Tuesday, 19 March 2024

MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA GEITA : PENEZA NI MCHUNGAJI MWEMA LAZIMA WAMFUATE WAFUASI WAKE



Na Joel Maduka,Geita

Kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa mhasibu wa kanda ya ziwa wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ,Upendo Furaha Peneza  na kurudi chama cha mapinduzi CCM , wanachama  481 wa vyama vya upinzani ambao walikuwa ni wafuasi wake wameamua kuungana naye pia na kujiunga na chama cha CCM.

Wanachama hao wamepokelewa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya GEITA, BARNABAS MAPANDE  kwenye viwanja vya Kata ya Kasamwa ambapo ndipo ulipofanyika Mkutano wa kuwapokea.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CCM wilaya BARNABAS MAPANDE amewataka wanachama hao kuwa na moyo wa uvumilivu na kuepukana na siasa za matusi ambazo zimekuwa aziwajengi watanzania.

“Ndugu zangu niwaambie ukweli kuwa Upendo Peneza anakuja na watu aliokuwa nao na mimi niwaambie ndugu zangu mchungaji mwema wa kondoo umfuata mchungaji wao sasa kwanini wengine wasimfuate Upendo Peneza”Barbabas Mapande Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita.

“Wale ndugu zetu wamekuwa na wasi wasi kuwa wataanikwa maovu yao nataka kuwaondoa shaka kuwa Peneza ajakulia kwenye familia ya matusi awezi kuwatukana wala kuwakashifu wao wawe na amani tu aliondoka amerudi Nyumbani sasa kwanini sisi tusimfanyie sherehe wao wawe wavumilivu tu Chama kipo kazini”Barnabas Mapande,Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya geita

 

Naye Upendo Peneza ambaye alijiunga na CCM Tar 22 January 2024 ,amesema kuwa yeye hayupo tayari kushiriki siasa za kuwadanganya watu na kwamba amekuwa siku zote akisimamia ukweli na kuachana na uongo.

“Niliona kundi nililokuwepo siliwezi na sikuwa tayari kuwaragai watanzania na kuonekana natumika kwenye kundi ambalo linasiasa zisizo za ukweli mimi ni mwanachama wa ccm nimechagua kundi hili sababu limekuwa likisimamia ukweli na mimi nitasema ukweli siku zote wala sitakaa kimya kwa hofu ya  kumuogopa mtu yoyote”Upendo Peneza Mwanachama wa CCM.

“Ninajua wengi watasema maneno mengi mimi kuhamia ccm nataka niwaambie mimi sikuongwa na mtu kuingia CCM ukweli wa dhati mimi ndio niliwatafuta viongozi wa Chama cha Mapinduzi na kuwaomba wanikaribishe CCM sasa mtu umeomba kweli utakuwa tena umeongwa tuachaneni na maneno ya uragai ambayo yanasemwa”Upendo Peneza Mwanachama wa CCM.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Chacha Wambura ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuwa tayari katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kukichagua chama cha mapinduzi CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji.

Share:

PROF. KABUDI- WAZAZI HIMIZENI WATOTO KWENDA SHULE KWA MANUFAA YAO YA BAADAE


Na Christina Cosmas, Morogoro

MBUNGE wa jimbo la Kilosa mkoani Morogoro Prof. Paramagamba Kabudi amewahimiza wazazi katika kijiji cha Kitange mbili kata ya Mtumbatu kuweka utaratibu wa kuwaruhusu watoto kwenda shule kwa manufaa yao na kuacha tabia ya kuwazuia na kusababisha kuwepo kwa idadi ndogo ya watoto walioripoti kuanza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari kitange.

Prof. kabudi ameyasema hayo katika ziara yake ya kukagua miradi ya shule ambapo amefika katika shule hiyo ambayo ujenzi wa vyumba vya madarasa unaendelea huku akiwataka wananchi hao kuhakikisha watoto wanakwenda shule ili kuunga mkono juhudi za serikali inayotoa fedha kwaajili ya ujenzi wa shule.

Shule hiyo mpya ya sekondari Kitange ujenzi wake ulianza mwaka 2022 kwa nguvu kazi ya wananchi baada ya wanafunzi kutembea umbali mrefu wa takribani zaidi ya kilometa 10 kufuata huduma ya shule ambapo hadi sasa ni madarasa mawili pekee ndio yaliyokamilika kwa hatua ya awali kwaajili ya wanafunzi kuanza masomo kwa kidato cha kwanza kwa mwaka huu wa 2024.

Akitoa taarifa ya mradi huo mkuu wa shule hiyo Cecilia Chipeta amesema Licha ya wananchi  kuanza kwa kujitolea nguvu kazi wadau na serikali haikuwaacha nyuma na sasa ujenzi wa vyumba vingine vya madarasa unaendelea huku akibainisha kuwa wanafunzi 84 pekee ndio walioripoti shule kati ya wanafunzi 198 wa kidato cha kwanza waliopangiwa katika shule hiyo.

Selina shayo ni katibu wa wazazi cha chama cha mapinduzi(CCM) wilaya ya kilosa anasikitishwa na taarifa hiyo ya watoto kutohudhuria shule na kuwahimiza wazazi kuona umuhimu wa elimu kwa watoto ikiwa ni Pamoja na kuwasaidia kujimudu katika maisha yao ya baadae.

Naye Diwani wa kata ya Mtumbatu Amani Sewando aliahidi kushirikiana na viongozi wa kijiji hicho  kutafuta wanafunzi ambao bado hawajaripoti shule na kuhakikisha wanaripoti shuleni.

Licha ya kutembelea shule hiyo ya sekondari kitange mbunge Prof. Kabudi amefanikiwa kukagua ujenzi wa shule ya sekondari Dumila ambayo ujenzi wake unagharimu takribani kiasi cha shilingi milioni 125 huku hadi sasa ambapo kiasi cha zaidi ya milioni 123 kikiwa kimeshatumika.
 

Share:

KAMATI YA PIC YARIDHISHWA NA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA TANGA UWASA








Na Oscar Assenga,TANGA

KAMATI ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeridhishwa na miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) huku wakizitaka mamlaka nyengine nchini kwenda kujifunza ubunifu ambao wanautumia katika kutekeleza miradi yao na hivyo kuwawezesha kuondoa changamoto hiyo kwa wananchi.

Hayo yalisemwa  na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Deus Sangu wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa na Tanga Uwasa ambapo wameridhishwa na miradi hiyo huku akiipongeza Serikali kwa namna inavyopeleka msukumo kwenye uwekezaji hasa kwenye sekta ya ya maji .

Alisema kamati hiyo imejionea shuguli uwekezaji na kuona ubunifu kamati imekagua mradi huo imerdhishwa na ubunifu huo huku kuwataka mamlaka nyengine ziweze kuiga mfano wa kuona namna ya kutatua changamoto ya maji katika maeneo yao.

“Mradi huu umetekelezwa kwa mkopo kutoka benki ya maendeleo asilimia 75 na sehemu inayobakia kama bilioni 3 ni makusanyo ya ndani hivyo mradi huu zaidi ya Bilioni 10 na umeleta mapinduzi makubwa sana kwa maana mahitaji ya maji jiji la Tanga lita milioni 45,000,000 “alisema

Aidha alisema wao kama kamati wameridhishwa na namna ambavyo Tanga Uwasa walivyoweza kubuni vyanzo vya kufadhili miradi yao na wameona mamlaka za maji wanategemea vyanzo kutoka serikali kuu lakini wao wenyewe wamebuni na kwenda kukopa fedha benki na mapato yao ya ndani wakaleta mapinduzi na kutatua changamoto ya maji karibunia takribinia asilimia 96.

Alisema pia kwanza kuja na hati fungani wamekuja na ubunifu wa kipekee kwa taaswanza Tanzania kuja na hati fungani ya kijani yenye thamani ya bilioni 53 itakayosaidia kuongeza kiwango cha maji kwa kiasi kikubwa huo mradi kwa kikasi kikubwa ilikuwa iongeze hiy ni heshima ya kipekee kwa Tanga Uwasa kuanzisha kwa jambo hilo.

“Sisi kama tunawapongeza na kuzitaka mamlaka za maji kuona namna kujifunza Tanga uwasa kwa jinsi wanavyofanya a Tanga Uwasa walivyotumia mapato yake ya ndani kuweza kwa kutekeleza miradi yake na kuwa na tija kubwa”Alisema

Awali akkizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo aliishukuru hiyo kwa kuwapa ushauri na maelekezo na ushauri wao ndio wameweza kufika hapo hiyo ni sehemu ya awamu ya awali ya mradi ambao baada ya kuchukua mkopo wa awali wa shilling zaidi ya bilioni 7.

Alisema hivyo walikuwa wanajenga uhalali na uzoefu wa kuchukua mkopo mkubwa zaidi na wanataraji kuanzia mwezi wa nne mwaka huu wataanza kutekeleza miradi mingine zaidi ili kufikia lita milioni 60 na kufikia wananchi wote wa Tanga,Pangani,Muheza,Pangani na Mkinga.

“Hivyo niwashukuru bodi kuhakikisha tunakuja na mipango mizuri ya kuhakikisha hkila siku hawalali na kuhakikisha wanakuja na mipango mipaya kuhakikisha wananchi waondokana na gharama za kugharamia huduma mbalimbali”alisema
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 19, 2024


Share:

Monday, 18 March 2024

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI JIJINI MBEYA KUHUDHURIA KONGAMANO LA NNE LA IDHAA ZA KISWAHILI

HABARI PICHA.. 






Na Mwandishi Maalum,Mbeya

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewalisi uwanja wa ndege wa Songwe Jijini Mbeya kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan  katika Kongamano la Nne la Idhaa za Kiswahili Duniani 2024 katika Hoteli ya Eden Highlands Jijini Mbeya tarehe 18 Machi, 2024. 

Kaulimbiu ya Kongamano hilo ni; “Tasnia ya Habari ni Fursa za Ubidhaishaji Kiswahili Duniani”


Share:

MVIWATA KUONGEZA USHIRIKIANO KIUCHUMI KUKUZA KILIMO

 

Na Christina Haule,  Morogoro

MTANDAO wa wakulima wadogo Tanzania (MVIWATA) unafanya juhudi za kuongeza 00pushirikiano ya kiuchumi  na kijamii kati ya nchi yetu na mataifa makubwa kama vile China na Brazil ili kuhakikisha wakulima  wanazalisha kwa wingi na kunufaika kutokana na jasho lao kupitia masoko yenye tija.

Hayo yameleezwa mjini Morogoro na Mkurugenzi MVIWATA,  Stephen Ruvuga, wakati akitambulisha taasisi ya Mashirikiano ya kimataifa Baobab  kutoka nchini Ghana na Brazil na taasisi ya Gorduana kutoka nchini China.

Anasema MVIWATA na mashirika hayo wanajadiliana namna ya wakulima wa mazao mbali mbali ikiwemo kahawa wanaweza kuzalisha kwa wingi na  kunufaika moja kwa moja kutoka kwa wanunuzi.

Anasema ushirikiano huo utaendelea kuwa mkombozi kwa kuhakikisha maisha ya wakulima wadogo yanakuwa bora zaidi kwa kuwezesha upatikanaji wa pembejeo na masoko ya mazao ya kimataifa  yenye tija.

Aidha Ruvuga alisema ujio wa taasisi hizo kubwa mbili umelenga kuanzisha ushirikiano kati ya wakulima wadogo wa hapa nchini hususani wanachama wa MVIWATA na wakulima na taasisi nyingine kutoka nchi za Ghana, Brazil  na China na kuboresha suala la kilimo nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utambulisho Mkurugenzi wa taasisi ya Gorduana, kutoka nchini China, Jit Zhou, alisema kuna mahitaji makubwa ya kahawa nchini humo. 

“ China ni nchi yenye idadi kubwa ya watu, na awali hakukuwa na watumiaji wengi wa kahawa, kwa sasa idadi ya watumiaji wa kahawa nchini humo imeongezeka sana, hivyo  bidhaa hiyo inahitajika kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya watumiaji. Alisema Zhou.

Naye Katibu Mkuu wa kampuni ya Baobab, Kyeretwice Opoku kutoka nchini Ghana alisema kuwa taasisi yake imepanga kushirikiana na wakulima  wa Tanzania kupitia MVIWATA  ili kuwezesha upatikanaji wa teknolojia ya kilimo na kuwafundisha wakulima kuzalisha mazao kwa kutumia mbolea za asili zisizo na kemikali  huku mkazo mkubwa ukiwa ni kuchechechemua uzalishaji wa mazao mbali mbali ikiwemo kahawa.

Akizungumza kuhusu fursa  hiyo kwa wakulima, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,  Dk Rose Rwegasira,  alisema  ujio wa mashirika hayo utasiadia kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao kwa kuwa kutaongeza upatikana wa pembejeo za kilimo  na masoko.

Share:

MAKALA: WANANCHI KATA 22 WASIKILIZENI WAGOMBEA, MPIGE KURA


Wagombea wa vyama mbalimbali wakiangalia fomu za uteuzi wa wagombea walioteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kugombea nafasi ya udiwani Kata ya Kimbiji iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam.


********"""
Na Mroki Mroki

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Machi 20,2024 kuwa ni siku ya kupiga kura katika Uchaguzi Mdogo wa udiwani katika Kata 23 za Tanzania Bara.


Tume ilitangaza uchaguzi huo baada ya kuketi katika kikao chake cha Februari 15 mwaka huu na siku hiyohiyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akatoa taarifa kwa umma juu ya uwepo wa uchaguzi huo mdogo.


Tayari mchakato wa Uchaguzi huo umeshaanza ambapo Februari 27 hadi Machi 4, 2024 wagombea walichukua fomu za uteuzi, uteuzi ulifanyika Machi 4,2024 na kampeni za uchaguzi zilianza Machi 5,2024 na zinaendelea hadi tarehe 19 Machi, 2024.


Hata hivyo, baada ya hatua ya uteuzi, Kata ya Nkokwa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ilipata mgombea mmoja tu aliyeteuliwa bila kupingwa hivyo hakutakuwa na kampeni kwenye Kata hiyo. Hivyo, uchaguzi utafanyika kwenye kata 22 zilizobakia.


Kata zitakazofanya uchaguzi huo mdogo ni Kimbiji (Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni), Kasingirima (Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji), Ndevelwa (Halmashauri ya Manispaa ya Tabora), Msangani (Halmashauri ya Mji Kibaha), Fukayosi(Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo), Mlanzi (Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti), Utiri (Halmashauri ya Mji Mbinga) na Mbingamhalule (Halmashauri ya Wilaya ya Songea).


Nyingine ni Isebya (Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe), Kibata (Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa), Mshikamano (Halmashauri ya Manispaa ya Musoma), Busegwe (Halmashauri ya Wilaya ya Butiama), Kamwene (Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba), Chipuputa (Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu), Buzilasoga (Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema), Mhande (Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba), Kabwe (Halmashauri ya Nkasi), Bukundi (Halmashauri ya Wilaya ya Meatu) Mkuzi (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza) na Boma, Mtimbwani na Mayomboni (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga).


Katika Uchaguzi huu wa Kata 22, Vyama vya siasa 18 vimesimamisha wagombea 127 kati ya hao wanaume ni 89 na wanawake ni 38. Wagombea kutoka kwenye vyama hivyo walichukua fomu za uteuzi na kuzirejesha na hatimaye wakateuliwa kuwania nafasi hiyo.

Wagombea wa vyama mbalimbali wakiangalia fomu za uteuzi wa wagombea walioteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kugombea nafasi ya udiwani Kata ya Kimbiji iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam.


Wagombea wote wameaminiwa na kupewa ridhaa na vyama vyao vya siasa kuwania nafasi zilizowazi, kwa kufanya hivyo, vyama hivyo vya siasa vimewatendea haki wanachama wao na wananchi kwa ujumla kwa kuwa wamepata haki ya kikatiba ya kugombea lakini pia wanachama na wananchi, watapata haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka.


Wagombea walioteuliwa na Tume ni wale waliopendekezwa na vyama vyao vya siasa kugombea kiti cha udiwani ambapo pia walijaza na kuwasilisha fomu za uteuzi katika Ofisi za Uchguzi katika Kata husika.


Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata walisimamia vyema majukumu yao ya kutoa fomu za uteuzi. Fomu za uteuzi za wagombea wote ziliwasilishwa siku ya uteuzi kabla ya saa kumi kamili (10:00) jioni.


Wagombea hawa wote siku ya uteuzi walijaza na kusaini mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Fomu Na. 10 ya maadili ya uchaguzi.


Wagombea hawa walijaza fomu hizo kukiri kuheshimu na kuyazingatia maadili ya uchaguzi yaliyosainiwa na viongozi wa vyama vyao mwaka 2020 wakati wa uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara.


Uwepo wa maadili ya Uchaguzi unalenga hasa kuwa na uchaguzi huru, wa haki, uwazi na wa kuaminika. Na kwamba amani, ustawi wa nchi, usalama wa raia, uhuru wa vyama vya siasa na utii wa sheria , kanuni na taratibu za uchaguzi ndio msingi wa uchaguzi ulio huru, haki na wenye kuzingatia ushiriki wa makundi yote ya jamii katika uchaguzi.


Vyama vya Siasa, Serikali na Tume walikubaliana kuwajibika kuyatekeleza Maadili hayo yanayotokana na kifungu cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343. Viongozi hao kwa pamoja walisema “Tutafanya jitihada za wazi kuhakikisha Maadili haya yanajulikana na kuheshimiwa na wagombea pamoja na wanachama wote wa vyama vya siasa”.


Sheria, Kanuni na miongozo yote iliyotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 bado inatumika na kufuatwa na vyama vya siasa, Tume ya Taifa ya Uchagzi na Serikali katika chaguzi hizi ndogo za udiwani.


Tayari Kampeni za uchaguzi zimeanza tangu siku moja baada ya uteuzi na zitaendelea hadi siku moja kabla ya siku ya kupiga kura.


Wakati wote wa kampeni wagombea wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni za uchaguzi, Maadili ya Uchaguzi na ratiba za kampeni.


Uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi na ratiba za kampeni utasaidia katika kuweka uwanja sawa katika kipindi chote cha kampeni na siku ya uchguzi.


Vyama vya Siasa na wagombea pamoja na wafuasi wao wanapaswa kuepuka kufanya siasa za fujo na za vitisho dhidi ya upande mwingine.


Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, imepewa jukumu la kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia taasisi au asasi za kiraia zinazotoa elimu hiyo.

Tume itatoa elimu kwa wananchi katika maeneo yote ambayo yanafanya uchaguzi mdogo. Lakini pia zipo asasi ambazo zimepewa kibali na Tume kutoa elimu hiyo kwa baadhi ya maeneo.

Elimu hiyo inayotolewa ni ile ya kumuwezesha Mpiga Kura kutambua sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kufunguliwa na kufungwa kwa vituo vya kupigia kura.

Lakini pia elimu hiyo itasaidia kutoa hamasa kwa wananchi kutumia haki yao ya kikatiba katika kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka.


Ni muhimu wananchi katika maeneo yote yanayofanya uchaguzi mdogo wakajitokeza kwa wingi kusikiliza sera za vyama na wagombea kisha kwa utashi wao wachague viongozi wanaowafaa kujaza nafasi zilizowazi katika Kata 23 za Tanzania Bara.


Mwandishi wa Makala haya ni Afisa Habari Msaidizi Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Share:

Sunday, 17 March 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 18,2024



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger