Thursday, 30 May 2024

SHINYANGA PRESS CLUB,UTPC WAKUTANA NA WADAU KUJADILI UHURU WA KUJIELEZA SHINYANGA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za Habari Tanzania (UTPC), imeendesha Semina ya Kijamii juu ya Uhuru wa kujieleza mkoani humo.

Semina hiyo imefanyika leo Mei 29,2024 na kukutanisha wadau mbalimbali wa habari, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi amesema Semina hiyo madhumuni yake ni kujadili kwa pamoja juu ya hali ya uhuru wa kujieleza, kwa muktadha wa kusukuma na kuchochea maendeleo kwa sekta zote, ili kuona umuhimu wa uhuru wa kujieleza unavyoleta tija ya maendeleo hapa nchini.

“Klabu yetu inatekeleza Mradi wa uhuru wa kujieleza kwa ushirikiano na UTPC ili kusukuma maendeleo ndani ya Mkoa wetu, na leo tupo hapa kujadili kwa pamoja ili kuona nafasi ya jamii, wadau, Serikali na vyombo vya habari namna tunavyoweza kuweka mazingira salama ya uhuru wa kujieleza ili kufikia maendeleo endelevu,”amesema Kakuru.
“ Uhuru wa kujieleza ndiyo msingi wa kusaidia Taifa letu kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 2030 katika maeneo 17 yaliyoainishwa kwa nia ya dhati ya kukomesha umaskini,kulinda mazingira ya hali ya hewa, na kuhakikisha watu kila Mahali wanaweza kufurahia Amani na ustawi, hivyo utatuzi wa Changamoto za kimaendeleo kwa watu ni kutumia haki ya kujieleza,”ameongeza.

Aidha, amewataka wadau wa habari kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari, katika kuimarisha hali ya uhuru wa kujieleza ndani ya jamii, ambapo bado kuna vizuizi ikiwamo Mifumo ya Mila na Desturi, uelewa duni mifumo ya sheria na urasimu wa utoaji taarifa katika Sekta binafsi na Umma.
“Klabu yetu kwa ufadhili wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) tunatekeleza Mradi wa kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, lakini tumeshuhudia Mifumo ya Mila na Desturi kandamizi jinsi inavyokandamiza uhuru wa kujieleza,”amesema Kakuru.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UTPC Severine Mapunda ambaye ni Mkuu wa Programu, amesema Semina hiyo wanaitekeleza kwa Klabu za Waandishi wa habari Mikoa Nane, ili kutoa fursa na kuelewa namna ambavyo uhuru wa kujieleza unavyoweza kuchangia Maendeleo ya Nchi.
“Uhuru wa kujieleza unaifanya jamii kuwa na Maendeleo ikiwamo kutatuliwa shida zao, na vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya katika kuchagiza uhuru huu wa kujieleza kwa kupaza maoni ya wananchi kupitia vyombo vyao, na kuleta mabadiliko chanya katika nchi yetu,”amesema Mapunda.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,amewapongeza Waandishi wa habari kwa Semina hiyo,na kuahidi kwamba katika uongozi wake Shinyanga,atahakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi zao kwa uhuru bila ya kubughuziwa, na hatopenda kusikia Mwandishi wa habari anaingizwa kwenye matatizo.
“Katika kipindi cha uongozi wangu hapa Shinyanga nikiwa Mkuu wa wilaya, nitafanya kazi pamoja na Waandishi wa habari kwa maendeleo ya Taifa letu, na siwezi kumnyima Mwaandishi yeyote habari, ‘nifiche habari ili iweje’ habari ni kwa ajili ya Maslahi ya Umma,”amesema Mtatiro.

“Uhuru wa habari ni Muhimu sana kwa sababu kupitia vyombo vya habari tunapata taarifa mbalimbali, na sisi kama viongozi tunachukua hatua, dunia ya sasa inapiga hatua kimaendeleo kutokana na kutatua matatizo ya wananchi, kwa sababu ya vyombo vya habari,”ameongeza.
Aidha, amesisitiza kwamba katika uhuru huo wa kujieleza kuwepo na mipaka na kuzingatia sheria za nchi, sababu hakuna ambaye yupo juu ya Sheria, ili kukwepa kuingia kwenye mikono sheria,vivyo hivyo kwa waandishi wa habari, pamoja na kuchakata habari zao kwa ufasaha na kuzibalance.

Katika hatua nyingine amewasisitiza waandishi wa habari, wasiogope kuibua mambo maovu ambayo hutendeka ndani ya jamii, yakiwamo masuala ya ubinywaji haki,dhuluma na ukatili ili wao kama viongozi wapate taarifa na kuchukua hatua.
Amewataka waandishi wa habari, pia kuandika habari za Ajenda za Kitaifa ikiwamo ujenzi wa Miundombinu mbalimbali, pamoja na kuhabarisha Umma juu ya Uchaguzi wa Serikali hatua ambazo zinaendelea ikiwamo uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Katika Semina hiyo ya Uhuru wa Kujieleza zilijadiliwa pia Mada mbalimbali ikiwamo ya Uhuru wa kujieleza, Utawala Bora kwa Maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga, na Umuhimu wa upatikanaji wa Taarifa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UTPC Severine Mapunda ambaye ni Mkuu wa Programu akizungumza kwenye Semina hiyo ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.

Wadau wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.

Viongozi wakiwa Meza Kuu.
adau wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.
Wadau wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.
Semina ya Uhuru ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza ikiendelea.
Wadau wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.
Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza ikiendelea.

Wadau wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakichangia Mada kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.
Wadau wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakiendelea kuchangia Mada kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.

Wadau wakiendelea kuchangia Mada.

Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Awali Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro (kulia) akiwasili kwenye Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.
Semina ya Kijamii ya Uhuru wa kujieleza.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 30, 2024

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger