Sunday, 17 March 2024

HATI 8,325 ZATOLEWA KWA WANANCHI KUPITIA KLINIK YA ARDHI DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akimueleza jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe, Timotheo Mzava wakati Kamati hiyo ilipokwenda kukagua utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Milki za Ardhi (LTIP) eneo la Bunju Dar es Salaam Machi 17, 2024.

Na Munir Shemweta, WANMM

Jumla ya hati 8,325 zimesajliwa na kutolewa kwa wananchi waliofika kupata huduma katika Klinik za Ardhi mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, wananchi 18,224 wamefika katika klinik ya ardhi kupata huduma mbalimbali mkoani humo.

Hayo yamebainishwa tarehe 17 Machi 2024 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Jerry Silaa wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii kukagua utekelezaji mradi wa uboreshaji Usalama wa Milki za ardhi (LTIP) katika mkoa wa Dar es Salaam.

Amsema, katika Klinik Hiyo migogoro mbalimbali imetatuliwa ikiwemo migogoro ya mipaka, mirathi, matumizi ya ardhi pamoja na migogoro ya umiliki wa ardhi.

Kwa mujibu wa Silaa, Serikali kupitia wizara ya ardhi imeendelea kuchukua hatua za makusdi ili kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma za ardhi unaboreshwa kupitia mradi wa uboreshaji Usalama wa Milki za ardhi.

Amezitaja hatua zinazochukuliwa kuwa ni kuunda timu za wataalamu wa ardhi katika ngazi za mitaa kwa ajili ya kukwamua kazi za urasimishaji wa makazi katika maeneo yaliyopangwa pamoja na kuendesha Klinik za ardhi katika maeneo mbalimbali.

Hatua nyingine ni kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya ardhi kupitia vipindi vya redio na telebisheni, mikutano ya wananchi katika mitaa yao sambamba na kuunda timu za kushughulikia kero na migogoro ya ardhi.

Mhe, Silaa ameweka wazi kuwa, azma ya wizara yake ni kuendelea kufanya mageuzi kwenye sekta ya ardhi yanayolenga kuboresha huduma za ardhi kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Akielezea zaidi kuhusu Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP), Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema, mradi huo ni miongoni wa nyenzo muhimu zilizoonesha mafanikio makubwa katika kuongeza usawa wa kijinsia katika umiliki wa ardhi.

‘’Kati ya Hatimiliki 8325 zilizosajiliwa katika mkoa wa Dar es Salaam Hatimiliki 2,461 sawa na asilimia 29.6 no za wanawake’’ alisema Mhe, Silaa

Amefafanua kuwa, mradi huo wa uboreshaji milki za ardhi umewezesha kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi nchini kutoka asilimia 25 hadi asilimia 41 huku idadi ya hati za pamoja baina ya wana ndoa zikiongezeka na kufikia asilimia 10 ya hati zilizotolewa.

Aidha, amesema Klinik za Ardhi zinazoendeshwa kupitia mradi wa LTIP zimekuwa jukwaa muhimu la kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa wanawake kumililki ardhi.

Kwa upande wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kupitia Mwenyekiti wake Mhe, Timotheo Mzava mbali na kuridhishwa na utekelezaji mradi wa LTIP imeipongeza Wizara ya Ardhi kwa kazi nzuri ya kutekeleza miradi ya uboreshaji miliki za ardhi hususan katika klinik za ardhi.

‘’Mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati tunaridhika na kazi inayofanyika na ki ukweli ni kazi ni nzuri na tunataka iendeleee’’ alisema Mhe, Silaa

Aidha, Kamati imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anaayoifanya ikiwemo kuwezesha upatikanaji fedha za mradi wa LTIP ili kusaidia utatuzi wa changamoto katika sekta ya ardhi.

Aidha, amemtaka Waziri wa Ardhi kuijenga taasisi ili muelekeo alio nao uende mpaka kwa watumishi wa chini kwa kuwa haitatosha maono aliyo nayo kubaki kwa viongozi pekee. ‘’Huwezi kuwa kila mahali lazima kuwemo mfumo wa kitaasisi utakaoshuka mpaka kwa watendaji wa chini na wimbo uende mpaka ngazi za chini na likifanikiwa hilo tutakwenda vizuri sana’’. Alisema Mhe, Mzava

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii mbali na kukagua utekelezaji mradi wa uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) ilishiriki pia kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa wananchi wa eneo la Bunju Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe, Timotheo Mzava pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Jerry Silaa wakimsikiliza mwananchi wakati kamati ya Bunge ilipokwenda kukagua utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Milki za Ardhi (LTIP) katika eneo la Bunju Dar es Salaam Machi 17, 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe, Timotheo Mzava akimkabidhi Hati milki ya ardhi mmoja wa wananchi wakati Kamati yake ilipokwenda kukagua utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Milki za Ardhi (LTIP) katika eneo la Bunju Dar es Salaam Machi 17, 2024.
Mbunge wa Viti Maalum Neema Mgaya akimpatia Hati milki ya Ardhi mwananchi wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii ilipokwenda kukagua utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Milki za Ardhi (LTIP) katika eneo la Bunju Dar es Salaam Machi 17, 2024.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Jerry Silaa akiwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii katika gari wakielekea kukagua utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Milki za Ardhi (LTIP) katika eneo la Bunju Dar es Salaam Machi 17, 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe, Timotheo Mzava alipowasili eneo la Bunju kukagua utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Milki za Ardhi (LTIP) katika eneo la Bunju Dar es Salaam Machi 17, 2024. Katikati ni Waziri wa Ardhi Mhe, Jerry Silaa (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Share:

DAWA KIBOKO KWA NGUVU ZA KIUME



Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu ,shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu. Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;

1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo

2. Kuvuta sigala na unywaji wa pombe

3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi

4. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

5. Kisukari

6. Kuwa na mawazo na wasiwasi

7. Matumizi ya madawa mbalimbali

8. Umri hasa wazee

9. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili

10. Kuwa na tatizo la kibofu

11. Tabia za kujichua kwa muda mrefu

12. Kutopata usingizi kamili

13. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine

DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Dalili za kuonesha kuwa una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume karibia zote zinahusiana na hali itakayo onekana katika tendo la ndoa au mda wa kujamiiana, hizo dalili zake ni kama;


1. Kuwahi kufika kileleni

2. Kukosa hamu ya mapenzi

3. Kushindwa kurudia tendo la ndoa

4. Uume kusimama kwa ulegevu au kushindwa kusimamisha

5. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu; Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo

7. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)

8. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji


TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

FULL POWER
⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.


ZAT 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonda vya tumbo, Kisukari, Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kung’oa


Ndugu mteja Epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahihi kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27 au 0754568767  utatumiwa sehemu yoyote ulipo
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 17,2024


Share:

Saturday, 16 March 2024

DKT. NCHIMBI AKUTANA NA BALOZI WA CHINA MHE. CHEN MINGJIAN

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amekutana na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian, leo Ijumaa, Machi 14, 2024, Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam na kufanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano na urafiki wa kidugu kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Tanzania na China.
Share:

WADAU WA SANAA YA UBUNIFU NA UTAMADUNI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUNADI KAZI ZAO


Na Rose Ngunangwa, Bagamoyo

Wadau wa Sanaa ya Ubunifu na Utamaduni wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa kunadi bidhaa zao ili kuwafikia wateja wengi zaidi.

Wito huo umetolewa leo mjini Bagamoyo wakati wa kikao kazi cha UNESCO cha kujadili na kuboresha maudhui ya Mkataba wa mwaka 2005 kwa muktadha wa Tanzania katika nyakati za kidijitali.

Akichangia mjadala huo, mdau katika sekta ya ubunifu na utamaduni bwana Robert Mwampembwa amesema matumizi sahihi ya kunadi bidhaa mtandaoni yanaweza kumfanya mbunifu akauza bidhaa katika nchi 50 duniani.

Kwa upande wake, Angela Kilusungu kutoka shirika la CDEA alishauri wauzaji wa bidhaa za ubunifu mtandaoni kuposti mara kwa mara ili kusaidia kuongeza uwezekano wa bidhaa hizo kuonwa na wanunuzi wanaoingia mtandaoni bila kujua wapi watapata huduma husika.

“ Unapouza bidhaa za ubunifu lazima utoe maelezo yanayojitosheleza sio unaandika mathalani kwamba unauza nguo. Ni vema ukasema ni aina gani ya nguo unauza. Ni lazima pia ujibu maswali kwa wakati na uwazi na uwe na mifumo ya kufikisha mizigo kwa wakati na kwa uaminifu. Mifumo yako ya malipo iwe ya uhakika ili watu wasidhani wewe ni tapeli,” alisisitiza Kilusungu.

Alitaja kuwa moja ya kitu kinachokimbiza wateja ni muuzaji wa bidhaa husika kumjibu swali linalohusiana na bei inbobo na kusema kuwa hiyo humfanya mnunuzi kuona kuwa anafanya biashara na mtu ambaye sio muaminifu.


Kikao kazi hicho kiliwajumuisha wadau wa sekta ya Sanaa na ubunifu zikiwemo taasisi zinazosimamia sekta kama Wizara ya utamaduni, Sanaa na Michezo, BAKITA, ZIFF, BASATA, BAKIZA, COSOZA, Chuo cha Sanaa Bagamoyo, waandishi wa habari pamoja na wawakilishi kutoka sekta binafsi.
Share:

Friday, 15 March 2024

MBINU YA KUWASHINDA MAADUI ZAKO KATIKA AJIRA YAKO!

 

Jina langu ni Bella kutokea Morogoro, Tanzania, mnamo 2017 nilipoteza kazi niliyokuwa nimeajiriwa kwa makosa ambayo sikuhusika, lakini upepelezi ulipokuja kufanyika nilionekana ni kama na mimi nilihusika kwenye huo wizi ingawa ukweli sikuhusika.

Sikujua chochote na wala sikula hata Sh100 ila wanasema siku ya kusulubiwa kwako manabii wa uongo watakuja ili kukutolea ushahidi wa uongo lengo uangamie, ndio kilichonitokea mimi.

Baadae ya kupoteza kazi Mungu alinipa ujasiri sana maana sikuwahi kujutia kupoteza kazi bali nilianza kuwaza naishije kwa sasa na nafanya nini ili maisha yaende?.

Sikuweza kupata kitu cha haraka haraka cha kufanya ili kiniingizie kipato cha kujikimu maisha, michongo haikuwa rahisi kupatikana, ghafla nikapata wazo jingine, nilichowaza ni kuchukua mafao yangu na nijiendeleze kielimu.

Niliamua kusoma QT kwa ajili ya kidato cha tano na sita maana nilikuwa na alama nzuri tu nilizopata kidato cha nne, nakumbuka nilianza kusoma kwa kuchelewa ila nashukuru nilifanya mtihani wa kidato cha sita.

Licha ya kusoma kwa muda mfupi sana, Mungu alisaidia nikapata ufaulu mzuri ulionifanya nikaingia chuo kikuu, nashukuru nilifanikiwa kumaliza chuo kikuu na kupata degree yangu.

Ila baada ya kumaliza chuo ikawa ni ngumu sana kupata kazi na kama nikipata kazi, basi visa vinaanza katika ofisi hiyo hadi najikuta nimeondoka, ilikuwa ni changamoto kubwa sana kwangu maisha, sikujua nini sababu.

Hali hiyo ilinitesa sana kwa muda ila baadaye nilikuja kupata suluhisho kutoka kwa Kiwanga Doctors ambao walinisaidia kupata kazi mpya na kunikinga na maadui katika kazi yangu.

Kwa sasa ni zaidi ya mwaka mmoja nimetulia katika kazi moja na hakuna chokochoko kazini kwangu.

Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.

Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.

Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.

Mwisho.


Share:

WADAU WA SANAA YA UBUNIFU NA UTAMADUNI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUNADI KAZI ZAO


Na Rose Ngunangwa, Bagamoyo

Wadau wa Sanaa ya Ubunifu na Utamaduni wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa kunadi bidhaa zao ili kuwafikia wateja wengi zaidi.

Wito huo umetolewa leo mjini Bagamoyo wakati wa kikao kazi cha UNESCO cha kujadili na kuboresha maudhui ya Mkataba wa mwaka 2005 kwa muktadha wa Tanzania katika nyakati za kidijitali.

Akichangia mjadala huo, mdau katika sekta ya ubunifu na utamaduni bwana Robert Mwampembwa amesema matumizi sahihi ya kunadi bidhaa mtandaoni yanaweza kumfanya mbunifu akauza bidhaa katika nchi 50 duniani.

Kwa upande wake, Angela Kilusungu kutoka shirika la CDEA alishauri wauzaji wa bidhaa za ubunifu mtandaoni kuposti mara kwa mara ili kusaidia kuongeza uwezekano wa bidhaa hizo kuonwa na wanunuzi wanaoingia mtandaoni bila kujua wapi watapata huduma husika.

“ Unapouza bidhaa za ubunifu lazima utoe maelezo yanayojitosheleza sio unaandika mathalani kwamba unauza nguo. Ni vema ukasema ni aina gani ya nguo unauza. Ni lazima pia ujibu maswali kwa wakati na uwazi na uwe na mifumo ya kufikisha mizigo kwa wakati na kwa uaminifu. Mifumo yako ya malipo iwe ya uhakika ili watu wasidhani wewe ni tapeli,” alisisitiza Kilusungu.

Alitaja kuwa moja ya kitu kinachokimbiza wateja ni muuzaji wa bidhaa husika kumjibu swali linalohusiana na bei inbobo na kusema kuwa hiyo humfanya mnunuzi kuona kuwa anafanya biashara na mtu ambaye sio muaminifu.


Kikao kazi hicho kiliwajumuisha wadau wa sekta ya Sanaa na ubunifu zikiwemo taasisi zinazosimamia sekta kama Wizara ya utamaduni, Sanaa na Michezo, BAKITA, ZIFF, BASATA, BAKIZA, COSOZA, Chuo cha Sanaa Bagamoyo, waandishi wa habari pamoja na wawakilishi kutoka sekta binafsi.
Share:

UJENZI WA DARAJA LA J.P MAGUFULI (KIGONGO-BUSISI) WAFIKIA 85%

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiwa wameshika bango linaloonesha maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), lenye urefu wa kilometa 3 ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 85, Mkoani Mwanza.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakipokea maelezo kutoka Msimamzi wa mradi kutoka Wakala wa Barabara (TABROADS), Eng. Katelula Kasagwa, kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), lenye urefu wa kilometa 3, Mkoani Mwanza.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi), lenye urefu wa kilometa 3, Mkoani Mwanza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (Mb), akizungumza wakati Kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye urefu wa kilometa 3, ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 85, Mkoani Mwanza.

Muonekano wa juu wa kazi za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye urefu wa kilometa 3 zikiendelea, Mkoani Mwanza. Ujenzi wa Daraja hilo umefikia asilimia 85.

..............

Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye Kilometa 3.2 pamoja na Barabara unganishi ya Kilometa 1.66, linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria umefika asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa Machi 15, 2024 Mkoani Mwanza katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Kakoso (Mb) ilipoambatana na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kukagua maendeleo ya mradi huo.

Katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (Mb) ameeleza kuwa Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo na imempongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ili mradi huo ukamilike kwa muda uliopangwa.

Kakoso ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha anamsimamia Mkandarasi wa daraja hilo kutoa fedha zitakazokwenda kuisaidia jamii inayozunguka mradi huo ambazo zitakuwa kielelezo kwa wananchi wa Wilaya ya Sengerema na Misungwi.

Aidha, Kakoso ameitaka Wizara ya Ujenzi kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama katika daraja hilo ambalo linatokana na kodi za wanachi ili liweze kudumu kwa muda wa miaka 100.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ambapo mpaka sasa jumla ya Shilingi Bilioni 441.3 zimetolewa kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo.

"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anautazama sana mradi huu kipekee, amekuwa akitoa fedha kwa kila hati za Mkandarasi zinapowasilishwa na zimekuwa zikilipwa kwa wakati ili Mkandarasi asikwame kutokana na kukosekana kwa fedha", amesema Bashugwa.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Doroth Mtenga ameeleza kuwa mradi huo unatumika kama darasa la mafunzo kwa wanafunzi na wataalamu wetu wa ndani kupata uzoefu wa kusimamia na kujenga madaraja mengine kama hayo hapa nchini.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger