Tuesday 27 August 2024

RC SENYAMULE AFUNGUA TAMASHA LA JINSIA...'RAIS SAMIA AMEUDHIHIRISHIA ULIMWENGU WANAWAKE WANAWEZA KUONGOZA'

Na Mwandishi wetu - Malunde Media

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka Wanawake nchini Tanzania kujiamini na kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao kwani Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameudhihirishia Ulimwengu kuwa Wanawake wanaweza kuwa viongozi.

Mhe. Senyamule ametoa kauli hiyo Agosti 27, 2024 wakati akifungua rasmi Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 na Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.

"Safari hii wanawake wote tujitokeze kugombea nafasi za uongozi kwa sababu yupo Mwanamke (Mhe. Rais Samia) aliyeonesha kuwa wanawake tunaweza. Ni imani yangu katika uchaguzi wanawake wengi watawania nafasi za uongozi kwa sababu jamii imejionea kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, jamii imeamini kuwa wanawake wanaweza na mfano hai ni Mhe. Rais Samia", amesema Mhe. Senyamule.

"Ili usawa wa kijinsia ufikiwe ni lazima wanawake tuchukue hatua, mazingira rafiki yamewekwa hivyo ni kazi kwetu kupambana. Ni lazima tuchukue hatua za kugombea na kuingia katika ngazi za maamuzi",ameongeza Mhe. Senyamule.

Aidha amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kufanya jitihada mbalimbali kutekeleza mpango kazi wa Beijing kufikia usawa wa kijinsia ambapo sasa wanawake wengi wameshika nafasi za uongozi na Rais Mhe. Samia Suluhu ameendelea kufanya teuzi mbalimbali kwa wanawake wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na taasisi mbalimbali.

"Tunaposherekea miaka 30 ya Beijing tunayo mengi ya kujivunia. Nafasi za wanawake katika uongozi zinazidi kuongezeka, tunaendelea kuboresha huduma za afya, elimu, upatikanaji wa maji safi na salama, umeme na ongezeko la madawati ya jinsia",ameeeleza.

Katika hatua nyingine ameitaka jamii kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia akibainisha kuwa mauaji yanayoongoza katika Mkoa wa Dodoma yanasababishwa na ulevi na wivu wa mapenzi.

"Tuweke nguvu kuelimisha jamii watu wasifanye ukatili, asilimia kubwa ya matukio ya ukatili yanafanyika majumbani na jamii inaficha taarifa za matukio, tusitumie nguvu kubwa kutetea wahalifu, tutoe maonyo na elimu kabla ya ukatili haujafanyika..Na lazima tuchukue hatua ya kuwafundisha watoto maadili mema",ameongeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amesema suala la usawa wa kijinsia ni suala la maendeleo hivyo amewahamasisha wananchi kutoa maoni kwenye dira ya Taifa 2050 kwa ajili ya mwelekeo wa taifa kwa miaka 25 ijayo kwa kuzingatia haki na usawa wa Kijinsia katika masuala yote ya maendeleo.

Liundi amesema nchi ya Tanzania imepiga hatua katika masuala ya usawa wa kijinsia ambapo sasa wanawake wanashika nafasi za uongozi akitolea mfano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.

"Tunatambua kuwa kwa sasa nchi yetu ina Rais Mwanamke kwa mara ya kwanza kabisa; kwa upande wa wabunge wanawake ni asilimia 37 tu ambao 9.5% ni wabunge wa kuchaguliwa na 29% ni wa vitimaalumu. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ni miongozi mwa wanawake wakuu mikoa wachache nchini na pia, mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa ni miongoni mwa wakuu wa wilaya wanawake wachache nchini", amesema Liundi.

Tamasha hilo la siku tatu  (Agosti 27 - 29 , 2024 linaloongozwa na mada kuu ‘Dira Jumuishi ya 2050: Miaka 30 Baada ya Beijing Tujipange’ linashirikisha Wanaharakati na Wadau zaidi ya 300 wanaotetea haki za wanawake na usawa wa jinsia kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali amesema Tamasha la Jinsia ni moja ya majukwaa ya TGNP katika ujenzi wa nguvu za pamoja ambapo Jukwaa hilo ni la wazi kwa ajili ya wanawake na wadau wa haki za binadamu ambao hukutana pamoja kila baada ya mwaka mmoja kubadilishana uzoefu, kusherehekea, kutathmini na kupanga mipango ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Akilimali amewasisitiza wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuepuka kuwa wapiga makofi na wasindikizaji wa wanaume kwenye uchaguzi.

"Wanawake tuwajibike, tujitokeze kugombea nafasi za uongozi badala ya kubaki kuwa walalamikaji na wapiga makofi tu",amesema.

Amesema ili kufikia mikakati juu ya matumizi ya nishati safi ameihamasisha Serikali kupunguza gharama za gesi na tozo za gesi ili kuwawezesha wananchi walipo vijijini na wengi kutumia nishati safi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati akifungua rasmi Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 na Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali Agosti 27, 2024  katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma. Picha na Malunde Media
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati akifungua rasmi Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 na Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akikata utepe ishara ya kufungua Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (wa pili kushoto) akipata maelezo kwenye banda la TGNP katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akisoma Ilani ya Madai ya wanawake katika uchaguzi (Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025) yenye lengo la kudai mabadiliko ya mifumo kandamizi inayohalalisha ubaguzi wa wanawake katika uchaguzi kama wapiga kura, wenye kuwania nafasi za teuzi na hatimaye kuwakwamisha kwenye kuchaguliwa kama wawakilishi katika ngazi mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akisoma Ilani ya Madai ya wanawake katika uchaguzi (Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake - Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025) 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitembelea mabanda ya wadau wa kutetea haki za wanawake

Share:

WILDAF YAJIPANGA KUWAPIGA MSASA WATIA NIA WANAWAKE

Na Rose Ngunangwa - Dar es salaam

Jamii imeaswa kuhakikisha kwamba wanaume na wanawake wanashirikiana ili taifa lisonge mbele kimaendeleo.

Wito huo umetolewa  na Mratibu wa Taifa wa WILDAF Wakili Anna Kulaya wakati akifungua mafunzo katika warsha ya kuwajengea uwezo waraghabishi ambao watakwenda kufanya mafunzo kwa wanawake watia nia yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

Katika kazi zetu tuligundua kwamba jamii haina shida ya kuwapigia kura viongozi wanawake lakini changamoto kubwa ilikuwepo kwenye michakato ya vyama ambako majina ya wanawake watia nia yalikuwa yakikatwa.

Wakili Kulaya alishukuru uwepo wa mabadiliko kwenye sheria za uchaguzi ambayo yanasisitiza masuala ya jinsia katika ngazi zote za vyama vya siasa na kusisitiza umuhimu wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika uchaguzi na ngazi za maamuzi.

Kwa upande wake, Dkt. Helen Bissimba ambae ni mwezeshaji wa mafunzo hayo amesisitiza umuhimu wa kuwafundisha wanawake watia nia umuhimu wa kuleta mabadiliko katika jamii yao pamoja na kutumia medani za uwezeshaji wa namna ya kuongea na hadhira.

“Ukatili wa kijinsia hushamiri sana wakati wa uchaguzi ikiwemo rushwa ya ngono. Upo umuhimu wa kuwajengea uwezo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kukabiliana na ukatili na kuongeza ushiriki wao katika chaguzi,” alisema.

Mafunzo haya yanafanyika chini ya Mradi wa WILDAF ujulikanao kama Wanawake Sasa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland na yanalenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi katika ngazi za maamuzi.

Watanzania wanatarajia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Novemba mwaka 2024.

Share:

DK. NDUGULILE KUIWAKILISHA TANZANIA WHO KANDA YA AFRIKA

Dkt. Faustine Ndugulile Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Kanda ya Afrika

Na Dotto Kwilasa.

Hatimaye mshindi kinyang'anyiro cha nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Kanda ya Afrika apatikana .

Mbunge wa Kigamboni Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile ndiye aliyeibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika leo Jumanne, tarehe 27 Agosti 2024 mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo na kuwashinda wagombea wengine watatu kutoka Senegal, Niger na Rwanda

Katika uchaguzi huo Dkt. Ndugulile amewashinda wagombea wengine watatu kutoka Senegal, Niger na Rwanda na hivyo kuitendea haki nafasi hiyo kwa kuwa Mara baada ya kuanza kazi rasmi, Tanzania kama nchi itapata nafasi pia ya kujitangaza kimataifa.
Ikumbukwe tu kuwa zoezi la uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika umefanyika kupitia Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afya Afrika chini ya Shirika la Afya Duniani.

Kabla ya kushinda uchaguzi huo Dkt. Ndugulile aliweka wazi vipaumbele vyake kuwa ni kuhakikisha Watu wanapata haki ya kupata huduma bora za afya; Kuboresha utayari wa nchi za Afrika katika kukabiliana na majanga ya magonjwa ya mlipuko, Kuimarisha uwajibikaji ndani ya WHO kanda ya Afrika pamoja kuimarisha mawasiliano baina ya nchi wanachama katika masuala ya Afya.

Share:

STAMICO YABAINI ASILIMIA 86.2 YA WANAWAKE WANAJIHUSISHA NA MADINI

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Matokeo ya utafiti mdogo uliofanywa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) umeonesha zaidi ya asilimia 80 ya wanawake kutoka mikoa ya Shinyanga, Geita, Mara na Simiyu wanajishughulisha na Shughuli za sekta ya Madini nchini.
Hayo yamesemwa leo Agosti 27, 2024 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti maalumu vya wanawake Fatma Hassan aliyetaka kujua idadi ya wanawake wanaomiliki migodi ya madini nchini.

Naibu Waziri amesema kuwa, shughuli za madini nchini zinafanyika katika maeneo mbalimbali kupitia watu binafsi na kampuni ambazo ndani yake kuna wanawake na wanaume.
Ameongeza kuwa, utafiti uliohusisha wanawake 992 umeonesha Wanawake 17 sawa na asilimia 1.7 wanamiliki migodi, wanawake 67 sawa na asilimia 6.8 wanamiliki maeneo ya uchimbaji (maduara) katika leseni za uchimbaji madini na wanawake 855 sawa na asilimia 8.2 wanajishughulisha na kazi zinazohusiana na uchimbaji pamoja na uchenjuaji madini huku wanawake 53 sawa na asilimia 5.3 wanatoa huduma maeneo ya uchimbaji.

Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa kulingana na umuhimu na mchango wanaotoa kwa taifa, Serikali itaendelea kuwasimamia na kuwapatia leseni wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini ili kuongeza mchango wao kwenye sekta pia kuimarisha uchumi wao.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ilibaini kuwa kuna takribani wanawake milioni 3 wanaoshiriki katika mnyororo mzima wa thamani madini.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger