Wednesday, 20 March 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 21, 2024





Share:

KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI YABAINI KASI NDOGO YA MKANDARASI TONTAN USAMBAZAJI UMEME VIJIJI 146 KAHAMA, CAG WAPIGILIA MSUMARI



Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Hesabu za Serikali (PAC) imefanya ziara ya kukagua miradi ya umeme Mkoani Shinyanga ambapo imeonesha kutoridhishwa na kasi ujenzi na usambazaji wa miundombinu ya umeme katika vijiji 146 Wilaya ya Kahama unaotekelezwa Kampuni ya Tontan Project Technology Co. Ltd Jv Group Six International kupitia Mradi wa Uwekezaji wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili(REA III awamu ya pili).

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ngongwa kata ya Ngongwa Wilayani Kahama, baada ya wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Kahama, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga amesema kamati hiyo imeona mradi wa usambazaji umeme vijijini umecheleweshwa Kahama.

Jambo ambalo tumeliona sisi hapa ni kwamba huu mradi umecheleweshwa na wananchi yale malengo yaliyokusudiwa bado hayajafikiwa. Sisi tutapima thamani ya fedha zaidi ya Bilioni 46 ambazo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kwa ajili ya Wilaya ya Kahama kwa ajili ya umeme pale ambapo wananchi wale ambao tulitarajia waunganishiwe umeme watakuwa na umeme, wananchi wanataka umeme. Kwa hiyo sisi kama kamati tutaenda kulisimamia”,amesema Hasunga.


Kamati imepewa ahadi ni kwamba watahakikisha kwamba mradi unakamilika ifikapo Aprili 30,2024 maana yake tuna mwezi mmoja. Na moja ya hatua zilizochukuliwa na REA watahakikisha kuwa wazabuni ambao walikuwa wanaogopa kumpelekea Mkandarasi kwa sababu hawalipi, sasa REA imechukua jukumu na imewahakikishia wazabuni wa kusambaza vifaa walete vifaa watalipwa. Hivyo hatutegemei hapo kuona ucheleweshaji, sasa kazi ya mkandarasi ni kuweka rasilimali watu ili kuona mambo yanakwenda”,ameongeza Mhe. Hasunga.

Aidha amesema Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuanzia Mei 2,2024 na kuendelea itaenda kwa wananchi wa Kahama kuangalia kama wameunganishiwa umeme, na ndipo itakapotathmini na kupima kwamba thamani ya fedha ya zilizotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wilayani Kahama zimefanya kazi iliyokusudiwa, kama wananchi watakuwa hawajaunganishiwa umeme basi watamwambia kuwa fedha hizo zimetupwa.


Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Uwekezaji wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili mkoani Shinyanga, Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amesema mkoa wa Shinyanga una jumla ya vijiji 509 ambapo vijiji 262 vimepatiwa huduma ya umeme ambapo kwa upande wa Wilaya ya Kahama yenye vijiji 146 ambapo vijiji pekee 63 vimepatiwa umeme bado vijiji 83.

Ameeleza kuwa, Mradi wa REA III awamu pili Wilayani Kahama unatekelezwa na Mkandarasi Tontan Project Technology Co. Ltd Jv Group Six International ambaye mshauri ni Mercados Aries International uliosainiwa Oktoba 29,2021 na kuanza kutekelezwa Februari 14,2022 ukitarajiwa kukamilika Aprili 30,2024 unatekelezwa kwa gharama ya shilingi 46,092,316,042.58/=.


Hata hivyo, Mkaguzi Mkuu wa Nje Wizara ya Nishati, Nyamisi Bituro amesema Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kuwepo kasi ndogo ya ujenzi na usambazaji wa miundombinu ya umeme katika vijiji 146 Wilaya ya Kahama katika Mkataba wa REA na Kampuni ya Tontan Project Technology Co. Ltd Jv Group Six International kwa ajili ya ujenzi na usambazaji wa miundombinu, uwekaji wa transfoma pamoja na uunganishwaji umeme wa wateja (REA III awamu ya pili) kwa vijiji vya wilaya ya Kahama kwa kiasi. cha shilingi 46,092,316,042.58/= baada ya marejeo ya kuongeza mawanda ya wigo wa kazi.

Ukaguzi ulibaini uwepo wa marejeo ya kipindi cha kumalizika kwa mktaba ambapo muda wa mkataba uliongezwa kwa miezi minne hadi Desemba 31,2023 na kisha kurejewa tena kwa kipindi cha miezi minne hadi Aprili 30,2024”,amesema Bituro.

Hata hivyo, uhakiki wa ripoti za utekelezaji wa miradi uliofanywa mwezi Machi 2024 pamoja na uhakiki wa mradi ulibaini bado kuna kasi ndogo ya ukamilishwaji wa mradi ambaopo mradi umefikia 61.46% ikiwa umebaki mwezi mmoja tu wa kufikia ukomo wa mkataba. Hali hii inapelekea kuwanyima fursa wakazi wa vijiji vya wilaya ya Kahama ya kunufaika na nishati hii muhimu ya umeme kwa wakati”,ameongeza Bituro.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Balozi Meja Jenerali (Mstaafu) Jacob Kingu amesema REA  itahakikishia inasimamia kuchukua hatua za kisheria kwa Mkandarasi Tontan ili kuhakikisha anatekeleza mradi ndani ya muda uliopangwa.

Kuhusu Mkandarasi tutashughulika naye kuanzia baada ya kikao hiki kuhakikisha kwamba anaweka mambo yake sawa, asiwe mtu wa kunyoshewa vidole na yeye yupo hapa anasikia na mkataba unasimama Aprili 30,2024 na ndiyo maana REA imemuandikia Notisi lakini pamoja na hayo tu, tunataka wananchi wapate umeme, kwa hiyo ni kazi kazi atimize mradi katika muda uliopangwa", amesema.


Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amesema kucheleweshwa kukamilika kwa mradi huo kunakotokana na kazi za Mkandarasi kudorora kunasababisha viongozi wa siasa na serikali kuchonganishwa na wananchi kutokana na ahadi za mara kwa mara juu ya upelekaji umeme kwa wananchi.

Wananchi wanataka umeme na wanaona viongozi wanawadanganya kuwapa umeme wakati changamoto iliyopo ni Mkandarasi hana uwezo wa kukamilisha kazi kwa wakati, amekuwa akiongezwa muda wa kukamilisha kazi lakini hamalizi matokeo yake viongozi wanakosanishwa na Mkandarasi, viongozi wanaonekana wanasema uongo kwamba umeme utawafikia wananchi”,ameongeza Mhe. Mhita.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tontan Project Technology Co. Ltd Jv Group Six International, bw. John Zheng amesema miongoni mwa changamoto zinazosababisha wasikamilishe mradi kuwa ni ucheleweshaji wa vifaa kutoka kwa mzabuni na wizi wa vifaa katika eneo la mradi lakini watajitahidi kuhakikisha wanakamilisha mradi ndani ya muda uliopangwa ili wananchi waanze kunufaika na nishati ya umeme.

Nao wananchi akiwemo Thomas Welelo na Nshoma John wameiomba serikali jitihada za kumhamasisha Mkandarasi aongeze kasi ya kusambaza umeme vijijini.





Share:

NAPE ATEMBELEA KIWANDA CHA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI ARUSHA

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb), alitembelea kiwanda cha TANZTECH jijini Arusha na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Bw. Gurveer Hans.

Mhe. Nape amefanya ziara hiyo leo tarehe 19 Machi, 2024 na kujionea kiwanda cha kuunganisha vifaa vya kielektroniki kama simu janja, vishikwambi, kompyuta, na vifaa vingine vya kielektroniki.

Katika ziara yake, Waziri Nape amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa uwekezaji mkubwa waliofanya katika sekta ya mawasiliano ya simu. 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Gurveer Hans amesema kiwanda cha TANZTECH ni kiwanda cha kwanza nchini Tanzania kinachoendeshwa kwa ushirikiano na wachina ambao pia wamewekeza kwenye kiwanda kama hiki katika nchi za Uganda na Ethiopia.

Akielezea kuhusu kiwanda hicho, Bw. Hans amesema hivi sasa kiwanda hicho kimeanza kuunganisha simu janja 40,000 kwa mwezi, vishkwambi 30,000 kwa mwezi, laptop 15,000 na projector 10,000 kwa mwezi.

Bw. Hans ameiomba serikali kuondoa kodi ya mapato kwenye vifaa vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi na wakati wa kuuza vifaa hivyo vya kielektroniki ili kupunguza gharama za uzalishaji.

Waziri Nape amewapongeza kwa uwekezaji huo na kupokea maombi yaliyowasilishwa na uongozi wa kiwanda na kuahidi kuyafanyia kazi. Ameupongeza pia uongozi wa kiwanda cha TANZTECH kwa kuajiri wafanyakazi wazawa ambapo asilimia 90 ya wafanyakazi hao ni wanawake.



Share:

WATANZANIA WANAJIVUNIA MIAKA 3 YA UWEZO MKUBWA; NCHIMBI


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amesema kuwa Watanzania wote kwa ujumla wao wanajivunia uwezo mkubwa wa kiuongozi, anaouonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka 3 ya uongozi wake, ukijidhihirisha kwa namna anavyoiongoza nchi, kwa ajili ya maendeleo ya watu, ustawi wa jamii na kuimarisha utaifa nchini.

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi wa Kusini, unaoendelea katika siku yake ya pili, kwenye Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe, Jumanne, Machi 19, 2024, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Nchimbi, amesema Chama Cha Mapinduzi pia kinajivunia uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa jinsi anavyoendelea kuiongoza Serikali katika kutafsiri kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025, akisisitiza kuwa CCM na wanaCCM wanamuunga mkono bega kwa bega.

“Kabla sijaanza kuwasilisha hapa…kwa ruhusa yako Mwenyekiti wa Kikao, imekuwa kama bahati nzuri zilizogongana leo…naomba niwataarifu Wajumbe wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika kwamba leo ni maadhimisho ya mwaka wa tatu tangu Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposhika Madaraka ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka mitatu iliyopita.

“Kwa kweli ninajivunia sana Rais Samia Suluhu Hassan, si kwa sababu tu mimi ni mpigania haki za wanawake, bali kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa uongozi mzuri anavyoendelea kuiongoza nchi yetu ya Tanzania. Kutokana na hilo, Chama Cha Mapinduzi kinajivunia sana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na Watanzania kwa ujumla wetu tunajivunia sana kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwezo wake mkubwa ambao ameuonesha ndani yah ii miaka mitatu,” amesema Katibu Mkuu Balozi Dk. Nchimbi.

Dk. Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia wajumbe kuwa kutokana na kuwa mwanamajumui wa kweli wa Afrika, Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati kuimarisha na kuboresha uhusiano wa nchi na vyama rafiki katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na kwamba anafuatilia mkutano huo wa 11 wa Makatibu Wakuu wa vyama hivyo kwa ukaribu, huku pia akiwaomba wajumbe kuungana nae kumtakia kila la heri Mhe. Samia na kumuunga mkono, ombi ambalo lilipokelewa na kukubaliwa na wajumbe.
Share:

Tuesday, 19 March 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 20,2024

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger