Wednesday, 27 September 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 28,2023





























































Share:

E ' MAJOR AMEACHIA JARA


E'major ni mwimbaji kutoka Nigeria wa Afro-fusion na Afro-rnb, mtunzi wa nyimbo, na mwanamuziki anayeishi Amerika. Muziki wake unachukuliwa kuwa wa kipekee, wenye mvuto kutoka kwa aina mbalimbali za muziki, hasa Pop, RNB, Hip Hop, Highlife na Contemporary Gospel.

E'Major alikuwa mwimbaji mkuu wa bendi ya "Sound City," iliyoshirikisha wasanii kama vile Flavour Nabania na Chris Odor. Yeye ndiye mtoto wa mwisho kati ya watoto 9 aliyezaliwa na mfanyabiashara wa ndani na baba mtumishi wa serikali. 
Alianzisha kikundi cha watu watano cha a-cappella "Lace" mnamo 1996, wakati wa enzi ya Lord Eli, ambaye sasa anajulikana kama 2face Idibia/2Baba. Kisha akaondoka hadi Amerika, ambako alijiimarisha kama mwanamuziki wa kisasa mwenye msukumo na pia akaongoza kwaya katika makanisa kama vile Christ family church international.

Mnamo 2019, E'Major alisaini na Motion Major Records na ametoa kazi nyingi ikiwa ni pamoja na single, EP na nyimbo zingine chache ambazo ameshirikiana na nyota wengine wa Afrobeats.
E’Major ambaye anaendelea kuboresha uhalisia wake wa muziki anatumia nyimbo zake kila mara kuchunguza mada za mapenzi, mapambano, furaha na mafanikio.

Lakini kwa sasa E major ameachia wimbo wake mpya ambao unafahamika kwa jina la Jara unapatikana katika mitandao yote ya kijamii na kusambaza muziki .


 

Share:

JKT -TANZANIA KUTUMIA UWANJA CCM KAMBARAGE MECHI ZA LIGI KUU YA NBC.... YATANGAZA KICHAPO CHA KIZALENDO ‘DOUBLE K’ KWA KAGERA SUGAR


Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya JKT Tanzania, Masau Bwire akizungumza na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Jumatano Septemba 27,2023
Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya JKT Tanzania, Masau Bwire akizungumza na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Jumatano Septemba 27,2023


Na mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Timu ya mpira wa Miguu ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)Tanzania  imethibisha rasmi kutumia uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kama uwanja wake wa nyumbani katika michezo yote ya Ligu Kuu ya NBC -Tanzania hadi pale uwanja wao wa Meja Jenerali Isamuyo uliopo Mbweni Dar es salaam utakapokamilika baada ya matengenezo makubwa yanayoendelea kufanyika.

Hayo yameelezwa na Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya JKT Tanzania, Masau Bwire katika Mkutano wake na vyombo vya habari  Mjini Shinyanga leo Septemba 27,2023.

Amesema wameuchagua uwanja wa CCM Kambarage kama uwanja wao wa nyumbani kwani wanataka maeneo yote nchini yanapata fursa hivyo furaha ya JKT Tanzania ni kuona wakazi wa Shinyanga wanapata furaha ya Soka hivyo kuwaomba wakazi wa Mkoa huo kuipa ushirikiano timu hiyo.

"Tutatumia uwanja huu hadi uwanja wetu utakapokamilika matengenezo..Uwanja wa CCM Kambarage umepitishwa na TFF kwa ajili ya kutumika kwa ajili ya mechi za ligi kuu ya NBC. Na tutaanza kuutumia uwanja huu katika Mchezo wetu na Kagera Sugar utakaofanyika Ijumaa hii Septemba 29,2023 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme",amesema Bwire.

"Tunaomba wakazi wa Shinyanga  waichukue na kuipokea  JKT Tanzania kama timu ya nyumbani na kuipa ushirikianao wote katika kuendelea kutumia uwanja wa CCM Kambarage", ameongeza Bwire.

Mechi ya Kagera Sugar na JKT Tanzania inayotarajiwa kufanyika Septemba 29,2023 utakuwa na viingilio rafiki ili  kila mmoja kushiriki katika mechi hiyo na shinyanga imekuwa na ukame wa muda mrefu wa kukosa mechi za ligi kuu.

"Double  K ni kichapo cha kizalendo kiheshimike kwa kuwa kila timu itakayofika hapa lazima ipate kichapo.  Mechi ya Ijumaa na Kagera Sugar ni kichapo cha kizalendo,  Kagera Sugar tutaipa Double K kwani tuna kikosi bora na makini na wachezaji wenye vipawa zaidi",amesema.

"Tumepanga  kiingilio ni Tshs 2000/=  kwa mzunguko na  Jukwaa kuu ni Tshs 3000/= kwa maana ya jukwaa kuu. Pia Mfumo wa N Card utatumika ili kusaidia kutoa huduma kwa mashibiki kukata tiketi zao

"Tunatumia N Card ili kuepusha msongamano na malalamiko na tumewasiliana na mamlaka husika wa kutekeleza jukumu hilo kutoka Dar es salaam  na ofisi ya TTCL na utaratibu wa kuuza tiketi utafanyika katika vituo vya Soko Kuu, Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga na ofisi za TTCL Shinyanga  na  siku ya mechi mageti katika uwanja wa CCM Kambarage  yatafunguliwa kuanzia  saa 4:00 asubuhi.

"Tungependa mashabiki wetu waje na sura ya JKT siku ya mechi kwa kuvaa jezi zenye ubora ambazo zinapatikana kwa Tshs 35,000/= na kofia kwa Tshs 10,000/=",ameeleza.

Share:

ZAIDI YA WAGONJWA 1000 WAFANYIWA UCHUNGUZI NA KUPATIWA MATIBABU KAMBI YA MADAKTARI BINGWA TANGA

 

Mratibu wa Kambi hiyo ambaye pia ni Mhazini wa Chama cha Madaktari Tanzania Dkt Mathew Shao kulia akiteta wakati wa kambi ya Huduma za Madaktari Bingwa wa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali inayoendelea kwenye viwanja vya Mkwakwani Jijini Tanga.

Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma mbalimbali wakati wa kambi hiyo inayoendelea kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani Jijini Tanga






Na Oscar Assenga, TANGA

ZAIDI ya wagonjwa 1000 wamefanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu katika kambi ya Huduma za Madaktari Bingwa wa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali inayoendelea kwenye viwanja vya Mkwakwani Jijini Tanga.

Kambi hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga Mhe. Ummy Mwalimu iliyoanza Septemba 25 mwaka huu na inayotarajiwa kumalizika leo tarehe 27 September ilikuwa ikitoa huduma za kibingwa katika magonjwa mbalimbali.

Akizungumza leo Mratibu wa Kambi hiyo ambaye pia ni Mhazini wa Chama cha Madaktari Tanzania Dkt Mathew Shao alisema mwamko wa wananchi umekuwa kuridhisha kutokana na kuongezeka idadi yao kila siku.

Dkt Shao ambaye pia ni Daktari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa alitaja magonjwa hayo ya kibingwa ni Moyo,Sukari,Mifupa,Pua/koo,
masikio,wanawake na uzazi,kinywa na meno,watoto ,mfumo wa mkojo(Urojolia) na Macho.

Aliyataja magonjwa mengine ni ya Upasuaji,utoaji wa dawa na vipimo vya sukari,moyo-Echo,ECG,Utrasound,Sickle Cell,Uzito na urefu,hali ya lishe,ukimwi/TB,Ushauri na nasaha na elimu juu ya magonjwa yasiyoambukiza (NCD)

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 27,2023

 



















         








  

    Share:

    Tuesday, 26 September 2023

    MPYA:MKUU WA WILAYA KENANI KIHONGOSI ATANGAZA KAZI YA KUTENGENEZA LOGO

     


    Maswayetu blog imenasa taarifa nyeti na nzuri kwa vijana watafutaji kutoka kwa Kihongosi,

    "Tunaandaa URAMBO TUMBAKU MARATHON itakayofanyika mwezi wa tatu mwaka 2024 Ikiwa na Lengo la Kuboresha Miundombinu ya Elimu.


    Sasa Naomba VIJANA wenye uwezo wadesign LOGO(Ambayo itakuwa ndio Medali Rasmi ya Marathon yetu) Logo ambayo Itashinda kwa vigezo Mshindi atapewa zawadi ya Shilingi Laki Tano(500,000). Tuma logo yako katika namba yangu ya Whatsup 0744940380 na namba ya Afisa Tarafa wetu wa Urambo 0677003189 @afisatarafaurambo

    Mwisho wa kusubmit LOGO hii ni kuanzia Leo hadi TAREHE 1 mwezi wa Kumi.

    Pia tutahitaji washiriki 600 katika Marathon yetu na kila Mshiriki atachangia shilingi 30,000/= ambayo utapewa MEDALI na TISHIRT itafanyika MWEZI WA TATU TAREHE 2 MWAKA 2024.

    Wale Mtaotaka kushiriki basi tutakuwa na Group la Whattsup kwaajili ya Marathon yetu hii.

    Naomba tuwasiliane kwa SMS tu kupata Taarifa au maelezo zaidi ASANTENI SANA.

    Share:

    MPYA:WANAFUNZI 17 WAFUKUZWA CHUO CHA SAYANSI NA AFYA YA BINADAMU LEO

     Habari zilizotufikia Maswayetu blog ni kwamba chuo cha sayansi na tiba cha DECCA kilichopo Mkoani Dodoma kimeamua kuwafukuza wanafunzi wake 17 ambao walihoji uhalali wa kozi wanayosoma kama ina uhalali.



    wanafunzi hao walifanikiwa kufika makao makuu ya wizara na kuuliza kama kozi wanayosoma inatambulika,ambapo mkurugenzi mafunzo NACTE aliwajibu kwamba kozi hiyo imefutwa tangu mwaka 2019.

    Taarifa kamili inawajia hivi punde..


    Share:
    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    Popular Posts

    Unordered List

    Pages

    Blog Archive


    Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger