Sunday, 26 May 2024

KASEKENYA AIPA TANROADS WIKI MOJA MALINYI KUFIKIKA




Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro kuhakikisha anarudisha Mawasiliano ya barabara kati ya wilaya ya Ifakara na Malinyi katika kijiji cha Misegese, mkoani humo ili kuruhusu magari kupita mara baada ya daraja la Mto Fulua kuharibika kutokana na mafuriko.

Kasekenya ametoa agizo hilo Mei 25, 2024 wakati alipowasili wilayani Malinyi mkoani humo kukagua miundombinu ya barabara na madaraja iliyoathiriwa na mvua za El-Nino ambapo amesisitiza kuchukuliwa kwa hatua za haraka kurekebisha miundombinu hiyo ambayo ni kiungo muhimu kwa wilaya hizo mbili.

"Nakupa wiki moja, hakikisha hadi kufikia Jumamosi ijayo magari yawe yanapita hapa, Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kujenga daraja la kudumu katika eneo hili pamoja na kuijenga barabara yote kwa kiwango cha lami", amesema Kasekenya.

Aidha, Kasekenya amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha za matengenezo ya dharura katika miundombinu iliyoathiriwa na mafuriko ili kurejesha mawasiliano katika maeneo hayo.

Kadhalika, Kasekenya ametoa rai kwa wananchi kutokufanya shughuli za kibinaadamu ikiwemo kilimo karibu na mito kwani hali hiyo huathiri mabadiliko ya tabia nchi na kusabisha mito kuhama na hivyo kuharibu miundombinu ambayo hujengwa kwa gharama kubwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba, ameipongeza TANRAODS Mkoa wa Morogoro kwa kuendelea kukarabati na kuweka Makalvati katika daraja la mto Fulua ili kurejesha mawasiliano katika eneo hilo ambalo liliathiriwa na mvua za El-Nino zilizonyesha mwaka huu.

Ameeleza kuwa kwa sasa magari hayawezi kupita kutoka Njia panda kwenda Malinyi Mjini kutokana na maji kukata barabara kwa mita 100 hivyo uongozi wa wilaya kwa kushirikiana na wananchi wamejenga daraja la muda ambalo linaruhusu kupitisha watumiaji wa njia ya miguu, baiskeli na pikipiki tu.

Naye, Meneja wa TANROADS, Mkoa wa Morogoro, Mhandisi, Alinanuswe Kyamba amemhakishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa tayari wamejipanga na wameanza kurejesha mawasiliano kuanzia eneo la Lupilo na kusisitiza kuwa wataendelea na kasi zaidi ili kurejesha mawasiliano eneo hilo ndani ya muda walioagizwa.

*Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi*

Share:

DAWA HII ITAKUSAIDIA KUTATUA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME



Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu ,shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu. Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;

1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo

2. Kuvuta sigala na unywaji wa pombe

3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi

4. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

5. Kisukari

6. Kuwa na mawazo na wasiwasi

7. Matumizi ya madawa mbalimbali

8. Umri hasa wazee

9. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili

10. Kuwa na tatizo la kibofu

11. Tabia za kujichua kwa muda mrefu

12. Kutopata usingizi kamili

13. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine

DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Dalili za kuonesha kuwa una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume karibia zote zinahusiana na hali itakayo onekana katika tendo la ndoa au mda wa kujamiiana, hizo dalili zake ni kama;


1. Kuwahi kufika kileleni

2. Kukosa hamu ya mapenzi

3. Kushindwa kurudia tendo la ndoa

4. Uume kusimama kwa ulegevu au kushindwa kusimamisha

5. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu; Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo

7. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)

8. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji


TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

FULL POWER
⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.


ZAT 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonda vya tumbo, Kisukari, Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kung’oa


Ndugu mteja Epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahihi kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27 au 0754568767  utatumiwa sehemu yoyote ulipo
Share:

Video Mpya Kali Kinoma!! NG'WANA KANG'WA - TABASAMU


Ng'wana Kang'wa anakualika kutazama video yake mpya inaitwa TABASAMU!! Bonge la ngoma mtu wangu!! Usiache kutabasamu hata kama una matatizo mengi kiasi gani
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 26, 2024

Share:

Saturday, 25 May 2024

SERIKALI YADHAMIRIA KUKAMILISHA MIPANGO SITA YA USALAMA WA CHAKULA NCHINI

Mkurugenzi wa masoko na Usalama wa chakula kutoa wizara ya kilimo Gungu Mibavu akizungumzia jambo wenye mkutano huo

Na Christina Cosmas, Morogoro

SERIKALI imedhamiria kukamilisha mipango sita ya malengo endelevu ya suala la usalama wa chakula nchini kupitia Maendeleo ya Milenia (SDG) ya mwaka 2021/30 kabla ya mwaka 2030.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa masoko na usalama wa chakula kutoka Wizara ya Kilimo Gungu Mibavu wakati akifungua mkutano wa wadau wa masuala ya kilimo ulioandaliwa na Shirika la Kilimo na chakula (FAO) na kufadhiliwa na UN na kufanyika mkoani Morogoro.

Mibavu ameitaja baadhi ya mipango hiyo sita ya usalama wa chakula nchini kuwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula, mifugo na uvuvi na kuongeza uhakika na ziada ya chakula nchini.

Mibavu anasema asilimia kubwa ya mipango ya usalama wa chakula nchini imeshakamilika.

Mratibu wa uhimilivu wa mifumo na chakula kutoka Zanzibar Sihaba Vuai amesema serikali katika Kufanya mageuzi ya chakula imeweka kipaumbele kwenye mazao ya kilimo sambamba na kushirikisha  wadau wa kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Washiriki wakimsikiliza mtoa mada hayupo pichani
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Share:

MWANACHAMA CCM ASHAURI ZOEZI LA UPIMAJI ARDHI KATIKA VIJIJI LIHARAKISHWE

 



Na Okuly Julius,  Dodoma 


Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka Wilaya ya Muheza mkoani Tanga ,  Ndg. Hamisi Sadick Rajabu ameishauri Serikali kuharakisha zoezi la upimaji wa Ardhi katika vijiji ili kutimiza adhima ya CCM kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani kuhakikisha vijiji vyote viwe vimeshapimwa hadi kufikia 2025.

Ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari Mei 24 , 2024  katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, mara baada ya kushuhudia uwasilishwaji wa Bajeti ya  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Ameishauri Serikali kuongeza Fedha ili kuhakikisha zoezi hilo linaharakishwa kwani kwa sasa linaonekana kusuasua

"Serikali inafanya jitihada kubwa sana ya kuhakikisha inamaliza migogoro ya ardhi kwa hilo nalipongeza na kufanya hivyo ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi na ilani hiyo pia ilielekeza ifikapo 2025 ardhi katika vijiji vyote iwe imepimwa hivyo nitumie fursa hii kama mwanachama wa CCM kuishauri serikali iharakishe zoezi hilo kwa kuongeza fedha katika eneo hilo la upimaji ardhi," ameleeza Hamisi


Amesema kwa mjadala huo wa bajeti ya Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaonesha dhahiri malengo ya serikali ni kutaka wananchi wake wamiliki ardhi na kuishi katika mazingira salama na kuondoa kabisa migogoro ya ardhi ila kuhakikisha jamii inanufaika na matumizi ya ardhi.


Share:

Friday, 24 May 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 25, 2024

Share:

TANROADS KUWEKA KAMBI BARABARA YA KIRANJERANJE-RUANGWA KUREJESHA MAWASILIANO


Huenda Adha ya usafiri na usafirishaji bidhaa inayowakabili wananchi wanaotumia barabara ya Kiranjeranje kwenda Ruangwa ikafikia tamati baada ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Lindi kutangaza kutia kambi eneo hilo ili kuhakikisha njia inapitika.

kambi hiyo inalenga kuondoa taabu wanayokutana nayo wananchi kwa sasa katika usafirishaji wa bidhaa wanazozalisha na hata wasizozalisha kutokana na kulazimika kutumia bodaboda kwani hakuna gari inayoweza kupita.

Hayo yamewekwa Bayana na Meneja wa Tanroads mkoa wa Lindi, Emil Zengo alipokuwa akieleza mikakati waliyonayo katika urejeshaji wa mawasiliano yote yaliyokatika ndani ya mkoa.

Zengo amesema barabara hiyo ina umuhimu mkubwa kwa watu wa Ruangwa na maeneo jirani ikiwemo Nanjirinji kwani ni wakulima wazuri wa ufuta, mbaazi na hata uchimbaji wa madini mbalimbali.

Barabara hiyo ni miongoni mwa zilizoathiriwa na mvua kubwa zilizonyesha nchini za El-Nino zilizofuatiwa na mvua zilizosababishwa na Kimbunga Hidaya.

“Mvua za El- Nino zilibeba daraja katika mto Ngurukuru na kukata mawasiliano kati ya Namichiga na Kilanjelanje,” amesema Zengo.

Amesema kambi watakayoiweka itakuwa kubwa huku wakiomba Serikali kuwaongeza nguvu ili waweze kuhakikisha barabara zote zinapitika muda wote.

“Kwa sasa barabara hii ina maeneo ambayo mvua zinaponyesha yanajaa maji kwa wingi na kuna maeneo ambayo yanahitaji kujengwa madaraja, bajeti ya Serikali itakaporuhusu kama TANROADS tuko tayari kwa muda wowote utakaohitajika kujenga miundombinu ya makaravati na madaraja ili barabara hii iweze kutumika muda wote,” amesema Zengo.

Kufanya hivyo kutasaidia kuunganisha wilaya ya Kilwa Masoko na Ruangwa na kuwawezesha wananchi kusafirisha mazao yao na kupata chakula ambacho hawawezi kulima

“Pia waweze kusafirisha madini mbalimbali ambayo yanapatikana kwa wingi sana katika eneo hili, kwa kuzingatia umuhimu wa eneo hili, sisi kama Wakala wa barabara Tanroads Lindi tuko tayari kusimamia matengenezo ya muda mfupi na muda mrefu yanayohutajika,” amesema Zengo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger