Saturday, 24 May 2025

ELIMU YA KODI YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA IRINGA KUPITIA RADIO NA MLANGO KWA MLANGO.


Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Mkumbwa akimuelimisha mlipakodi wa eneo la Miyomboni Iringa wakati wa zoezi la utoaji wa elimu ya kodi mlango kwa mlango linaloendelea mkoani humo.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akimpatia zawadi Meneja wa Radio ya Shamba FM ya Mkoani Iringa Bw. Laurian  Deogratius baada ya kumaliza kipindi kilichoangazia masuala ya haki na wajibu wa mlipakodi pamoja na umuhimu wa kulipa kodi ikiwa ni sehemu ya zoezi la utoaji wa elimu ya kodi mlango kwa mlango linaloendelea mkoani humo.
Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Shaga Gagunda  akimuelimisha mlipakodi wa eneo la Miyomboni Iringa wakati wa zoezi la utoaji wa elimu ya kodi mlango kwa mlango linaloendelea mkoani humo.
Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Frola  Fulgence akimuelimisha mlipakodi wa eneo la Miyomboni Iringa wakati wa zoezi la utoaji wa elimu ya kodi mlango kwa mlango linaloendelea mkoani humo.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akizungumzia mada ya haki na wajibu wa Mlipakodi katika kipindi cha radio cha kivulini kinachorushwa na Shamba FM iliyoko mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya zoezi la utoaji wa elimu ya kodi mlango kwa mlango linaloendelea mkoani humo.
Meneja Msaidizi wa Huduma kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Iringa Bw. Musa Haruni akizungumzia mada ya umuhimu wa kulipa kodi katika kipindi cha radio cha kivulini kinachorushwa na Shamba FM iliyoko mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya zoezi la utoaji wa elimu ya kodi mlango kwa mlango linaloendelea mkoani humo.
Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Haika Mallya akimuelimisha mlipakodi wa eneo la Miyomboni Iringa wakati wa zoezi la utoaji wa elimu ya kodi mlango kwa mlango linaloendelea mkoani humo.
Share:

MADINI YA ALMASI YENYE THAMANI YA TSH 1.7 BILIONI YAKAMATWA YAKITOROSHWA UWANJA WA NDEGE MWANZA



▪️Waziri Mavunde awapongeza RC Mtanda,Kamati ya Usalama,Uwanja wa Ndege na Kikosi kazi Madini

▪️Aelekeza uchunguzi zaidi kubaini mtandao wote wa wahusika

▪️Atoa rai kwa wadau wa madini kuzingatia sheria ya biashara ya madini nchini

▪️Raia wa Kigeni mwenye asili ya India ashikiliwa 


Mwanza

Madini ya almasi yenye thamani ya zaidi ya Sh1.7 bilioni yamekamatwa yakitoroshwa kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari ljumaa usiku,Mei 23, 2025, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema madini hayo yalikamatwa Mei 18, 2025 kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na taasisi mbalimbali za Serikali na kutumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda,Vyombo vya usalama,uongozi wa uwanja wa Ndege wa Mwanza na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kwa kazi kubwa na ya kizalendo ambayo wameifanya.

“Mtu mmoja raia wa kigeni ambaye ana asili ya India , anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi na taratibu

Katika tukio hilo,almasi ghafi yenye uzito wa karati 2,729.82 na thamani ya takriban USD 635,887.66 (sawa na Shilingi za Kitanzania 1,715,434,129.67) yaligunduliwa yakiwa yamefichwa kwenye mabegi manne na raia mmoja mwenye asili ya India kwa lengo la kuyasafirisha bila vibali halali wala kufuata taratibu za kisheria.

Nitoe rai kwa wadau wote wa Sekta ya Madini nchini kuhakikisha wanafuata sheria ya biashara ya madini nchini Tanzania ili wasipate hasara kwa kupoteza madini hayo ambayo hutaifishwa na serikali” Alisema Mavunde

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Saidi Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza unaendelea kuimarisha ulinzi na udhibiti wa biashara zote haramu ili kuhakikisha nchi yetu ya Tanzania inanufaika na rasilimali madini.

 

Share:

Friday, 23 May 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 24,2025


Magazeti 
Share:

WANANCHI 1,640 WAPATIWA ELIMU YA KUJIKINGA NA WANYAMA WAKALI NA WAHARIBIFU



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na wanyama wakali na waharibifu, ambapo jumla ya wananchi 1,640 kutoka vijiji vya Engikaret na Kiserian, Wilaya ya Longido mkoani Arusha, wamefikiwa kati ya Julai 2024 hadi Aprili 2025.

Hayo yameelezwa leo Mei 23, 2025 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Zaytun Seif Swai, kuhusu mikakati ya Serikali katika kukabiliana na uvamizi wa tembo katika Kata ya Engikaret.

Akifafanua, Mhe. Kitandula amesema kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya doria za mwitikio wa haraka. Amesema kuwa kati ya Julai 2024 na Machi 2025, jumla ya doria 34 zimefanyika katika Kata ya Engikaret kwa lengo la kukabiliana na matukio ya wanyamapori wakali.

Aidha, Naibu Waziri huyo amebainisha kuwa Serikali ilianzisha kituo maalum cha askari mwaka 2021 katika Wilaya ya Longido ili kuimarisha ulinzi dhidi ya wanyamapori hao. Kituo hicho kina jumla ya askari 18 wakiwemo wahifadhi 8 na askari wa wanyamapori wa vijiji (VGS) 10. 

Vituo hivyo vimewezeshwa kwa vitendea kazi ikiwemo gari moja na pikipiki nne ili kufanikisha shughuli za ulinzi.

Katika hatua nyingine, Kitandula amesema Serikali inaendelea kushirikiana na wananchi kwa kuwajengea uelewa juu ya namna bora ya kuripoti matukio ya wanyama wakali kwa wakati, ili hatua za haraka zichukuliwe. Amesisitiza kuwa elimu hiyo inatolewa kwa njia ya mikutano ya hadhara, vipeperushi, na kupitia vyombo vya habari vya jamii.

Vilevile, Serikali inaendelea na jitihada za kuongeza idadi ya askari wa wanyamapori na kuwawezesha vifaa vya kisasa zaidi ili kuongeza ufanisi wa operesheni za kuwalinda wananchi, mali zao pamoja na uhifadhi endelevu wa wanyamapori nchini.
Share:

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAOMBA KUIDHINISHWA BAJETI YA BIL. 476.7 KWA KWAKA 2025/2026



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Bunge la bajeti likiwa linaendelea Jijini hapa,Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewasilisha ombi la bajeti ya shilingi bilioni 476.7 kwa ajili ya mwaka wa fedha 2025/2026, lengo likiwa ni kuendeleza shughuli za sekta hizo muhimu nchini.

Akiwasilisha makadirio hayo bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 101.5 zimetengwa kwa matumizi ya kawaida huku shilingi bilioni 375.1 zikiwa ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Kwa mujibu wa Waziri huyo,Matumizi ya kawaida yanahusisha mishahara ya wafanyakazi (PE) ambayo ni shilingi bilioni 47.3 na matumizi mengineyo (OC) yenye jumla ya shilingi bilioni 54.3.

Katika fedha za maendeleo, Dkt. Kijaji amesema shilingi bilioni 228 zinatarajiwa kutoka ndani ya nchi, huku shilingi bilioni 147.1 zikitarajiwa kutoka kwa wahisani wa nje.

Wizara imesisitiza kuwa fedha hizo zitalenga kuboresha mifumo ya uzalishaji na usindikaji wa mazao ya mifugo na uvuvi, sambamba na kuimarisha upatikanaji wa masoko kwa wafugaji na wavuvi nchini.




Share:

Thursday, 22 May 2025

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO ASHIRIKI MKUTANO WA PILI WA BRAZIL NA AFRIKA KUHUSU USALAMA WA CHAKULA NA MAENDELEO VIJIJINI



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki Ufunguzi wa Mkutano wa pili wa Brazil na Afrika kuhusu Usalama wa Chakula, Mapambano dhidi ya Njaa na Maendeleo Vijijini unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazil (Itamaraty Palace) Jijini Brasilia . Tarehe 22 Mei 2025.




Share:

“NILIWANASA PALE KWENYE KITANDA CHETU CHA NDOA,” MWAMBA ASIMULIA


“Si uliniambia umeenda Dar?”. Ndivyo alivyoniuliza mke wangu, sauti yake ilisikika usiku wa manane wenye kimya kingi. Mimi, Eric, nilikuwa nikishuku uaminifu wa mke wangu katika ndoa yetu kwa muda mrefu.

Nakumbuka tulikuwa tumefunga ndoa ya kanisani, tumefungwa na viapo vitakatifu, lakini sikuweza kuondoa shaka kwamba alikuwa akiwatamani wanaume wengine huko nje.

SOMA ZAIDI <HAPA>



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger