Thursday, 29 May 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 29,2025





Magazeti
Share:

Wednesday, 28 May 2025

DIWANI AWAWASHIA MOTO WANAOMKASHIFU NA KUMTUKANA RAIS SAMIA,

 Na Woinde Shizza ,moshi

Diwani wa kata ya Boma Mbuzi Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Juma Rahibu, amewajia juu baadhi ya Watanzania wanaomkashifu na kumtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisema ni ishara ya kuporomoka kwa maadili katika jamii na kudhalilisha heshima ya taifa.

Akizungumza kwa hisia kali katika sherehe za uzinduzi wa kikundi cha mtetezi wa mama , Rahibu alisema ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya watu wakitumia majukwaa ya mitandao ya kijamii na mikusanyiko ya watu kumvunjia heshima kiongozi mkuu wa nchi ambaye, kwa mujibu wake, amekuwa akitekeleza majukumu yake kwa bidii na mafanikio makubwa.

“Huu si ustaarabu Rais Samia anajitahidi kutuletea maendeleo kama barabara, afya, elimu halafu mtu anajitokeza tu na kuanza kumtukana? Tunataka vyombo vya dola viwajibike,” alisema Rahibu.

Diwani huyo alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuenzi maadili ya taifa, hasa heshima kwa viongozi walioko madarakani, huku akionya kuwa uhuru wa kutoa maoni haupaswi kuwa kisingizio cha matusi, kashfa na propaganda zisizojengwa kwenye hoja za msingi.



Katika hatua nyingine, Rahibu alielekeza lawama kwa baadhi ya raia kutoka mataifa jirani ya Kenya na Uganda kwa kile alichokieleza kuwa ni tabia ya kudhalilisha na kumsema vibaya Rais Samia kwenye mitandao ya kijamii.


“Sasa imefika hatua hata baadhi ya Wakenya na Waganda wanathubutu kumtukana Rais wetu? Hii ni dharau ya hali ya juu ,Tanzania si uwanja wa mazoezi wa siasa za kejeli,” alisema kwa msisitizo.


Alisema Tanzania imekuwa nchi ya mfano wa heshima na ustaarabu kwa viongozi wa mataifa jirani, hivyo si haki kuona baadhi ya watu kutoka nje ya nchi wakitumia vibaya uhuru wa mitandao kwa maneno ya matusi dhidi ya kiongozi wa Tanzania.


“Tunawaheshimu viongozi wao, hatujawahi kusikia Watanzania wakimtukana Rais wa Kenya au wa Uganda ,Na wao wajifunze kutufanyia heshima hiyo hiyo,” aliongeza.



Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wakazi wa Moshi wameonyesha kuguswa na kauli hiyo, wakisema kuwa ni kweli kuwa maadili yanaporomoka na watu kutumia mitandao ya kijamii vibaya.


Esther Kilave, mkazi wa Pasua, alisema:


“Mitandao inatumika kama sehemu ya matusi sasa huu si utamaduni wetu ,Rais Samia anastahili kuheshimiwa kwa kazi anayoifanya.”


John Mlay, fundi umeme mjini Moshi, alisema:


“Tunaona mabadiliko mengi nchini Watu wanapaswa kutoa hoja za maana, si kejeli na matusi na niseme Wanapotukana Rais, wanatudhalilisha sisi sote. Acheni siasa za matusi.”


Rais Samia ameendelea kupokea pongezi kutoka kwa wananchi wa makundi mbalimbali nchini, kufuatia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na msimamo wake wa kudumisha amani, umoja wa kitaifa na usawa wa kijinsia.


Share:

JUMUIYA YA WANADIPLOMASIA YAKARIBISHWA NCHINI



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Jumuiya ya wanadiplomasia nchini imetakiwa kufikisha taarifa katika Serikali za nchi zao kuwa Dodoma ipo tayari na kwamba Serikali hizo zinatakiwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya ofisi na makazi ya balozi kwenye viwanja vilivyotolewa bure kwenye mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) kwenye Mkutano maalum wa Jumuiya ya Wanadiplomasia nchini uliondaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kufanyika jijini Dodoma Mei 27, 2025.

Waziri Kombo aliwaeleza Mabalozi hao kuwa siri kubwa ya mafanikio yoyote duniani ni kuwa na imani na jambo unalolidhamiria kulitekeleza. Serikali ya Tanzania tangu ilipofanya uamuzi wa kuhamishia makao makuu ya nchi jijini Dodoma mwaka 1973 ilikuwa na imani na uamuzi huo na leo imani hiyo inatekelezwa kivitendo kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika maeneo ya miundombinu na huduma za kijamii ili kuuweka mji wa Dodoma katika mazingira mazuri ya kuishi, kwa watu wa aina yote, wakiwemo Mabalozi.

Balozi Kombo alisema kutokana na ujenzi wa mji wa Dodoma, fursa nyingi za uwekezaji zimeibuliwa, hivyo ametoa wito kwa Mabalozi kuwaleta wawekezaji jijini Dodoma kuchangamkia fursa hizo. Ametoa wito pia kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoa taarifa ya kila hatua ya ujenzi wa mji huo kwa wadau kwa lengo la kuwahamasisha kufanya uamuzi sahihi kuhusu Dodoma. Alisema mkutano huo ni jukwaa muhimu la kupeana taarifa kuhusu maendeleo ya mkoa wa Dodoma na kupendekeza uwe unafanyika kila mwaka.

Mwenyeji wa Mkutano huo uliobeba kaulimbiu "Dodoma Ipo Tayari: Ipeleke Dodoma Duniani na Ilete Dunia Dodoma", Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule alitumia jukwaa hilo kueleza hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa mji huo, hususan katika maeneo ya miundombinu ya huduma za afya, elimu, maji, umeme, usalama, usafiri na burudani. Alusema huduma hizo zinapatikana kwa ubora wa kimataifa, hivyo jumuiya ya wanadiplomasia isihofie chochote inakaribishwa Dodoma na Dodoma ipo tayari kwa ajili yao.

Mhe. Mkuu wa Mkoa pia alibainisha fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana jijini Dodoma katika sekta za kilimo, utalii, logistics, viwanda & ujenzi na madini na kuwakaribisha wawekezaji kuchangamkia fursa hizo.

Alisema Serikali ipo katika mchakato wa kujenga Hombolo Thermatic Satelite City na kubainisha kuwa hiyo ni fursa kubwa na adhimu kwa wawekezaji kushirikiana na Serikali kufanikisha ujenzi wa mji huo.

Naye, Mwakilishi wa Kiongozi wa Mabalozi ambaye alikuwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Isaac Njenga alisema kuwa yeye na Mabalozi wenzake wameshuhudia hatua kubwa iliyopigwa katika ujenzi wa mji wa Dodoma hasa baada ya kutembelea na kujionea mji wa Serikali uliopo eneo la Mtumba, Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato. Amesema kwa niaba ya Mabalozi wenzake wameridhika na hatua iliyofikiwa na wameahidi kuzishawishi Serikali za nchi zao kutenga fedha za kuanza ujenzi wa ofisi na makazi ya balozi jijini Dodoma.

Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wapo jijini Dodoma kushiriki uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 tarehe 28 Mei 2025.


Share:

WAZIRI DKT. GWAJIMA AANISHA VIPAUMBELE VITANO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII 2025/2026




Na
 WMJJWM, Dodoma 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii. Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameainisha vipaumbele vya Wizara vikubwa vitano katika utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Mhe. Dkt. Gwajima ameainisha hayo wakati akiwasilisha Bajeti ya  Wizara hiyo kwa Mwaka husika wa Fedha leo Mei 27, 2025 Bungeni jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa Wizara kupitia Idara na Taasisi zilizo chini yake zitatekeleza vipaumbele hivyo  ambavyo ni kukuza ari ya Jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ngazi ya msingi, kuratibu na kuimarisha utoaji wa huduma za ustawi wa maendeleo ya jamii, kutambua pamoja na kuratibu maendeleo ya ustawi kwa Makundi Maalum.

Mhe. Dkt. Gwajima ameongeza kuwa vipaumbele vingine ni pamoja kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia katika Taasisi na Vyuo vya Ustawi na Maendeleo ya Jamii na kuimarisha mazingira ya ushiriki na mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa.

Amesema Wizara imeendelea kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kuhamasisha na Kusimamia Maendeleo katika Ngazi ya Msingi (2022/23 – 2025/26) ambao unalenga kuwawezesha wananchi kuwa kitovu cha maendeleo na kuchochea mageuzi ya kifikra, mtazamo na kiutendaji kwa timu ya wataalam ngazi ya msingi ili kuboresha utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katika kuhakikisha Watoto wanalindwa na ukatili Waziri Dkt. Gwajima amesema Wizara imeratibu na kusimamia Kampeni ya Taifa ya Usalama wa Mtoto Mtandaoni (Child Online Protection - COP) katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Kampeni ilikuwa na lengo la kuelimisha Wazazi au Walezi na Watoto wenyewe kuhusu Usalama wa Mtoto anapokuwa anatumia mitandao.

Aidha Mhe. Dkt. Gwajima amefafanua kuwa Wafanyabiashara ndogondogo 601 (Me 274; Ke 327) wamekopeshwa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1,101,650,000 na zoezi hilo linaendelea. Vilevile maombi 2,092 yanaendelea kuchakatwa yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3,590,477,000.

"Wizara kwa kushirikiana na OR - TAMISEMI imeendelea kuratibu na kufuatilia maendeleo ya ya Ujenzi wa Ofisi za wafanyabiashara ndogondogo katika ngazi ya mikoa ambapo hadi kufikia Aprili 2025 mikoa 17 kati ya mikoa 26 imekamilisha ujenzi wa Ofisi hizo" ameeleza Mhe. Dkt Gwajima. 

Akichangia hoja, Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Dkt. Thea Ntara amesizitiza Serikali kuchukua hatua na kusimamia maadili nchini, kutokana na kuwepo kwa matukio mengi ya uvunjifu wa maadili.

Naye Mbunge wa kuteuliwa Dkt. Shukurani Manya ameshauri  kuongezeka kwa juhudi za kuelimisha Jamii kuhusu elimu ya malezi ili kuepusha kutelekezwa kwa watoto ili waweze kupata malezi ya baba na mama.

Share:

MWENYEKITI WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE KAHAMA AWAKARIBISHA WANANCHI KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI

  

Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Wilaya ya Kahama aliebeba shajala akiwakaribisha wananchi wote wa Manispaa ya Kahama na viunga vyake kushiriki katika mkutano mkubwa wa injili utakaoanza kesho, tarehe 28 Mei 2025, na kudumu kwa siku tano.


NA NEEMA NKUMBI - KAHAMA


Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Wilaya ya Kahama amewakaribisha wananchi wote wa Manispaa ya Kahama na viunga vyake kushiriki katika mkutano mkubwa wa injili utakaoanza kesho, tarehe 28 Mei 2025, na kudumu kwa siku tano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 27, 2025, Mwenyekiti huyo amesema maandalizi yote yamekamilika na tayari wageni waalikwa kwa ajili ya mkutano huo wamewasili.

Mkutano huo utaanza kesho asubuhi kwa semina ya Neno la Mungu itakayofanyika kuanzia saa 1:00 asubuhi katika kanisa la Shalom Temple na  baada ya semina hiyo, shughuli za mkutano wa injili zitaendelea katika Uwanja wa Magufuli uliopo eneo la Majengo, Manispaa ya Kahama.

“Nawakaribisha watu wa dini zote na rika zote kushiriki nasi katika mkutano huu wa kiroho, Tuanze na semina ya Neno la Mungu saa 1:00 asubuhi katika kanisa la Shalom Temple, kisha tuhamie katika viwanja vya Magufuli kuendelea na mkutano wa injili,” amesema Mwenyekiti huyo.

Mkutano huo unatarajiwa kuwaleta pamoja maelfu ya wakazi wa Kahama na wageni kutoka maeneo mbalimbali, kwa ajili ya kushiriki ibada, maombi, na mafundisho ya Neno la Mungu.


Mwisho.
Share:

Tuesday, 27 May 2025

ALIYENIFUKUZA KISA NILIKATAA KULALA NAYE, AKUMBWA NA MAZITO!


Naitwa Judithi kutokea Mwanza, miezi sita iliyopita, nilianza safari ya mabadiliko maishani kwa kuhama kutoka kwenye kazi yangu ya zamani na kwenda nyingine ambayo nilikuwa na matumaini makubwa nayo.

Uamuzi huu ulitokana na hamu ya kupata changamoto mpya ili kuwa na ukuaji katika kazi yangu katika maeneno mbalimbali hasa upande wa kiuchumi.

Licha ya kuwa mdogo, kupata nafasi kama mfanyakazi wa kitengo cha mawasiliano katika hoteli ya kifahari ya nyota tano, ilikuwa hatua kubwa kwangu hasa upande wa kupata uhuru wa kifedha.

Hata hivyo, msisimko wangu wa awali ulibadilika na kuwa mfadhaiko nilipojikuta nikikabiliana na mambo yasiyokubalika kutoka kwa Meneja wa hoteli ili ambayo nilikuwa naifanyia kazi.

Wiki mbili tu baada ya majukumu yangu mapya, Meneja alianza kutembelea ofisi yangu mara kwa mara kwa madai ya mazungumzo ya kawaida ambayo yanalenga kuboresha kazi lakini akavuka mstari kwa kunigusa sehemu ambayo sio sawa.

Nikiwa nimeshtuka na kuchukizwa, nilikataa kitendo chake kwa ajili ya usalama wa kazi. Hata hivyo, kukataa kwangu kulinigharimu maana alipanga mipango ya kulipiza kisasi.

Meneja alibuni mashtaka ya uongo na kushawishi nifukuzwe kazi. Licha ya juhudi na majaribio yangu ya kujitetea, nilijikuta nimefukuzwa kazi kwa madai ya matumizi mabaya ya ofisi.

Nikiwa nimekata tamaa, nilimweleza rafiki yangu mkasa huo, mara moja alinielekeza kwa Kiwanga Doctors, wataalamu wa tiba asilia ambao wamesaidia watu wengi ukanda wa Afrika Mashariki.

Kutokana sikuwa na chochote cha kupoteza, nilifika kwa Kiwanga Doctors ili kupata suluhisho la shida yangu. Kupitia uganga na uchawi wao, walifanya mambo ambayo yalimtesa Meneja hadi akakubali kosa lake na kuomba nirudishwe kazini.

Kama walivyosema, ndani ya saa 24, Meneja huyo alisalimu amri kutokana na kusumbuliwa na misukosuko isiyoelezeka na magonjwa katika familia yake.

Hivyo basi niliweka masharti ya maridhiano ili aweze kuondokana na shida hizo, moja ya masharti ni pamoja na kujiuzulu, jambo ambalo alitekeleza kwa muda muafaka na punde tu niliweza kurejeshwa kazi tena katika nafasi yangu ile ile ya mwanzo.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +255 763 926 750 au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi.
Share:

SERIKALI YAMWAGA MILIONI 815 KUBORESHA HUDUMA YA MAJI KWA VIJIJI VINNE MTWARA



Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara Mhandisi Hamis Mashindike aliyeshika fimbo,akimuonyesha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2025 Ismail Ali Ussi miundombinu ya mradi wa maji Dihimba uliofanyiwa ukarabati mkubwa ili kuboresha hduma ya majisafi na salama kwa Wananchi wa Vijiji vinne vya Dihimba,Mpondomo, Kinyamu na Ndumbwe.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2025 Ismail Ali Ussi,akiangalia kisima cha maji katika kilichofanyiwa ukarabati mkubwa kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa Wananchi wa Vijiji vya Ndumbwe,Dihimba,Mpondomo na Kinyamu Wilayani Mtwara,kushoto Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mtwara Hamis Mashindike na kulia Mkuu wa Wilaya
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mtwara Hamis Mashindike aliyeshika fimbo akitoa maelekezo kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ismail Ali Ussi wakati alipokwenda kukagua kisima cha maji kilichokarabatiwa na kuboreshwa kwaajili ya huduma ya wananchi wa vijiji vinne wilayani humo


Na Regina Ndumbaro-Mtwara 

Serikali kupitia Wizara ya Maji imetoa Shilingi 815,453,185 kwa ajili ya kukarabati Mradi wa Maji wa Dihimba unaohudumia wakazi zaidi ya 7,489 katika vijiji vya Dihimba, Mpondomo, Kinyamu na Ndumbwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara. 

Mradi huu ni hatua muhimu katika kuboresha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi waliokuwa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji kwa muda mrefu.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mtwara, Mhandisi Hamis Mashindike, amesema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi 694,271,895 zilitumika kumlipa mkandarasi na Shilingi 121,181,200 zilinunulia mabomba kupitia RUWASA Makao Makuu. 

Ukarabati huo ulianza Januari 2024 na unatarajiwa kukamilika Juni 2025 baada ya kuchelewa kutokana na changamoto kama mvua nyingi na ucheleweshaji wa malipo. 

Mradi huu unatekelezwa na wakandarasi M/S Zonghi Plumbing & General Supplies na M/S Seba Construction, ambapo hadi sasa umekamilika kwa asilimia 75.

Kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa tenki la lita 100,000 katika kijiji cha Mpondomo, ukarabati wa matenki mawili ya lita 200,000 katika Ndumbwe, ujenzi wa vituo 17 vya kuchotea maji, nyumba ya muhudumu, ofisi ya Jumuiya ya Watumia Maji (CBWSO), pamoja na ulazaji wa bomba wa zaidi ya kilometa 24. 

Utekelezaji wa mradi umeongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 37.04 hadi 93.47 kwa mwaka 2025.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi, alipata fursa ya kutembelea na kukagua miundombinu ya mradi huo huku akielezwa mafanikio yaliyopatikana. 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Patrick Sawala, ameeleza kuwa mradi huo ulioanzishwa mwaka 1989 haujawahi kufanyiwa ukarabati mkubwa na sasa umeleta ahueni kubwa kwa wananchi, ambao awali walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata maji.

Mwananchi wa Kijiji cha Dihimba, Mwanahawa Rashid, ameeleza kuwa kabla ya ukarabati huo walilazimika kutembea hadi vijiji vya jirani kwa ajili ya maji.

 Ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kusikiliza kilio cha wananchi na RUWASA kwa usimamizi mzuri wa mradi huo ambao sasa umewapunguzia adha kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger