Thursday, 14 March 2024

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MTAMBO WA MKONGO WA TAIFA SHINYANGA, YAITAKA TTCL IJIENDESHE KIBIASHARA




Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu imetembelea ujenzi wa mkongo wa taifa wa mawasiliano uliopo manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.

Ziara hiyo ya ukaguzi imefanyika leo Machi 14, 2024 katika ofisi za Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL mkoani humo.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa mkondo wa taifa wa mawasiliano mbele ya kamati ya kudumu ya bunge mtendaji mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Peter Ulanga amesema ujenzi wa mitambo ya kuongeza uwezo kituo cha mkongo Shinyanga umekamilika kwa 100% na mitambo inafanya kazi ambapo ujenzi huo umegharimu zaidi ya kiasi cha bilioni 1 huku akieleza changamoto katika utekelezaji wa mitambo hiyo.


"Awamu ya kwanza ya ujenzi wa mkongo wa taifa ilianza 2009 ikiwa na uwezo wa 40G na baadae kuongeza uwezo kwa 200G hadi 400G kwa Singida - Shinyanga - Mwanza, ujenzi wa faiba kutoka Shinyanga mpaka Kahama umekamilika kwa 100% ambao umegharimu kiasi cha milioni 594", Peter Ulanga.

"Zipo Changamoto ambazi tulikumbana nazo katika utekelezaji wa ujenzi huu ni pamoja na kupata tatizo la umeme, imekuwa ni changamoto TANESCO kuzima umeme kwa wakati ili kupisha ujenzi huu ambapo imepelekea kuchelewa kukamilika kwa mradi, hali ya hewa ya mvua ni moja ya changamoto ya mazingira ya kufanyia kazi katika usimikaji nguzo na kuvuta waya", ameongeza 

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye ameeleza ushirikiano uliopo kati ya TTCL na TANESCO katika usambazaji wa mkongo wa taifa kwenye maeneo mbalimbali.


"Katika kupanua mtandao wa mkongo huu hadi kwenye mipaka ya nchi yetu tumeendelea kusambaza kwenye nchi jirani ikiwemo Kenya, Uganda na Rwanda na sasa tunataka kuingiza mkongo huu nchini Congo ambapo mpaka sasa taratibu kadhaa zimekwisha chukuliwa, nikuhakikishie Mwenyekiti kuwa tunatambua kuwa tuna dhamana kibwa ya kuhakikisha tunaziunganisha nchi za pembezoni", amesema Nnape.

Mwenyekiti wa kamati Selemani Kakoso mbunge wa jimbo la mpanda vijijini ameipongeza wizara hiyo kwa jitihada mbalimbali inazofanya kuhakikisha uwepo wa uhakika wa mawasiliano sehemu zote na kuitaka TTCL kujiendesha kibiashara.


"Kamati inampongeza sana Mheshimiwa waziri kwa sababu tunaona jitihada inayofanywa na wizara yake kwa kufanya mapinduzi makubwa ya mawasiliano kwa kipindi kifupi, tunachoomba msimamie kikamilifu mkondo wa taifa ujisamie kibiashara sababu mnatoa huduma zinaleta fedha nyingi kwa kufanya ubunifu na usimamizi mzuri, suala la mkataba wa TTCL na TANESCO naomba Mheshimiwa waziri mkapitue upya mkataba huu muangalie maeneo ambayo yatakuwa na afya ili TTCL iweze kujisimamia", amesema Kakoso.


Mtambo wa usambazaji mkongo wa taifa uliopo mkoani Shinyanga.


Kamati ya bunge ikikagua mtambo huo.








Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa kikao hicho.


Kikao kikiendelea.

Jengo la ofisi ya TTCL Mkoa wa Shinyanga.


Picha ya pamoja.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 14, 2024




Magazeti
Share:

Wednesday, 13 March 2024

NILIUMWA GHAFLA KISA BETTING ILA SASA NI BINGWA!

Jina langu Baraka kutokea Arusha nchini Tanzania, kuna siku nilikuwa na kama Sh150,000 mkononi, hapo nilikuwa najichanga ili niweze kulipa kodi ya nyumba, kila simu ninayopiga majibu ni yaleyale, subiri mwisho wa mwezi.

Hapo mama mwenye nyumba haelewi na amenipa siku tatu niwe nimempa Sh300,000 yake au niwe nimerudisha chumba chake ili aweze kupangisha mtu mwingine mwenye fedha.

Baada ya mawazo mengi na mipango mingi kufeli, nikajiwazia moyoni, "kwanini nisi-bet?", hapo ni baada ya kila mpango ulikuwa kushindikana, nitafanya nini naSh150,000 yangu?.

Mwanaume nikaingia kazini, nikaanda mkeka wangu wenye odds za uhakika, mzigo ukasoma Sh350,000 kama uki-tick, ila sharti ni lazima niweke hela yote niliyonayo yaani Sh150,000.

Ikumbukwe kiwango changu kikubwa kabisa ku-bet ilikuwa ni Sh5,000, basi nikajipa moyo na ile potelea mbali, nikaweka mkeka wangu.

Dah nakumbuka ilikuwa asubuhi, ile kuweka tu na jamaa washachukua hela yao nikaanza kuumwa, mawazo yakaongezeka mara 10 yake, nikaanza kujilaumu kwanini nimefanya vile. Ikabidi nipige simu kwa ile kampuni niliyobetia wanirudishie hela yangu ila wakagoma.

Niliwabembeleza sana aisee, tena niliwaambia hiyo Sh50,000 wachukue na wanirudishie Sh100,000 yangu lakini bado hakunielewa. Jibu lao lilikuwa ni moja, hela ishaingia kwenye system na haiwezi kutoka na hivyo nisubiri majibu yangu.

Mchana sikula, nipo nawaza nafanyaje na hapo mkononi ndio sina hela kabisa, muda wa mechi nilikaa kitandani sikutaka kupata hata matokeo maana nilijua nishaliwa.

Nashukuru ule mzigo ulitema, mechi zangu tatu zote ziliisha kama nilivyotabiri, sikuamini, kesho yake mapema nikafanya muamala kwa mama mwenye nyumba na nikabakiwa na Sh500,000.

Sitasahau ile presha, sitarudia tena kufanya ule ujinga maana unaweza kufa, ila nilitamani kuendelea kubet tena kwa kuweka fedha nyingi na kushinda fedha nyingi, hivyo nilianza kutafuta mbinu mbalimbali za ushindi.

Katika kupekua kwenye mitandao ya kujamii ndipo nikakutana na tangazo la Kiwanga Doctors kuwa anatoa dawa na mbinu za kushinda katika betting, nilichukua namba yake (+254 769 404965) na kuwasiliana nao na kuwaeleza kiu yangu ya ushindi.

Kweli waliweza kunisaidia na tangu wakati huo nikaanza kushinda fedha nyingi za betting, ni juzi tu hapa nimeshinda zaidi ya Sh5 milioni, fedha ambazo nimeamua kununua pikipiki mbili za biashara ambazo zinaniingizia  fedha kila siku.

Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.

Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.

Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.

Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.

Mwisho.

 


Share:

WANANCHI VISIWANI ZANZIBAR WAKABIDHIWA MITUNGI YA KUPIKIA 700 YA GESI YA ORXY

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy Adhuruu Makame Kombo katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.

*************

Na Mwandishi Wetu

WAKATI Serikali ikiendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kwa kushirikiana na Kampuni ya gesi ya Oryx wamegawa mitungi 700 ya gesi kwa wananchi wakiwemo baba lishe na mama lishe visiwani Zanzibar.

Akizungumza leo Machi 13,2024 wakati wa kugawa mitungi hiyo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar, Waziri Masauni amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuchukua hatua  mbalimbali.

Hivyo amesema kitendo cha Oryx kushirikiana naye kugawa mitungi hiyo bure kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kunakwenda kusaidia kuifanya jambii hiyo kuachana na kuni na mkaa na badala yake kutumia nishati safi ambayo inafaida nyingi.

“Tunaamini waliopata majiko haya gesi pamoja na kupatiwa mafunzo ya namna ya kuyatumia watakuwa mabalozi wazuri kwa kuwahamasisha wananchi wengi zaidi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar na Tanzania wahame sasa kutoka katika matumizi ya kuni na mkaa na waje sasa kutumia gesi.

“Faida ya kutumia gesi ni nyingi tumezoa kutumia mkaa tukiamini tukaokoa fedha lakini kimsingi kwa mujibu wa maelezo ya watalaam gharama za matumizi ya mkaa ni kubwa zaidi ukilinganisha na gesi.

“Hivyo hakuna sababu ya mtu kutumia kuni au mkaa ambao unakwenda kuleta madhara ya kiafya na mazingira,”amesema Waziri Masuni na kusisitiza wametumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa wananchi wawe na uelewa wa  kutumia majiko hayo kwa usalama na wakawe walimu kwa wengine.

Awali Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema wanaamini ukipika kwa kutumia gesi, inaleta maendeleo mengi kwa jamii yetu sambamba na kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti.

“Zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake kwa kuwaepusha kuvuta moshi na mvuke unaoathiri mapafu na afya yao unaotokana na kuni na mkaa.Hivyo tunakushuru Waziri Masauni kwa kushirikiana nasi katika kuhakikisha wananchi wa Jimbo la Kikwajuni wanapata niashati safi ya kupikia.”

Pia kutumia gesi ya Oryx kunawezesha  watoto kuwa na muda mwingi zaidi kusoma na sio kwenda kutafuta kuni huku akisisitiza kutumia gesi kunaepusha wamama na watoto kuumia kwa kubeba kuni nzito na kuepuka kujeuriwa na Wanyama wakali wakiwa wanatafuta kuni.

Aidha amesema kwa miaka mingi Oryx Gas imekuwa kampuni kiongozi katika kukuza matumizi ya gesi nchini Tanzania na kuanzia mwaka Julai mwaka 2021 wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Serikali.

Amefafanua maelekezo hayo yaliyopokea kutoka kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo mwaka 2023 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

“Kupitia mipango hii, Oryx Gas inataka kutokomeza matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa ambayo si tu mbaya kwa afya zetu bali pia ni hatari kwa mazingira yetu na Oryx inatekeleza juhudi za kueneza matumizi ya nishati safi kwa Watanzania wengi ipasavyo ambayo ni ndoto kubwa ya Rais Mama Samia.

Ameongeza Oryx Gas Tanzania inajipongeza kwa kujulikana kuwa kampuni kinara katika usambazaji wa gesi ya kupikia kwa Watanzania kwa sasa na kwamba wataendelea kuwekeza zaidi katika kuratibu kubadilisha na kueneza nishati safi kutumika kwa wananchi wengi.

Araman amesema Oryx Gas inajulikana kwa kuuza mitungi ya gesi pamoja na kufunga mifumo salama ya gesi kwenye taasisi na viwanda vinavyotumia gesi kwa wingi.

“Hivi majuzi tumezindua mfumo wa gesi katika shule ya Sekondari ya Hasnuu iliyopo Kizimkazi. Kupitia mipango ya kusambaza nishati safi ya kupikia, Oryx Gas itaendelea kuhimiza matumizi ya nishati safi katika familia, taasisi zenye watu zaidi ya 100 na viwanda.

Aidha amesema anamshukuru Waziri Masauni kwa kuwa balozi mzuri wa kuleta maendeleo kwa jamii kiujumla kwa kuwaunga mkono katika mpango huo wa matumizi ya nishati safi katika jimbo la Kikwajuni.

Wakati huo huo Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Peter Ndomba pamoja timu nzima ya kampuni hiyo wametoa mafunzo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia lengo likiwa kuiwezesha jamii kuwa salama na kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa kutokuwa na uelewa wa kutumia mtungi wa oryx.

Akizungumza mbele ya wananchi waliopatiwa mitungi na majiko yake, Ndomba amesema pamoja na kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi matumizi sahihi ya gesi ni kipaumbele chao na wamekuwa wakitoa mafunzo kabla ya kugawa mitungi.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy Hudhaima Shaban Sururu katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.

Mama lishe wa visiwani Zanzibar wakiwa katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.Mitungi hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kwa kushirikiana na Kampuni ya gesi ya Oryx.
Mama lishe wa visiwani Zanzibar wakiwa katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.Mitungi hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kwa kushirikiana na Kampuni ya gesi ya Oryx.
Katibu Tawala Wilaya ya Mjini Dkt. Said Haji Mrisho akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Baadhi ya mitungi ya kupikia ya Oryx ambayo imekabidhiwa kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar. Mitungi hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kwa kushirikiana na Kampuni ya gesi ya Oryx
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy Haroub Ali Abdallah katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy Rahima Bakari katika hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akiwa pamoja na Katibu Tawala Wilaya ya Mjini Dkt. Said Haji Mrisho na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman wakiwa kwenye picha ya pamoja na baba lishe na mama lishe wa visiwani zanzibar wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Gesi ya Orxy, Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.
Meneja Masoko Msaidizi wa Kampuni ya Gesi ya Oryx Angela Bitungwa akitoa elimu ya matumizi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi 700 ya kupikia ya Oryx kwa baba lishe na mama lishe Machi 13, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger