Wednesday, 29 May 2024

GRUMETI FUND YATOA ELIMU YA KIJINSIA KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1,000 BUNDA

SHIRIKA la Grumeti Fund  kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imewaleta pamoja Wanafunzi wa kike 704 na wakiume 634 kutoka katika shule za Tirina,Chamriho na Hunyari Wilayani Bunda, kwa lengo la kutoa Elimu sambamba na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wa kike na kiume ili kujenga jamii yenye usawa na yenye kujitambua  kwa vijana wa jinsia zote.


Katika kongamano la wasichana lililofanyika katika shule ya Sekondari Hunyari iliopo Wilayani Bunda Mkoani Mara, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Grumeti Fund Bi. Frida Mollel amesema  lengo la Grumeti Fund kufanya kongamano hilo ni kuwaelimisha watoto wa kike kutambua thamani yao sambamba na kuwajengea uwezo wa kujiamini na kufikia ndoto zao.

"Kutokana na utafiti tulioufanya juu ya uchache wa watoto wa kike katika kuchangamkia fursa za kimasomo zinazotolewa na Grumeti Fund, moja ya njia za kutatua changamoto hii ni kufanya makongamano kwa nia ya kutoa elimu kwa mabinti, kwanza wafahamu thamani yao na pili wafahamu kwamba wanaweza kuwa mtu yeyote watakae katika maisha yao  na kukataa kukatishwa tamaa na mtu yeyote. Nataka mfahamu kwamba mnaweza"

 Aidha, Bi. Frida amewataka wasichana hao kutokata tamaa kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili bali watumia elimu wanayoipata ili iweze kuleta tija na mabadiliko chanya katika jamii na kusisitiza kuwa elimu ndio dira na njia ya kufikia ndoto za vijana hao. 

Katika kongamano hilo shirika la Grumeti Fund imetoa msaada wa taulo za kike  zinazoweza kutumika  kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu (reusable pads) kwa wanafunzi wa kike 704 zenye thamani ya Shilingi Milioni tisa laki nane na elfu hamsini na sita (9,856,000) katika shule za sekondari Tirina,Chamriho na Hunyari 

Naye mgeni rasmi katika katika kongamano hilo, Neema Paul ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti amewataka wasichana kuzingatia nidhamu sambamba na kuweka malengo katika masomo yao ili waweze kufanikiwa huku akiwataka kutokata tamaa katika masomo yao

"Mwanafunzi yeyote yule unatakiwa kuwa na malengo,hujaja shuleni kutembea Wala kukua weka malengo kuwa unataka kuwa nani na hakikisha unapambania malengo yako kwa kuweka mikakati sahihi", alisema Bi. Neema.


Kwa upande wake  mkufunzi kutoka  chuo cha Afya Kisare Mwl. Restuda Murutta amewaasa wanafunzi hao kuzingatia elimu ya afya ya uzazi sambamba na kuepuka vishawishi vitakavyo waingiza katika kufanya mapenzi katika umri mdogo na mwisho kupelekea ndoa za utotoni. 

“Inasikitisha binti ana umri chini ya miaka 18 ameshaanza kujiingiza kwenye mahusiano ya ngono kitu ambacho sio salama, kabla ya kuingia kwenye mambo hayo kwanza jiulize je ni umri sahihi wa kuingia kwenye Mambo hayo ukishapata jibu acha" alisema Bi. Restuda.

Nao miongoni mwa wanafunzi waliopata mafunzo hayo ameishukuru kampuni ya Grumeti Fund kwa namna wanavyowajali na kuwathamini mabinti  na kuahidi kuyaweka katika vitendo mafunzo hayo na kusambaza elimu kwa wengine.

Awali kongamano hili lilitanguliwa na kongamano la vijana wa kiume takribani 634 kutoka shule za Sekondari Tirina,Chamriho na Hunyari ambapo Bi. Frida Mollel Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii kutoka Grumeti Fund amesema baada ya jamii kuwekeza nguvu kubwa katika kutoa Elimu kwa watoto wa kike imefanya watoto wa kiume kusahaulika ndipo Grumeti Fund katika kuleta usawa katika hilo ikaamua kuanzisha makongamano kwa watoto wa kiume ili kujenga jamii shirikishi na yenye usawa na kawaasa vijana kutokuiga tabia na tamaduni za kigeni zinazoweza kuharibu kabisa thamani yao na maisha yao kwa ujumla sambamba na kushiriki katika kutokomeza Mila na desturi kandamizi kwa watoto wa kike. 

Naye aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo Ndg. January Kizumba ambaye ni Afisa Elimu Sekondari kwa upande wa taaluma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda akawataka vijana wa kiume kusisitiza usawa katika jamii sambamba na kuwekeza nguvu katika masomo yao ili kuleta mapinduzi katika jamii.


  "Nyie ndio kizazi cha kesho hivyo tunatarajia,ili tuwe na jamii yenye usawa ni lazima tuwaelimishe pande zote mbili ili muwe na uelewa juu ya Mambo yakijisia maana yake tutajenga jamii endelevu na yenye usawa" ,alisema Kizumba.

Kwa takribani miaka saba kampuni ya Grumeti Fund imekuwa ikitoa elimu ya kijinsia kwa wanafunzi wa kike na kiume katika shule za sekondari mbalimbali Wilayani Serengeti na Bunda ambapo tangu mwaka 2017 hadi awamu hii ya pili  ya kongamano hili kwa Mwaka 2024  imefanikiwa kutoa elimu ya kijinsia kwa wasichana 11,796 na kutoa taulo za kike kwa kila binti anayeshiriki mafunzo hayo, huku ikifanikiwa kutoa mafunzo kwa wavulana zaidi ya 4,629 tangu mwaka 2021 hadi awamu hii  ya kongamano la Mwaka 2024 na kutoa zawadi za jezi na mipira  kwa kila shule iliyoshiriki kwenye kongamano.

Share:

CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO CHATUMIA MAADHIMISHO YA ELIMU,UJUZI NA UBUNIFU KUTANGAZA FURSA

Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga kimeshiriki maadhimisho Kitaifa ya Elimu, ujuzi na ubunifu yanayofanyika jijini Tanga kwenye viwanja vya Shule ya sekondari ya Popatlal.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo Mkuu wa Chuo hicho Paschal Shiluka amesema Serikali imeboresha maonesho ya mwaka huu, yamekuwa na utofauti mkubwa kwa kuchanganya vyuo vikuu na vyuo vya kati nchi nzima,lakini pia kutoa chachu ya kutamani kupandisha hadhi vyuo vya kati na kuwa vyuo vikuu.

Akizungumzia mafanikio wanayoyapata kupitia maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka kwa mikoa tofauti, amesema kubwa zaidi ni kujifunza kutoka kwa wengine walioshiriki,kuonesha ubunifu na ujuzi wanaotumia kufundisha fani za Afya vyuoni pamoja na kujitangaza kwa kuwa wanakutana na watu wapya wengi.

Ameeleza mafanikio mengine waliyopata kama Chuo tangu walivyoanza kushiriki maonesho mwaka 2022, ambapo mwaka 2023 Kwa maonesho yaliyofanyika jijini Arusha waliibuka washindi namba tatu katika vyuo vya Afya vya kati nchini.

Kwa upande wake Afisa masoko wa chuo hicho Josephine Charles amesema mbali na kozi za awali za Uuguzi na Ukunga, Maabara, Utabibu na Famasia kwa sasa Chuo chao kimepata kibali cha kuongeza kozi mbili za Radiology na Physiotherapy ambazo zitaanza mwaka huu, hivyo ametumia nafasi hiyo kuwataarifu wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na wenye ufaulu wa masomo ya sayansi kuanzia alama D 4 wanaweza kutuma maombi kupitia tovuti ya chuo www.kchs.ac.tz au kupiga simu namba 0742 155 623 au wanaweza fika chuoni.

Amedokeza kuwa kwa wanafunzi wenye sifa ya kujiunga na kozi za Maabara, Radiology na Physiotherapy wanaweza omba mkopo serikalini kwa kuwa Serikali ilishatoa fursa hiyo ya mikopo kwenye vyuo vya kati kwa wanafunzi wa kozi hizo.

Aidha maadhimisho ya mwaka huu yalianza tangu 25 May 2024 na yatahitimishwa 31 May 2024,ambapo yamefunguliwa na Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda yakiwa yanaongozwa na kauli mbiu isemayo Elimu, ujuzi na ubunifu kwa uchumi shindani.
Mkuu wa Chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga Paschal Shiluka akizungunza na waandishi wa habari.
Afisa masoko wa chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga akizungumza na waandishi wa habari Tanga.


Share:

Tuesday, 28 May 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 28, 2024


Share:

UPOTOSHAJI WA VIVUKO KIGAMBONI UNA MASLAHI BINAFSI: WAZIRI BASHUNGWA


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewatoa hofu Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam wanaotumia usafiri wa vivuko eneo la Kigamboni -Magogoni juu ya taharuki kuhusu huduma inayotolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) nakueleza kuwa imetengenezwa na watu wenye maslahi binafsi.

Ameyasema hayo leo Mei 28, 2024 wakati alipokuwa akifanya mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambapo amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha inaimarisha huduma ya usafiri wa vivuko nchini.

"Niwatoe wasiwasi Wananchi wa Dar es salaam pamoja na kigamboni, taharuki ambayo imetengenezwa hakukuwa na sababu ya kutengenezwa. Lakini sisi tunaofahamu yapo maslahi binafsi nyuma ya utengenezaji wa hii taharuki" Amekaririwa Bashungwa

Ameeleza kuwa sasa vivuko vingi vinaendelea na matengenezo, lakini pia Mkandarasi Songoro Marine anaendelea na ujenzi wa vivuko vipya katika karakana yake mkoani Mwanza kwa ajili yakupelekwa kwenye maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha, Bashungwa amesema kuwa tayari ameikutanisha TEMESA na Kampuni ya AZAM Marine na kujadili namna bora yakushirikiana kwa pamoja kuboresha utoaji huduma ya usafiri wa vivuko katika eneo la Magogoni - Kigamboni.

"Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan tumejipanga vizuri kuhakikisha tunaboresha vivuko na tutaweka machaguo kwa abiria ambapo watakuwa na chaguo. Ukitaka kutumia kivuko cha TEMESA sawa au ukitaka cha AZAM muda mchache kuvuka kwasababu zile ni ndogo siyo kama kivuko kikubwa ambacho unasubiri kupakia magari na abiria ili muweze kuondoka pamoja" Amesisitiza

Bashungwa amesema Wizara inatambua changamoto ya wananchi ni huduma bora ya vivuko nakusema kuwa kuanzia mwezi Agosti mwaka huu wataanza kutekeleza mpango huo utakaotoa wigo kwa wananchi kuchagua huduma wanayotaka kutumia.

"Wapo wanaotaka kushinikiza ili utaratibu na mwelekeo uende kama wanavyotaka wao, sisi hatuendi hivyo"amesema Bashungwa huku akisema kuwataja watu hao ni kuwapa sifa.
Share:

NMB YATOA FURSA KWA VIJANA WENYE BUNIFU MBALIMBALI HAPA NCHINI

MENEJA wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka  Ladislaus akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda ambapo alisema kwamba benki hiyo inatambua umuhimu wa ubunifu katika maendeleo ya nchi.
MENEJA wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka  Ladislaus kulia akifurahia Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda kushoto wakati alipotembelea banda lao wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo 



Na Oscar Assenga, Tanga.

BENKI ya NMB imeshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya elimu, ujuzi na ubunifu yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly huku wakitoa fursa kwa vijana wenye bunifu mbalimbali kwenda kufanya majaribio kwenye benki hiyo.

Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda ambapo alisema kwamba benki hiyo inatambua umuhimu wa ubunifu katika maendeleo ya nchi.

Alisema kwamba wao kama benki pamoja na ufadhili wanatoa Jukwaa Maalumu (Platfom) kuwakaribisha vijana kufanya ubunifu, maendeleo ya kibunifu na miradi hiyo wamekuwa wakiifadhili.

“Kwa niaba ya Benki ya NMB niwaambie kwamba tunatambua umuhimu wa ubunifu na ndio maana tumeungana nanyi katika wiki hii kwa kuwa elimu ndio inachochea ubunifu sisi kama Benki pamoja na mfadhili tunatoa jukwaa maalumu kuwakaribishasha vijana kuja kufanya ubunifu kufanya maendeleo ya kibunifu na miradi hiyo tunaifadhili”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba na inasaidia kuleta chachu ya kuendelela kuleta mendeleo ya ubunifu Tanzania hivyo wataendelea kuwaunga mkono kuhakikisha maendeleo ya sekta hiyo yanapiga hatua kubwa.

“Mh Waziri niwakaribiha vijana wenye bunifu mbalimbali waje kufanya majaribio yao kwenye benki ya NMB tuna platfomu NMB Sign Box nzuri inatoa nafasi nzuri ya bunifu tupo tayari kushirikiana nao kama Wizara kuhakikisha ubunifu unaleta chachu ya maendeleo ya kiuchumi hapa nchini”Alisema

Awali akizungumza wakati akifungua maadhimisho hayo Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda Serikali imesema ipo katika mchakato wa kujenga shule 100 za mafunzo ya Amali nyanja ya ufundi nchi nzima ili kuwawezesha vijana wa kitanzania kuweza kujiajiri au kuajiriwa kupitia ujuzi watakaopata kupitia vyuo hivyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Pastrobas Katambi amesema dunia ya sasa ina mabadikiko makubwa hasa kwenye masuala ya sayansi na teknolojia ujuzi na ubunifu hivyo ni wakati wa vijana wa kitanzania kwenda sambamba na mabadiliko hayo.

Awali Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Profesa Carolyne Nombo alisema wanafunzi 27 walishinda shindano la ujuzi na ubunifu ngazi ya vyuo ambao watafanyiwa mchakato na kupatikana wanafunzi 3 wa fani tofauti ambao watakwenda kushiriki mashindano ya kikanda na kimataifa mapema mwaka 2025.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko amesema bunifu zinazoibuliwa katika maeneo mbalimbali nchini zitengenezwe katika uhalisia ili kuleta tija kwa jamii na kiuchumi.

Mwenyeji wa maadhimisho hayo ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani alisema mkoa wa Tanga umepokea trilioni 2 na milioni 600 kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya elimu ambapo shule mpya 27 zimejengwa pamoja na vyuo vya kati ambavyo vipo katika hatua mbalimbali.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger