Friday, 5 April 2024

BENKI YA CRDB YAKABIDHI MADAWATI URAMBO

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi,  Jumanne Wambura Wagana (kushoto) akimkabidhi madawati Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mh. Eribariki Bajuta.
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Ndg Jumanne Wambura Wagana amekabidhi madawati 50 kwa mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe.  Elibariki Bajuta ikiwa ni mwendelezo wa benki hiyo ya CRDB katika kutekeleza sera yake ya uwekezaji kwa jamii lakini kuunga mkono jitihada za Serikali kwenye sekta ya elimu wilayani Urambo. 

Akipokea Madawati hayo Aprili  4,2024, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Elibariki Bajuta ambaye aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo , Wakuu wa Idara wa Halmashauri pamoja na viongozi wengine ameishukuru sana Benki ya CRDB kwa msaada huo mkubwa na kuahidi kuendelea kuwapa mashirikiano makubwa zaidi kibiashara.



Share:

WANAFUNZI WANAOTARAJIA KUHITIMU KIDATO CHA SITA WAHIMIZWA KUTUMIA VYEMA ELIMU WALIYOIPATA



Wanafunzi wanaotarajia kuhitimu   masomo ya kidato cha Sita katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamehimizwa kutumia elimu waliyoipata shuleni kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka na kujiepusha na makundi yasiyofaa hasa wakati watakaokuwa wakisubiri matokeo ya mitihani yao.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Bukoba Mjini James Nyamanza wakati alipokuwa mgeni Rasmi katika Mahafari ya Kidato cha Sita ya  Umoja wa Wanafunzi Wasabato  Kanda ya Bukoba Mjini(ASSA) yaliyofanyika shule ya Sekondari Nyakato.

Nyamanza amewahimiza wanafunzi hao wanaotarajia kufanya mitihani yao ya kuhitimu kidato cha sita kuhakikisha elimu waliyoipata inakuwa chachu ya maendeleo katika jamii zao na sio kwenda kuwa kikwazo kwa kujiingiza katika makundi yasiyofaaa wakati watakaokuwa wakisubiri matokeo ya mitihani yao.

Amesema kuwa walimu wao wametumia muda mwingi kuhakikisha wanapata elimu hiyo lakini pia wazazi wametumia gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wanatakiwa kuwa mfano mzuri kwenye jamii na kuwa mfano bora wa kuigwa na wanafunzi wengine wanaoendelea na masomo.

Katika mahafali hayo mgeni Rasmi  aliendesha Harambee kwa kushirikiana na Wazazi,Viongozi wa dini, Walimu na Wageni waalikwa  ambapo katika harambee  hiyo kiasi kilichopatikana kilielekezwa   kukarabati  Kanisa lililopo jirani na shule ya Sekondari Nyakato.

Mahafali hayo yameshirikisha shule zote za Sekondari zenye wanafunzi Wasabato ambao wameshiriki kwa pamoja kuwaaga wanafunzi wenzao wanaotarajia kuhitimu kidato cha Sita  ikiwemo shule ya Sekondari Nyakato, Ihungo, Kahororo,Rugambwa, Kagemu,Bukoba Sekondari, Mugeza, Buhembe, Maruku na Bakoba.



Share:

Thursday, 4 April 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 5,2024

Share:

DCEA YAFANIKIWA KUKAMATA JUMLA 54, 506.553 KG YA DAWA ZA KULEVYA

 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.

*****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imefanikiwa kukamata Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya aina ya methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema Methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) ni dawa mpya ya kulevya iliyo katika kundi la vichangamshi inayotengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu.

"Dawa hii ina kemikali inayoweza kuleta madhara ya haraka kwa mtumiaji ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya. Pia, imeongezwa nguvu ya kilevi inayozidi cocaine, heroin na methamphetamine". Amesema

Amesema, dawa hiyo ya kulevya huuzwa kwa njia ya mtandao (internet) na husafirishwa kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi na hufichwa kwa kuwekwa chapa za majina bandia kama vile bath salts, Ivory Wave, plant fertilizer, Vanilla Sky, na Energy.

Aidha amesema wamefanikiwa kukamata jumla ya Kilogramu 54,506.553 za dawa za kulevya za mashambani na viwandani pamoja na kuteketeza ekari 262 za mashamba ya bangi.

Amesema watuhumiwa 72 wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na baadhi yao tayari wamefikishwa mahakamani.

"DCEA kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wakala wa misitu (TFS) tulifanya operesheni katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Iringa, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata dawa hizi". Amesema.

Amesema dawa zilizokamatwa ni bangi kilo 54,489.65, mirungi Kilogramu 10.3, heroin gramu 90.93, cocaine gramu 1.98 na Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya inayoitwa methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32).
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Share:

Ngoma Mpya : BHUDAGALA MWANAMALONJA - NZUNA WANE


Hii hapa ngoma Mpyaa kabisa ya Bhudagala Mwanamalonja inaitwa Nzuna Wane
 
Share:

DKT. TAX AELEZA MAFANIKIO YA WIZARA YAKE KWA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA MUUNGANO





 Na Dotto Kwilasa,DODOMA

WAZIRI Wa  Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Dkt. Stergomena Tax , amesema wizara yake kupitia JWTZ imechangia katika kulinda mipaka ya nchi pamoja na kujenga uchumi imara ambao umepelekea wananchi hujishughulisha na  uzalishaji mali bila hofu.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi Wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60  ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Amesema kwa kipindi cha miaka 60 ya muungano Serikali kupitia Wizara  hiyo imeendelea kutekeleza, na kuliimarisha Jeshi kwa kulipatia zana na vifaa bora na vya kisasa, rasilimali watu, na nyenzo za kufanyia mazoezi ili kuwa imara wakati wote.

"Mchango mwingine mkubwa wa Jeshi hilo  katika miaka 60 ya Muungano, ni ulinzi madhubuti wa mipaka yetu, uhuru, na katiba. Nchi imeendelea kuwa imara na yenye amani katika awamu zote;

Pia , katika miaka 60 ya Muungano, Wizara ya Ulinzi na JKT  Pamoja taasisi zake zimeendelea kufanya na kuendeleza tafiti na uhawilishaji wa teknolojia kwa ajili ya kuzalisha bidhaa na huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia, "ameeleza Waziri huyo wa ulinzi. 

Licha ya hayo ametaja mafanikio mengine ya muungano kuwa ni pamoja na Serikali kuanzisha viwanda vya kijeshi likiwemo shirika la Tanzania Automotive Technology Centre (TATC) maarufu kama NYUMBU, pamoja na Shirika la MZINGA. 

"Katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, serikali kupitia wizara ya Ulinzi na JKT, imeendeleza pia kudumisha uhusiano na mataifa mbalimbali duniani, kupitia mafunzo na mazoezi ya kijeshi, misaada ya kitaalam, vifaa, zana na mitambo,

Pamoja na hayo tumefanikiwa pia kupitia ubadilishanaji wa wataalam, ubadilishanaji taarifa za uhalifu unaovuka mipaka, shughuli za ulinzi wa amani, mapambano dhidi ya ugaidi, uharamia baharini, uvuvi haramu, na usafirishaji haramu wa binadamu, .


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger