Friday, 23 June 2023

MASHINE ZA SLOTI MADUKA YA MERIDIANBET CHIMBO JIPYA LA HERI



Meridianbet wakali wa odds kubwa, bonasi na promosheni kali, wamekuja na kitu kipya kwa wateja wanaobeti madukani, kuanzia sasa mchongo ni kucheza mashine za sloti zizopo kwenye maduka yote ya Meridianbet. Hizi ni sloti mashine kama zinazopatikana kasino ya mtandaoni.

Kwenye maduka ya Meridianbet utakutana na mashine za Sloti zinazokupa nafasi ya kucheza kasino ya Mtandaoni, Soma Yafuatayo>>>

Unachopaswa kufanya ni kwenda kwa Keshia wa madukani na atakuweka Kiwango unachohitaji kwenye mfumo ambapo kila Mashine ya Sloti ina Namba zake, kiwango cha chini kucheza ni michezo 8 na kiwango cha juu zaidi ni michezo 10 lakini michezo hii inategemea na mashine za sloti unazotumia.

Kumbuka mashine za sloti hazitumii mfumo wa Shilingi bali zinatumia Credit kwa mfano, Mteja akiweka Shilingi 1000 kwenye mfumo itasoma Credit 100, kwa maana hiyo 1 Credit= 10 TZS.

 

 

Kiwango cha chini kuweka kwenye mashine za Sloti ni Shilingi 1000 na kiwango cha juu ni Milioni moja. Mashine za Sloti zinazokupa uhalisia wa michezo ya kasino ya mtandaoni zinalipa mpaka Milioni Kumi ikiwa ni kiwango cha juu.

 

Dau la chini kucheza Sloti ni Shilingi 10 sawa na 1 Credit.

 

Aina ya Michezo Pendwa Kwenye Sloti Mashine

 

Katika Mashine za SlotI kuna michezo pendwa na rahisi zaidi kushinda kwa mfano utakutana na mchezo wa Matunda "Sizzling Hot", Mchezo wa Karata "American Poker", kuna Mchezo wa "The Money", Mwingine ambao ni rahisi zaidi ni mchezo wa King Card nao ni mchezo wa Karata, Bila kusahau "Book of RA" miongoni mwa michezo maarufu ya Misri "Egyptian Game".

 


Share:

AJALI YA BASI LA KILIMANJARO EXPRESS GARI DOGO YADAIWA KUUA WATU WAWILI


Watu wawili wanahofiwa kufa katika ajali iliyohusisha basi la Kilimanjaro Express lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam kugongana na gari dogo katika Kijiji cha Kijomu, kilichopo kata ya Hedaru wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.


Kwa mujibu wa Mtendaji wa kijiji cha Kijomu Veran Mtenga amesema ajali hiyo imetokea leo Juni 23, 2023 saa 12 asubuhi likihusisha basi la Kilimanjaro na gari dogo ambalo lilikuwa limeharibika ambapo kwenye gari dogo kulikuwa na watu miwili, mwanamke na mwanaume.
Share:

WALIOENDA KUTALII BAHARINI WATANGAZWA KUFARIKI


Mkuu wa Walinzi wa Pwani ya Marekani John Mauger amesema kwamba utafutaji na uopoaji wa miili ya abiria watano wanaoamini kuwa huenda wamepoteza maisha baada chombo cha chini ya maji kupoteza mawasiliano kwa siku ya tano leo unaendelea licha ya uwepo wa mazingira magumu.

Watu watano waliofariki baada ya chombo cha Titan kupoteza mawasiliano na mabaki yake kuonekana mita chache na yalipo mabaki ya Meli ya Titanic chini ya Bahari ya Atlantiki.

Kwa upande wa kampuni ya OceanGates imesema kuwa, "Sasa tunaamini kwamba Mkurugenzi Mtendaji wetu Stockton Rush, Shahzada Dawood na mwanawe Suleman Dawood, Hamish Harding, na Paul-Henri Nargeolet, wameaga dunia".

Aidha roboti ya ROV kutoka Meli ya Horizon Artic ilipata mabaki matano tofauti ya chombo hicho cha chini ya maji (Submarine) ikiwemo pua na mkia wa chombo hicho cha Titan pamoja na sehemu ya chemba ya presha ya chombo hicho.


Kifaa kilichokuwa kimewabeba watu hao watano

Walinzi wa Pwani ya marekani wamesema kwamba wataendelea kuchunguza eneo la bahari ambako mabaki ya chombo hicho yamepatikana ikiwa ni mita chache tu na yalipo mabaki ya Meli ya Titanic iliyozama mwaka 1912.

Chombo hicho (Submarine) kilipoteza mawasiliano siku ya Jumapili ikiwa imepita saa 1:45 tangu kianze safari yake ya kupeleka watalii chini ya bahari mita 3,800 yanakopatikana mabaki ya Meli ya Titanic.

Kampuni ya OceanGate huwatoza wageni $250,000 sawa na takribani milioni 500 za Kitanzania katika msafara wake wa siku 8 ili kuona mabaki ya Meli hiyo ambayo iko mita 3,800 chini ya usawa wa Bahari ya Atlantiki.
Share:

MUME ARUDI NYUMBANI BADA YA KUTUTELEKEZA KWA MIAKA SABA

Mahusiano yetu ya muda mrefu yaliniaminisha kuwa Isack ni baba bora wa maishani ni mwanaume ambaye hakuna mtu angeopena ampoteze katika maisha yake kwa namna yoyote ile lakini hili ndilo lililo nipofua macho japokuwa tulikuwa kwenye kipindi cha uchumba kwa muda mfupi tabia zake ndizo zilizo ni changanya nikafanya maamuzi ya kuzaa naye mtoto wa kwanza kisha nikaanza kuishi naye.


Ujauzito ulikuwa nikajifunguwa baada ya miaka mitatu nikabeba ujauzito mwingine hapo nikawa na watoto wawili wote wenye jinsia ya kiume ambawo Isack pia alioneshwa kufurahishwa sana na familia yetu nzuri, maisha yetu yahakuwa mazuri sana lakini kwa kuwa baba wa familia alikuwa ni muuzaji wa duka la mahitaji ya nyumbani ni pia haya kuwa mabaya sana kulingana na pale tulipokuwa tukiishi ni yeye pekee ndiye aliyekuw a na duka maeneo hayo kwahivyo pesa ndogondogo hazikutupiga chenga kabisa.


Mtoto alipokuwa akafikisha miaka miwili  kwa kweli hatukupata changamoto yoyote ile kwenye ulezi sasa nikawa nimekuza vijana na upendo wa Isack na tabia zake wala hazikuvadilika hakuna mtu ambaye angewaza kuwa Isack ni mtu wa kutukimbia familia kwani alifanya kila aliloweza kipindi chote cha kuishi pamoja na hakukuwa na tofauti wala magomvi yoyote katika ndoa yetu iliyoharalishwa na wazazi wetu wa pande mbili zote.


Asubuhi mmoja mtoto wa pili , Ndinagwe alionesha hali ya kuuguwa sana alikuwa akisumbuliwa sana na tumbo baba yake alituaga akasema anaenda kumtafutia dawa ya tumbo huko madukani jini akanywa chai kisha akaondoka alibeba kibegi chake cha mgongoni kidogo ambacho mara zote alikuwa akikibeba anapokwe nda mjini kwahivyo sote hatukujuwa kama ilikuwa ni kwaheri tulifahamu anaenda mjini kutafuta dawa na bidhaa za dukani kwake, wote tulijuwa hilo kichwani mwetu.

Muda ukaenda sana kutokea saa tatu asubuhi mpaka saa kumi jioni baba hakuwa amerudi nyumbani nikapiga simu kwa wazazi wake na marafiki zake wa karibu niliowajuw anao wakasema hawana taarifa za popote pale alipo mume wangu, nikaenda kituon jirani cha polisi kutoa tarifa huko wakanipa rb na utafutaji ukaanza.


Siku tatu baadaye baba wa watoto wangu hakuwa amepatikana bado, nikaenda mjini kule ambapo huwa ananunuwa bidhaa za dukani nawo pia wakasema ile siku hakufika, ushauri wa mwishho polisi wakasema nipeleke rb ile hospitali pengine alifariki wanipe ruhusa ya kuangalia miili lakini kila hospitali ya jirani hatukukuta mwili wa mume wangu.

Nikazoea nikajuwa kuwa baba amenitelekeza na watoto wake sikuishiwa nguvu nikaendelea kupeleleza polepole nikiwa nimejuwa sasa familia ile ni majukumu yangu tu na hakuna mwingine.Nafasi ya baba nikaichukua nikawa mama na nikawa baba sasa dukani pake pale nikawa mimi ndio nauza , biashara ilikuwa ngumu lakini nilipambana kidogokidogo miaka saba baadayae nikawa mzoefu wa bishara .


Jioni mmoja baada ya kufunga ofisini nikawaandalie wanangu cakula nilipita genge mmoja kununua mkaa nikakuta mdada mmoja aliyekuwa jirani sana na mume wangu akihadithiana na shoga yake juu ya habari za BAKONGWA, walikuwa wakimsifia kuhusu jinsi alivyobeba ujauzito wake wa mara ya kwanza, sikutaka kujionesha kama nilikuwa na shida nikangoja amalize mazungumzo kisha nikamuita pembeni nikamuuliza juu ya habari za dakari waliokuwa wanamzungumzia , aliniambia chukua nambari zake hizi za whatsapp +243990627777 mtafute atakusaidia tu shoga.

Niliporudi nyumbani tu baada ya kuwapikia watoto chakula cha usiku nikaandika namba zile kisha nikampigia tuliongea kwa undani sana nikamuelezea jinsi baba alivyoondoka ghafla mpaka kututelekeza wake kwa miaka yote hiyo saba na jitihada zote nilizofanya bila mafanikio.Alinipa pole kish akaniuliza majina yangu nay a mume wangu matatu , akaniambia nitume pesa kiasi kidog cha kuangalia jnyota na kisha akaniambia ipo dawa atanitumia asubuhi ya siku ya pili inayofuata.

Kesho yake nilipokea kifurushi kilichokuwa na dawa na maelekezo ya kutuia katika kipande cha karatasi, maelekezo yalinitaka nitumie dawa kwa muda wa siku mbili tu, nilianza kufanya hivyo mara mmoja nilipopata ile dawa maajabu ni kuwa kabla hata ya hizo siku mbili nilianza kuona namba ngeni kwenye simu ikinipigia alikuwa nimume wangu aliyeomba msamaha kuwa alipotelea huko kagera mipakani mwa Uganda sasa anarudi .


Sikuwahi kufikiria kama hii lingewezekana baada ya miaka yote ambayo ume wangu na baba wa familia alipotea bila taarifa ninakushukuru sana daktari Bakongwa kwa tiba zako nzuri .


Share:

NEEMA YAWASHUKIA WAKULIMA NA WAFUGAJI MBARALI KAMATI KUWASILISHA PENDEKEZO BUNGENI

 


Na Jacob Kasiri - Mbarali

Kamishna Msaidizi wa Ardhi - Mkoa wa Mbeya, Syabumi Mwaipopo amesema serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imerejesha hekta 74,432 kwa wananchi wa Mbarali  ili waendeleze kilimo na ufugaji lengo la kujikwamua kiuchumi tofauti na awali  ambapo maeneo hayo yalikuwa chini ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.

Kamishna Mwaipopo ameyasema hayo leo alipokuwa akiwasilisha ripoti kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea Shamba la Kapunga lililoko wilayani Mbarali kufanya tathmini ya utekelezaji wa uwekaji wa mpaka unaoendelea katika wilaya za Mbarali na Chunya mkoani Mbeya.

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa (MB) alisema kuwa baada ya kamati hii kutembelea uwandani na kujionea hali halisi itawasilisha mapendekezo ya walichokiona bungeni ili kubadili GN.28 na kuja na GN. mpya ambayo itakuwa ni suluhu kwa mgogoro uliodumu zaidi ya miaka 18.

"Ndugu zangu wana Mbarali, eneo lote hili lilorudishwa kwenu lilikuwa chini ya uhifadhi,na hivyo serikali kulitoa kwenu ina dhamira ya dhati kwa wananchi wake. Niwaombe, acheni zoezi hili liendee na kukamilika kwa wakati  ili muweze kufanya shughuli zenu za kilimo na ufugaji kwa manufaa yenu na taifa kwa ujumla" alisema waziri.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera akiwakaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii alisema kuwa ni kweli kama wananchi wanavyolalamika shamba la Kapunga halijapunguzwa.

 Shamba hili halikupitiwa na GN ya zamani na hata hii mpya haijapita pia kwa sababu GN mpya inapita katika maeneo yale yale yaliyopitiwa na GN.28 na wala haianzishi maeneo mapya. Hata, hivyo wananchi watambue kuwa Kapunga Estate ni shamba la serikali na huyu mwekezaji amepewa awekeze tu kwa muda maalum, na mkataba wake utakapoisha shamba hili litarudi serikalini.


Zoezi la uwekaji mpaka wilaya za Mbarali na Chunya limekamilika, ambapo vigingi 671 vimewekwa kwa umbali wa kilometa 344  kwa uwiano wa mita 500 kila kigingi ili kuwawezesha wananchi na wahifadhi kutambua maeneo yao ili kuepusha muingiliano.
Share:

Thursday, 22 June 2023

MAADHIMISHO YA SIKU YA MABAHARIA DUNIANI YAFUNGULIWA MWANZA....WAZIRI MAKAME ASISITIZA MASLAHI

Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Makame (mwenye tai nyekundu) akisikiliza ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na mabaharia wakati alipotembela na kukagua mabanda hayo.


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Makame amezitaka taasisi zinazosimamia mabaharia hapa nchini ziweze kuboresha maslahi ya mabaharia hao ili kazi hiyo iweze kua yenye tija kama zilivyo kazi nyingine.


Waziri Makame ameyasema hayo Alhamis Juni 22, 2023 wakati akifungua maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani yanayofanyika kitaifa jijini Mwanza akimwakilisha Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman.

"Nikubaliane na waliosema na mimi nalisema hii kwa sababu nimeiona na nimeisikia maslahi duni ya mabaharia zipo taasisi hapa ambazo zinasimamia mabaharia naomba hili mlichukue mwenyekiti amesema chungu kipo jikoni lakini lisikawie basi",amesema.


Katika hatua nyingine Waziri Makame amepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini ikiwemo ujenzi wa meli mpya ya MV. Mwanza pamoja na ukarabati wa meli ya MV. Mapinduzi II.

Aidha pia Mh. Makame pia ameongeza kwa kuitaka jamii iweze kuondokana na dhana potofu ambazo zimekua zikiihusisha kazi ya baharia na uhuni kwani kazi hiyo husomewa na fani kama zilizo fani nyingine.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi ambae aikua akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. Amosi Makalla amesema serikali ya awamu ya sita imekua ikifanya shughuli mbalimbali za maendeleo katika sekta ya bahari na maziwa ambapo mwa mkoa wa mwanza serikali imetoa kiasi cha silingi bilioni 21 kwa ajili ya ujenzi wa vizimba vya samaki huku pia ikitekeleza mradi wa ujenzi wa meli mya ya MV. Mwanza ambayo imegharimu kiasi cha billion 111 na kukamilika kwa miradi hiyo kutaibua fursa ya ajira kwa watu mbalimbali hapa nchini.

Naye mjumbe wa bodi ya wakurugenzi TASAC Captain. King Chiragi amesema wao kama TASAC wanaridhika na namna serikali inashughulikia tasnia ya bahari kwani serikali imekuwa ikitunga sera ambazo zimekuwa zikilenga kuimarisha ustawi wa baharia.

Aidha amewaomba wananchi wote waweze kuwaheshimu mabaharia wote hapa nchini kwani wamekuwa wakijtoa sana katika kulinda ustawi wa jamii.

Katibu Chama cha Mabaharia Zanzibar, Ally Mzee ambaye amezungumza kwa niaba ya mabaharia, amesema kada hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira za uhakika, maslahi duni, mazingira rafiki kazini hususani kwa wanawake pamoja na vyama kushindwa kuwatetea mabaharia wanapokumbana na changamoto kazini.


Maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani yanafanyika kitaifa katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kuanzia Juni 22-25, 2023 ambapo yataambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji elimu usalama majini, kufanya usafi katika fukwe za Ziwa Victoria pamoja na mbio ya riadha itakayowashirikisha mabaharia yakiambatana na kauli mbiu isemayo “Miaka 50 ya Marpol, uwajibikaji unaendelea”.
Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Makame akifuatilia ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani yaliyofanyika katika uwanja wa furahisha jijini Mwanza
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Shekilage akitoa salamu kwa mabaharia kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Amos Makala
Msimamizi mkuu wa bandari Zanzibar Sheikha Mohamed akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani
Mjumbe wa bodi ya shirika la meli Tanzania TASAC King Chiragi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani
Mwakilishi wa kampuni za huduma za meli ndug Anselm Namala akiendelea kupata taarifa katika mabanda ya maonyesho ya siku ya mabaharia duniani.
Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Makame akisikiliza ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na mabaharia wakati alipotembela na kukagua mabanda hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa jukwaa kuu wakifuatilia ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani.
Wadau mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa maadhimisho ya mabaharia duniani.
Share:

TAFITI ZA KISAYANSI KUTUMIKA KUONGEZA UZALISHAJI NA VIPATO VYA MAKUNDI MAALUM




Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt John Jingu,akizungumza wakati akifungua Warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Makundi Maalum,Bw.Juma Samwel ,akielezea lengo la warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa uratibu na uendelezaji wa Utafiti,Tume ya Sayansi na Utafiti (COSTECH) Dkt Bugwesa Zabron Katale, akizungumza wakati wa Warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.


Afisa Maendeleo ya Jamii Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,akizungumza wakati wa Warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.


Sehemu ya Washiriki wakiwa katika warsha ya iliyoratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Utafiti (COSTECH) ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt John Jingu,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

KATIBU Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jmii,Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk. John Jingu,amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za kisayansi kufanya tafiti mbalimbali zitazotoa majibu ya kuongeza uzalishaji na vipato vya watu walio katika makundi maalum nchini.

Dk.Jingu ameyasema hayo leo Juni 22,2023 jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo ya utengenezaji wa Vijarida sera vitakavyotatua changamoto za Makundi Maalum.

Dk. Jingu amesema kuwa sayansi na teknolojia inaweza kutumika katika kusaidia kupata majawabu yenye ushahidi ili kusaidia makundi maalum.

“Ni matarajio yetu kikao kazi hiki ni makubwa kwani tunatarajia majawabu yenye ushahidi na yanatokelezeka ili kupata njia nzuri zaidi za kusaidia Makundi Maalum katika kuinua hali yao ya kiuchumi”Alisema Dk. Jingu.

Amesema Mazingira yanaruhusu kuja na majawabu yenye ushahidi kwani miundombinu ipo na imesambaa nchini ikiwemo barabara, nishati, taasisi binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Mkurugenzi wa idara ya Makundi Maalum kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Juma Samwel amesema serikali inapambana kuhakikisha wafanyabiashara ndogondogo wanakua kiuchumi.

“Tunatamani Makundi haya maalum yaweze kurahisishiwa mazingira ya kufanyia kazi kwa kushirikishwa kwa ukaribu katika masuala yanayowahusu lakini pia mamlaka husika na yanayowagusa wazalishaji hawa wadogo kufanya nao kazi kwa ukaribu ili kurahisisha uzalishaji wao kwa mfano Latra kuweza kuongeza ukaribu nao ikiwemo kuwaelemisha juu ya masuala mbalimbali”

Aidha, Mkurugenzi wa uratibu na uendelezaji wa Utafiti, Tume ya Sayansi na Utafiti (COSTECH) Dk. Bugwesa Zabron Katale amesema lengo kubwa la taasisi ni kutatua changamoto zinazokumba Jamii katika kada mbalimbali.

“Lengo kubwa la Tume ya Sayansi na Utafiti ni kutatua changamoto zinazoikumba jamii kupitia tafiti mbalimbali na kuja na masuluhisho yatauowezesha kuleta mabadiliko na maendeleo katika Taifa.Hivyo kuwa na Taifa linalofanya vitu kitaalam na si kwa mazoea”
Share:

ADMIN WA GROUP LA WHATSAPP AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMPIGA 'REMOVE' MWANACHAMA

Mahakama nchini Uganda imemuamuru msimamizi wa WhatsApp wa kundi moja kumrejesha mwanachama aliyemshtaki kwa kumfukuza kwenye kundi hilo.

Mwanaume mwenye hasira kutoka Uganda aliyetambulika kwa jina la Herbert Baitwababo alikwenda mahakamani kuwashtaki wasimamizi wa kundi la WhatsApp la 'Buyanja My Roots' kwa kumuondoa kwenye kundi hilo baada ya kuuliza maswali kuhusu utumizi wa pesa walizokuwa wamechanga.

Katika ripoti ya gazeti la Daily Monitor, Herbert, kwenye stabadhi za mahakama, alisema shida ilitokea wakati alipoanza kuuliza jinsi ukaguzi na uwajibikaji wa fedha zilizochangwa kwenye kundi la WhatsApp.

Wanachama walikuwa wakichanga KSh 1,000 kama ada ya uanachama, na kundi hilo lilikusudiwa kusaidia kazi za hisani, lakini alipouliza kuhusu jinsi pesa hizo zilivyotumika, alifukuzwa.

Mnamo Jumatatu, Juni 19, 2023 Herbert alipata ahueni baada ya mahakama kwamba kufukuzwa kutoka kwa kikundi cha WhatsApp ni kinyume na uhuru wake wa kujumuika. 

"Agizo la kudumu pia limetolewa kumzuia mlalamikiwa, mawakala wake au wasaidizi wake kuendelea kukiuka haki ya ushirika ya mwombaji," alisema hakimu.

Share:

CHEZA AVIATOR MWEZI HUU UNYAKUE BETI ZA BURE



Imagine upo ndani ya ndege na wewe ndio rubani wa hiyo ndege kuna raha eeh! Tulia hivyo hivyo nikusanue mchongo mkubwa wa kupiga mpuga wa kutosha unapocheza kasino ya mtandaoni ya Meridianbet mchezo wa Aviator.


 

Kila ukirusha ndege ya Aviator unajiweka kwenye nafasi ya kupata bonasi ya Mvua za bure za kuendelea kurusha ndege ya Aviator na kuusaka ushindi mkubwa.

 

Promosheni hii inapatikana kwa kucheza mchezo wa aviator kutoka kasino ya mtandaoni, huku ukiweka dau lako utakalo, kumbuka ushindi mkubwa unategemea ukubwa wa dau uliloweka.

 

Namna ya Kupata Bashiri za Bure za Aviator

 

Promosheni “Bashiri za Bure na Aviator Bonanza, 20.06.2023 hadi 30.06.2023. na inapatikana kwa wateja wote wa Meridianbet.

 

Wakati wa promosheni hii, wachezaji wa kasino ya mtandaoni kwenye mchezo wa Aviator watapewa zawadi ya BASHIRI ZA BURE mara 20 kwa siku kwa wateja 25 wenye kasi zaidi ya kurusha ndege ya Aviator kila muda kwa kubofya kitufe cha TUMIA utapatiwa bashiri za bure zenye thamani ya shilingi 500.

 

Kwa kufungua sehemu ya ‘Andika Ujumbe’ ndani ya mchezo wa Aviator kasino ya mtandaoni, bofya alama upande wa juu kulia na, tegemea mvua ya bashiri za bure. Baada ya mteja kutumia bashiri za bure, kwenye sehemu ya orodha ya mchezo wa Aviator, atapaswa kubofya sehemu ya “BASHIRI ZA BURE” na kuchagua bashiri ya bure kama dau.

 

Ushindi wa odds ya 1.95 na kuendelea ndio unaweza kuwekwa kwenye akaunti ya pesa halisi. MVUA ya BASHIRI ZA BURE itashuka bila mpangalio, mara 20 kwa siku wakati wote wa promosheni ya kasino ya mtandaoni, kila mvua itanyesha kwa dakika 10.

 

Mara baada ya bashiri ya bure kutumika, mteja atakua na takribani dakika 10 za kuitumia bashiri ya bure kucheza mchezo huu wa kasino ya mtandaoni, Ikitokea bashiri ya bure haijatumika, mteja hatoweza kuitumia tena.

 

N.B: Mbali na Mchezo wa Aviator, Meridianbet wanakupa zawadi ya mizunguko ya bure kucheza kwenye kasino ya mtandaoni kwa mteja mpya baada ya kujisajili.


Share:

MWANAMKE AJIFUNGUA KWENYE TRENI


Mwanamke mmoja nchini Kenya amejifungua wakati akiwa kwenye treni ya Madaraka Express iliyokuwa ikielekea Mombasa.

Kwa Mujibu wa mtandao wa Twitter wa shirika la reli la Kenya, mwanamke huyo alimkaribisha mtoto wake kwa usaidizi wa daktari ambaye alikuwa ndani ya usafiri huo na mhudumu wa abiria.

"Tulibarikiwa kuwa na Dkt. Indanyenyi Luseso ambaye alitoa huduma hiyo, akisaidiwa na Mhudumu wetu wa Abiria, Bi. Mary Nyiha" Shirika la Reli la Kenya liliandika pamoja na picha zinazoonyesha mhudumu akiwa amemshika mtoto.

Mwanamke huyo baadaye alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Mariakani kwa usaidizi zaidi wa kimatibabu
Share:

VIONGOZI WA MKOA WA MTWARA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MGONGANO WA MASLAHI




Kamishna wa Maadili Mh Jaji Sivangilwa Mwangesi aliyesimama akiwahutubia viongozi, kulia kwake ni Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Bw Enoch Ngailo na kushoto kwake ni Katibu msaidizi kanda ya kusini Mtwara Bw Philoteus Manula.


Kamishna wa Maadili Mh Jaji Sivangilwa Mwangesi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Mtwara baada ya kikao kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Sekretarieti mkoani Mtwara leo Juni 22,2023.

Na.Mwandishi Wetu.

Viongozi wa Umma mkoani Mtwara wametakiwa kujiepusha na mgongano wa maslahi wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku ili kujenga imani kwa serikali na wananchi wanaowaongoza.

Kauli hiyo, imetolewa na Kamishna wa Maadili Mh Jaji Sivangilwa Mwangesi katika kikao chake na viongozi mkoani humo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mkoani Mtwara leo Juni 22,2023.

Mh Mwangesi katika hotuba yake amefafanua kuwa, kiongozi wa umma akifanya kazi kwa uadilifu atatoa huduma bora na taratibu, kanuni na sheria na kwamba mianya ya mgongano wa maslahi utapungua.

Mh Mwangesi amebainisha kuwa, kiongozi akiwa muadilifu, atakuwa jasiri katika kutoa maamuzi ya haki uwazi na usawa katika utekelezaji wa majukumu yake.

Aisha Mhe, Mwangesi ameongeza kuwa,kiongozi akiwa muadilifu atafata taratibu na sheria pia atasimamia misingi ya maadili ya viongozi kwa uwazi bila upendeleo na kwamba wananchi watakuwa na imani na viongozi wanaowaongoza.

Kuhusu suala la zawadi Mh Mwangesi amewakumbusha viongozi hao kuwa, sheria inamtaka kiongozi kupokea zawadi isiyozidi shilingi laki mbili, iwapo zawadi hiyo itazidi kiasi hicho anatakiwa kuipeleka kwa Afisa masuhuli kwa ajili ya kuitolea maamuzi.

Kamishna wa maadili amefanya kikao hicho na viongozi wa mkoa wa Mtwara ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma kitaifa iliyoanza rasmi tarehe 16 juni na inatarajiwa kukamilika tar 24 juni 2023.

Kikao hicho cha viongozi wa mkoa wa Mtwara kimehudhuriwa na vionhozi zaidi ya 50 kutoka katika Taasisi za umma na mashirika ya umma pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mtwara.
Share:

Je? UNASUMBULIWA NA MATATIZO YA NGOZI? ZAHA SOAP NDIYO SULUHISHO UTASHANGAA



Je?  unasumbuliwa na harara, muwasho, chunusi, makunyanzi, mba,vipele na matatizo mengine ya ngozi??? Ondoa shaka!! Zaha Soap ndiyo suluhisho! Tunazo Sabuni asili zitakazokufanya uwe na ngozi nyororo na ya kuvutia!!


Tuna Sabuni ya Kahawa!! Sabuni ya Mchele!, Sabuni ya Alovera! Sabuni ya Papai! Sabuni ya Maziwa na Sabuni ya Manjano!!


Tupo Shinyanga Mjini!! na tunatuma mzigo popote ulipo.


Wasiliana nasi 0677656443
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger