Friday, 22 March 2024

CCM YAWAPONGEZA WANANCHI BAADA YA USHINDI WA UCHAGUZI WA MADIWANI KATA 23


Share:

JESHI LA POLISI TANGA LAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA 35 KWA MAKOSA MBALIMBALI




Na Oscar Assenga, TANGA

JESHI la Polisi Mkoani Tanga katika kuhakikisha wanaendelea kudhibiti uhalifu wamefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa (35) ambapo wamehukumiwa vifungo mbalimbali.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi alisema watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani na kuhukumiwa vifungo mbalimbali ni.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni wa makosa ya kubaka, ulawiti, wizi na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani ambapo watuhumiwa 20 walipatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo gerezani.

Kamanda Mchunguzi aliwataka waliohukumiwa vifungo vya maisha Jela ni Deogratius Alex (22), Samwel Ghamuga (25) wote kwa kosa la kubaka na Athumani Rajabu (19) akihukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti huku Anthony Agunstino na Twaha Rajabu wakihukumiwa miaka (30) jela kwa kosa la kubaka.

Aidha aliwataja watuhumiwa wengine ambao ni Omari Mganga na Hussein Amiry (41) wamehukumiwa kifungo cha miaka nane jela kwa kosa la wizi pamoja ana Salim Jumbe ambaye amehukumiwa miaka 27 jela kwa kosa la kubaka.

Akizungumzia kwa upande wa makosa ya usalama barabarani madereva wawili wameondolewa madaraja kwenye leseni zao za udereva na 1 amefungiwa leseni ya udereva ambapo wengine wamelipa faini mahakamani kwa makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.

Hata hivyo Kamanda Mchunguzi alisema ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia mwezi February 21 hadi Machi 21 Jeshi hilo katika Operesheni ya kuimarisha doria na misako wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 94 wakiwa na makosa mbalimbali ikiwemo makosa ya uvunjaji,mauaji,kujeruhi,kusafirisha wahamiaji haramu,kuharibu mali pamoja na kupatikana na silaha sita aina aya Gobole.

Mwisho.

 

Share:

ORXY GAS YAKABIDHI MITUNGI YA KUPIKIA 700 KWA WAJASIRIAMALI FERI


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mmoja wa mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.


***************

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

NAIBU SPIKA wa Bunge Hassan Zungu, amewahakikishia Mama Lishi na Baba lishe katika Soko la Samaki la Kimataifa Feri kuwa watafungiwa mtambo wa nishati safi ya kupikia ili kuwaepusha kutumia fedha nyingi kununua gesi kupitia mitungi midogo.

Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kulinda mazingira kuwaweka wanawake katika nafasi nzuri ya kujiendeleza kiuchumi.

Zungu alisema hayo leo sokoni hapo, jijini Dar es Salaam wakati wa kugawa mitungi 200 kati ya 700 iliyotolewa kwa Mama na Baba lishe hao ambayo imetolewa kwa ushirikiano wa Zungu na kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania.

Naibu Spika Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, alitoa ahadi hiyo baada ya kupokea maombi ya wafanyabiashara hao kupitia kwa kiongozi Zone Namba 7 katika soko hilo, Said Mpinji aliyelalamika kuwa wanalazimika kutumia sh. 110,000 kila siku kujaza gesi ya kuendeshea shughuli za baba na mama lishe.

Akijibu kilio hicho, Zungu alisema ni cha muda mrefu na kwamba tayari amezungumza na kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake, Benoit Araman ambaye amekubali kufunga mifumo ya gesi ya kisasa kasha kusambaza huduma hiyo kwa wafanyabiashara hao kwa gharama nafuu.

“Mkombozi wetu ni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye alianzisha kampeni ya nishati safi ya kupikia, kuhakikisha Watanzania wanaishi maisha mazuri.

“Oryx wamekubali kuweka mtungi mmoja mkubwa na mifumo ya usambazaji, kasha watasambaza huduma kwa mama na baba lishe waliopo hapa na kuwafungia mita halafu watakuwa wakilipia huduma kama wanavyofanya katika umeme,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Gesi ya Oryx Benoit Araman alisema Oryx wamewafikia wajasiriamali hao kwa lengo la kutekeleza mkakati wa Rais Dk. Samia wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kulinda mazingira na afya za wananchi.

Alisema kuwa tangu Julai mwaka 2021, walianza mkakati huo baada ya Rais Samia kutangaza kwamba serikali yake inataka kuona hadi mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Wakati huohuo Mwenykiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abbasi Mtemvu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema kilichofanyika ni utekelezaji wa Ilani na kumpongeza Zungu kwa namna anavyowatetea wananchi katika jimbo lake.

“Zungu ni mfano wa kuigwa, amefanya makubwa. Nimekuwa naye bungeni kwa miaka 10 muda wote ameonyesha dhamira ya kutetea wananchi wa jimbo lake, anastahili pongezi,” alisema.

Aliipongeza serikali kwa kuendelea kupeleka maendeleo kwa wananchi huku akiwataka mama na baba lishe wa sokoni hapo kujiandaa kupokea mitaji kutoka serikali ili kunua biashara zao.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Meneja Mauzo wa Kampuni ya Gasi ya Orxy , Shaban Fundi (wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Zone no.7 wa Soko la Samaki la Kimataifa Feri Jijini Dar es Salaam, Saidi Mpinji wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kulia).
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Happy Kiondo wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Salma Mohammed wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu ( kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gesi ya Orxy, Benoite Araman wakiwasikiliza wafanyabiashara wa samaki katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu ( kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gesi ya Orxy, Benoite Araman katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.


Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Baadhi ya wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali hao, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Gesi ya Orxy Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy katika hafla ya makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Share:

Thursday, 21 March 2024

RAIS DKT. SAMIA APONGEZWA KUENDELEZA MIRADI YA KIMKAKATI

NA MWANDISHI WETU

MWANZA. Rais Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa juhudi kubwa anazozionesha za kuruhusu kuendelea ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo inayotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq, wakati wajumbe wa kamati hiyo walipofanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa hoteli ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo Jijini Mwanza, tarehe 18 Machi, 2024.

“Nimpongeze sana Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mradi huu ulikuwa umesimama kwa muda mrefu, lakini alipoutembelea mwezi Juni 2023, aliwatia moyo na kuwataka NSSF waendelee na mradi huu, akijua utakuwa na tija kwa wananchi wa Mwanza na mikoa ya jirani na kuongeza mapato kwa Serikali,” amesema Mhe. Fatuma.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Mhe. Neema Mwandabila (Mb), amempongeza Rais, Dkt. Samia kwa uamuzi wake wa kuruhusu miradi iliyosimama iendelee kutekelezwa. Aidha, ameipongeza NSSF kwa ujenzi wa mradi huo kwani Mkoa wa Mwanza unauhitaji wa hoteli ya aina hiyo.

Naye, Mhe. Mwita Getere (Mb), amesema NSSF ina nidhamu ya hali ya juu hasa katika kutekeleza miradi ya uwekezaji ukiwemo wa hoteli ya nyota tano iliyopo Jijini Mwanza.

Mhe. Mariam Kisangi (Mb) amempongeza Rais, Dkt. Samia kwa kuhakikisha miradi iliyosimama inatekelezwa na kuwa mradi huo wa hoteli utaleta manufaa kwa NSSF, jamii na Taifa kwa ujumla.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye aliridhia mradi huo uendelee baada ya kusimama kwa muda mrefu.

Mhe. Profesa Ndalichako amesema mradi huo ulianza tarehe 1 Novemba, 2013 na ulipangwa ukamilike ndani ya miaka mitatu, lakini kutokana na changamoto mbalimbali zilizotokea mradi utakamilika tarehe 30 Desemba, 2024.

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa maoni na michango yao ambayo wameichukua na wataenda kuyafanyia kazi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema upo mpango wa kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza ili iwe rahisi watalii kupita kwa wingi na kuiwezesha hoteli hiyo kupata wageni wengi.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba amesema Mfuko unaendelea kutekeleza majukumu yake mbalimbali, ambapo kwa upande wa ulipaji wa mafao ya wanachama, wanalipa kiasi kikubwa zaidi ya kile ambacho mwanachama amechangia na ndio maana wanafanya uwekezaji wenye tija.
Share:

Wednesday, 20 March 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 21, 2024





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger