vya ufuatiliaji wa utekelezaji wa haki za binadamu hapa nchini na Tume ipo kisheria pamoja kwamba katiba na sheria zetu zinaruhusu kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ndani na nje ya nchini kufanya utafiti na kutoa ripoti zao kwa uwazi.

Alipoulizwa kuhusu taarifa iliyotolewa hivi karibuni na shirika lisilo la kiserikali la nchini Canada (Canada Mining Watch) kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za Binadamu wakati wa upanuzi wa shughuli za mgodi katika vijiji vya Komolela na Kewacha katika wilaya ya Tarime kata ya Nyamongo ,alisema Serikali tayari ilishayafanyia kazi kupitia vyombo vyake na kubaini ukweli juu ya suala hilo kama ambavyo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania (CHRAGG) ilifanya uchunguzi wa kina dhidi ya tuhuma hizo na kutoa ripoti yake.

"Bahati nzuri Tanzania hatuishi kisiwani na sisi tuna vyombo vya kuangalia , kufuatilia na kuzingatia haki za binadamu na vyombo vyetu vimekuwa mstari wa mbele kwa jambo lolote kama linakwenda kinyume hatua zitachukuliwa kikamilifu", alisema Waziri Mavunde.
Aliendelea kusisitiza “Hoja kubwa za wananchi wanazouliza wanaozunguka maeneo ya migodi ni jinsi ya kupata maeneo ya kuchimba, kushiriki kwenye uchumi , huduma za kijamii na uwajibikaji wa wamiliki wa migodi kwa wananchi wa maeneo husika.

“ Hizo ndio hoja kubwa ambazo mimi mwenyewe nimezisikia masikio mwangu nilipoenda na kuzungumza na wananchi wa maeneo husika haya unayoniuliza sio hoja za wananchi,” alisema Mavunde.

Mnayoniuliza sio malalamiko ya wananchi mie mwenyewe nimekwenda na kufanya mikutano na wananchi wa maeneo hayo ni kilio chao zaidi ni ajira , kupata maeneo ya kuchimba na uwajibikaji wa wamiliki wa migodi kwa wananchi wanaozunguka migodi husika hicho ndio takwa la wanakijiji,” alisisitiza Waziri Mavunde.

Alisema katika juhudi za kuendelea kuvutia uwekezaji hapa nchini na kutoa ufafanuzi wa taasisi za nje ambazo zimekuwa zikitoa taarifa potovu za kufifisha uwekezaji nchini,Serikali itaendelea kushiriki katika mikutano ya kimataifa na kikanda na kuhakikisha kwamba taarifa zote zinatokana katika vyombo rasmi vya Serikali na Jeshi la Polisi litaendelea kutoa taarifa sahihi mara kwa mara ili kuondoa huu upotoshaji unaondelea ili kuendelea kuvutia wawekezaji kwenye sekta ya madini hapa nchini.

Awali akizungumza hali katika sekta ya madini alisema sekta hiyo inaendelea kukua siku hadi siku kwa kuongeza ajira, tozo , kodi ya serikali na pato la taifa na katika pato la taifa sekta hiyo inachangia asilimia 9.0 na 2021 na 2022 ilichangia asilimia 7.2 la pato la taifa.

“Sekta hii ya madini itaendelea kutegemewa hapa nchini katika kupunguza tatizo la ajira na kuchangia pato la taifa kwa maendeleo ya nchini yetu,” alisisitiza.

Aliongeza kwamba mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2017 , kwenye maudhui ya ndani (Local content) uwajibikaji kwa jamii (Corporate Social Responsibility- CSR) imechangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo ya wananchi kupitia sekta husika.

“Hapo awali wenye leseni ya uchimbaji wa madini wao ndio walikuwa wanaamua kwamba mradi huu tusaidie kuchimba na kujenga matundu ya vyoo au zahanati ila baada ya mabadiliko ya sheria , mradi unaanza kuibuliwa kutoka kwa wananchi wenyewe ngazi ya kitongoji , kata mpaka juu ndio wananchi wanaamua nini wafanyiwe na wenye leseni ya uchimbaji wa madini,” alisisitiza .

Hivi karibuni Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania (THBUB) kupitia Mwenyekiti wake (Jaji Mstaafu) Mathew Mwaimu ilitoa taarifa baada ya uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu katika mgodi wa North Mara zilizotolewa na taasisi ya Canada Mining Watch na kubainisha kuwa taratibu za kisheria na taratibu za nchi zilifuatwa na ulifanyika kwa uwazi na ushirikishwaji wakati wa mgodi huo kupanua shughuli zake za uchimbaji katika vijiji tajwa vya Komarera na Kewanja

Mgodi wa North Mara unamikiwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga.
Share:

LEMA : VURUGU ZILIZOJITOKEZA ZILICHOCHEWA NA BENSON KIGAILA


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amedai vurugu zilizojitokeza juzi wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa chama Mkoa wa Arusha zilichochewa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Benson Kigaila.

Lema ameyabainisha hayo leo Novemba 16,2024 wakati akizungumza na wanahabari jijini Arusha.


"Hii ilikuwa ni organised crime kati ya watu wa CHADEMA na ndiyo maana na ninyi waandishi wa habari mlipatikana.Cha kusikitisha zaidi na hii ninaogopa kusema kwa sababu ninalisema, lakini ninaumia sana.


"Cha kusikitisha zaidi yale mambo mimi nilimuomba Naibu Katibu Mkuu Bara ateremke,Bw.Benson Kigaila...ateremke na nilimuomba ateremke awazuie wale wafanya fujo kwa sababu mmoja wa wafanya fujo ni rafiki yake mkubwa.


"Ambaye siku chache zilizopita alifanya fujo Monduli, mmoja wa wafanya fujo na alipofanya fujo Monduli mpaka uchaguzi wakamtukana msimamizi.


"Halafu wakati wakifanya fujo Monduli, mimi nilishuhudia kwamba, msimamizi alinipigia simu, nikamwabia afadhali hapa nipo na msimamizi wa uchaguzi Bw.Benson Kigaila unaweza ukaongea naye akasema hawa wanataka kunipiga.


"Wamepora na matokeo ya mabaraza,sasa sijui waliongea nini, lakini alisema kama uchaguzi wa wilaya haujatimia funga, halafu watu wa hamasa wakuondoe hapo muondoke.


"Kesho yake, mimi nikiwa na Benson Kigaila mmoja wa wafanya fujo akampigia simu, akaongea nae kama dakika 20.


"Niko na Benson, Moshi nikamwambia Benson, Naibu Katibu Mkuu Bara hawa watu wamefanya fujo, wamedhalilisha watu.


"Unapowapa audience ya kuongea nao na unapokuwa submissive kwao, alikuwa akiongea naye yeye akionekana kuwa mnyenyekevu kwao.


"Unatunyima sisi wengine mamlaka ya kichama, nikamwambia hii sio sawa sawa.


"Nikamwambia the ways unavyoongea na huyu Bwana hauongei sawa ni rafiki yake sana, Boni ni rafiki yake sana Benson Kigaila.


"Benson Kigaila akija hapa, anafikia kwa Boni na wakati mwingine wanatembea kwa pamoja, wanakula pamoja.


"Ni marafiki wa karibu sana,sasa nilipoona fujo zimechangamka na polisi wanataka kupanda ukumbini, mimi nilimuomba Naibu Katibu Mkuu ashuke chini, Naibu Katibu Mkuu ashuke chini amwambie rafiki yake asilete fujo.


"Naibu Katibu Mkuu...mtu wa kwanza, wa pili wa tatu baadaye nikatuma mtu mwingine nikasema kama hawezi kushuka nikamtuma Katibu wa Kanda, lakini ninaomba Naibu Katibu Mkuu ashuke chini.


"Baadaye alishuka, Naibu Katibu Mkuu alikuwa mgumu kuwafuata, nilimwambia wale ni rafiki zako, wafuate sisi hatuna mamlaka nao kwa sababu wewe una-communicate nao frequently.


"Mimi sina mamlaka, nimeshawaambia waondoke hapa, hawaondoki. Alitoa maelekezo ambayo kama yale maelekezo yangezingatiwa lazima ule uchaguzi ulikuwa unaharibika na polisi wangepanda juu kuondoa watu wote pale.


"Mimi niliwaambia vijana wetu wa hamasa...tumieni akili, watoeni pembeni bila kufanya jambo lolote lile.


"Naibu alirudi juu, aliporudi juu mimi niliendelea kuwasii polisi pale chini, nikawaambia tafadhali uchaguzi hauna muda mrefu sasa.Unaisha muda sio mrefu.


"Conclusion yangu ni nini? Huyu mmoja ambaye alikuwa anatukana sana ni rafiki sana na Naibu Katibu Mkuu Bara.


"Ni rafiki sana na Naibu Katibu Mkuu Bara, huyu aliyekuwa anatukana sana, lakini kinachonishangaza sana ni kwamba hata yule wa Ngorongoro aliyekuwa anatukana akisema kwamba... mimi nimekata majina yao.


"Sasa, hili jambo nitalisema kwamba mimi kwenye usaili huu maamuzi yoyote yakifanyika yanafanyika with collective responsibility.


"Lakini, mtu aliyeleta taarifa za Kuyaa, za tabia zake mbaya huko Ngorongoro, mbaya sana ni Naibu Katibu Mkuu Bara na akashawishi wajumbe kwamba huyu mtu hana sifa za kuwa kiongozi,"amedai Lema.


Hata hivyo, Lema amedai tayari ameagiza wote waliofanya fujo wachukuliwe hatua.


"Lakini, msimamo wa kwanza nimeagiza viongozi wa chama kanda mahali popote, kwa yeyote aliyehusika kwa sababu wako waliotoka Mkoa wa Kilimanjaro walikuja kufanya fujo Arusha.


"Kwamba taarifa ziende na wameziona hawa wanachama waliofanya huo upumbavu wa kiwango kile na kusababisha taharuki kubwa na udhalilishaji kwa chama chetu.


"Wachukuliwe hatua mara moja za kuvuliwa uanachama katika matawi yao mara moja na haraka iwezekanavyo,kwa sababu wamekidhalilisha chama sana,"ameongeza Lema.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 17,2024


magazeti ya leo
 


Share:

Saturday, 16 November 2024

Video Mpya : NG'WANA TELI - MAISHA

Share:

GHOROFA LAPOROMOKA KARIAKOO, UOKOAJI UNAENDELEA


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mpaka Sasa limefanikiwa kuwaokoa watu nane ambao walikwama kwenye jengo lililoanguka Kariakoo na tayari wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Zoezi la uokoaji linaendelea kwa kuwakwamua watu ambao wamekwama katika ghorofa ya chini.

Share:

Friday, 15 November 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 16,2024




Share:

MPENZI WANGU KAMPONYA BIBI YANGU UGONJWA WA KISUKARI


Unajua kutokana na mtindo wa maisha kwa dunia ya sasa ulioletwa na mageuzi ya viwanda, watu wengi wamekuwa wakikumbwa na magonjwa mbalimbali kama kisukari ingawa kuna wengine huwa wanarithi ugonjwa huo.

Jina langu ni Emmy, ni binti wa miaka 22, ninaishi na Bibi yangu Kakamega, Kenya, mwanzoni mwa mwaka 2019 Bibi yangu alianza kuumwa, sikuweza kujua ni kitu gani hasa kinamsumbua Mzee huyo ambaye nilikuwa namtunza.

Nilimpeka hospitali ambayo ipo eneno la jirani, baada ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi wa kina, Bibi akagundulika kuwa ana ugonjwa kisukari, binafsi mwenyewe sikuweza kutarajia ugonjwa huo!.

Pale hospitali tulipewa dawa na Bibi akaanza kuzitumia, nilikuwa na matumaini mengi kuwa siku sio nyingi ataanza kupata nafuhu, huku mimi nikiendelea na kazi zangu za kila siku za kuniingizia kipato ambacho kitaniwezesha kuendesha familia hii.

Hata hivyo, Bibi hakuweza kupata nafuhu au kupona kwa muda ambao nilidhani ambao ndio alikuwa anamalizia dawa zake, tuliamua kwenda Hospitali nyingine ya kisasa zaidi kupata huduma ya kukabiliana na maradhi hayo.

Huko nako alipewa aina tofauti ya dawa  ambazo mwanzo zilionekana kufanya kazi na kuwa na mategemeo kuwa siku za usoni atapona kabisa na kurejea katika hali yake ya kawaida ambayo tulimzoea nayo siku zote.

Siku zilienda Bibi akiendelea kuumwa, baadhi ya watu ambao niliwaeleza kuhusu kuumwa kwa Bibi yangu, walinishauri nijaribu kutafuta dawa za mitishamba ambazo zimekuwa zikiwasaidia watu wengi.

Huu ni ushauri ambao mpenzi wangu James alinipa, licha ya wasiwasi wangu kuhusu tiba asilia, aliendelea kunisisitiza kuchukua hatua hiyo, kutokana nilikuwa namwamini kwa jinsi ambavyo amekuwa akifanya mambo yake, nilikubali wazo lake.

"Unajua Emmy hili jambo ambalo nimekuambia nina uhakika nalo kwa asilimia 100, watu wengi wamepona kupitia tiba zake," aliniambia James.

Basi nikachuka namba ya Dr Bokko ndipo nikawasiliana naye na kumueleza shida hiyo ya Bibi yangu na yeye mara moja aliweza kunitumia dawa ambazo zimeleta tabasamu usoni kwake.

Katika mazungumzo yetu mafupi, Dr Bokko aliniambia pia anatibu magonjwa sugu kama presha, kisonono na kaswende, anatatua shida kama kumrudisha mpenzi aliyekuacha, kupata mum au mke wa ndoto zako n.k. Mpigie kwa namba +255618536050.

Mwisho.


Share:

TAKUKURU SHINYANGA YABAINI UFISADI UKARABATI WA BARABARA KISHAPU, VIGOGO WATATU MATATANI


Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 13,2024 -Picha na Kadama Malunde
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 13,2024

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imefanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa watatu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mamlaka, kuisababishia serikali hasara, na kughushi nyaraka katika mradi wa ukarabati wa barabara ya Isoso – Mwabusiga, wilaya ya Kishapu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 13,2024 Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja, ameeleza kuwa changamoto kubwa katika miradi ya barabara, hasa ile inayotekelezwa na wakandarasi, ni kutotekelezwa kwa viwango vinavyohitajika. Hii husababisha barabara kuharibika haraka baada ya matengenezo.

“Katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2024, TAKUKURU ilifuatilia mradi wa ukarabati wa barabara za Isoso – Mwabusiga, Kishapu – Mwakipoya, na Gimagi – Magalata, miradi ambayo ilikuwa inafanywa na Kampuni ya Advance Construction Ltd chini ya usimamizi wa TARURA Wilaya ya Kishapu,” amesema Masanja.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi 206,214,500/=, ulijumuisha kipande cha barabara cha urefu wa kilometa 3 kutoka Isoso hadi Mwabusiga.

Amesema katika ufuatiliaji wa mradi, TAKUKURU iligundua kwamba mkandarasi alikosa kufanya baadhi ya kazi muhimu, ikiwa ni pamoja na ushindiliaji (compaction) wa kifusi cha barabara, jambo ambalo lilileta mapungufu katika ubora wa barabara hiyo.

Hata hivyo, ameeleza kuwa, licha ya mkandarasi kulipwa kiasi cha fedha kilichokubalika katika mkataba, maelekezo ya TAKUKURU kwa meneja wa TARURA wilaya ya Kishapu ya kumsimamia mkandarasi kutekeleza marekebisho hayakutekelezwa.

“Tulielekeza meneja wa TARURA kuhakikisha mkandarasi anarekebisha mapungufu hayo, lakini maelekezo hayo hayakufanyiwa kazi. Hali hii ilitusababishia kuanzisha uchunguzi wa kina, ambapo tulibaini kuwa mkandarasi alilipwa kiasi cha shilingi 29,100,000/= bila kufanya kazi inayohitajika,” amesema Masanja.

"Uchunguzi wa TAKUKURU ulifunua pia kughushiwa kwa nyaraka za matokeo ya vipimo vya ubora wa ushindiliaji, ambapo nyaraka hizo zilikuwa zimeandaliwa na mhandisi wa mafunzo (Trainee Engineer) wa TANROADS Shinyanga, ambaye hakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo",ameongeza Mwamba.

Amebainisha kuwa, baada ya uchunguzi, watuhumiwa watatu walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mamlaka, kuisababishia serikali hasara, na kughushi nyaraka. Watuhumiwa hao ni Mhandisi Juma Mkela, Msimamizi Mkuu wa Kampuni ya Advance Construction Ltd, Charles Emmanuel, Mhandisi wa Mafunzo wa TANROADS Shinyanga, na Mhandisi Wilfred Gutta, Meneja wa TARURA Wilaya ya Kishapu.

"Katika kesi hiyo, washtakiwa walikiri makossa yao na kutiwa hatiani. Mahakama ilitoa adhabu ya faini ya shilingi 500,000/= kwa kila kosa na kuamuru watuhumiwa kurejesha serikalini kiasi chote cha shilingi 29,100,000/= walicholipwa mkandarasi isivyo halali.

Watuhumiwa wote walilipa faini ya jumla ya shilingi 2,500,000/= na wamefanikiwa kurejesha shilingi 10,000,000/= kati ya shilingi 29,100,000/= wanazopaswa kurejesha. Aidha, washtakiwa wanaendelea na urejeshaji wa kiasi kilichobaki cha shilingi 19,100,000/= kama ilivyoamriwa na mahakama",amesema.

TAKUKURU inasisitiza kuwa itaendelea kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha matumizi bora ya fedha za umma na kuzuia vitendo vya rushwa na udanganyifu katika utekelezaji wa miradi ya serikali.
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 13,2024 . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 13,2024
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 13,2024

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Thursday, 14 November 2024

Video Mpya : MASHILI GIDEKA - DUNIA

 

Share:

BENKI KUU YA TANZANIA YAENDESHA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA

 


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog                                         

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeendesha semina kwa waandishi wa habari kutoka Kanda ya Ziwa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuelimisha umma kuhusu majukumu ya benki hiyo na masuala ya kifedha muhimu kwa taifa.

Semina hiyo ya siku mbili inafanyika katika Ukumbi wa BOT Tawi la Mwanza, na inahusisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Simiyu, Mara na Geita.

Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo,ameeleza kuwa, mafunzo hayo yatagusia masuala muhimu kama vile muundo na majukumu ya Benki Kuu, maana ya sera ya fedha inayotumia riba ya Benki Kuu, umuhimu wa dhahabu kama sehemu ya akiba ya fedha za kigeni, na utekelezaji wa sheria na kanuni zinazohusu huduma ndogo za fedha.

Aidha, Mwaikambo amesema mada nyingine itahusu ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kuondoa noti za zamani kutoka mzunguko, alama za usalama wa fedha na utunzaji wake, pamoja na mtazamo wa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania.

Semina hii inatoa fursa kwa waandishi wa habari kuwa na uelewa wa kina kuhusu masuala ya kifedha na sera za Benki Kuu, ili waweze kutoa taarifa sahihi na za kitaalamu kwa umma, hivyo kusaidia kuongeza ufanisi katika ushirikiano kati ya vyombo vya habari na taasisi za kifedha.

Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa leo Jumatano Novemba 14,2024 katika ukumbi wa BOT Tawi la Mwanza - Picha na Kadama Malunde

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger